WANANCHI CHANGAMKIENI SMART 6 MPYA YA VODACOM

October 21, 2015

 Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(kushoto)akiwanesha  waandishi wa habari(hawapo pichani) simu mpya aina ya Smart 6 wakati wa uzinduzi wa simu hiyo yenye kioo kikubwa kinachomuwezesha mtumiaji kusoma na kuangalia taarifa kwa urahisi na ina kamera ya kisasa na uwezo zaidi wa kuperuzi intanet ya 3G,itapatikana kwa bei nafuu kabisa shilingi
90,000/- inapatikana katika maduka yote ya kampuni hiyo.Mteja yeyote atakayenunua simu hiyo atajipatia ofa kabambe kabisa ya kupata 500MB bure na uwezo wa kutuma jumbe fupi za maneno zipatazo 200 kila mwezi kwa kipindi cha miezi 6 bure.Kulia ni Mkuu wa huduma na bidhaa wa kampuni hiyo,Samson Mwongela. 
KATIKA kuhakikisha wateja wake kutokuwa nyuma kiteknolojia na kupata huduma bora za mawasiliano ya kisasa kwa kutumia mtandao wa intanet,kampuni ya Vodacom Tanzania imezindua simu mpya ya Smart 6 ya gharama nafuu ambayo wananchi wengi wanaweza kumudu kuinunua.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa simu hii Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo,Kelvin Twissa amesema kuwa simu hii  imelenga wateja wake wenye vipato vya kawaida ili kuwawezesha kufurahia huduma za kisasa za matumizi ya simu za mkononi za Smartphone ili waweze kwenenda na teknolojia.

“Vodacom siku zote tumekuwa tukiwasikiliza wateja wetu na ndio maana tumeingiza sokoni simu hii ili kuwawezesha kufurahia matumizi ya simu za kisasa za smart ambazo zinawawezesha kupata huduma za internet na program nyinginezo za kurahisisha maisha yao na kuwa murua ikiwemo kupiga picha wazipendazo kwa kutumia simu zao,”Alisema Twissa.

Aliongeza kuwa simu hii ya Smart 6 ambayo itakuwa inauzwa kwa bei nafuu kabisa ya shilingi 90,000/- ina kioo kikubwa kinachomuwezesha mtumiaji kusoma na kuangalia taarifa kwa urahisi,ina kamera ya kisasa,uwezo zaidi wa kuperuzi intanet ya 3G, nafasi kubwa ya kuweka kumbukumbu na inakaa na betri kwa muda mrefu. Hii ni simu ya kipekee ambayo kila mteja anatakiwa kuwa nayo.

Alisema simu hizi zinapatikana katika maduka yote ya Vodacom na katika matamasha yote yanayofanywa na kampuni yetu nchi nzima ya Vodacom tumekufikia.Mteja yeyote atakayenunua simu hii atajipatia ofa kabambe kabisa ya kupata 500MB bure na uwezo wa kutuma jumbe fupi za maneno zipatazo 200 kila mwezi kwa kipindi cha miezi 6 bure.

Aliwataka wateja wa Vodacom na wananchi wengine kwa ujumla kuchangamkia fursa hii na kukamata Smart 6 kwa gharama nafuu ili kuendelea kupata taarifa za huduma mbalimbali zinazopatikana kwa kuperuzi mtandao wa intanet.Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetu www.vodacom.co.tz au kurasa zetu za Facebook na Twitter.
 Mkuu wa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Samson Mwongela(kulia)akimshuhudia Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(kushoto)akiwanesha  waandishi wa habari(hawapo pichani) simu mpya aina ya Smart 6 wakati wa uzinduzi wa simu hiyo yenye kioo kikubwa kinachomuwezesha mtumiaji kusoma na kuangalia taarifa kwa urahisi na yenye kamera ya kisasa na uwezo zaidi wa kuperuzi intanet ya 3G, itapatikana kwa bei nafuu kabisa shilingi 90,000/- inapatikana katika maduka yote ya kampuni hiyo.Mteja yeyote atakayenunua simu hiyo atajipatia ofa kabambe kabisa ya kupata 500MB bure na uwezo wa kutuma jumbe fupi za maneno zipatazo 200 kila mwezi kwa kipindi cha miezi 6 bure.
 Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(kushoto) pamoja na Mkuu wa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Samson Mwongela,wakijipiga selfiii kwa kutumia simu mpya aina ya Smart 6 waliyoizindua leo yenye kioo kikubwa kinachomuwezesha mtumiaji kusoma na kuangalia taarifa kwa urahisi na yenye kamera ya kisasa na uwezo zaidi wa kuperuzi intanet ya 3G, itapatikana kwa bei nafuu kabisa shilingi 90,000/- katika maduka yote ya kampuni hiyo.Mteja yeyote atakayenunua simu hiyo atajipatia ofa kabambe kabisa ya kupata 500MB bure na uwezo wa kutuma jumbe fupi za maneno zipatazo 200 kila mwezi kwa kipindi cha miezi 6 bure.

MAMA SAMIA AKUTANA NA WANAWAKE WA UWT, WALEMAVU NA WAJASIRIAMALI MKOA WA DAR ES SALAAM KUJUA CHANGAMOTO ZAO

October 21, 2015

 Mgombea Mwenza wa nafasi ya urais kupitia  Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (kushoto), akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Wajasiriamali pamoja na wanachama kutoka Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu (Shivyawata), baada ya kupokea changamoto zao Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo.
 Mwenyekiti wa UWT Taifa, Sophia Simba akizungumza katika mkutano huo.
 Mmoja wa viongozi kutoka Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu (Shivyawata), Nasria Nasri (kushoto), akimueleza Mama Samia changamoto walizonazo.
 Mhasibu wa Kitengo cha Fedha, Magogoni, Charles Temba akizungumza katika mkutano huo kuhusu changamoto mbalimbali ambapo alimuomba mama Samia, watu wenye ulemavu watengewe luzuku.
 Mwakilishi wa Walemavu, Kuruthum Dindili akimueleza Mama Samia changamoto walizonazo.
TAMWA KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA EUROPEAN CENTRE FOR ELECTORAL SUPPORT (ECES) YATOA MAFUNZO KWA WAHARIRI WA VYOMBO MBALI MBALI ZANZIBAR.

TAMWA KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA EUROPEAN CENTRE FOR ELECTORAL SUPPORT (ECES) YATOA MAFUNZO KWA WAHARIRI WA VYOMBO MBALI MBALI ZANZIBAR.

October 21, 2015

1
AFISA WA TAMWA BI SHIFAA SAID AKIWAKARIBISHA WASHIRIKI MBALI MBALI WALIOHUDHURIA MAFUNZO YA UHARIRI KWA AJILI YA KUIMARISHA AMANI YA NCHI YANAYOHUSIANA NA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015 MAFUNZO YALIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA WIZARA YA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO ZANZIBAR.
7
WAHARIRI MBALI MBALI WALIOHUDHURIA KWENYE MKUTANO ULIOANDALIWA NA TAMWA KWA KUSHIRIKIANA NA EUROPEAN CENTRE FOR ELECTORAL SUPPORT (ECES) KATIKA UKUMBI WA WIZARA YA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO ZANZIBAR.
8
AFISA WA TAMWA BI MZURI ISSA AKITOA TATHMINI YA MICHANGO MBALI MBALI KUTOKA KWA WAHARIRI WALIOHUDHURIA KATIKA MKUTANO HUO ULIOFANYIKA UKUMBI WA WIZARA YA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO ZANZIBAR.
2
MKUFUNZI ALI SULTAN KUTOKA ASSOCIATED PRESS AKITOA MADA INAYOHUSU UHARIRI WA HABARI KWA WASHIRIKI KUTOKA VYOMBO MBALI MBALI JUU YA KUTOA HABARI ZA UHAKIKA KATIKA MKUTANO WA WAHARIRI ULIOFANYIKA UKUMBI WA WIZARA YA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO MJINI ZANZIBAR.
3
MKURUGENZI TUME YA UTANGAZAJI ZANZIBAR AMBAE NI MWENYEKITI WA MKUTANO HUO CHANDE OMAR AKIFAFANUA JAMBO KUHUSIANA NA TOFAUTI KATI YA MUHARIRI NA MUANDISHI WA HABARI KWENYE MKUTANO HUO.
4
MKUU WA MRADI WA KUSAIDIA UCHAGUZI SALAMA (ECES) UNAOFADHILIWA NA UMOJA WA ULAYA BI VICTORIA FLORINDER AKITOA SHUKURANI KWA WAHARIRI WALIOHUDHURIA MKUTANO HUO.
5
MUANDISHI MUANDAMIZ SALIM SAID AKICHANGIA MAADA KATIKA MKUTANO WA WAHARIRI ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA WIZARA YA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO ZANZIBAR.
6
MUHARIRI MKUU WA SHIRIKA LA MAGAZETI YA ZANZIBAR LEO RAMADHAN MAKAME AKICHANGIA MADA KWENYE MKUTANO HUO.
9
WASHIRIKI WA SEMINA, WAKUFUNZI NA WAFADHILI WAO KATIKA PICHA YA PAMOJA.
PICHA ZOTE NA ABDALLA OMAR HABARI MAELEZO.
DK. JOHN POMBE MAGUFULI AUNGURUMA JIJINI DAR ES SALAAM

DK. JOHN POMBE MAGUFULI AUNGURUMA JIJINI DAR ES SALAAM

October 21, 2015

????????????????????????????????????
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Jakaya Kikwete akiongozana na Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM wakati alipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J. K, Nyerere Rais Jakaya Kikwete akielekea mkoani Ruvuma na Dk. John Pombe Magufuli akitokea mkoani Mwanza na kufanya mazunguzo mafupi uwanjani hapo kabla ya kuagana.
Dk. John Pombe Magufuli ameendelea na kampeni zake mkoani Dar es salaam ambapo amepokelewa na vyama mbalimbali vya kisiasa kwa kupamba bendera za vyama vyao kufuatia ujio wa mgombea huyo ambaye alikuwa akiendelea na kampeni zake za kuwania Ikulu ya Magogoni mikoani kabla ya kurejea jijini Dar es salaam kuendelea na kampeni hizo ambazo atazifunga rasmi kwenye uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza Oktoba 24 mwaka huu tayari kwa watanzania kumpigia kura za ndiyo.
Mgombea huyo amefanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Kigamboni, Mbagala, Temeke, Ubungo na Kinondoni huku akiwanadi wagombea ubunge na udiwani wa majimbo hayo, Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika jumapili Oktoba 25 mwaka huu.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
????????????????????????????????????
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Jakaya Kikwete akiagana na Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM wakati alipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J. K, Nyerere mara baada ya mazungumza yao.
????????????????????????????????????
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Jakaya Kikwete  na Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM   wakati alipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J. K, Nyerere
????????????????????????????????????
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Jakaya Kikwete  na Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM wakitaniana na mpiga picha wa gazeti la Jambo Leo Bw. Richard Mwaikenda wakati  kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J. K, Nyerere.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akiwahutubia wananchi na kuomba kura za ndiyo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Biafra Kinondoni jijini Dar es salaam
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Biafra Kinondoni jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba akimpigia debe Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Biafra Kinondoni jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akisisitiza jambo katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Sinza katika jimbo la Ubungo jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akiwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Sinza jimbo la Ubungo jijini Dar es salaam leo.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akipokelewa kwa shangwe na mapambo ya bendera za vyama mbalimbali zilizopambwa kuanzia Ubungo mataa mpaka kituo cha mabasi cha ubungu kufuatia ujio wa mgombea huyo jijini Dar es salaam kwa ajili ya mikutano ya kampeni.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akiwanadi wagombea ubunge na udiwani jimbo la Mbagala kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Zakhem Mbagala jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni wa CCM kwenye uwanja wa Zakhem Mbagala.
????????????????????????????????????
Mgombea Udiwani kata ya Kimbangulile Ndugu Said Fella wa kwanza kushoto akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wagombea wenzake.
????????????????????????????????????
Makada wa CCM wakifurahia Kampeni kwenye uwanja wa Biafra.
????????????????????????????????????
Mbagala Zakhem ikiwa imetema.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Machava Kigamboni leo.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akimnadi mgombea ubunge jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akimkabidhi ilani ya uchaguzi na kumnadi mgombea ubunge jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akiwanadi wagombea ubunge jimbo la Kinondoni  Ndugu Idd Azzan na wagombea wa viti maalum kutoka kushoto na Mama Madabida na Mama Janet Masaburi.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akimnadi na kumkabidhi ilani ya uchaguzi mgombea ubunge Kinondoni Ndugu Idd Azzan.
????????????????????????????????????
Kundi la Orijino Komedi likifanya vitu vyake jukwaani kwenye mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Biafra huku Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM na viongozi wengine  wakiangalia.

TFDA NA TAASISI YA TRADEMARK EAST AFRICA (TMEA) WAZINDUA MFUMO WA UTOAJI VIBALI KWA MFUMO WA KIELEKITRONIKI

October 21, 2015

 Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi (kulia), akibonyeza kituvye Dar es Salaam leo asubuhi, kuashiria uzinduzi wa mfumo wa utoaji vibali kwa njia ya kielekitroniki (e-portal) ambao utawezesha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), kuhudumia wateja wake kwa kutumia mtandao wa intaneti. Mpango huo unaendeshwa kwa ushirikiano wa TFDA na Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA)
Viongozi wakiwa meza kuu wakifuatilia uzinduzi huo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo ya uzinduzi.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Viongozi wakiwa tayari kuzungumza na wanahabari. Kutoka kulia ni Meneja wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA), Josephat Kweka,  Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi na Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo.
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo (kushoto), akizungumza na wanahabari.
……………………………………
Na Dotto Mwaibale
MAMLAKA ya Chakula na dawa nchini (TFDA), imezindua mfumo mpya wa utoaji vibali kwa mfumo wa kielektroniki ujulikanao kama ‘e-portal’.
Mfumo huo uliogharimu kiasi cha sh. milioni 300 kwa ushirikiano wa taasisi ya Trademark East Afrika(TMEA) kwa kutoa dola za marekani 250,000 lengo ikiwa ni kuboresha mfumo wa utoaji huduma kwa njia ya mtandao.
Akizungumza Dar es Salaam leo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando, Dk.Mkuu wa Serikali Muhammad Kambi alisema mfumo huo uliozinduliwa umekuja wakati muafaka kwani utasaiduia kuboresha huduma katika sekta ya afya kwa kuongeza uwazi, ukweli na kwa uharaka zaidi.
“Mfumo huu uliozinduliwa leo utarahisisha katika kufanya maamuzi ya kudhibiti katika utoaji wa vibali vya kuingiza bidhaa nchini na kutoa bidhaa nje ya nchi kwa kuwa wa kuandaa vibali utafupishwa na utaongeza faida katika mamlaka hiyo,”alisema.
Alisema mfumo huo utasaidia kuhudumia wateja na katika kusajili na kufuatilia ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za chakula,dawa, vipodozi na vifaa tiba sokoni sanjari na kuongeza kiwango cha wateja katika kuzingatia matakwa ya kisheria.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo alisema mfumo huo mpya unatumiwa na watu takribani 300 ambao wamethibitisha kuwa hauna matatizo yeyote kwani lengo la mamlaka hiyo ni kuhakikisha wanapunguza muda wa wateja wao katika kuomba vibali ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za huduma hiyo.
“TFDA inatambua mchango wa TMEA katika kuendeleza mfumo wa e-portal ambao utarahisha ukusanyaji wa takwimu, uchambuzi na uhifadhi wa taarifa za usajili, uratibu na ufuatiliaji wa taarifa za ubora na usalama wa vyakula dawa, vipodozi, vifaa tiba nchini,”alisema.  
Mkurugenzi wa TradeMark East Afrika Tawi la Tanzania, Dk. Josephat Kweka alisema mfumo huo utasaidia kuweka mazingira mazuri ya kibiashara hasa katika kuingiza na kutoa bidhaa katika soko la ushindani.
“Portal inatarajia kuongeza kasi ya usajili, kupunguza kwa kiasi kikubwa muda wa kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi na muda wa kusafirisha bidhaa nje ya nchi. Tumewawezesha portal hiyo ili kukuza biashara ya kikanda na ushirikiano wa kiuchumi kwa nchi za jumuia za Afrika Mashariki,”alisema.
Aidha uzinduzi huo ni hitimisho la maboresho ya mfumo huo ulioanza mwaka 2011 ambapo utawawezesha wafanya biashara kuomba na kupata vibali vyote muhimu kwa njia ya mtandao bila kulazimika kufika ofisi za mamlaka hiyo.
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AZINDUA NEMBO YA BWANA SUKARI

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AZINDUA NEMBO YA BWANA SUKARI

October 21, 2015

3
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua nembo mpya ya sukari inayotengenezwa na kiwanda cha Kilombero Sugar Company iitwayo Bwana Sukari kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam Oktoba20,  2015.
4
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baada ya viongozi wa Bodi ya Sukari Tanzania na viongozi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero baada ya kuwasili kwenye hoeli ya Serena jijini Dar es salaam Oktoba 20, 2015 kuzindua nembo mpya ya sukari ya kiwanda hicho IITWAYO  Bwana Sukari . Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es slaam, Meck Sadiki.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NHIF kuwekeza Vituo vya mfano Kigoma, Mtwara

NHIF kuwekeza Vituo vya mfano Kigoma, Mtwara

October 21, 2015

1 2
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Michael Mhando (meza kuu katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mikakati ya Mfuko huo ya ujenzi wa Vituo vya mfano vya matibabu.
……………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu. MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unatarajia kuanza ujenzi wa vituo vya matibabu vya mfano katika mikoa ya Mtwara na Kigoma katika mwaka huu wa fedha wa 2015/2016.
Mikakati hiyo imesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusiana na mikakati ya Mfuko katika uboreshaji wa miundombinu ya Matibabu.
“Tunatarajia kuwanza ujenzi wa Kituo cha matibabu cha mfano mkoani Mtwara na hasa kwa kuzingatia kuwa Wizara yetu ya afya pia inao mpango wa kujenga Hospitali mkoani humo. Tunawasiliana na Wizara ili tuunganishe nguvu zetu. Eneo tayari lipo na Mfuko umetenga kiasi cha Tsh bilioni 3 kwa mwaka 2015/16, lakini pia ujenzi Kituo cha Matibabu cha Mfano Mkoani Kigoma ambacho kitatoa huduma kwa wanachama na wananchi wa mkoa huo na mikoa ya jirani,” alisema Bw. Mhando.
Aidha Mfuko umejipanga kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo umeanza kushirikiana na Uongozi wa mkoa ili kuziwezesha hospitali za Amana, Mwananyamala na Temeke kuwa na vifaa vya kisasa zaidi ili kuhudumia wanachama wengi kupitia huduma za matibabu na kliniki maalum zitakazokuwa zinaendeshwa na madaktari bingwa wa hospitali hizo.
“Katika Jiji la Dar es Salaam mfuko utajenga kituo cha madaktari bingwa (Doctors Plaza) katika eneo la Ubungo Maziwa ambako mfuko utaweka pia miundo mbinu kwa ajili ya huduma mbalimbali. Kituo hicho kitawawezesha wanachama na wananchi kupata huduma za kuwaona madaktari bingwa wa fani mbalimbali kwa urahisi na katika eneo moja, hali ambayo itapunguza msongamano wa wagonjwa katika baadhi ya vituo na kuboresha huduma jijini.
Bw. Mhando alisema kuwa mbali na juhudi za uboreshaji wa huduma za afya zilizotajwa hapo juu, Mfuko pia umewekeza katika ujenzi wa Ofisi zake katika Mikoa ya Mbeya, Dodoma na Tabora ambapo majengo hayo yatawezesha upatikanaji wa nafasi kwa huduma za Hospitali za Doctors Plaza ambazo zimekuwa zikihudumia wanachama wengi wa Mfuko.

Mama Mwanamwema Shein Azungumza na Viongozi wa UWT Wilaya ya Mjini Unguja Kumuombea Kura Dk Shein na Dk Magufuli

October 21, 2015

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Mjini Bi Waridi Juma akisoma risala ya Wanawake wa Mkoa wa Mjini wakati wa mkutano na Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, Mama Mwanamwema Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar.
Viongozi wa UWT Mkoa wa Mjini Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati wa mkutano wake na Viongozi hao uliofanyika Afisi ya CCM Mkoa Amani Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Salama Aboud Talib akizungumza wakati wa mkutano huo na kuwakaribisha Viongozi wa Ujumbe wa Kampeni ya Mama Mwanamwema Shein, kuzungumza na Viongozi wa UWT Mkoa wa Mjini Unguja. 
Makamu Mwenyekiti wa Mstaaf wa UWT Zanzibar Balozi Amina Salum Ali, akitoa nasaha zake kwa Viongozi wa UWT kutumia nafasi zao kuwahamasisha Wanawake kukipigia kura Chama cha Mapinduzi kwa Wagombea wao wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli na Wagombea wote wa CCM. 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja Silima Borafya akizungumza na Viongozi wa UWT katika mkutano wao na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati wa kumuombea Kura Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.
Muasisi wa Umoja wa Wanawake Tanzania Bi Asha Simba akiwasalimia Viongozi wa UWT na kuwaomba kukipigia kura Chama cha Mapinduzi na Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, mkutanom uliofanyika katika ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar. 
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akitowa nasaha zake kwa Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania kukipigia kura ya Ndio Chama cha Mapinduzi na Wagombea wao wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.   
Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Mjini Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akizungumza wakati wa mkutano huo wa kuwaombea kura Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli. na Wagombea wote wa CCM.
Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania wakionesha mikono juu kuashiria kuwapigia Wagombea wa CCM Kura ya Ndio kwa Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli. 
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Viongozi wa Umoja wa Wanawake wa Mkoa wa Mjini Unguja na kuwaomba kumpigia Kura ya Ndio Mgombea wa Urais wa CCM Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli na Wagombea wote wa CCM.
Viongozi wa UWT Mkoa wa Mjini wakifuatilia hutuba ya Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimuombea kura Dk Shein.
Umoja wa Wake wa Viongozi wa CCM Wabunge na Wawakilishi wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar  wakijumuika na Mke wa Rais wa Zanzibar kumuombea Kura Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein. 
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com
Mob. 0777424152 or 0715424152.
Email. othmanmaulid@gmail.com