TCAA YATAKIWA KUONGEZA VIWANGO VYA UTOAJI HUDUMA.

October 30, 2023

 


Na Karama Kenyunko Michuzi tv
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) kuongeza viwango vya utoaji huduma sambamba na kuimarisha mifumo ya udhibiti wa matumizi mabaya ya viwanja vya ndege nchini.

Amesema viwanja vya ndege havipaswi kuwa vichochoro vya kusafirishia bidhaa haramu kwani itaharibu sifa za nchi na hivyo, kutokuwa miongoni mwa nchi zenye udhibiti wa anga.

Akizungumza leo Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 20 ya TCAA tangu kuanzishwa kwake mwaka 2003, Waziri Majaliwa amesema mifumo ya udhibiti inapaswa kuimarishwa kwa lengo la kudhibiti na kusimamia huduma za usafiri wa anga nchini.

"TCAA hakikisheni viwanja vya ndege kote nchini haviwi vichochoro vya kusafirishia bidhaa haramu ili nchi iendelee kuwa na sifa ya kuwa kati ya nchi zenye udhibiti wa anga ," amesema Majaliwa.

Pia amesema mamlaka hiyo inapaswa kujifunza kutoka kwa mataifa yaliyoendelea ili kuongeza viwango vya utoaji huduma.

Pamoja na mambo mengine, ameitaka TCAA kuwa wabunifu kwa kuwa na mikakati ya kuimarisha soko ili nchi isiachwe nyuma kimaendeleo.

"Niagize wadau wa usafiri wa anga nchini, mtekeleze majukumu yenu kwa kufuata sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayosimamia masuala ya usafiri wa anga kitaifa kwa ajili ya kipaumbele namba moja katika usafiri wa anga ni usalama," amesisitiza.

Vilevile aliitaka TCAA kubuni na kuongeza vyanzo vipya vya mapato ya mafunzo ya ndege ili kuongeza idadi ya marubani wanaopata ufadhili wa masomo.

Majaliwa ameagiza Bodi ya Mikopo kufanya marejeo ya viwango vya mikopo vinavyotolewa kwa wanafunzi wa urubani ili kutoa kipaumbele kwa wahitaji wa fani za masuala ya usafiri wa anga.

"Watanzania endeleeni kuviamini na kutumia vyuo vilivyopo nchini kwani vinatoa mafunzo ya uhakika ya utalaamu wa anga wa uhakika," ameeleza.

Majaliwa ameongeza kuwa serikali imepanga kuimarisha sekta ya anga kwa kuwezesha ununuzi wa rada za kisasa nne za kuongoza ndege za kiraia ambazo zimefungwa katika viwanja vya ngege vya mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro na Songwe.

"Hivi karibuni, viwanja vya ndege vya Zanzibar na Julius Nyerere vilikaguliwa na kupata asilimia 86.7 hatua hiyo imeowezesha nchi yetu kushika nafasi ya nne badani Afrika ikitanguliwa na nchi ya Nigeria ,Kenya, Ivory Cost, huu ni ushindani tosha kwamba uwezo wa nchi yetu katika kidhibiti usalama wa anga unaendelea kuimarika,"amesema.

Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amewapongeza TCAA Kwa kusimamia ukaguzi huo na kuiweza nchi kupata alama 86.7 katika viwanja vya Dar es Salaam na Zanzibar.

Amesema serikali imeboresha miundombinu mbalimbali ya viwanja vya ndege hivyo kutokana na maboresho hayo anaamino ukaguzi ujao nchi itafikia asilimia 90.

Naye, Mkurugenzi wa TCAA, Hamza Johari, ameeleza kuwa mamlaka hiyo inaendeshwa kwa kutumia mapato ya ndani na kwamba haitegemei ruzuku ya serikali.

"Kwa miaka mitano tumekusanya bilioni 319.9 na bilioni 24.5 tumechangia katika mambo mbalimbali ya kijamii,"amesema Johari

Alisema TCAA imefungua mikataba mbalimbali ya usafiri Kwa nchi 80 hivi karibuni wameingia mkataba na nchi ya Marekani hivyo kuviwezesha ndage ya Air Tanzania kwenda kwenye nchi hiyo.

"TCAA wataacha kusomesha marubani nje ya nchi na kusomesha kwenye Chuo cha Taifa cha Usafirishaji nchini (NIT) Kwa mwaka tulikuwa tunapeleka marubani 10 nje ya nchi sasa tunasomesha marubani 30 nchini na fedha kubaki nchini,"amesema.





DKT. BITEKO AFUNGA SEMINA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI KUHUSU MKATABA WA WAKALA WA KIMATAIFA WA NISHATI JADIDIFU (IRENA)

DKT. BITEKO AFUNGA SEMINA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI KUHUSU MKATABA WA WAKALA WA KIMATAIFA WA NISHATI JADIDIFU (IRENA)

October 30, 2023

 




Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati akihitimisha Semina iliyotolewa kwa wabunge hao kuhusu Mkataba wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu (IRENA), Tarehe 30 Oktoba 2023, Bungeni Dodoma.

………………………

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amefunga Semina ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo ililenga kuwapa uelewa Wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu Mkataba wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu (IRENA) ambapo Tanzania imeonesha nia kujiunga na mkataba huo kutokana na faida zake.

Akihitimisha semina hiyo iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 30 Oktoba 2023,
Dkt. Biteko amesema Tanzania ikijiunga na IRENA itanufaika na mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya nishati jadidifu na pia itanufaika na programu za nchi za kusini na Mashariki mwa Afrika kwa ajili ya mifumo unganishi ya kusafirisha umeme.

“Faida nyingine ambazo Tanzania itapata ikijiunga na Mkataba wa IRENA ni kunufaika na mikopo mbalimbali ya kufanya tafiti, kuibua na kuendeleza miradi ya Nishati Jadidifu inayotolewa kwa nchi wanachama na kupata misaada ya kiteknolojia kwa ajili ya uendelezaji wa nishati Jadidifu.” Amesema Biteko

Ameongeza kuwa, Tanzania pia itanufaika na ufadhili wa mafunzo ya Nishati Jadidifu kwa kuwajengea uwezo watalaamu wa kitanzania katika kusimamia utekelezaji wa mipango ya Nishati Jadidifu pamoja na kunufaika na tafiti za kiteknolojia za nishati jadidifu kupitia vyuo vya hapa nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Mathayo David Mathayo amesema kuwa, kamati yake inaunga mkono Tanzania kuingia katika mkataba huo wa IRENA ili kuweza kunufaika na fursa zilizopo.

IRENA ni Taasisi iliyoanzishwa Januari mwaka 2009 na ilianza kutekeleza majukumu yake Aprili 2011 ambapo Tanzania ipo katika taratibu za kujiunga na Taasisi hiyo.



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati akihitimisha Semina iliyotolewa kwa wabunge hao kuhusu Mkataba wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu (IRENA), Tarehe 30 Oktoba 2023, Bungeni Dodoma.



Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati wa Semina iliyotolewa kwa wabunge hao kuhusu Mkataba wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu (IRENA), Tarehe 30 Oktoba 2023, Bungeni Dodoma.



Katibu Mkuu Wazara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati wa Semina iliyotolewa kwa wabunge hao kuhusu Mkataba wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu (IRENA), Tarehe 30 Oktoba 2023, Bungeni Dodoma.



Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala, Mhandisi Innocent Luoga akiwasilisha Mada kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati Semina kwa wabunge hao kuhusu Mkataba wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu (IRENA), Tarehe 30 Oktoba 2023, Bungeni Dodoma.



Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakipotia nyaraka wakati Semina kuhusu Mkataba wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu (IRENA), Tarehe 30 Oktoba 2023, Bungeni Dodoma.

WADADISI NA WATAFITI WA MASUALA YA KIUCHUMI WATAKIWA KUWA WASIRI

October 30, 2023

 Na Karama Kenyunko Michuzi TV

WADADISI na wasimamizi wa utafiti wa masuala ya kijamii na kiuchumi wametakiwa kuzingatia weledi na usiri mkubwa wakati wa ukusanyaji wa taarifa hizo.

Akizungumza Dar es Salaam jana Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashim Abdallah amesema hatutawavumilia wale watakaotoa taarifa kabla hazijachakatwa na wakibainika watawachukulia hatua za kisheria.

Ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi hao zaidi ya 500 kutoka mikoa yote Tanzania Bara yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Dkt. Abdallah amewahimiza wenye viwanda na wafanyakazi watakaoombwa taarifa kutoa ushirikiano kwa ajili ya kupata takwimu sahihi kwa manufaa ya taifa.

"Kila mmoja anatakiwa ajue amebeba dhima ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan, hivyo mzingatoe usiri na weledi wakati wa kukusanya taarifa," amesema Dkt Abdallah.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi wa NBS, Dkt. Amina Msengwa amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwanoa watafiti hao ili kwenda kufanya utafiti nchi nzima, kujua idadi kamili ya shughuli za kiuchumi kwenye Viwanda, shule, maduka na hospital utakaosaidia katika utekelezaji wa maendeleo ya nchi.

Amesema mara ya mwisho kukusanya tafiti za kiuchumi ni mwaka 2015 hivyo, baada ya mafunzo hayo ya siku tano, washiriki watafanya kazi hiyo kwa siku 60 katika mikoa yote.

"Taarifa zitasaidia kuthamini na kuchambua mwenendo wa uchumi, tutajua wamiliki na biashara zao, takwimu zitakuja kutumika katika maendeleo ya nchi,"amesema.
 




CPC WAWEZESHA VIJANA 50 KUPATA MAFUNZO SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU NYERERE KIBAHA

October 30, 2023
Naibu Katibu Mkuu CCM  bara Anamringi Macha  akizungumza  na washiriki  wakati alipokua mgeni  rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku kumi  Uongozi  hao  yaliyodhaminiwa  na  Chama Cha Kikomunisti Cha China kwa vijana 50 yanayofanyika katika  Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kwa Mfipa Wilayani Kibaha Mkoani Pwani  leo Oktoba 30,2023.

Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
CHAMA Cha Kikomunisti cha nchini China (CPC), kimetoa ufadhili wa mafunzo mafupi ya siku kumi kwa wanachama 50 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Umoja wa Vijana na UWT ambao wamechaguliwa kote nchini lengo likiwa ni kuwajengea uwezo masuala ya Siasa, uchumi na mkakati wa kuendeleza mahusiano kati ya nchi ya China na Tanzania.

Hayo yamesemwa wakati akifungua mafunzo hayo Naibu Katibu Mkuu CCM bara CDE Anamringi Macha katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha Mkoani Pwani leo Oktoba 30,2023.

CDE Anamringi amesema kuwa mafunzo haya ni mahsusi kwa ajili ya kuwajengea uwezo Viongozi ili na wao waweze kwenda kutoa elimu ya mafunzo watakayo yapata baada ya kuhitimu.

Macha amesema kuwa viongozi hao watapata fursa ya kupewa mafunzo hayo kupitia wawezeshaji ambao pia ni Viongozi Wasomi wabobezi na wanazuoni pia ni viongozi wakongwe katika historia ya nchi kwa kufanya kazi kwa miaka mingi serikalini ili wawafundishe viongozi hao uvumilivu katika kulitumikia taifa.

Amewataja baadhi ya Wawezeshaji hao kuwa ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa na Katibu Mkuu kwa kipindi cha miaka kumi,pia alikua Mkuu wa Chuo Cha CCM Kivukoni Mzee Philip Mangula, Komredi Stephen Wassira, alikuwa Naibu Katibu Mkuu Visiwani Abdallah Mabodi, Prof. Samuel Wangwe , Prof. Paramagamba Kabudi.

Aidha katika mafunzo haya wakufunzi kutoka CPC ambao ni Jiang Wen,Wang Yao na Tan Xin watatoa mada ya mahusiano ya nchi mbili hizi katika sekta ya uongozi, kibiashara, mahusiano na ushirikiano wa China kiuchumi, na siasa ili waweze kuiva na kuwa mabalozi katika kizazi hiki na kijacho.

"Tutawafundisha mbinu kwa nini CPC wameweza kudumu na kuwa chama kikongwe kilichodumu madarakani kwa miaka 100 tangu kilipoanzishwa" amesema Macha.

Aidha amesema kuwa Viongozi hao watafundishwa masuala ya maendeleo, mafanikio ya nchi ya China kwa sasa na mikakati iliyopo kuelekea miaka ijayo.

Ameongeza kuwa CCM kimewakusanya viongozi hao wa UVCCM na UWT ili kuendelea kuwafunda vijana wake ili watambue kuwa wana wajibu nini cha kufanya kwa Taifa lao badala ya kuendelea kutegemea taifa liwafanyie kitu gani.

"Moja ya matatizo makubwa kwa vijana wetu sasa hivi wanakosa uvumilivu wanaingia katika maeneo wakitaka mambo yabadilike kwa haraka yakiwahusu wao kwahiyo tunapowaweka hapa tunawafunda na kuwaeleza umuhimu wa uongozi" amesema

Aidha amesisitiza kuwa viongozi wataendelea kuwaweka vijana kwenye nafasi za uongozi na kwamba mabadiliko ya nafasi yanapotokea ni kutaka kuona nani anafaa kwenye nafasi hiyo hasa katika utendaji na kuleta maendeleo.

Hatahivyo Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM bara ameonya tabia ya baadhi ya viongozi vijana kulewa madaraka na badala yake wametakiwa kufanyakazi kwa kuzingatia weledi.

Amesema baadhi ya viongozi vijana wa sasa wengi wamekuwa hawana uvumilivu na kwamba baadhi ya nafasi za uongozi walizonazo wamekuwa wakizitunia vibaya na kwamba CCM haita sita kuwaondoa na kuwachukulia hatua.

"Lazima tuwe wakweli tatizo tulilonalo sasa hivi vijana wanakosa uvumilivu wanaingia kwenye uongozi na kutaka mambo kubalika Kwa haraka huku wengine wanalewa madaraka badala ya kutumia nafasi kwa kufanya kazi iliyokusudiwa na kuanza kufanya vitu kinyume na inavyotakiwa, mtu huyo hatuwezi kumuacha tutamuondoa mara moja" amesema

Aidha Macha amesema lengo la Chama Cha Mapinduzi ni kuwalea vijana na kuwa viongozi bora na kwamba mafunzo hayo yanalengo la kuwafunda kiungozi na wanawajibu wa kulifanyia taifa mambo makubwa.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Baraza la Umoja wa Wanawake Taifa (UWT), Mariamu Ulega amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha hayo mafunzo "hii ni fursa kubwa kwa wanawake kwa sababu ukimuelimisha mwanamke umeielimisha jamii nzima" hivyo elimu hii tutakayoipata tutakwenda kuipeleka kwa jamii hususani katika ziara mbalimbali ambazo zinafanywa UWT" amesema.

"Kama sasa hivi kumekua na ziara zinazoendelea kupitia Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda ambapo wanapita kufanya mikutano mbalimbali katika ngazi za Kata, Vijiji na Mkoa.

Akizungumzia kuhusu chaguzi za serikali za mitaa mwakani amesema Ulega amesema kuwa wanawake wajitokeze kuchukua fomu za kugombea huku ametoa wito kwa wanawake wengine kuwasapoti kuwasaidia ili waweze kushinda" amesema Mariamu.

Mariamu amewakumbusha wananchi kujitokeza kwenye mikutano mbalimbali ya chaguzi zijazo na kusikiliza sera za chama na kukipa nafasi zaidi CCM.

Naye mshiriki wa mafunzo hayo Mhandisi Fatma Rembo amesema kuwa anategemea kuwa baada ya kupata mafunzo haya wanatarajia kuja kuwa viongozi bora zaidi kwa kuliongoza taifa.

Wakufunzi kutoka Chama Cha Kikomunisti Cha China (CPC) Jiang Wen,Wang Yao na Tan Xin wakifuatilia ufunguzi  wa mafunzo  ya viongozi hao.
Mjumbe  wa Kamati ya Utekelezaji  wa Baraza UWT Mariam Ulega, akizungumza  na waandishi wa habari katika ufunguzi wa mafunzo ya siku kumi ya Uongozi yaliyodhaminiwa  na  Chama Cha Kikomunisti Cha China kwa vijana 50 yanayofanyika katika  Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kwa Mfipa Wilayani Kibaha Mkoani Pwani  leo Oktoba 30,2023.
Mhandisi  Fatma  Rembo ambaye pia ni mshiriki  wa mafunzo, akizungumza  na waandishi wa habari katika ufunguzi wa mafunzo ya siku kumi ya Uongozi yaliyodhaminiwa  na  Chama Cha Kikomunisti Cha China kwa vijana 50 yanayofanyika katika  Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kwa Mfipa Wilayani Kibaha Mkoani Pwani  leo Oktoba 30,2023.



RAIS SAMIA AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA BURUNDI IKULU DAR ES SALAAM

October 30, 2023

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye ambaye ni Waziri wa Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Vijana Michezo na Utamaduni Mhe. Balozi Gervais Abayeho (pamoja na ujumbe wake) mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 30 Oktoba, 2023.

BALOZI NJALIKAI AKUTANA NA BALOZI WA KWANZA WA ALGERIA NCHINI TANZANIA

October 30, 2023

 Balozi wa Tanzania Nchini Algeria Iman Njalikai leo Oktoba 30, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Balozi Noureddine DJoudi, Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Marafiki wa Algeria tangu kipindi cha Ukombozi ambaye ndiye Balozi wa Kwanza wa Nchi hiyo nchini Tanzania mara tu baada ya kujipatia uhuru wake mwaka 1962.


Mazungumzo na Balozi huyo mwenye historia na kumbukumbu kubwa ya uhusiano wa Algeria na Tanzania yalifanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers na yalilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya Algeria na Tanzania.

Mheshimiwa Balozi Joudi alifika Ubalozini kufuatia mwaliko wa Balozi Njalikai kwa lengo la kufahamiana na kumpongeza kwa majukumu mapya aliyokabidhiwa na Serikali ya Algeria.

Aidha, sambamba na kumhakikishia ushirikiano zaidi Balozi Njalikai alimshukuru Balozi Joudi kwa kuendelea kuwa kiungo muhimu katika kuimarisha mahusiano kati ya Ubalozi na Mamlaka mbalimbali za Algeria ikiwemo sekta binafsi.

Kwa upande mwingine, Ubalozi umepokea na unafanyia kazi ombi la Balozi Joudi kuhusu kuimarisha kituo cha Kiswahili kilichopo Ubalozini ikiwa ni pamoja na kuitangaza zaidi Lugha hiyo adhimu kwa kuifundisha kwa WaAlgeria.




WATEJA WATANO WASHINDA FEDHA TASLIMU KUPITIA DROO YA KOPA

October 30, 2023

 Jumla ya wateja watano wa benki ya Letshego Faidika wameshinda zawadi  za fedha taslimu kupitia droo ya kampeni ya mpya ya Kopa Tukubusti.

Wateja hao ni Lucas  Skale wa Kaliua aliyeshinda sh 1,042,500, Spear Malipotea  wa Babati aliyeshinda sh3,015, 000 na Pamela Kenyuko wa Ushetu  aliyeshinda sh187,533.

Wengine ni Issa Kitangu wa Kasulu aliyeshinda sh 147,872na Fatuma Lugongo aliyeshinda sh 133,141.

Wateja hao wameshinda kiasi tofauti cha fedha baada ya kukopa fedha ambapo benki hiyo uwazawdia  asilimia 50 ya kiasi cha fedha waliyokopa baada ya kuchezesha droo kila baada ya wiki mbili.

Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw Asupya Nalingigwa aliwapongeza washindi hao kwa kujipatia fedha hizo ambazo uwekwa kwenye akaunti ya mshindi moja kwa moja.

Nalingigwa alisema kuwa kampeni hiyo inazidi kushika kasi na kuwaomba wateja wao kuchangamkia mikopo yao ili kushinda zawadi mbalimbali na kuweza kusaidia kugharimia mahitaji mbalimbali.

Benki hoyo imetenga kiasi cha Sh50 billion kwa ajili ya kuwazawadia wateja wao kupitia kampeni hiyo.

 “Tumeweka jumla ya Sh50 biliioni kwa ajili ya kukopesha wateja wetu. Mteja anaweza kushinda fedha ya ziada (Bonus) ya asilimia 50 ya kiasi cha fedha alichokopa kupitia kampeni hii mpya ya Kopa Tukubusti. Lengo hapa ni kubadili maisha ya wateja wetu. Kwa mfano, mteja  anaweza kukopa mpaka kiasi cha Sh milioni 150 ambapo akishinda kupitia kampeni ya Kopa Tukubusti, atazawadiwa Sh milioni 75,” alisema Bw. Nalingigwa.

Kwa mujibu wa Bw Nalingigwa, vigezo mbalimbali vimewekwa kwa washiriki wa kampeni hii ikiwa pamoja na umri kuanzia miaka 18, lazima awe mfanyakazi aliyethibitishwa wa serikali na taasisi binafsi na lazima awe na sifa za kupata mkopo kwa mujibu wa vigezo na masharti.

Kwa upande wake, Afisa Msimamizi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Pendo Mfuru aliipongeza benki ya Letshego Faidika kwa kuendesha droo hiyo ambayo inawafaidisha wateja wake.

Mfuru alisema kuwa droo hiyo imekidhi vigezo vyote na kuwaomba wateja wa benko hiyo kuchangamkia fursa hiyo ili kunufaika nayo.

Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Benki ya Letshego Faidika Bw. Asupya Nalingigwa (kulia) akizungumza wakati wa droo ya kutafuta washindi wa kampeni ya Kopa Tukubusti yenye lengo la kuwafaidisha wateja wao. Kushoto ni Afisa Msimamizi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Pendo Mfuru.


Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw. Asupya Nalingigwa (kulia) akisisitiza jambo wakati wa droo ya kampeni ya Kopa Tukubusti. Kushoto ni Afisa Msimamizi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Pendo Mfuru. Madhumuni ya kampeni Kopa Tukubusti ni  kuwafaidisha wateja wa benki hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha  Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw Asupya Nalingigwa (kulia) akimsikiliza kwa njia ya simu mmoja wa washindi wa kampeni ya Kopa Tukubusti yenye lengo la kuwafaidisha wateja wao. Kushoto ni Afisa Msimamizi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Pendo Mfuru. Madhumuni ya kampeni Kopa Tukubusti ni  kuwafaidisha wateja wa benki hiyo.

DC TANGA AZINDUA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO AIPONGEZA TAASISI YA ANSAAR MUSLIM KWA KUJITOA KWA JAMII

October 30, 2023
Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji akisalimiana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre Shekh Salim Baarahiyani  JANA wakati alipokwenda kuzindua zoezi la uchangiaji damu salama  lililoratibiwa na Taasisi hiyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo  kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Athumani Kihara,ambapo vijana wa taasisi hiyo 600 wanatarajiwa kushiriki kwenye zoezi hilo kulia ni Mwenyekiti wa Idara ya Ustawi wa Jamii katika Taasisi ya Ansaar 
MKUU wa wilaya ya Tanga James Kaji akizungumza wakati wa uzinduzi huo kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo na kulia ni Matroni wa Hospitali hiyo Beatrice Rimoy
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo Dkt Athumani Kihara akizungumza wakati wa halfa hiyo



Zoezi la Uchangiaji damu likiendelea 
Zoezi la Uchangiaji damu likiendelea
Sehemu ya vijana kutoka Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Center wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji ambaye hayupo pichani
MKUU wa wilaya ya Tanga James Kaji akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Cantre mara baadaa ya kuzindua zoezi la uchangiaji damu mapema leo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo
MKUU wa wilaya ya Tanga James Kaji akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Cantre mara baadaa ya kuzindua zoezi la uchangiaji damu mapema leo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo
MKUU wa wilaya ya Tanga James Kaji katikati akiagana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre Shekh Salim Baarahiyan mara baadaa ya kuzindua zoezi la uchangiaji damu lililoendeshwa na Taasisi hiyo kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Athumani Kihara




Na Oscar Assenga, TANGA.

Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji leo amezindua zoezi la uchangiaji watu wanaochangia damu kwa wahitaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo.

Zoezi hilo lililokuwa limeratibiwa na Taasisi ya Ansaar Muslm Youth Centre kupitia Idara yake ya Ustawi wa Jamii Makao Makuu amba wameshirikiana na kituo cha Mahad Imam Shafii Tanga ambapo zaidi ya vijana 600 wanatarajiwa kuchangia damu.

Akizungumza mara baada ya kulizindua zoezi hilo, Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba kitengo cha taasisi hiyo kutoa damu wamefanya jambo kubwa la dhawabu kuliko kitu chochote.

Alisema kwamba kwani wanapofanya hivyo wanawezesha kuwasaidia watu wengine wenye uhitaji ambao wanakumbana na matatizo mbalimbali ya kiafya yanayowahitaji kuongezewa damu.

“Niwapongeze sana na niwaambie kwamba jambo mnalolofanya hapa ni kubwa mnoo kutokana na kwamba unasaidia jamii yenye uhitaji”Alisema

Aidha alisema kwamba ni watu wachache ambao wanaweza kubuni jambo hilo hivyo niendelea kuiasa jamii kuwa na mwamko wa kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuwa sehemu ya kusaidia wenye uhitaji.

“Niwapongeze kwa kuona umuhimu wa kuchangia damu nyie mmekuwa kuokoa maisha ya watu wengine kwani wakati mwengine wanapoteza maisha wengine hata ndugu zao wanaogopa kuwatolea damu lakini nyie mmejitoa hii ni sadaka kubwa asanteni sana”Alisema

Hata hivyo Mkuu huyo wa wilaya aliwaomba waandishi wa habari kuendelea kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa jamii.

Awali akizungumza Mkurugenzi wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Center Shekh Salim Baarahiyan alisema taasisi hiyo kwa niaba ya vijana wao wameamua kujitokea damu kwa ajili ya wagonjwa.

Alisema huo ni utaratibu wao ambao wamekuwa wakiufanya mara kwa mara kusaidia jamii yenye uhitaji kwa kuhakikisha wanachangia damu katika maeneo mbalimbali.

Aidha alisema uanzishwaji wa taasisi hiyo malego yake ni kuelimisha jamii, kuhudumia jamii pamoja na kwamba ni taasisi ya kidini lakini wanatoa mafunzo hazimu ya mtume wao.

Alisema katika mafunzo hayo sio kwamba dini ni ibada tu bali ni huduma kwa jamii na yamekuja mafunzo mengi sana kuhusu umuhimu wa kuwasaidia wanyonge wa aina zote,masikini,walemavu.

“Lakini pia tunasaidia watu wenye mahitaji maalumu, waliopata matatizo ya kiafya wa aina zote za unyonge na sisi ndio mafunzo tunayopewa na mtume kuhudumia jamii na katika jumla ya kuhudumia jamii ni kuchunga afya za watu kwa sababu ibada haziwezi kufanyika kama watu ni wagonjwa”Alisema

Hata hivyo alisema pampoja na kwamba wao wamebobea katika masuala ya kielimu lakini huduma za jamii upande wa afya wameziona ni muhimu sana na walishawahi kufanya kambi mbalilmbali za kuwahudumia watu hasa wa macho kwa kutumia wataalamu wa ndani.

Pia alisema wao wamekuwa mstari wa mbele kuifikia jamii kwenye zoezi la kujitokea damu na litakuwa ni endelevu kwenye mkoa wa Tanga na nje ya mkoa huo.


Naye kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt Athumani Kihara aliwashukuru Taasisi ya ya Ansaar Muslim Youth Center kwa jambo ambalo wamelifanya kwa kujitolea huduma ya damu kwa wahitaji.

Dkt Kihara ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya wakina mama na Uzazi alisema kwamba jambo wanalo lifanya ni muhimu sana kwa jamii kutokana na kwamba katika idara ambazo zinaathirika sana suala la damu ni la uzazi.

Alisema wamekuwa wakipata matatizo mengine ya wakina mama wamekuwa wakipata kutokana na upungufu wa damu kipindi cha ujauzito, kujifungua na baada ya kujifungua matatizo mengi yakiwemo moyo na figo .

Hata hivyo Mkuu wa Idara ya Maabara Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo Sinde Mtobu alisema mwaka huu hamasa imeendelea kuwa kubwa kwa mwezi sasa wastani wanapata chupa 600 kwa mwezi.

Alisema hali hiyo imepunguza gepu la wahitaji ingawa bado wapo wahitaji wapo hivyo niwapongeze sana na wanawaomba waendelee kuwa pamoja nasi.


Hata hivyo alisema ikiwa kwenye Taasisi kila jamii yenye watu ikiwa na tukio la kuchangia damu mara moja tu kwa mwaka hakika changamoto ya damu itakuwa imekwisha hivyo wataendelea kushirikiana.

Mwisho.