MAPOKEZI YA YAYO LUTIMBA YALIKUWA YA AINA YAKE.

August 07, 2013
MENEJA WA KLABU YA COASTAL UNION YA TANGA,AKIDA MACHAI AKIWA NA MSHAMBULIAJI WA TIMU HIYO KUTOKA URA YAYO LUTIMBA MARA BAADA YA KUWASILI UWANJA WA NDEGE MKOANI TANGA.


Add caption

Na Oscar Assenga, Tanga.
MAPOKEZI wa Mshambuliaji Mpya wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga aliyetokea timu ya Mamlaka ya Mapato nchini Uganda (URA),Yayo Lutimba  kwenye uwanja wa Ndege Mkoani Tanga jana yalikuwa ya aina yake kutokana na kulakiwa na wingi wa mashabiki,viongozi na wanachama wa timu hiyo.

Mapokezi hayo yalianza saa mbili asubuhi na mchezaji huyo kutua saa nne katika uwanja wa ndege akiwa na Meneja wa timu hiyo Akida Machai ambaye alikuwa ameambatana naye kutoka nchini Uganda.

Awali aliripotiwa katika gazeti la Uganda New Vision la jana (juzi) liliripoti kuwa mchezaji huyo alisajiliwa na Yanga ya Tanzania.

Akizungumza katika mapokezi hayo,Katibu wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga,Kassim Eli Siagi alisema wameingia mkataba wa miaka miwili na mchezaji huyo ambaye ataitumia timu hiyo kuanza msimu mpya wa ligi kuu utakaoanza Agosti 24 mwaka huu.

El Siagi alisema kuwepo kwa mchezaji huyo katika kikosi kuteleta chachu na upinzani mkubwa na hivyo kuipa mafanikio timu hiyo.

Awali akizungumza mara baada ya kuwasili uwanjani hapo,Lutimba alihaidia kucheza kwa kujituma ili kuweza kuipa mafanikio timu hiyo pamoja na kushirikiana na wachezaji wenzake ili kutimiza malengo yao.