FAMILIA YA MFANO KUOKOA WATOTO WANAOFANYIWA UKATILI

FAMILIA YA MFANO KUOKOA WATOTO WANAOFANYIWA UKATILI

July 18, 2016
PRETTY binti mdogo mwenye umri wa kama mwaka mmoja na nusu unapomzungumzisha, kama watoto wengine wenye afya na uhakika wa malezi anatabasamu na kucheka.

Binti huyu mdogo ambaye analelewa na familia iliyomuasili kwa malezi (hajaasiliwa kisheria) ni miongoni mwa watoto kadhaa nchini ambao wanafaidika na mpango mpya wa kusaidia watoto waliokumbwa na ukatili na unyanyasaji.

Pretty (ambaye si jina lake la ukweli-nimempa jina hilo kulinda haki yake) maisha yake mpaka sasa ni kama kitendawili kibaya ambacho ni Mungu tu alitaka kukifumbua.

Nasema ni Mungu tu kwa kuwa Pretty aliokolewa kutoka katika shimo la choo alilotumbukizwa akiwa ndani ya mfuko wa rambo uliofungwa vyema.

Sajini taji (Staff Sergeant) Pundensiana Baitu wa Dawati la jinsia wilaya ya Kipolisi Mbalizi, anasema kwamba Pretty wakati alipoopolewa katika choo cha mtu binafsi alikuwa na hali mbaya sana kiafya na juhudi kubwa sana ilifanywa na hospitali ya Meta kumrejeshea afya yake.

Akisimulia tukio hilo la kuhudhunisha alisema kwamba usiku wa Machi Mosi, mwaka jana alipokea simu iliyomtafadhalisha msaada ili kuokoa maisha ya mtoto aliyetupwa katika choo kinachotumika, katika eneo la Mlimareli huko Mbalizi.
Sajini taji Pundensiana Baitu wa Dawati la jinsia wilaya ya Kipolisi Mbalizi akizungumza na mwandishi wahabari wa Modewjiblog (hayupo pichani) hivi karibuni.(Imeandaliwa na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Alisema wakati anajaribu kuwasiliana na askari kwenda kuona kama wanahitaji msaada wa Kikosi cha zimamoto, akapokea simu nyingine kwamba wananchi wamebomoa choo hicho na kumtoa mtoto huyo ambaye alikuwa amefungwa katika mfuko wa rambo na kwamba alishaanza kuliwa na wadudu wa chooni.

Aidha aliambiwa katika simu kwamba mtoto huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa wiki moja alikuwa bado anapumua hali iliyomfanya aelekeze polisi kuitengeneza PF 3 haraka na kumpeleka mtoto huyo katika hospitali ya Ifisu ambao nao kutokana na kukosa vifaa vya watoto wa aina yake katika hali ile, walimkimbiza hospitali ya Meta.

Anasema yeye alifika asubuhi kuona hali ya mtoto huyo akiambatana na Ofisa Ustawi wa Jamii na hakupendezwa na hali aliyomkuta nayo mtoto.

Anasema kwamba juhudi za upelelezi kujua mama wa mtoto huyo hazikufanikiwa kwani mtoto alitupwa katika choo binafsi karibu na klabu ya pombe. Hata hivyo anasema baada ya kushindwa waliwaambia wananchi wa eneo hilo kumtazama mtu ambaye wanamtilia shaka na kumfikisha kwao kwa mahojiano.

Mpaka wakati wa kuandika makala haya mtu huyo hajapatikana.

Anasema kutokana na mfumo mpya wa familia ya mfano baada ya wao kama polisi kukamilisha kazi ya usalama na kumkabidhi mtoto huyo kwa Ofisa Ustawi wa Jamii, ofisa huyo alimtafuta mtu ambaye yuko tayari kulea mtoto na kumkakabidhi kwao.

Sajini taji huyo anasema kuwa kuna ongezeko la vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto na kwamba jamii inatakiwa kubadilika na kukubali wajibu wake katika kuhakikisha usalama wa mtoto.
Afisa Ustawi wa Jamii Hospitali ya Kanda ya Nyanda za juu Kusini, Gerald Mwaulesi akielezea tukio la mtoto Pretty mbele ya kamera ya Modewjiblog jijini Mbeya hivi karibuni.

Anasema kabla ya kuanzishwa kwa wilaya mpya wakati bado iko Mbeya amekuwa akishuhudia vurugu nyingi kuhusu ukatili kwa watoto na kwamba dawati lake inachofanya ni kutoa ushauri hasa kwa wadada ambao wanatoa mimba na wengine kutupa watoto wanapopatikana.

Alisema ingawa kuna taratibu ndefu za sheria, mfumo mpya uliokubaliwa na serikali wa kupata familia ya mfano ni mfumo bora wenye kuhakikisha malezi mema na kizazi bora kijacho.

Pretty ambaye kwa sasa anaishi na familia ya mfano yenye watoto sita na yeye akiwa wa saba katika kijiji cha Muvwa kilichopo kata ya Mshewe wilayani Mbalizi ana uhakika na malezi kutokana na mfumo huo mpya.

Na Si ajabu akikua hakuna mtu hata yeye mwenyewe atakayejua kwamba aliokolewa kutoka kwenye shimo la choo alikotupwa na mama katili wiki moja baada ya kuzaliwa kwake na kusaidiwa malezi yake na mfumo wa familia ya mfano.
Dk Sipora Harison Kisanga wa UNICEF kanda ya Iringa akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari wa Modewjiblog (hayupo pichani)

Dk Sipora Harison Kisanga ambaye anafanyakazi na UNICEF kanda ya Iringa anasema kwamba ulinzi na usalama wa mtoto ni eda ya wananchi wote kwa ujumla, lakini kutokana na dosari zilizopo ndio maana UNICEF na Tanzania zimetia saini makubaliano yanayowezesha maandalizi ya watu wa kuwapokea watoto waliotelekezwa na wale wenye mazingira magumu ili nao waweze kuwa sehemu ya familia zilizobora.

Anasema kuufanya mfumo huo uwe na utekelezaji uliobora waliendesha mafunzo na kutambua watu wanaoweza kukaa na mtoto, na baada ya kuwakagua wapo katika orodha wakisubiri mtoto yeyote atakayepatikana.

Anasema kutokana na maandalizi hayo ndio maana hata walipompata mtoto Pretty walijua kwamba watampelaka Muvwa kwa familia ambayo iko tayari kupokea mtoto wa aina yoyote na wa umri wowote.

Anasema ni lengo la UNICEF kuhakikisha kwamba haki za watoto zinatekelezwa ikiwamo ya ulinzi na usalama dhidi ya vitu na watu wabaya, huduma za afya, huduma za elimu, haki ya kucheza na haki ya kufundishwa yaliyo mema kutoka kwa wakubwa wao.
Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Mbeya, Lilian Kilongumtwa akielezea tukio la mtoto Pretty aliyetupwa kwenye shimo la choo jijini Mbeya kwa mwandishi wa habari wa mtandao wa Modewjiblog.

Anasema Ofisa huyo wa UNICEF kwamba Mradi wa familia ya mfano ulianzia Temeke na sasa upo Mbeya, Mbarali, na Mbalizi kwa lengo lile lile kuwawezesha watoto hawa kuwa na familia na kuwa salama kuliko kuwapeleka katika vituo vya kulelea yatima.

Mama anayemtunza mtoto huyo pamoja na mumewe, Mama Christer Eliston Mwashusa anasema amefurahi sana kupata mtoto huyo kwani alikuwa tayari kumsaidia kutokana na hofu ya Mungu aliyonayo.

Anasema yeye angelifurahi kama mtoto angemuasili kisheria kwani hali ya sasa ya ulezi pekee anaiona kama haimpi nafasi ya kufanyakazi yake vyema ya kumtunza. Anataka awe mali yake moja kwa moja.

Anasema amepata changamoto nyingi tangu alipomkuta mtoto Pretty hospitali ya Meta, changamoto ambazo zilimuumiza kwanza kama mzazi kwa kutambua kwamba mtoto yule hana wazazi na pia kwa kutambua kwamba ametelekezwa kikatili.
Familia Bw. Juma Mbuza (48) na Bi. Christer Mwashusha (43) inayomlea mtoto Pretty wakifurahi jambo na binti yao baada ya mahojiano na mwandishi wa habari wa Modewjiblog (hayupo pichani).

Pia changamoto ambayo alikumbana nayo ni kule kutambua kwamba mtoto yule kwa sababu ya kuwekwa chooni alikuwa na dhiki kubwa ya afya na hivyo kumfanya kuwa dhaifu.

Anasema hata wakati alipoanza kumtunza changamoto za afya yake zilikuwa kubwa na hasa alipoambiwa kwamba ana ugonjwa ambao ameurithi kwa mama yake, ugonjwa ambao ni upungufu wa kinga na kuanza kumlisha dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI kuanzia alipokuwa na miezi miwili hadi minne.

Hata hivyo katika mahojiano na Ofisa Ustawi wa Jamii kutoka hospitali ya kanda ya rufaa Mbeya (Meta) aliyempokea mtoto huyo Gerald Godfrey Mwambesi alisema kwamba Pretty hakuwa na virusi tangu awali walipompima na kusema kwamba hata vipimo vya hospitali nyingine vilivyosema kwamba ana virusi havikuwa sahihi.

Anasema Pretty alipoteza nguvu ya kinga ya mwili kutokana na kukaa chooni kwa muda na hivyo siku zilivyozidi ndivyo alivyokuwa akiongeza kinga.

Anasema baada ya siku tatu ya kukabiliana na vidonda vyake vilivyotokana na kutafunwa na wadudu chooni na baada ya wiki tatu alionekana kuwa nafuu sana na ingawa mlezi alipata changamoto kiukweli mtoto huyo hakuwa na virusi zaidi ya kupoteza kinga za kawaida ambazo zilitakiwa kurudishwa taratibu.
Dada na kaka wa kufikia mtoto Pretty wakifurahi na mdogo wao mara baada ya kutoka shule.

Anasema mtaalamu huyo kwamba waliongea na wataalamu wa watoto kuhusiana na shida hiyo ya hospitali Mbalizi kumuona mtoto na virusi wakati wao walimpima mara mbili bila kuviona na kusema kwamba hali hiyo inatokana na maambukizi yaliyosababishwa na kutupwa ndani ya choo ambayo yalihitaji tiba ya muda mrefu.

Mlezi anasema kwamba baada ya miezi miwili ya kukaa na mtoto huyo kwa uzuri aliona afya yake inadorora kiasi cha kuhitaji msaada wa tiba na kuanza kwenda hospitali kupata msaada.

Anasema hospitali aliyoenda ilisema mtoto ana maambukizi kutoka kwa mama na kushauri tiba hivyo alipelekwa katika kiliniki ya Beira ambako walimpima na kumwanzishia dozi waliyokuja kuikatisha baada ya kumpima tena kutokana na ufuatiliaji wa hospitali ya Meta na kugundua kwamba hana tatizo la maambukizi ya UKIMWI.

Mlezi wa mtoto huyo alishukuru sana watendaji wa taasisi ya Kihumbe ambao walimsaidia fedha za nauli kwenda katika hospitali kutetea afya ya Pretty na kwamba baada ya matumizi ya dawa na dawa lishe mtoto huyo mwezi uliopita (Juni 16,2016) aliambiwa kwamba mtoto wake hana maambukizi tena.

KIHUMBE, ni taasisi inayofundisha wawezeshaji namna ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hasa familia zao ili waweze kujimudu wenyewe na kuondokana na matatizo hayo.

Baba mlezi katika familia hiyo yenye watu saba akiwamo Pretty, Juma Mbuza amesifu juhudi za mke wake katika kuhakikisha kwamba Pretty anapata mapenzi yote ya kimama na kuendelea kustawi akiwa katika familia hiyo.

Anasema familia yake inawiwa.kulea mtoto huyo kwa kuwa ndiyo ilikuwa nia yao tangu awali na kwamba awali walitaka kuwachukua watoto waliotelekezwa katika kijiji jirani kwenye tarafa yao. Kuendelea kusoma makala hii bofya hapa
-- Zainul A. Mzige, Operation Manager, MO BLOG, www.modewjiblog.com +255714940992.

WANAWAKE WAFUGA NYUKI KUOKOA MISITU YA PUGU NA KAZIMZUMBWI

July 18, 2016
Maofisa wa taasisi ya Mfuko wa Wanawake wa Afrika (WAF) Anna Salado na Alicia (kushoto) wakipata maelezo ya fugaji nyuki katika msitu wa hifadhi wa Pugu.

WANAWAKE wanaofuga nyuki wataokoa hekta 7,270 za misitu ya hifadhi ya Pugu na Kazimzumbwi, imefahamika.
Misitu hiyo, ambayo ni miongoni mwa Misitu ya Hifadhi 486 iliyopo nchini, imekuwa hatarini kutoweka kutokana na shughuli za kijamii hususan uvamizi wa mipaka na ukataji wa miti kwa ajili ya uchomaji mkaa ambao kwa muda mrefu umekuwa ukifanywa na wananchi mbalimbali.
Meneja wa Misitu hiyo kutoka Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Mathew Mwanuo, anasema kwamba, misitu hiyo iliyopo katika wilaya za Ilala mkoani Dar es Salaam na Kisarawe mkoani Pwani, imekuwa hatarini kutoweka licha ya jitihada za serikali za kukabiliana na wavamizi hao.
MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MAJI

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MAJI

July 18, 2016

ncc1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano Mkuu wa 10 wa  African Ministers Council on Water   (AMCOW) knew Kituo cha Mimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ncc2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Rais Mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki kuingia kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  jijini Dar es salaam kufungua    Mkutano Mkuu wa 10 wa  African Ministers Council on Water   (AMCOW)  Julai 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ncc3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Rais Mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki kuingia kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  jijini Dar es salaam kufungua    Mkutano Mkuu wa 10 wa  African Ministers Council on Water   (AMCOW)  Julai 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ncc4 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais Mstaafu wa Kenya Mwai   Kibaki kabla ya kufungua  Mkutano Mkuu wa 10 wa  African Ministers Council on Water   (AMCOW) kwenye  Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ncc5 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana  na Rais Mstaafu wa Kenya Mwai   Kibaki  katika   Mkutano Mkuu wa 10 wa  African Ministers Council on Water   (AMCOW) kwenye  Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
MAKAMISHNA WA POLISI WALA KIAPO CHA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA IKULU LEO

MAKAMISHNA WA POLISI WALA KIAPO CHA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA IKULU LEO

July 18, 2016

1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk. John Pombe Magufuli akizungumza Ikulu mara baada ya Makamishna Wasaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) waliopandishwa vyeo  kula kiapo cha maadili ya Utumishi wa Umma Ikulu leo, Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Lameck Nchemba na Naibu Waziri Injini Hamad  Masauni.(PICHA NA JOHN BUKUKU WA FULLSHANGWE-IKULU)
2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk. John Pombe Magufuli akifafanua mambo mbalimbali mara baada ya makamishna hao kula kiapo cha Maadili katika utumishi wa Umma Ikulu leo.
3 4Makamishna Wasaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) waliopandishwa vyeo wakiapa mbele ya Rais Dk. John Pombe Magufuli na viongozi mbalimbali wa serikali Ikulu leo.
5 6Makamishna Wasaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) waliopandishwa vyeo wakiapa mbele ya Rais Dk. John Pombe Magufuli na viongozi mbalimbali wa serikali Ikulu leo.
7 8Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya Kamishna wa Sekretariati ya Maadili ya Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda.
9Baadhi ya Makamishna wa jeshi la Polisi nchini na viongozi wa vitengo mbalimbali Makamo Makuu ya Jeshi la Polisi wakifuatilia kiapo hicho.
10Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kulia Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu na Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa Bw. Othman Rashid wakiperuzi mtandao  huku wakifurahia jambo wakati wa hafla ya kuwaapisha Makamishna Wasaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) Ikulu leo
12Katibu Mkuu Kiongozi Injinia Balozi John Kijazi akisamiana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika hafla hiyo.
13Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati Kamishna wa Sekretariati ya Maadili ya Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda. akiwaongoza Makamishna Wasaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) Ikulu leo wakati alipokuwa wakila kiapo kulia ni Mh. Angela Kairuki Waziri Katika Ofisi ya Rais Utumishi wa tatu kutoka kulia ni Mh. Mwigulu Nchemba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na wa nne ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni
14Makamishna Wasaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) wakitia saini mara baada ya kula kiapo cha Maadili ya Utumishi wa Umma Ikulu leo
15 16Baadhi ya Viongozi Mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo
18Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na baadhi ya Makamishna Wasaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) Ikulu leo 
19Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Pamoja na Makamishna wa Jeshi la Polisi
20Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Kamishna wa Sekretariati ya Maadili ya Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda mara baada ya kiapo hicho kukamilika kulia ni Waziri Ofisi ya Rais Utumishi Mh. Angela Kairuki na katikati ni nyuma ni Balozi John Kijazi Katibu Mkuu Kiongozi.
21Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk. John Pombe Magufuli akitoa huduma ya kugawa vitafunwa kwa wageni wake mara baada ya hafla hiyo kumalizika
22Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk. John Pombe Magufuli akitoa huduma ya Vitafunwa kwa Kamishna wa Magereza Bw. John Casmir Minja mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo leo.
23Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk. John Pombe Magufuli akitoa huduma ya Vitafunwa kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai,(CP) Diwani Athuman mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo leo.
MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII.

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII.

July 18, 2016

mali1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Wazara ya Maliasili na Utalii   kwenye  Kituo cha  Kimataifa cha Mikutano cha LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam Julai 18, 2016 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mali2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Wazara ya Maliasili na Utalii   kwenye  Kituo cha  Kimataifa cha Mikutano cha LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam Julai 18, 2016 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mali3 
Baadhi ya Watumishi wa Wizar ya Maliasili na Utalii wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza nao kwenye  Kituo cha  Kimataifa cha Mikutano cha LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam Julai 18, 2016 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mali4 mali5 
Baadhi ya Watumishi wa Wizar ya Maliasili na Utalii wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza nao kwenye  Kituo cha  Kimataifa cha Mikutano cha LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam Julai 18, 2016 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BIHARAMULO WAANZA MAFUNZO YA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA PS3 MKOANI KAGERA

July 18, 2016

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Deusdedith Kinawiro akifuyngua mafunzo ya siku nne ya Madiwani kutoka Hlamashauri mbii za Kyerwa na Biharamuo juu ya namna ya utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za umma (PS3) chini ya ufadhili wa Serikali ya Marekali kupitia shirika ake la misaada la Kimataifa (USAID) ikishirikiana na serikali kuu.
Mradi huo ulizinduliwa Julai 12 mwaka huu ambapo Halmashauri hizo mbii ndio zitatekeeza mradi huo mkoani Kagera kwa awamu ya kwanza.
Kinawiro alisema anatarajio kuona mafunzo haya elekezi yanatumika kama ilivyokusudiwa, na waheshimiwa madiwani wanapata uelewa na maarifa kuhusu uendeshaji wa Serikali za Mitaa, pamoja na wajibu na majukumu yao katika kusimamia uendeshaji wa Mamlaka hizi
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali (Mstaafu), Shabaan Lissu akiwa na Mkuu wa Wiaya ya Biharamulo, Saada Malunde wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya madiwani yaliyofanyika mjini Bukoba leo.
 Mwenyekiti wa Hlamashauri ya Kyerwa, Kashunju Runyogote (kushoto) akiwa na madiwani wenzake wa Kyerwa wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.
 Baadhi ya Madiwani na Watendaji wa Hamashauri za Kyerwa na Biharamuo mkoani Kagera wakifuatilia ufunguzi huo.
Kiongozi wa timu ya Uzinduzi ya PS3 Mkoani Kagera na Mtaalam wa Fedha wa Mradi huo wa PS3, Abdul Kitula akizungumza juu ya mafunzi hayo kwa madiwani.
Kitua aliwataka watendaji hao kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo ambayo ndio utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za  Umma ambao nchini unatekelezwa katika mikoa 13 na kuzinufaisha Halamashauri 93. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

SERIKALI YATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU BENKI YA TWIGA BANCORP

July 18, 2016

 Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu msimamo wa Serikali kuhusu Benki ya Twiga Bancorp. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Cosmas Kimario na Mkurugenzi  Rasilimali Watu na Utawala, Amina Lumuli.
 Maofisa wa Benki hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Mpiga picha za magazeti Loveness Benard akiwa kazini ‘ hapana kuchezea kazi hapa kazi tu’
……………………………………………………………………
 
MSAJILI wa Hazina Ndugu Lawrence Mafuru ametolea ufafanuzi taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari kuhusu msimamo wa Serikali kwa Benki ya Twigabancorp.
 
Taarifa hiyo ilieleweka vibaya kuhusu msimamo wa Serikali kwa benki hii ya Twiga Bancorp. Naomba nieleze kwamba kwa hivi sasa Serikali inasubiri mapendekezo ya kitaalamu yatakayowezesha kutatua changamoto za kimtaji za Twiga Bancorp. 
 
Ninaposema changamoto za kimtaji sijasema kwamba benki hiyi ipo kwenye hali mbaya ya kushindwa kujiendesha, ila inahitaji nyongeza ya mtaji kwa ajili ya kutekeleza matakwa ya kisheria na vilevile kuimarisha na kusambaza huduma mbalimbali katika maeneo ya nchi. Hatua hizo zinafuatia agizo la Mheshimiwa Rais kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipangokufuatilia utendaji wa benki ya Twiga Bancorp na kuhakikisha kasoro zilizopo zinatatuliwa.
 
“Kuna njia mbalilimbali za kuiwezesha benki kupata mtaji ikiwemo nje ya utaratibu wa Serikali, ndiyo maanaWizara na Ofisi ya Msajili wa Hazina ikishirikiana na Manejiment ya Twiga Bancorp zinaandaa mapendekezo yatakayoiwezesha Benki hii kupata mtaji ili kuiwezeshakutimiza malengo yake ya kiukuaji na kujiendesha kwa faida.”
 
Hatua mbalimbali zilianza kuchukuliwa na Wizara ya Fedhana Mipango na ofisi ya Msajili wa Hazina kwa ajili ya kuboresha utendaji wa Benki ya Twiga Bancorp. Kwa mfano, mnamo mwaka 2015, Muundo wa Shirika ulibadilishwa ambao pamoja na mambo mengine ulipelekea kuteuliwa kwa Menejimenti mpya, kwa kupitia Menejimenti hiyo mpya  umetengenezwa Mpango Mkakati wa miaka mitano ambao umeanza kutumika Januari 2016, serikali pia ilifanya mabadiliko katika bodi ya wakurugenzi kwa kuteuaBodi mpya ya Wakurugenzi. 
 
Kwa ujumla kuna mabadiliko makubwa ya kiutendaji baada ya hatua hizo kuchukuliwa. Kwa mfano benki imeweza kupata Hati Safi ya Mahesabu (Unqualified Opinion) kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Heasabu za Serikali kwa mara ya kwanza kwenye hesabu zake za mwaka 2015 jambo ambalo halikuwezekana toka Mwaka 2011. 
 
“Hizi taarifa zinazosambaa kuwa benki inafungwa sio za kweli. Kwenye benki kuna pesa za wananchi, kuna mikopo iliyotolewa kwa watu mbalimbali, kuna rasilimali za benki ikiwemo rasilimmali watu. Yote hayo yana Utaratibu wake wa kuyasimamia.. Hata ukisikiliza hotuba ya Rais hakusema funga benki ya Twiga Bancorp aliagiza hatua zichukuliwe na kwamba Katibu Mkuu asimamie.” 
 
Hivyo tuna wahakikishia kuwa fedha za wananchi zilizo katika benki ya Twiga Bancorp zipo salama na kwamba uongozi uliopo hivi sasa unaendelea kushughulikia changamoto za kiutendaji zilizokuwepo na kama yalivyokuwa maagizo ya Rais hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa kwa ajili ya kuhakikisha mambo yote yanakuwa sawa. Pia benki hii inaendelea kutoa huduma zake kwa wateja kama kawaida.”
 
Mwisho, Serikali itaendelea kutoa msukumo kwa benki hiiili kuhakikisha tatizo lililopo sasa la mtaji linatatuliwa na kuhakikisha inajiendesha kwa faida. 
 
MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AKISHIRIKI MKUTANO WA AU KIGALI RWANDA

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AKISHIRIKI MKUTANO WA AU KIGALI RWANDA

July 18, 2016

mak1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifuatilia kwa makini ufunguzi wa mkutano wa 27 kwa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi  Wanachama wa Umoja wa Afrika AU ulioanza jana katika Ukumbu wa KCC mjini Kigali Rwanda. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na OMR)

WAZIRI MBARAWA AITAKA TPA KUJENGA GATI

July 18, 2016

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemuagiza  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kuanza ujenzi wa maegesho ya meli katika bandari ambazo meli mbili mpya zinazojengwa na Mamlaka hiyo katika bandari ya Itungi Wilayani Kyela, zitatoa huduma ya usafiri baada ya kukamilika.


Waziri Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo alipokagua bandari ya Mbambabay iliyopo Wilayani Nyasa ambayo ni miongoni mwa bandari ambazo meli hizo zitatoa huduma na kubaini kuwa bado bandari hiyo haina maegesho kwa ajili ya meli hizo.

"Nataka kuona maegesho ya meli yanakamilika haraka ili kuwezesha meli mpya kupakua na kupakia mizigo katika bandari hii", amesema Waziri Prof Mbarawa.

Ameeleza kuwa meli hizo mbili za mizigo ambazo zinatarajiwa kukamilika mwezi Agosti na Oktoba zitaongeza kasi ya utoaji wa huduma katika bandari hiyo na kuwa chachu ya maendeleo hususan katika shughuli za biashara na kiuchumi katika mkoa wa Ruvuma na nchi jirani.

Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amemtaka Meneja wa Bandari ya Kyela kuisimamia kampuni ya M/s Songoro Marine Transport Boart Yard inayojenga meli hizo ili zijengwe kwa ubora na viwango vinavyotakiwa kulingana na thamani ya fedha ambazo zinatokana na kodi za wananchi.

Katika Hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua barabara ya Mbinga- Mbambabay yenye urefu wa Km 66 ambayo Serikali iko katika hatua ya kumtafuta mkandarasi atakayejenga kwa kiwango cha lami.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutaimarisha huduma ya bandari ya Mbambabay na kupunguza adha ya usafiri kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa Ruvuma Eng. Lazeck Alinanuswe amesema kuwa kwa sasa wakala unakamilisha zoezi la kulipa fidia kwa wananchi waliopo katika hifadhi ya barabara wakati hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa zinakamilishwa.

Naye Meneja wa Bandari ya Kyela Percival Salama amemueleza Waziri kuwa pamoja na changamoto ya kukosa wa chombo cha usafiri majini kinachotoa huduma katika bandari hiyo pia ameomba kuboresha huduma za miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami ili kuwezesha ufanisi wa bandari.

"Kuimarika kwa barabara ya  mbinga-mbambabay na barabara nyingine za maingiliano katika bandari hii  kutaongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuongeza fursa za uwekezaji na biashara na Mkoa na nchi jirani", Waziri Prof. akame Mbarawa, yuko katika ziara ya Kikazi Mkoani Ruvuma kukagua miradi ya Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Meneja wa Bandari ya Kyela, Percival Salama (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) ya namna shughuli za biashara ya makaa ya Mawe zinavyoweza kuongeza pato kwa bandari ya Bambabay Mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia) akisalimiana na baadhi ya Madereva wa Malori wanaosafirisha makaa ya mawe Mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, Mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akiongea jambo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Mahenge (wa pili kushoto) wakati alipokagua uwanja wa Songea Mkoani Ruvuma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akiongea jambo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Mahenge (wa pili kushoto) wakati alipokagua uwanja wa Songea Mkoani Ruvuma.
Muonekano wa uwanja wa ndege wa Songea Mkoa ni Ruvuma, ambao uko kwenye mradi wa upanuzi wa viwanja kumi na moja.
Waziri wa Ujenzi, Uchuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tano kushoto) akitoa maelekezo kwa Meneja wa kiwanja cha ndege cha Songea, Valentine Fasha (wan ne kulia) wakati alipokagua barabara ya kutua na kuruka ndege katika uwanja huo Mkoani Ruvuma.
Muonekano wa Barabara ya Mbinga-Mbambabay KM 66 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha Lami unatarajiwa kuanza hivi karibuni. Kukamilika kwa barabara hiyo kutachochea uchumi wa Mkoa wa Ruvuma kupitia bandari ya Mbambabay.