KIUNGO
Samir Nasri ameendeleza wiki nzuri za mafanikio katika soka, baada ya
jioni ya leo kufanya kazi nzuri Manchester City ikicheza mchezo wa
kirafiki na Al Ain katika ziara yake ya Falme za Kiarabu.
Mfaransa
huyo atakwenda na kulala na tabasamu zuri baada ya kutengeneza mabao
mawili katika ushindi wa 3-0 wa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England
kwenye Uwanja wa Hazza bin Zayed.