MAHUJAJI WA 5 KUTOKEA TANZANIA WATHIBITISHWA KUFA HUKO MAKKA
WATU wasiopungua
700 wamekufa, huku wengine 816 wakijeruhiwa jana jirani na mji
Mtakatifu wa Makka walikokwenda kuhiji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa
moja ya nguzo muhimu katika Imani ya dini ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa
Baraza la Taasisi na Jumuiya za Kiiislam nchini, kati ya mahujaji
2,000,000 waliokwenda Saudi Arabia mwaka huu, 1,500 wanatoka
Tanzania.Kwa mujibu wa taarifa ya Sheikh Abu Bakari Zuberi Mufti wa Tanzania, kwa vyombo vya habari amesema tayari wamethibitisha kutokea vifo vya watu watano waliotokea Tanzania miongoni mwao mmoja ni raia wa Kenya na wengine wanne ni Watanzania.Amesema Watanzania waliotambuliwa hadi jana usiku wametajwa.
UPENDO NKONE KUZINDUA ALBAMU YA NYIMBO ZA INJILI YA “OMBA YESU ANASIKIA” JUMAPILI HII
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Upendo Nkone akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na uzinduzi wa Albanu ya nyimbo kumi ikiwa mpaka sasa ametimiza miaka kumi ya kuinjilisha kwa nyia ya nyimbo hapa nchini.
ALBAMU ya OMBA YESU ANASIKIA kuzinduliwa Septemba 27 mwaka huu(Jumapili hii) katika kanisa la TAG la upanga mkabala na chuo cha Uzumbe kwa Askofu Mwanesongore.
hayo yalisemwa na Mwimbaji wa nyimbo za Injili,Upendio Nkone wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, alisema kuwa Mungu amemuokoa katika kifo ndio maana ameona aimbe kwaajili ya kumshukuru Mungu kutokana na mambo aliyoyapitia, pia kumshukuru Mungu wa kutimiza miaka kumi ya kuinjilisha kwa njia ya Nyimbo.
Nkone alisema kuwa katika uzinduzi huo wa albamu ya OMBA YESU ANASIKIA kutakuwepo waimbaji wa nyimbo za Injili ambao watatumbuiza katika uzinduzi wa albamu hiyo atakuwepo Masanja mkandamizaji, Bahati Bukuku, Bonny Mwaitege, Kwaya ya Kijichi, Mather Baraka, Christina Matai, Mesi Chengula pamoja na Bendi.
Pia alisema kuwa katika uzinduzi wa albamu hiyo kutakuwa na viingilio tofauti, watu wazima watalipia kiasi za shilingi elfu tano(5000) na watoto shilingi elfu mbili (2000).
WAKAZI WA DAR ES SALAAM WARIDHISHWA NA UTENDAJI WA WAZIRI LUKUVI KATIKA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake waliotaka kujua jinsi
alivyoshughulikia migogoro ya Ardhi nchini.
Waziri
wa Ardhi Mhe. William Lukuvi pamoja na Naibu wake Mhe. Angela kairuki
wakipokea malalamiko ya wananchi wenye migogoro ya ardhi katika mkoa wa Dar es salaam
Waziri wa Ardhi akimsikiliza kwa makini mwananchi mwenye malalamiko ya mgogoro wa ardhi kutoka manispaa ya kinondoni.
Baadhi ya Wananchi wa Dar es salaam wenye Migogoro ya Ardhi wakiwa katika mkutano huo.
picha na KITENGO CHA MAWASILIWANO SERIKALINI
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
DKT FENELLA MUKANGARA AKUTANA NA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI NA KUNADI SERA ZAKE.
Mgombea
Ubunge jimbo la Kibamba kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mhe.Dkt
Fenella Mukangara akiwa kwenye mazungumzo na wakazi wa
jimbo la kibamba(kwa Yusuph) wakati alipotembelea vikundi vya vicoba
ili kuwaskiliza kero zao ili kujua matatizo wanayowakabili kwa ujumla.
Mkazi
wa kata ya Msigani(aliyesimama) akielezea matatizo yanayowakabili
wakazi wa eneo ilo na kumwomba mgombea wa Jimbo ilo kwa tiketi ya Chama
cha Mapinduzi Dkt Fenella Mukangara kuyatafutia ufumbuzi atakapopata
nafasi ya kuwatumikia.
Mgombea
udiwani kata ya Msigani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Siraju Hassan
Mwasha(aliyesimama) akiwa anazungumza na wakazi wa Maramba mawili na
kunadi sera za chama chake.Bw Mwasha aliambatana na mgombea Ubunge wa
jimbo la kibamba kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dkt Fenella
Mukangara.
Mgombea
Ubunge jimbo la Kibamba kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mhe.Dkt
Fenella Mukangara akiwaaga wakazi wa kwa Msigwa kata ya msigani baada ya
kuzungumza na wakazi hao pamoja na vikundi vya kijasiriamali ili kujua
ni kero gani zinawasibu ili kuboresha makundi hayo na maeneo yao kwa
ujumla.
Mmmoja
wa wanakikundi wa Vicoba mtaa wa Temboni,Mbezi(aliyesimama) akimwuliza
maswali mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(aliyekaa
amesuka) Dkt Fenella Mukangara ni jinsi gani atawasaidia kuboresha
vikundi vyao vya vicoba na jinsi gani atawasaidia ili wapate mafunzo ya
ujasiriamali.
President Kikwete officiates ATA’s 10th Annual Presidential Forum on Tourism
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete delivers his keynote speech during the 10th Africa
Travel Association Annual Presidential Forum on Tourism held at New
York University Kimmel Center in United States of America this morning.
President Dr.Jakaya Mrisho
Kikwete in conversation with the Minister for Natural Resources and
Toursim Hon. Lazaro Nyalandu during the 10th Africa Travel Association Annual Presidential Forum on Tourism held at New York University Kimmel Center.
The Director Africa House and
Economics Professor at the New York University Yaw Nyariko presents
souvenir gift to President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete during the 10th
Annual Presidential Forum on Tourism held at New York University Kimmel
Center in New York this morning. Center is the Minister for Tourism and
Natural Resources Hon. Lazaro Nyalandu
Africa Travel Association ATA Executive Director Mr.Edward Bergman welcomes President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete to the 10thATA Annual Presidential Forum on Tourism held at New York University Kimmel Center in United States of America this morning.
The Minister for Natural
Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu Speaks during an open Forum
on “ Africa Tourism,” during to the 10th ATA Annual
Presidential Forum on Tourism held at New York University Kimmel Center
in United States of America this morning. Other panelists from left
Mali’s Minister for Culture, Crafts and Tourism Hon. N’Diaye
Ramatoulaye Diallo , Namibia’s minister for Environment and Tourism
Hon. Pohamba Shifeta,(third left), Uganda’s Minister for Tourism
Wildlife and Antiquities Hon.Dr. Maria Mutagamba(fouth left) and on the
right is Kenya’s Cabinet Secretary in the Ministry of East African
Affairs, Commerce and Tourism Hon. Phyllis Kandie.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in a group photo with panelists and coordinators of the ATA 10th
Annual Presidential Forum on Tourism held at at New York University
Kimmel Center in United States of America this morning. From left
Executive Director Africa Travel Association(ATA) Mr. Edward Bergman,
Namibia’s Minister for Environment and Tourism Hon. Pohamba
Shifeta,(second left), Kenya’s Cabinet Secretary in the Ministry of East
African Affairs, Commerce and Tourism Hon. Phyllis Kandie(Third left),
Mali’s Minister for Culture, Crafts and Tourism Hon. N’Diaye
Ramatoulaye Diallo(fourth left),The President, The Minister for Natural
Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu, Director Africa House and
Professor of Economics Dr. Yaw Nyarko(seventh left), ), Uganda’s
Minister for Tourism Wildlife and Antiquities Hon.Dr. Maria
Mutagamba,(eight left) and the panel moderator who is also the CBS News
Travel Editor Mr. Peter Greenberg(photos by Freddy Maro)
WAZIRI CELINA KOMBANI AFARIKI DUNIA NCHINI INDIA
Habari zilizotufikia zinasema kwamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeashi Kombani (pichani),
amefariki dunia leo huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani.
Alikuwa na umri wa miaka 56.
Taarifa kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na
kueleza kwamba mwili wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku
ya Jumatatu, ambapo Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya
maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko
Mahenge ambako alikuwa Mbunge wa jimbo la Ulanga Mashariki.
Subscribe to:
Posts (Atom)