KIZIMBANI YAIADHIBU JAMHURI LIGI KUU ZANZIBAR.

September 06, 2013
Na MASANJA MABULA,ZANZIBAR.
TIMU ya soka Kizimbani Leo imeanza vema michuano ya Ligi Kuu Zanzibar baada ya kuibamiza Jamhuri mabao 2-0,katika mchezo uliochezwa dimba la soka Gombani kisiwani Pemba.

Mchezo huo ambao ulianza kwa kasi kubwa ambapo Kizimbani waliweza kuandika bao lao la kwanza kupitia Othumani Mussa katika dakika ya 30 baada ya kupiga shuti kali lililomshindi lililotinga moja kwa moja wavuni.

Bao hilo lilidumu mpaka timu zote zinakwenda mapumziko ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi,ambapo Jamhuri iliweza kuingia uwanjani hapo kwa lengo la kusawadhisha bao hilo huku Kizimbani wakiwa na lengo la kuongeza bao hilo.

Wakionekana kujipanga na kupeleka mashambulizi ya mara kwa mara langoni mithili ya mbogo aliyejeruhiwa alimanusura Jamhuri wapata bao lakini mchezaji wao alishindwa kuunganisha vizuri pasi aliyeipokea na kucheza fungo na kutoa mpira huo nje ya uwanja huo.

Kutokana na shambulio hilo,Kizimbani waliweza kuzinduka na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa Jamhuri na kufanikiwa kuongeza bao lao la pili ambalo lilifungwa na Mfanyeje Mussa na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa Kizimbani kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jamhuri.

AFRICAN SPORTS KUWAVAA MGAMBO SHOOTING KESHO MKWAKWANI.

September 06, 2013
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
TIMU ya Mgambo Shooting kesho itashuka kwenye dimba la CCM Mkwakwani kuwavaa African Sports "Wanakimanumanu"ikiwa ni mchezo wa kirafiki utakaochukua nafasi majira ya saa kumi jioni.

Akizungumza na Tanga Raha,Ofisa Habari wa timu ya African Sports "Said Karsandas amesema maandaliiz ya kuelekea mchezo huo yanaendelea vizuri na kila kitu kimekamilika kwa asilimia kubwa.

Karsandas alisema mchezo huo ni maalumu kwa Mgambo shooting kujiandaa na michezo yao ya ligi kuu Tanzania bara ili kuweza kufanya vema wakati African sports watatumia mchezo huo kwa ajili ya maandaliiz ya ligi ya mkoa wa Tanga.

Aidha aliwataka mashabiki na wadau wa soka mkoani hapa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kushuhudia mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa na upinzani mkubwa.


Akizungumza mechi yao inayofuata ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati yao na Ruvu Shooting,Kocha Mkuu wa Mgambo Shooting ya Tanga,Mohamed Kampira alisema maandalizi ya kuelekea mechi hiyo yamekamilika kwa asilimia kubwa .

Kampira alisema matumaini yao makubwa ni kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo yao iliyosali kwenye michuano hiyo ili kuweza kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa katika nafasi tatu za juu.

BAVARIA WAFADHILI MASHINDANO YA LUGHA YA KIINGEREZA KWA SHULE ZA SEKONDARI MKOA WA TANGA .

September 06, 2013
WANANFUNZI WAKIFUATILIA MASHINDANO YA LUGHA YA KIINGEREZA AMBAYO YALIANZA JANA KATIKA HOTEL YA REGAL NAIVERA YAKIFADHILIWA NA KINYWAJI KISICHO NA KILEVI CHA  BAVARIA HOLLAND




Na Oscar Assenga,Tanga.
IMEELEZWA kuwa mashindano ya Lugha yatawapa chachu wanafunzi kutambua uwezo wao ikiwemo kutoa mwamko kwao kupenda kutumia lugha ya kiingereza zaidi hali ambayo itapeleka kufanya vizuri katika masomo yao.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Msaidizi anayeshughulikia masuala ya elimu Mkoa wa Tanga, Ramadhani Chomola wakati akifunga mashindano ya lugha ya kiingereza kwa wanafunzi wa shule za sekondari mkoa wa Tanga "Bavaria Malt English Competitio For Tanga Secondary 2013 yaliyojumuisha wanafunzi zaidi ya 100
kutoka wilaya tano mkoani hapa.

Chomola alisema mashindano hayo yatawapa mwanga mzuri washiriki kuongeza ubunifu na bidii ya kuzungumza lugha ya kiingereza popote wanapokuwa ili waweze kujijenga lakini pia kufahamu namna ya kuzungumza lugha hiyo.

Katika mashindano hayo shule ya Wasichana ya St.Christina ilifanikiwa kuwa mshindi kati ya sekondari 22 zilizoshiriki mashindano yakuzungumza lugha ya kiingereza na kuzawadiwa  seti moja ya kompyuta na printa ambapo sekondari ya Popatlaly iliyoshika nafasi ya pili ilizawadiwa seti ya kompyuta,Sekondari ya Rosmini iliyoibuka mshindi wa tatu ilijinyakulia runinga yenye ukubwa wa inchi 40.

Mashindano hayo ya siku mbili yalifanyika katika viwanja vya Regal Naivera na Mkwakwani kwa udhamini wa Bavaria Holland kupitia kampuni ya Jovet (T) limited inayosambaza kinywaji baridi cha Bavaria Malt yalilenga  kuhamasisha wananfunzi ili waone umuhimu wa kuzungumza kingereza.

Kwa upande wake,Meneja wa Uendeshaji Masoko wa Bavaria Holland,Rogerter Horst alisema kampuni hiiyo inamaanini kwamba ni jambo jema kuisaidia jamii kufikia malengo yake ya kupata maendeleo yake ya kuichumi kupitia jamii.
 


BAADHI YA WALIMU KUTOKA SHULE MBALIMBALI MKOA WA TANGA WAKIFUATILIA MASHINDANO HAYO.

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI POPATLALY NA ST.CHRISTINA WAKIWA TAYARI KWA AJILI YA MASHINDANO HAYO.

MEZA YA MAJAJI WA MASHINDANO HAYO WAKIWA KWENYE MICHAKATI YAO KUHAKIKISHA KILA KITU KINAKWENDA SAWA NA BINGWA ANAPATIKANA BILA MALALAMIKIO.


OPERATIONS MANAGER WA JOVET (T) LIMITED,CATHERINE MUNGUTI  AMBAYE ALIMUWAKILISHA MANAGING DIRECTOR JOHN KESSY KWENYE HALFA HIYO KULIA NA KUSHOTO KWAKE NI MWENYEKITI WA KAMATI YA ELIMU HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA,MUSTAPHA SELLEBOSS WAKIFUATILIA MASHINDANO HAYO.

HAPA WAKITETE JAMBO.





OPERATIONS MANAGER WA JOVET (T) LIMITED,CATHERINE MUNGUTI  AMBAYE ALIMUWAKILISHA MANAGING DIRECTOR JOHN KESSY KWENYE HALFA HIYO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI AMBAO HAWAPO PICHANI KUHUSU MASHINDANO HAYO.

PICHA ZOTE NA PASKAL MBUNGA,TANGA.