BODA BODA KILINDI WALILIA HUDUMA ZA TRA.

January 02, 2014

IMEWEKWA Januari 3.
WAENDESHA Boda Boda wilayani Kilindi mkoani Tanga wameiomba Mamlaka ya Mapato mkoani Tanga (TRA)kuwapeleka wilayani humo huduma ya upatikanaji wa leseni kutokana na vijana wengine kutokuwa nazo hali inayochangiwa na kutokwepo kwa ofisi inayoshughulika na masuala hayo.

Kilio hicho kilitolewa hivi karibuni na wananchi wa kata ya Kwediboma wilayani hapa wakati wakizungumza ambapo walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakiikosa kitendo ambacho kinawalazimu kusafiri mpaka Tanga mjini ili kufuata huduma hiyo

REA KUPELEKA UMEME WILAYA SITA MKOANI TANGA.

January 02, 2014
Na Oscar Assenga,Tanga.

WAKALA wa nishati ya Umeme Vijijini (REA)unatarajiwa kukamilisha miradi ya Umeme katika vijiji mbalimbali mkoani Tanga ambapo ikikamilika itaongeza huduma  hiyo kwa wananchi na wawekezaji waliopo kwenye maeneo yao hali ambayo itachangia kasi maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa aliyasema hayo juzi wakati akitoa taarifa ya mafanikio kwa mkoa wa Tanga kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2012 hadi Octoba 2013 ambapo alisema kwenye mpango  huo jumla ya wilaya sita zitanufaika.

Gallawa alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2013-2014 wakala umepanga kupeleka umeme katika maeneo ya wilaya ya Handeni kwenye vijiji vya Kideleko,Kigombe, Madebe,Nyasa na Gole ili kuwawezesha wananchi hao kufaidika na huduma ya nishati.

Alisema kwenye wilaya ya Korogwe mji wakala wa nishati ya umeme vijiji watapeleka kwenye maeneo ya Maili Kumi,Taasisi ya Utafiti ya Tafori,Kwamgwe, Jambe,Kamsisi, Kwamndolwa, Kwakombo,Kwameta, Kwange,Msambiazi, Darajani,Gereza, Kwamzindawa,Mgobe, Kituo cha Afya Kwalukonge,Miradi ya Kilimo cha Umwagiliaji ya Kitivo na Mombo.
January 02, 2014
WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUKUTWA NA BUNDUKI AINA YA SHORT GUN.
JESHI  la Polisi Mkoa wa Tanga linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kukutwa na bunduki moja aina ya short gun pamoja na sare za jeshi la polisi ambazo zilikutumika katika matukio ya kiuhalifu wilayani Korogwe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Constatine Massawe ameiambia TANGA RAHA BLOG  kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Desemba 28 mwaka jana majira ya saa nne usiku katika eneo la kambi ya Mkonge ya Gomba kata ya Makuyuni Tarafa ya Mombo.

Massawe alisema watuhumiwa hao walikuwa wakiitumia bunduki hiyo yenye namba za usajili 807028 ikiwa na risasi tatu na ganda moja ambapo ilikuwa katika harakata za kufanyia uhalifu katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Aliwataja majina ya watuhumiwa hao kuwa Zakaria Jelas(50),Moses Jonas(44),Selemani Hassani (21),Taratibu Hemed (74) na Hemed Taratibu(32) wote wakazi wa Makanya wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Aidha Kamanda Massawe alisema baada ya upekuzi watuhumiwa hao walikamatwa na sare mbili mali ya Jeshi la Polisi Tanzania  ambapo katika mahojiano na Jeshi hilo watuhumiwa hao walikiri kuhusika na matukio mbalimbali ya unyang’anyi na utekaji wa magari barabarani.

Katika tukio lengine,Jeshi la Polisi Mkoani Tanga linawashikilia wakazi watatu kwa kupatikana na mali inayodhaniwa kuwa ni mali wizi katika kuzuizi cha Polisi kilichopo Kijiji Kwasunga kata ya Makuyuni Tarafa ya Mombo wilayani Korogwe.

Kamanda Massawe alisema tukio hilo lilitokea Desemba 31 majira ya saa sita mchana baada ya watuhumiwa hao kufika kwenye kizuizi hicho wakiwa na pikipiki mbili za wizi ambazo ziliibiwa Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Jackson Aloyce (25), Leonard Fredick(21) wakiwa na pikipiki yenye namba za usajili T.274 CQV aina ya Boxer rangi ya blue na Karist Adolf (22)akiwa na pikipiki yenye namba T.162 CKL aina ya Boxer rangi nyeusi  ambapo watuhumiwa hao wote ni wakazi wa Dar es Salaam.

Hata hivyo alisema katika mahojiano na polisi watuhumiwa hao walikiri kutenda kosa hilo  maeneo ya Kariakoo mkoani Dar es Salaam na wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.
January 02, 2014

KAJALA MASANJA KUTOKA NA FILAM MPYA YA LAANA MWEZI FEBRUARI

MSANII wa filam za Kibongo nchini, Kajala Masanja, yupo katika hatu za mwisho za maandalizi ya kuanza kurekodi filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Laana', inayotarajia kukamilika mwezi Februari mwaka huu.

Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.com, Kajala alisema kuwa hivia sasa wapo katika maandalizi ya kuanza kurekodi filamu hiyo, itakayowashirikisha wakali kibao wa movie za Kibongo.

Aidha Filamu hiyo inayoanza kurekodiwa wiki ijayo chini ya Kampuni ya Sophia Records, inatarajia kukamilika na kuzinduliwa na kuingia sokoni mwishoni mwa mwezi wa pili.

Kajala aliwataja baadhi ya wasanii watakaoshiriki katika Filamu hiyo iliyotungwa na Leah Richard, kuwa ni Gabo, Lutwaza, Mama Kawele, ambapo Sterling wa Filam hiyo atakuwa ni Kajala, Gabo na Mama Kawele. 
Kajana akipozi kwa 'Snap' baada ya mazungumzo na Sufianimafoto.