SERIKALI YA MOROCCO KUWEKEZA KATIKA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI.

SERIKALI YA MOROCCO KUWEKEZA KATIKA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI.

April 07, 2017
SS
Kulia Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina katika Mazungumzo kuhusina na suala la NIshati ya jua na Balozi wa Morocco Nchini Mhe. Benryane Abdelilah (katikati) kushoto ni Msaidizi wa Balozi Bw. Mrabet Yazane.
SS 1
Katikati Balozi wa Morocco Nchini Mhe. Benryane Abdelilah akimsalimia Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, alipomtembelea Ofisini kwake, Kulia ni Msaidi wa Balozi Bw. Mrabet Yazane.
SS 3
Kulia Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipena Mkono na Balozi wa Morocco nchini  Mhe. Benryane Abdelilah alipomtembelea ofisini kwake Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo.
SS 2
Kulia msaidizi wa Balozi wa Morocco Bw. . Mrabet Yazane akimsalimia Naibu Waziri Mpina, kulia kwake ni Mhe Balozi . Benryane Abdelilah. (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)
……………
NA ; Evelyn Mkokoi Dar es Salaam
Serikali ya Morocco iko tayari kushirikiana na Tanzania katika suala zima la kukabiliana na athari zitokanano na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwekeza kati mradi mkubwa wa Nishati ya jua.
Akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Mpina Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, Balozi wa Serikali ya Kifame ya Morocco Mhe. Benryane   Abdelilah  amesema kuwa, Morocco ipo tayari kuwekeza katika mradi mkubwa wa nishati ya Jua yani Solar energy, ili kuweza kusaidiana na Tanzania katika suala zima la kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi, kuongeza kipato katika sekta mbali mbali pamoja na kupunguza uzalishaji wa gas joto.
Pamoja na hilo, Balozi Abdelilah ameitaka idara, kuainisha maeneo ya vipau mbele kwa upande wa mazingira na kusema  kuwa, mradi huo mkubwa wa uzalishaji wa  Nishati ya jua utakaotekelezwa na kampuni kutoka Morocco ya Masen Campany Limited, utasaidia kuongeza matumizi ya nishati mbadala, pamoja na kujenga mahusiano mazuri baina ya nchi hizi mbili hasa katika sekta husika.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi hya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, alisema kabla ya uwekezaji wa mradi mkubwa wa aina hiyo, inatakiwa kufanyika kwa tathmini ya athari ya mazingira na kumuahaidi balozi kuwa watakapokuwa tayari zoezi hilo litafanyika kwa haraka , kwani uwekezaji huo utasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira utokanao na ukataji wa miti kwa matumizi ya nishati ya kupikia na mradi utawafikia wananchi wengi walio mbali na gridi ya taifa.
“kutokana na kukauka kwa vyanzo vingi vya maji kunakosababishwa na athari za mabadiliko ya tabianchi, mradi huu utakuwa mbadala wa tatizo hilo, huu ni mradi ambao utatusaidia, Alisisitiza Mpina.”
Balozi wa Morocco Mhe. Benryane Abdelilah alimtembelea Naibu Mpina Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Saalam ikiwa ni katika kufahamiana katika utendaji baada ya kufunguliwa kwa Balozi hiyo Nchini.

MD KAYOMBO AKABIDHIWA MADARASA MATATU SHULE YA MSINGI MSAKUZI

April 07, 2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwasisitiza walimu juu ya utunzwaji wa madarasa ya shule ya Msingi Msakuzi katika dhifa ya makabidhiano ya madarasa

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kuwasili shule ya Msingi Msakuzi katika dhifa ya makabidhiano ya madarasa
 Madarasa matatu ya shule ya Msingi Msakuzi yaliyokabidhiwa kwa MD Kayombo
Baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Ubungo walioshiriki kwenye dhifa ya makabidhiano ya madarasa ya shule ya Msingi Msakuzi

Na Nasri Bakari, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amekabidhiwa madarasa matatu yaliyokamilika na mkandarasi katika shule ya msingi Msakuzi.

Makabidhiano ya madarasa hayo ambapo ujenzi wake umegharimu shillingi millioni sitini na mbili (62 Mil) yamefanyika katika shule hiyo iliyopo katika Kata ya Mbezi Manispaa ya Ubungo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi Kayombo amesema kuwa amefurahi kuona ujenzi wa madarasa hayo umemalizika kwa wakati na kutoa ahadi mbalimbali katika shule hiyo.

"Kwanza napenda nichukue fursa hii kukupongeza mkandarasi kwa kumaliza ujenzi ndani ya muda tuliokubaliana kwa hakika umeonyesha ni jinsi gani unajali kazi yako" Alisema MD Kayombo.

MD Kayombo amesema kuwa mpaka kufikia kesho tarehe 06/04/2017 madawati 120 yanapaswa kufikishwa kwenye shule hiyo huku akisema kuwa kila darasa yanapaswa kukaa madawati arobaini(40) kila chumba katika vyumba vitatu vya madarasa alivyokabidhiwa.

Pia ameahidi kuweka tarazo katika vyumba viwili vya madarasa ya zamani ambapo pia ameahidi kutoa mifuko Hamsini ya Saruji kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya walimu na kuahidi kuhakikisha shule hiyo inakuwa ya mfano.

"Fedha hizi za kununua mifuko ya Saruji nitatoa kwenye mshahara wangu hivyo namsihi Mheahimiwa Diwani wa eneo hili naye aweze kuchangia ujenzi huu" Alisema MD Kayombo
 "Tunakushukuru sana Mkurugenzi kwa jitihada ulizozionesha katika shule hii kwa kipindi kifupi kwa kutununulia eneo la shillingi Millioni 35 na kutujengea madarasa matatu mungu akubariki sana" Alisema Bi Shahiri.

Mkurugenzi Kayombo amewasihi walimu wa shule hiyo kujitahidi kutunza mali za serikali zikiwemo madarasa, madawati na samani nyingine.

WADAU WAOMBA MIUNDOMBINU STENDI YA MABASI MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM

April 07, 2017
 Kijana akisukuma tolori huku akipita kwenye matope katika Stendi ya mabasi ya Mbagala Rangitatu jijini Dar es Salaam jana. Watumiaji wa stendi hiyo wameomba Manispaa ya Temeke kuwawekea miundombinu mizuri ili kuruhusu maji kupita katika kipindi hiki cha mvua.
 Muonekano wa stendi hiyo katika kipindi hiki cha mvua.
Wafanyabiashara wakiendelea na biashara zao kwenye stendi hiyo.

Na Dotto Mwaibale

WATUMIAJI wa Stendi ya Mabasi ya Mbagala Rangitatu jijini Dar es Salaam wameiomba Manispaa ya Temeke kuboresha miundombinu ya stendi hiyo katika kipindi hiki cha mvua ili kuondoa adha wanayokabiliana nayo ya kujaa maji.

Ombi hilo limetolewa Dar es Salaam jana na wafanyabiashara na madereva wanaotumia stendi hiyo wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto hiyo waliyonayo ya kujaa maji hasa katika kipndi hiki cha mvua za masika.

Mfanyabiashara ndogo ndogo katika stendi hiyo,  Afidh Abdallah alisema katika kipindi hiki cha mvua stendi hiyo imekuwa ikijaa maji na kusababisha matope hivyo kuwa kero kwao.

"Mvua ikinyesha hatuwezi kufanya biashara katika stendi hii tunashindwa kuzunguka kufuata wateja" alisema Abdallah.

Abdallah alisema kwa kutumia fedha wanazolipa ushuru kila siku manispaa hiyo inaweza kuwawekea hata molamu kwa kipindi hiki cha mvua ili kupunguza madimbwi ya maji wakati wakisubiri kujenga miundombinu ya kudumu.

Mama Lishe katika stendi hiyo Mwajabu Mohamed alisema maji yanapo jaa katika stendi hiyo wateja wao wamekuwa wakishindwa kufika kupata chakula kutoka maeneo mengine kwa kuhofia madimbwi na matope yanayokuwepo.

Said Khatibu ambaye ni dereva wa basi la Manshallah linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na mikoa ya kusini alisema wakati huu wa mvua changamoto kubwa inayokuwepo eneo hilo ni kushindwa kupata nafasi ya kupakia na kushusha abiria kutokana na maji yanayojaa.


MD KAYOMBO ATEMBELEA OFISI YA MTENDAJI KATA YA UBUNGO

April 07, 2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Ofisi Mtendaji wa Kata ya Ubungo, kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Kata Ya Ubungo Ndg Isihaka Waziri
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa maelekezo kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ubungo kuhusu namna ya kuyatoa marobota yaliyobaki baada ya kuwagawia wananchi vyandarua
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiongea na baadhi ya watumishi aliowakuta ofisini
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua eneo La Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Ubungo Mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo April 6, 2017 amefanya ziara katika Ofisi ya Ofisa Mtendaji Kata ya Ubungo ili kujionea utendaji kazi katika Ofisi hiyo.

Akizungumza na baadhi ya watumishi Mara baada ya kukagua eneo la Ofisi hiyo MD Kayombo Alisema kuwa amefanya ziara hiyo ya kushtukiza ili kujionea hali ya ufanisi wa kazi na kubaini kama kuna watumishi ambao hawafanyi kazi ya kuwatumikia wananchi kwa weledi na badala yake wanafika ofisini Asubuhi kwa ajili ya kusaini na hatimaye wanaondoka.

"Watumishi wengi hutumia muda mwingi kufanya kazi zao badala ya kufanya kazi za utumishi wa wananchi, Japo nawapongeza katika Ofisi hii mmeendelea kuwa waumini wazuri wa kazi na ufanisi wenu unawasaidia wananchi kuzidi kuiamini serikali yao" Alisema MD Kayombo

Akiwa Ofisini hapo MD Kayombo ameagiza Marobota ya vyandarua zilizobaki ambazo zilitolewa kwa ajili ya kuwagawia wananchi kutotolewa hovyo ama kuhamishwa badala yake zitolewe kwa utaratibu mahususi utakaoelekezwa na Ofisi ya Mkurugenzi.

Robota hizo zipo 34 katika Ofisi hiyo ya Mtendaji wa Kata ya Ubungo zimesalia nyingi kutokana na wananchi wengi kutojitokeza kuzichukua kutokana na sababu mbalimbali.

MD Kayombo pia ameelezea mpango kabambe wa Manispaa ya Ubungo juu ya Ofisi hiyo ya Mtendaji kubomolewa na hatimaye kuwa na uwekezaji mkubwa ambao utaongeza wigo wa ukusanyaji mapato ya Manispaa hiyo.
DK.MENGI ASISITIZA WATANZANIA KUONDOA UOGA

DK.MENGI ASISITIZA WATANZANIA KUONDOA UOGA

April 07, 2017
WATANZANIA wametakiwa kuingia katika ubia kama wajasiriamali badala ya kufikiria kwamba wao ni maskini na hawana fedha za kuingia ubia na makampuni ya nje. kauli hiyo imetolewa katika wiki ya Ufaransa ambapo makampuni 50 yanashiriki kuonesha uwezo wa utayari wa ushiriki wao katika ujenzi wa uchumi wa kati wa Tanzania unaotegemea viwanda. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi ambaye aliwasilisha haja na matamanio ya Watanzania kwenye sekta binafsi katika kushirikiana na wawekezaji kutoka Ufaransa, alisema watanzania wamekuwa waoga kuomba ubia wakidhani kwamba hawana kitu cha kutoa wakati wao wana akili na rasilimali. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi akizungumza katika kilele cha wiki ya Ufaransa ambapo wawekezaji kutoka makampuni 50 ya Ufaransa walishiriki katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliombatana na maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wafaransa. (Picha zote Thebeauty.co.tz)[/caption] Kauli hiyo ambayo aliisema kwenye mazungumzo na wawekezaji hao wa Ufaransa wakati akielezea utayari wa sekta binafsi kushirikiana na Wafaransa alisema kwamba watanzania wengi hawajiamini na kwamba wakati umefika kwa Watanzania kujitambua kwa kuwa wao (wafaransa) walijaribu wakaweza kwani kama sisi walikuwa na vitu vya ziada katika uthubutu wao. Katika mazungumzo yake Dk. Mengi akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye alisema kwamba sekta binafsi ambayo ina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi inawezekana kwa watanzania kuthubutu. Aidha alisema uwapo wa Wafaransa utaweza kusaidia kupandisha uwezo, teknolojia na utaalamu hali ambayo inawezekana kupitia uwapo wa shughuli za ubia kati ya wawekezaji wa Kitanzania na Wafaransa. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye (kulia) akizungumza wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano huo wa kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.[/caption] Alisema baada ya sekta ya umma kuweka miundombinu mahala pake, ni kazi ya sekta binafsi kutumia miundombinu hiyo kubuni na kuwekeza katika viwanda na kuzalisha bidhaa mbalimbali. Dk.Mengi alisema kwamba TPSF inaamini kwamba sekta binafsi ni ufunguo katika kuongoza na kuimarisha uchumi wa Tanzania ambao unatakiwa kuwa endelevu kama awamu ya tano inavyotaka. Aliwaambia wafanyabiashara wa Ufaransa kwamba Tanzania ina kila kitu wanachohitaji na kwamba makampuni makubwa ya Ufaransa kama Airbus, Renault, Alstrom, Systra wana mtandao mpana duniani wa kufanyabiashara na wawawekezaji wadogo duniani hivyo wanaweza kufanya hivyo hapa nchini. Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira akiuliza swali kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.[/caption] Alisema changamoto za utaalamu zitaondoka kwa ushirikiano na uwezeshaji. Aliwataka wawekezaji hao wa Kifaransa kwamba Tanzania kwa sasa ndio nchi ya uwekezaji na kusema changamoto zilizopo ni fursa za uwekezaji nchini Tanzania hasa katika nishati ambapo taifa hili litahitaji megawati 10,000 ifikapo mwaka 2040. Aidha alisema anaamini kwamba wengi wa watanzania wapo tayari kushirikiana na Ufaransa katika kuhakikisha kwamba wanaingia ubia katika biashara halali na yenye kusaidia pande zote. Naye Simbeye alisema anatamani kuona kwamba wafaransa wanawekeza kiwanda cha magari nchini kwani inawezekana kutokana na mabadiliko makubwa ya mfumo wa uwekezaji kwa sasa. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo katika mkutano huo kwenye kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa. Mmoja kati ya wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa akiuliza swali kwa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) katika kilele cha mkutano wa wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi, Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira katika mkutano wa kilele cha wiki ya Ufaransa uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa. Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (wa pili kulia) pamoja na baadhi ya viongozi wa wizara walioshiriki mkutano huo wa kilele cha wiki ya Ufaransa iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa
UWT YAWAPONGEZA WABUNGE KWA UCHAGUZI, YALAANI KAULI ZA MHE MBOWE

UWT YAWAPONGEZA WABUNGE KWA UCHAGUZI, YALAANI KAULI ZA MHE MBOWE

April 07, 2017
Inline image 1

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:

Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) unatoa pongezi kwa Wabunge wa Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia haki yao  ya kidemokrasia, kikatiba na kikanuni kufanikisha uchaguzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki uliofanyika tarehe 4/4/2017 bungeni mjini Dodoma.

Pia unawapongeza Wabunge waliochaguliwa kuiwakilisha nchi yetu katika Bunge la Afrika Mashariki, tunawataka kuwa wazalendo, waadilifu, wachapakazi
na wenye kutanguliza maslahi ya nchi yetu Tanzania kwanza.

Pia, UWT imeridhishwa na hatua za mchakato wa uchaguzi huo ndani ya Bunge na inapongeza demokrasia pana, komavu na shirikishi iliyooneshwa na wabunge kwa kupiga kura ya HAPANA kwa wagombea waliotokana na CHADEMA kwa sababu uteuzi wao haukuzingatia misingi ya demokrasia, uwakilishi wa Kitaifa wala jinsia.

Uteuzi uliofanywa na CHADEMA hata baada ya kushauriwa, unadhihirisha dharau kubwa na kutothamini mchango wa Wanawake wa Tanzania katika maendeleo ya nchi yetu.


Bunge na Wabunge lazima wawe mstari wa mbele katika juhudi za kuimarisha demokrasia yetu kama Taifa na ndani ya vyama vya siasa, kamwe Bunge lisiruhusu kutumika kama “rubber stamp” kama ambavyo CHADEMA walipanga kwa kuteua wagombea wawili pekee na kwa kufanya hivyo tayari waliamua nani awe mbunge na kulinyima Bunge fursa na uhuru wa kuchagua miongoni
mwa wagombea.

Tigo waungana na Tecno kuzindua simu mpya ya Tecno Camon CX

April 07, 2017
Meneja mawasiliano Tigo, Woinde Shisael akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa simu mpya ya Tecno Camon CX mapema jana katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
Meneja mkuu wa Tecno Tanzania Daniel Xu akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa simu mpya ya Tecno Camon Cx mapema jana katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.





Mkuu wa kitengo cha masoko Tigo, Olivier Prentout akipiga picha(selfie photo) na wakaribisha wageni wa hafla hiyo(ushers)
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael na Mkuu wa Idara ya uendeshaji wa Tecno, Anuj Khosla wakipiga  picha ya pamoja kuashiria uzinduzi wa simu mpya ya Tecno Camon CX mapema jana katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.

Mkuu wa kitengo cha masoko Tigo, Olivier Prentout akipiga picha(selfie photo) na wakaribisha wageni wa hafla hiyo(ushers)
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael na Mkuu wa Idara ya uendeshaji wa Tecno, Anuj Khosla wakipiga  picha ya pamoja kuashiria uzinduzi wa simu mpya ya Tecno Camon CX 
mapema jana katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.

Selfie zikiendelea ukumbini mara baada ya uzinduzi wa simu mpya ya Tecno Camon Cx



Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akipiga Selfie na wadau  mara ya uzinduzi wa Simu hiyo mapema jana katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tigo, Tecno na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo mapema jana katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.

HAYA NI MAENEO 5 YANAYOKUMBWA NA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM KILA MWAKA

April 07, 2017
Na Jumia Travel Tanzania

Kama sio mwenyeji wa jiji la Dar es Salaam basi ni vema ukauliza kwanza kabla ya kuhamia sehemu na kuanza kuishi. Usipofanya hivyo kwenye kipindi cha mvua kama hiki usishangae unaamka ukiwa umezungukwa na maji kama sio kuelea kabisa.

Kuwa na vipindi virefu vya jua na joto kali haimaanishi kuwa maeneo yote ya Dar es Salaam hubakia hivyo mwaka mzima. Jumia Travel imekusogezea maeneo haya 5 ambayo miaka nenda rudi lazima yakumbwe na mafuriko.