WATUMISHI WA HOSPITAL YA SEKOUR TOURE, HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA NA CHUO CHA IFM WASHIRIKI ZOEZI LA USAFI LA KILA MWEZI.

January 30, 2016
Dkt.Magreth William Magambo ambae ni Daktari Bingwa wa Mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure akitoa ufafanuzi juu ya Ushiriki wa Watumishi wa Hospitali hiyo la kushiriki Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Amesisitiza wananchi kuwa na desturi ya kufanya Usafi wa mara kwa mara (Kila Siku) katika mazingira yao ili kuepukana na hatari ya kupata magonjwa ya kuambukiza ikiwemo kipindupi huku akikumbusha zaidi pia wanajamii kuzingatia kanuni za usafi katika maeneo muhimu kama vile vyooni. Kunawa mikono kwa maji safi na sabuni baada ya kutoka chooni.
Dkt.Peter Maziku ambae ni Daktari katika kitengo cha CTC katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure akizungumza wakati wa zoezi la usafi la kila mwisho wa mwezi lililofanyika hii leo Jijini Mwanza. 
Anasema watoa huduma mbalimbali (Madaktari, Waalimu, Wafanyabiashara nk) katika jamii lazima wawe mfano wa kuigwa katika kuwajibika kuweka mazingira katika hali ya usafi ili kuwezesha wananchi wengine kuiga mfano huo.
Baadhi ya Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Baadhi ya Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Kulia ni Dkt.Peter Maziku ambae ni Daktari katika kitengo cha CTC katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure akiwa pamoja na Dkt.Charles Ludibuka ambae ni Mfamasia katika Hospitali hiyo Sekour Toure walishiriki zoezi la usafi katika Mazingira ya Hospitali hiyo.
Katika picha wakichoma uchafu baada ya usafi.
Baadhi ya Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Hapa wakiwa katika barabara ya Machemba Jijini Mwanza ambayo inatoka na kuingia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sour Toure.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Hapa wakiwa katika barabara ya Machemba Jirani na Kituo cha mafunzo ya Lugha mbalimbali cha International Language Training Centre Jijini Mwanza ambayo inatoka na kuingia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sour Toure.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Hapa wakiwa katika barabara ya Machemba Jirani na Kituo cha mafunzo ya Lugha mbalimbali cha International Language Training Centre Jijini Mwanza ambayo inatoka na kuingia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sour Toure.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Hapa wakiwa katika barabara ya Machemba Jirani na Kituo cha mafunzo ya Lugha mbalimbali cha International Language Training Centre Jijini Mwanza ambayo inatoka na kuingia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sour Toure.
Wanafunzi pamoja na Watumishi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM tawi la Mwanza, pia nao walishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.

SERIKALI YAKITWAA KIWANDA CHA CHAI CHA MPONDE

January 30, 2016
Lushoto, SERIKALI imekitwaa kiwanda cha Chai cha Mpondwe kilichopo Bumbuli na kusema kuwa mwekezaji alivunja mkataba wa uendeshaji jambo lililowawasababishia wakulima na mwekezaji kuingia katika mivutano ya mara kwa mara.
Utwaaji wa kiwanda hicho ulifanywa kwa ulinzi mkali wa kikosi cha polisi waliokuwa na silaha kwa kushirikiana na, Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza, Kamanda wa Polisi Tanga, Mihayo Misikhella pamoja na Mbunge wa jimbo la Bumbuli, Januari Makamba.
Kiwanda hicho ambacho kwa zaidi ya miaka mitatu kimesimama uzalishaji na kuingia migogoro ya mara kwa mara baina ya wakulima na mwekezaji jambo lililopelekea wakulima kutishia kubadilisha aina ya kilimo badala ya Chai.
“Kwa mamlaka niliyonayo niliyopewa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli, kuanzia sasa kiwanda hiki cha chai cha Mponde kinatwaliwa na Serikali" alisema Msajili wa Hazina Laurenced Mafuru
Mafuru alisema mwekezaji ambaye alikuwa ni Umoja wa Wakulima wa Chai, Korogwe na Lushoto (UTEGA) walishindwa kukiendesha kiwanda hicho na kuvunja mikataba ya uendeshaji kiwanda.
Alisema kwa kipindi chote hicho Serikali ilikuwa inafuatilia kwa umakini kisha kubaini kuwa kuna ukiukwaji mkubwa wa mkataba wa uendeshaji hivyo kuona ni vyema kukichukua na kuliokoza zao la Chai Wilayani humo.
“Katika ufuatiliaji wetu tuliona zao la chai hapa linatoweka na wakulima wengi wamebadilisha aina ya kilimo na kulima mahindi, hakuna sababu yoyote wakati kiwanda chenye mitambo iliyokamilikka kufa hivi hivi” alisema Mafuru
Akizungumza na wananchi mara baada ya kiwanda hicho kuchukuliwa na Serikali, Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, aliwataka wakulima kurejea mashambani na kulima Chai na kusema kuwa neema inakuja.
Alisema hakutakuwa na mivutano tena ya bei na uendeshaji wa kiwanda kwani Serikali inatambua hivyo ni wajibu wa kila mkulima kurudi shambani na kusema kuwa kiwanda hicho karibuni kitaanza kununua na kuanza uzalishaji.
“Wazee wangu na wajomba na mashangazi kile kilio chenu cha muda mrefu leo kimetimia, hakuna jambo lisilo na mwisho na leo najua kila mmoja hapa kwa furaha ataenda kupika biriani” Alisema Makamba
Aliwataka wakulima hao kila mmoja kurejea katika eneo lake la na wale ambao waliuza au kubadilisha aina ya kilimo kurejea kulima Chai kwani Serikali imejipanga kuwakomboa na umasikini wakulima wa Chai.
                                              Mwisho



  Aliekuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Chai (UTEGA) kiwanda cha Chai cha Mponde Bumbuli Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, William Shelukindo, akilalamika mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza mara baada ya Serikali kukitwaa kiwanda hicho baada kukaa zaidi ya miaka mitatu bila uzalishaji na wakulima kuteseka kutafuta masoko ya kuuza Chai.

 Aliekuwa Mwekezaji kiwanda cha Chai Cha Mponde Lushoto Tanga, Nawab Mullah, akilalamika kutwaliwa kiwanda hicho na Serikali mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza, Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru na maofisa wengine wa Serikali.




 Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru akipokea maelekezo ya kiwanda cha Chai Cha Mponde ambacho amekitwaa na kukikabidhi kwa Serikali baada kushindwa kufanya kazi kwa miaka mitatu baada ya Mwekezaji Umoja wa Wakulima Lushoto na Korogwe (UTEGA) kushindwa kutekeleza mkataba wa kuendesha kiwanda hicho.
Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (kulia) akiwana Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza (kushoto) wakitoka nje baada ya kukagua mitambo ya kiwanda cha Chai Cha Mponde baada ya Serikali kukitwa kutoka kwa Mwekezaji (UTEGA) kushindwa kutekeleza mkataba wa kukiendesha kiwanda.

SUMAYE AIANGUKIA SERIKALI WANANCHI KUVAMIA SHAMBA LAKE LA EKARI 33 MABWEPANDE

January 30, 2016
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye  Dar es Salaam leo asubuhi mara baada ya kuwasili eneo la Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kuangalia eneo la ekari 33 la Sumaye lililovamiwa na wananchi.
 WAZIRI Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (wa pili kulia), na mke wake mama Esther (kushoto), wakimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia) eneo la shamba lake la ekari 33 lililopo Mabwepande Manispaa ya Kinondoni lililovamiwa na wananchi walipotembea eneo hilo Dar es Salaam leo asubuhi.
 Hapa Sumaye na viongozi wengine wakitafakari jambo.
 DC Makonda akihutubia katika mkutano huo. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mabwepande, Suzan Masawe.
 Mheshimiwa Sumaye (kushoto), akiongoza kuonesha mpaka wa shamba lake.
 Mhe. Sumaye akielezea uhalali wake wa kumiliki eneo hilo.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mji Mpya,  Justine Chiganga (kulia), akizungumza katika mkutano huo 
 Moja ya kibanda kilichojengwa na wananchi waliovamia eneo la Mhe Sumaye.
 Baadhi ya vibanda vilivyojengwa na wananchi katika eneo la Sumaye.
 Askari Polisi wakiimarisha ulinzi wakati wa mchakato wa kutembelea eneo hilo lililovamiwa.
 Wananchi wa eneo la Mabwepande wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mkazi wa eneo hilo Athuman Mnubi akielezea jinsi walivyovamia eneo la Sumaye.
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabwepande Abdalla Omari Kunja akizungumza katika mkutano huo.
 Diwani wa Kata ya Mabwepande, Suzan Masawe akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Ardhi Manispaa ya Kinondoni, Matinga Ernest akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya Ardhi katika Manispaa hiyo.
…………………………………………………………………………………………..
Dotto Mwaibale
 
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, ameiangukia serikali na kuomba msaada baada ya wananchi kuchukua sheria mkononi na kuvamia eneo lake la ekari 33 lililopo Mabwepande katika Manispaa ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
 
Serikali imemuahikikishia Sumaye kuwa haina mpango wa kumkandamiza mtu mnyonge wala tajiri hivyo itahakikiha inatoa haki kwa kila mmoja baada ya wiki mbili kwa kua imesikiliza pande zote mbili katika mgogoro huo. 
 
Akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya wananchi wa kitongoji  cha Kimondo mtaa wa mji mpya Kata ya Mabwepande na Sumaye  Dar es Salaam leo asubuhi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda alisema ili kumaliza mgogoro huo ambao Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye ameiomba serikali kuingilia kati ni lazima busara kutumika.
 
Alizitaka pande hizo mbili kuiachia serikali kwa wiki mbili ili kutafuta njia bora ya kumaliza tatizo hilo huku wananchi wakitakiwa kuache kuendelea na ujenzi na kugawiana maeneo katika shamba hilo.
 
“Serikali ya Rais Magufuli ni sikivu na ndio maana ilikuwa tayari kumsikiliza Waziri Mkuu wetu Mstaafu Sumaye na kusikiliza wananchi ili kutenda haki tunatambua migogoro ya ardhi ilivyokuwa na athari kwa jamii hatuna mpango wa kumkandamiza tajiri wala mnyonge,”alisema.
 
Alisema katika eneo hilo anajua jinsi wananchi walivyotumia nguvu katika kuwekeza ujenzi na rasilimali zao lakini kwa sasa wasitishe shughuli hizo na kuendelea kugawana maeneo na Sumaye pia kuacha uwekezaji ili kutafuta suluhu.
 
Zipo njia nyingi tutazitumia kumaliza mgogoro huu ikiwemo kufuata sheria kwa kuangalia iwapo mzee wetu alikiuka taratibu kweli za kumiliki ardhi kama ilivyodaiwa na wananchi hatua gani serikali tuchukue,”alisema.
 
Alisema pia wanaweza kukaa na Sumaye na kuzungumza naye ili kukubali hasara kwa kutoa eneo kidogo na kuwapatia wananchi  hao ambao hawana makazi au Manispaa kutafuta eneo mbadala na kuwauzia kwa bei nafuu.
 
Alizitaka pande hizo mbili kutambua umuhimu wa kulinda amani katika mgogoro huo kwa changamoto zilizopo kutatuliwa bila kutumia nguvu.
 
Makonda pia aliagiza serikali ya kijiji kufanya utambuzi wa wananchi hao wenye makazi katika shamba la Sumaye.
 
Awali katika mkutano huo Sumaye alimueleza Makonda jinsi serikali ilivyo na kazi ngumu ya kushughulikia migogoro ya ardhi na kuomba kutumia busara zake kumpatia eneo hilo analomiliki kihalali.
 
“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kama nilivyokueleza awali serikali yetu inakazi ngumu sana hasa kutokana na viongozi wa chini kutokuwa wasikivu na wakweli eneo hili namiliki kihalali nina nyaraka zote na ninalipia kila mwaka na nilikuwa katika mpango wa kutafuta wafadhili ili kuliendeleza kwa kujenga Chuo Kikuu,”alisema.
 
Alisema  yeye na familia yake waliuziwa eneo hilo toka mwaka 1997 na anaamini serikali itatenda haki.
 
 Diwani wa kata hiyo Suzan Masawe alisema anauthibitisho kuwa eneo hilo lilikuwa pori na Sumaye alilitelekeza kwa muda mrefu na kusababisha uhalifu ikiwemo wanawake kubakwa,mali za wizi kufichwa na uhalifu mbalimbali.
 
Alisema kutokana na hatua hiyo   walimtafuta Sumaye lakini hakuwa na ushirikiano kwakuwa hata alipofanya uwekezaji kwa kuchimba kisima cha maji alikataa kuwapa wananchi .
 
Suzan alisema kutokana na hasira za wananchi hao kwa kukosa huduma za kijamii kwa muda mrefu ikiwemo eneo hilo kutokuwa na shule,Zahanati wala kituo cha polisi waliamua kuvamia na kujigaia maeneo. 
 
Mmoja wa wananchi hao Athuman Mnubi alikiri kweli hawana umiliki halali wa eneo hilo na katika hatua ya kutafuta makazi walivamia msitu huo uliotelekezwa na Sumaye.
Alisema wanaamini kutokana na ahadi ya serikali ya Rais Magufuli katika kupora maeneo yaliyotelekezwa  na wawekezaji watasaidiwa.
 
WAKATI huo huo Makonda alisimamisha na kukamata baadhi ya malori ya kokoto na mchanga, wafanyakazi na Mwekezaji wa kigeni kutoka India  Sules Waljan wanaochimba mchanga,kokoto na kifusi katika eneo la Mabwepande.
 
Hatua hiyo imekuja baada ya kuona uharibifu mkubwa wa mazingira na alipowahoji wafanyakazi na Mwekezaji huyo kama wanavibali walisema hawana.
 
Makonda amewafikisha watuhumiwa hao kituo cha polisi cha Wazo Hill ili kutoa maelezo ya kina na kusema kuwa serikali inatumia gharama kubwa kwa uhalibifu huo wa mazingira ambao pia unafanywa katika vyanzo vya maji na matengenezo ya madaraja yanayoharibiwa ni makubwa.
 
WADAU WAHAMASISHWA KUWEKEZA TASNIA YA UONGEZAJI THAMANI MADINI

WADAU WAHAMASISHWA KUWEKEZA TASNIA YA UONGEZAJI THAMANI MADINI

January 30, 2016

MAD1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesa James Mdoe akiangalia madini mbalimbali kupitia kifaa kinachotumika kukuza mawe ya madini ili yaweze kuonekana vizuri ikiwemo kubaini kasoro . Kabla ya kutunuku vyeti Wahitimu 14 wa Mafunzo ya kunga’risha na kukata madini ya Vito, Prof. Msofe amepata fursa ya kuangalia bidhaa mbalimbali za mapambo zilizotengenezwa na wahitimu hao ikiwemo vifaa vinavyotumika wakati wa mafunzo. Anayemwonesha kushoto ni Mtumishi katika  cha Jimolojia Tanzania, Salome Tilumanywa (kushoto). Wengine wa kwanza kulia ni Kaimu Mratibu wa Kituo hicho John Mushi, anayefuata ni Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia masuala ya Uchumi na Biashara ya Madini, Salim Salim.
MAD2
Mmoja wa Walimu katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), Ramadhan Haizer (kushoto) akimwonesha mfano wa mapambo ya vito ambayo Wahitimu wamepata mafunzo ya kutengeneza katika mikato mbalimbali katika fani za Unga’rishaji na uchongaji madini ya vito Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesa James (wa pili kushoto). Katikati ni Kaimu Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Ally Samaje.
MAD3
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesa James  akiangalia  madini ya vito yaliyokatwa katika maumbo mbalimbali kutoka kwa Baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo ya Unga’rishaji na Ukataji wa Madini ya Vito katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC).
MAD4
Baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo ya Ukataji na Unga’rishaji Madini ya Vito wakitumia mashine mbalimbali za Kuchonga katika maumbo mbalimbali na kungarisha madini ya  Vito.
MAD5
Baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo ya Ukataji na Unga’rishaji Madini ya Vito wakitumia mashine mbalimbali za Kuchonga katika maumbo mbalimbali na kungarisha madini ya  Vito.
MAD6 MAD7
Wahitimu wa Mafunzo ya Ukataji na Unga’rishaji Madini ya Vito wakiwa wameshika mchoro wa umbo la Ramani ya Tanzania ambalo lililowekwa  Madini ya aina katika maumbo mbalimbali kulingana aina za  madini hayo yanavyopatikana katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo wamemkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe ikiwa ni njia ya kuonesha ubunifu wao  baada ya kuhitimu mafunzo.
MAD9
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesa James Mdoe (katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini kutoka Makao Makuu na walio katika ofisi za Madini za ARusha na Moshi na Kituo cha Jemolojia Tanzania, wakati wa Mahafali ya Pili ya  Mafunzo ya Ukataji na Unga’rishaji Madini ya Vito.
……………………………………………………………………………………………………….
Na Asteria Muhozya, Arusha
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imetoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje katika  Sekta ya Madini kuwekeza katika kuanzisha  Vituo vya Uongezaji Thamani Madini ili kuendeleza fani hiyo kwa manufaa ya uchumi wa taifa.
Wito huo umetolewa leo jijini Arusha na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesa James Mdoe wakati  wa Mahafali ya Pili katika fani za Ukataji na Unga’rishaji Madini ya Vito katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGDC).
Profesa Mdoe amesema kuwa, uongezaji thamani madini unalenga kuongeza fursa za ajira, kwa Watanzania watakaofanya kazi katika vituo hivyo, ikiwemo pia kutoa fursa za wataalamu wa sekta hiyo kujiajiri na hivyo kuongeza mapato kwa Serikali jambo ambalo pia litasaidia kuongeza mchango wa sekta hiyo katika Pato la Taifa.
Ameongeza kuwa, Kituo hicho kina historia ya  ya pekee katika historia ya sekta ya Madini  kwa kuwa kimekuwa kituo cha kwanza na pekee kuanzishwa hapa nchini,  na kuongeza kuwa, uwepo wake ni kielelezo sahihi cha kazi za ubunifu na uongezaji thamani madini ya vito.
Pia amesema kuwa, kuanzishwa kwa kituo hicho ni moja ya hatua za Serikali za kutimiza malengo yaliyomo katika Sera ya Madini ya Mwaka 2009 yenye lengo la kuongeza mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la taifa na ajira kwa watanzania kupitia uongezaji thamani madini, ikiwa pamoja na mafunzo ua Jemomojia, ukataji na unga’rishaji wa madini ya vito , utengenezaji wa bidhaa za mapambo na uchongaji wa vinyago vya mawe.
Aidha, Profesa Msofe ametoa wito kwa Kampuni zinazofanya biashara ya madini ya vito na wadau wengine kuchangia maendeleo ya Kituo hicho ili kiwe kitovu cha kutoa Wataalamu wanaokidhi mahitaji ya tasnia ya madini ya vito nchini.
Akizungumzia zuio la mwaka 2010 la kusafirisha Tanzanite ghafi inayozidi gramu moja nje ya nchi, amesema lengo la zuio hilo ilikuwa ni kuhamasiaha ujenzi wa vituo , vyuo, taasisi na viwanda vya kuongeza thamani ya madini hayo nchini  na kuongeza kuwa, jambo hilo pia ndilo lililopelekea Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kuanzisha kituo hicho.
Awali, akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo hayo, Monica Laiton, amesema kuwa, mafunzo hayo  yamewapa  ujuzi wa kukata madini ya aina tofauti ikiwemo Tanzanite katika mikato mbalimbali na kuongeza kuwa, ujuzi  huo utawawezesha kuajiliwa au kujiajiri na  kuongeza kuwa, mafunzo hayo yamedhihirisha wazi kuwa, wanawake wanaweza kufanya kazi katika sekta hiyo tofauti na dhana iliyokuwepo awali kwamba shughuli za sekta hiyo zinafanywa na wanawake pekee.
Jumla ya Wahitimu 14 wamehitimu mafunzo hayo kwa muda wa miezi sita, ambapo walipata ufadhili   kupitia Kamati inayoandaa Maonesho ya Vito ya Arusha  (Arusha Gem Fair)  chini ya Mfuko wa kuendeleza Wanawake katika tasnia ya madini.  Maonesho ya Arusha huandaliwa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA) kwa ushirikiano na Wizara ya Nashati na Madini. Mwaka huu maonesho hayo yatafanyika jijini Arusha katika Hotel ya Mount Meru kuanzia tarehe 19- 21, Aprili, 2016.

WAZIRI MKUU MAJALIWA KASSIM MAJALIWA KUSHIRIKI IBADA YA KUMUINGIZA KAZINI ASKOFU MKUU WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHELI TANZANIA (KKKT) MJINI MOSHI.

January 30, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizung4umza na wanahabari ofisini kwake kuhusu ugeni wa Waziri mkuu ,Majaliwa Kassim Majaliwa mkoani Kilimanjaro.

Baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amosi Makala ali-pozung4umza nao ofisini kwake.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

WAZIRI mkuu, Majaliwa Kassimu Majaliwa, leo  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ibada maalum ya kumuingiza kazini askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kiluteri Tanzania(KKKT),Askofu Dk Frederick Shoo katika kanisa kuu la Moshi mjini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla,amesema waziri mkuu anatarajiwa kuwasili  mkoani Kilimanjaro kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) ambapo atapokea taarifa ya mkoa kabla ya kufanya shughuli za kanisa.

Alisema waziri mkuu hataongozana na waziri yeyote wa serikali ya awamu ya tano bali wasaidizi wake na baada ya ziara hiyo maalum atarejea Dodoma kuendelea na shughuli za serikali.

Ibada hiyo maalumu itajumuisha viongozi mbalimbali wa serikali ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro sanjari na viongozi wa madhehebu tofauti ya dini,wadau wa maendeleo,waumini na wananchi kwa ujumla.

Kutokana na ujio huo wa waziri mkuu, mkuu wa mkoa,aliwataka wananchi hususani katika wilaya za Hai na Moshi kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo ambaye pia atapokea changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa

Kadhalika waziri mkuu anatarajiwa kutoa maelekezo ya serikali kulingana na changamoto zitakazojitokeza wakati anapewa taarifa ya mkoa.

Dk Shoo ambaye pia ni askofu wa dayosisi ya Kaskazini amechaguliwa kuongoza kanisa hilo kwa miaka minne na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na mtangulizi wake askofu Dk Alex Malasusa ambaye amemaliza muda wake wa uongozi.

Askofu Dk Shoo alichaguliwa mapema mwezi Agosti mwaka jana katika mkutano mkuu wa 19 wa kanisa hilo uliofanyika chuo kikuu cha Tumaini jijini Arusha baada ya kuwashinda wenzake wawili.

Uchaguzi wa nafasi hiyo  uliwashindanisha askofu Dk Stephen Munga wa dayosisi Kaskazini Mashariki na Askofu Charles Mjema wa dayosisi ya Pare.

Mwisho



WATANZANIA WENGI WANAKOSA FURSA ZA KIMAENDELEO KUTOKANA NA KUTOJUA LUGHA.

January 30, 2016
Charles Mombeki (Kulia) ambae ni Mkurugenzi wa International Language Training Centre akizungumza na George Binagi kuhusiana na Umhimu wa Watanzania kujifunza lugha za Kimataifa hususani Kiingereza kwa ajili ya kuendana na muingiliano wa Kimataifa uliopo katika shughuli mbalimbali ikiwemo biashara.
"Watanzania wengi wanakosa fursa mbalimbali zilizopo. Wengine wanakosa fursa za kibiashara pamoja na kazi kutoka katika Mashirika na Makampuni mbalimbali duniani kutokana na kushindwa kufahamu lugha za Kimataifa hususani kiingereza, Kijerumani, Kifarasa, Kichina na hata lugha nyingine. Hivyo niwasihi waamue kujifunza lugha, kwa kuwa lugha inafungua milango ya mafanikio maishani". Anasema Mombeki.

Anasema, Watanzania wawaandae watoto wao katika lugha ya Kiingereza katika kupata elimu, akiunga mkono shule za watu ama Mashirika binafsi kutumia lugha ya Kiingereza kufundishia, tofauti na ilivyo kwa shule za Serikali kutumia lugha ya Kiswahili katika kufundishia katika shule za msingi akitanabaisha kwamba bado kiswahili hakijawa na nafasi kubwa kutumika kimataifa kama ilivyo kiingereza ambayo ni lugha inayowaunganisha watu wote Kimataifa. 

Mombeki anadokeza kuwa wanafunzi waliofundishwa kwa misingi ya kiingereza tangu wakiwa wadogo wana nafasi kubwa ya kufikia malengo yao ikilinganishwa na wale walioanza elimu yao ya  awali na msingi kwa lugha ya kiswahili.

Anabainisha kuwa kuna wanafunzi wengi kutoka Mataifa ya Afrika, Amerika na Ulaya wanapenda kufika katika Centre hiyo ambayo ilianza kutoa elimu ya lugha mbalimbali tangu mwaka 1998. Pia inafundisha lugha ya Kiswahili pamoja na lugha za asili ikiwemo Kisukuma pamoja na Mila na Desturi za Tanzania.
Imeandaliwa na George Binagi