RC MOROGORO AONGOZA MAMIA KUMZIKA MKE WA MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO KUSINI.

July 27, 2014


Mkuu wa mkoa akimpeleka Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh  Innocent Kalogeris  kupokea mwili wa mpendwa mke wake,kulia ni dada wa mbunge huyo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Dr Joel Bendera Leo amewaongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Morogoro kumzika Mke wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, Mh lnocenti Kalogeris watu mbali mbali wakiwemo wabunge,wakuu wa mikoa wa staafu na watu mashuhuri wamefurika nyumbani kwa mbunge huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro CCM

 Marehemu Elizabeth Kapoloma enzi za Uhai wake , Bi,Elizabeth Kapoloma alifariki Alhamisi Kwa Ugonjwa Moyo.
 Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani kwake kwajili ya Heshima za Mwisho na Ibada kabla ya Mazishi leo
  Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh Dk Joel Bendera akimbembeleza Mume wa marehemu Mhe lnocent Kalogeris
MATUKIO NA VIJANA

MAMA KIKWETE AHIMIZA WANAFUNZI WA KIKE WA VYUO VYA UALIMU KUVAA MAVAZI YA HESHIMA

July 27, 2014
Na Anna Nkinda - Maelezo,  Nachingwea

Wanafunzi wa kike wa vyuo vya ualimu nchini wametakiwa kuvaa mavazi  nadhifu  yanayoendana na maadili ya kazi yao  ili wanafunzi na jamii inayowazunguka ijifunze  kutoka kwao kwani wao ni kioo cha jamii.

Mwito huo umetolewa  hivi karibuni  na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na baadhi ya wanafunzi wa kike  wa chuo cha Ualimu Nachingwea mara  baada ya kumalizika kwa futari aliyoiandaa kwa ajili ya viongozi wa wilaya iliyofanyika  chuoni hapo. 

Mama Kikwete ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa kupitia wilaya ya Lindi mjini alisema siyo jambo jema kwa mwalimu kuvaa mavazi yanayoonyesha sehemu za miili yao ikiwemo kata mikono, nguo zinazobana na sketi fupi  kwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na haiba ya ualimu. 

Alisema, “Sikuhizi kuna baadhi ya watu  wanavaa mavazi yasiyoendana  na utamaduni wa mtanzania,  nyinyi kama walimu ambao ni kioo cha jamii na mnawafundisha  wanafunzi madarasani msifanye hivyo  kwa kufanya hivyo watoto  wataiga na kufikiria  kuwa kuvaa mavazi hayo ni sawa”.

Mama Kikwete pia  aliwataka wanafunzi hao kutokuchagua  maeneo ya kwenda kufanya kazi pindi wamalizapo masomo yao na kupangiwa vituo vipya vya kazi kwani kazi ya ualimu ni wito na kama mtu  hakuipenda kazi hiyo basi angechagua fani nyingine za kusoma.

“Baadhi ya walimu wamekuwa wakikataa kwenda kufanya kazi katika maeneo ya vijijini, na wengine wakipangiwa vituo vya mbali na mjini wanaogopa na kudiriki hata kuacha kazi,  kama ni hivyo kwa nini ulipoteza fedha  na muda wako kusomea ualimu?” , aliuliza Mama Kikwete.

MNEC huyo alimalizia kwa kuwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kujiepusha na mahusiano ya kimapenzi wawapo masomoni kitendo ambacho kitawasaidia  kumaliza masomo yao salama na kurudi nyumbani bila ya kufukuzwa chuo kwa ajili ya kupata ujauzito.

Mama Kikwete ambaye kitaaluma ni mwalimu miaka ya nyuma alisoma chuo cha ualimu Nachingwea na juzi akiwa chuoni hapo alitembelea Bweni la wasichana la Kawawa  ambalo ndilo alilokuwa analala wakati akiwa mwanafunzi wa chuo hicho.

SERENGETI BOYS KWENDA AFRIKA KUSINI KESHO

July 27, 2014

Msafara wa watu 25 wa kikosi cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) unaondoka kesho (Julai 28 mwaka huu) kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos).
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili itachezwa Jumamosi, Agosti 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto, Johannesburg kuanzia saa 9 kamili mchana kwa saa za Afrika Kusini.
Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyofanyika Julai 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam. Mshindi atacheza raundi ya mwisho ya michuano hiyo ya Afrika na mshindi wa mechi kati ya Misri na Congo Brazzaville.
Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitafanyika mwakani nchini Niger.
Wachezaji wanaounda kikosi cha Serengeti Boys katika msafara huo utakaoondoka saa 2 usiku kwa ndege ya Fastjet ni Abdallah Jumanne Shimba, Abdulrasul Tahil Bitebo, Abutwalibu Hamidu Msheri, Adolf Mtsigwa Bitegeko, Ally Aziz Mnasi, Ally Shaban Mabuyu na Athanas Enemias Mdamu.
Wengine ni Badru Haji Othman, Baraka Yusuph Baraka, Issa Backy Athuman, Juma Ally Yusuph, Kelvin Longnus Faru, Martin Kiggi Luseke, Metacha Boniface Mnata, Mohamed Mussa Abdallah, Omary Ame Omary, Omary Natalis Wayne, Prospal Alloyce Mushin na Seif Said Seif.
Benchi la Ufundi linaongozwa na Kocha Mkuu Hababuu Ally Omary akisaidiwa na Stewart John Hall (Mshauri wa Ufundi), Peter Manyika (Kocha wa makipa), Richard Yomba (Daktari), na Edward Venance (Mtunza vifaa).
 
Msafara wa timu hiyo itakayorejea nyumbani Agosti 4 mwaka huu unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Khalid Mohamed Abdallah.
DC MUHEZA AAHIDI KUSIMAMIA UPIMAJI ARDHI WANANCHI WAPATE MAENEO

DC MUHEZA AAHIDI KUSIMAMIA UPIMAJI ARDHI WANANCHI WAPATE MAENEO

July 27, 2014


Mkuu wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Subila Mgalu
 
Mkuu wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Subila Mgalu, ameahidi kusimamia upimaji ardhi wa shamba la mkonge Kibaranga ili wananchi wapate ardhi ya kulima.
 
Alitoa ahadi hiyo jana wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Kibaranga, baada ya kutokea mgogoro kati ya wananchi na maafisa ardhi waliyopewa kazi ya kupima shamba hilo.
 
Alisema kuwa kazi ya kupima shamba hilo imeanza lakini kuna baadhi ya watu wanaendeleza mgogoro kati ya wananchi na serikali.
 
Hatua hiyo inafuatia maafisa ardhi wilaya ya Muheza kuanza kupima shamba hilo ili wananchi wapatiwe maeneo ya kilimo.
 
Alisema kuwa baadhi ya watu  wanadanganya wananchi hao kuwa tayari maafisa ardhi wanagawa mashamba kwa kupewa kitu kidogo, kitu ambacho si cha kweli.  Alisema amesikitishwa na kitendo cha  wananchi hao kufukuza maafisa ardhi kwa kutumia mapanga wakati mchakato huo ukiwa unaendelea vizuri baada ya agizo la Rais Jakaya Kikwete la kukubali shamba hilo wapewe wananchi.
 
Alisema kuwa kwa sasa wanafanyakazi hiyo ya upimaji kwa shida kwani inatakiwa zaidi ya Sh. Milioni 100 lakini wanapima kwa Shilingi Milioni nane tu ambazo wamepewa na wafadhili kufanya kazi hiyo.
 
Mgalu alisema kuwa yupo tayari kufa ili kuhakikisha shamba hilo linapimwa ili wananchi wapewe ardhi hiyo.
 
Aliwataka wananchi kuwa wavumilivu ili zoezi hilo liende vizuri ili wananchi wapate ardhi.
 
Kwa upande wake Afisa ardhi ambae alikuwa anaendesha zoezi la upimaji shamba hilo, Daniel Mkwizu, alisema kuwa zoezi lilikuwa linaendelea vizuri lakini wananchi waliwafukuza  na mapanga na kulisitisha.
CHANZO: NIPASHE

WASHIRIKI WA WARSHA YA MASHIRIKIANO BAINA YA TANAPA NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI.

July 27, 2014


Bwawa la Viboko katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Kilimanjaro Ramadhan Ng'anzi akichukua Taswira katika bwawa la Viboko.

Baadhi ya Washiriki wa Warsha wakifurahia Mandhari tofauti katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Sehemu ya Bwawa la Viboko lililopo katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Baadhi ya Wanahabari wapata Taswira katika Bwawa la Viboko katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ,Datomax Selanyika akitoa taarifa ya Hifadhi hiyo kwa  Washiriki wa Warsha ya Mashirikiano baina ya TANAPA na Vyombo vya Ulinzi na Usalama walipotembelea Hifadhi hiyo.
Baadhi ya Washiriki wakifuatlia kwa makini taarifa ya Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ,Datomax Selanyika aliyotoa wakati  Washiriki wa Warsha ya Mashirikiano baina ya TANAPA na Vyombo vya Ulinzi na Usalama walipotembelea Hifadhi hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo akitoa neno la shukurani mara baada ya Washiriki wa Warsha ya Mashirikiano baina ya TANAPA na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliyeko Morogoro.
MATOKEO YA TUZO ZA AFRIMMA 2014 ALIZOKUA ANAWANIA DIAMOND MAREKANI.

MATOKEO YA TUZO ZA AFRIMMA 2014 ALIZOKUA ANAWANIA DIAMOND MAREKANI.

July 27, 2014

Screen Shot 2014-07-27 at 9.43.50 AMZinaitwa African Muzik Magazine Awards ambapo za mwaka huu 2014 zimetolewa huko Eisemann Center Texas Marekani na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Diamond wa Tanzania ambaye pia alikua mmoja wa wanaowania tuzo hizo


Habari njema za  ushindi wote huu ni kwa mujibu wa meneja wake Babu Tale ambaye nae kahudhuria tuzo hizi Marekani ala ametuma ujumbe mfupi wa simu  akisema Diamond ameshinda tuzo mbili moja ya Msanii bora wa Afrika Mashariki na nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana ambao ni ‘number one rmx’ alioufanya na Davido wa Nigeria.

*RAIS KIKWETE ATUNUKU WAHITIMU WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI KATIKA MAHAFALI YA KOZI YA PILI JANA JUMAMOSI

July 27, 2014

 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kanali James Ruzibiza Stashahada ya Usalama na Stratejia (Diploma in Security and Strategic Studies) katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Kanali Ruzibiza, ambaye anatokea Rwanda, ni mmoja wa washiriki tisa wa kozi waliotoka nchi za nje. Washiriki wengine kutoka nje y nchi walitoka Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Uganda, zambia na Zimbabwe. Jumla ya wahitimu 30, wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali. 
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Luteni Jenerali C.L. Makakala Shahada ya Uzamili ya Falsafa ya Usalama na Stratejia katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Luteni jenerali Makakala, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi wa kwanza, amekuwa mtunukiwa wa kwanza wa Shahada hiyo hapo chuoni.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia baada ya kutunuku shahada katika  mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.Jumla ya wahitimu 30 wamehudhuria kozi hiyo wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali. Washiriki wengine tisa wametoka  nchi za nje ambazo ni Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Rwanda Uganda, Zambia na Zimbabwe.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaambia kuwa sasa ni zamu yao kupiga picha ya kumbukumbu bila yeye wahitimu wa Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.
Picha ya Pamoja.PICHA NA IKULU

*MWIGULU NCHEMBA ALIVYOLITEKA JIJI LA MWANZA

July 27, 2014

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, akiwasili kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, kuhutubia mkutano wa hadhara, uliofanyika leo jioni. Katika Mkutano huo, Mwigulu amezungumzia mambo mbalimbali ikiwemo, umuhimu wa wanasiasa na Watanzania kwa jumla kutolifanyia mzaha suala la mchakato wa Katiba mpya akivitaka vyama vya upinzani kuthamini zaidi vikao vya Bunge la Katiba ili kukamilisha mchakato huo kwa mazungumzo na mjadala uliojaa hekima badala ya kwenda mitaani kusumbua wananchi.
 Mwigulu akisalimia wananchi kwenye Uwanja huo.
 Mwigulu akuhutubia wananchi kwenye Viwanja hivyo vya Furahisha jijini Mwanza.
Wananchi kwenye mkutano huo.Picha zote na Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara.

WAZIRI MKUU MHE MIZENGO PINDA AANDAA FUTARI NYUMBANI KWAKE DAR ES SALAAM

July 27, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum alipowasili kwenye makaazi ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda (nyuma yao) Oysterbay jijini Dar es salaam kwa ajili ya Futari leo Jumamosi Julai 26, 2013. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na wa pili kulia ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova
 Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakijumuika na waumini wengine katika Swala ya Magharibi katika  makaazi ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda Oysterbay jijini Dar es salaam alikoandaa Futari leo Jumamosi Julai 26, 2013
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongea na baadhi ya waalikwa kwenye futari aliyoandaa, wakiwemo waigizaji Mpoki wa Ze Komedy, Stephen JB, na watangazaji wa redio
 Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Ndg Ramadhani Madabida wakipakua futari
 Mawaziri wakuu Wastaafu Mzee Cleopa Msuya na Jaji Joseph Sinde Warioba wakiwa wameketi pamoja na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu (kulia, mwenye baraghashia) na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio
 
 
 Wazee Mashuhuri wa mkoa wa Dar es salaam mezani pao
 Mufti wa Tanzania Sheikh Shaaban Issa Simba akiongoza dua baada ya futari
 Rais Kikwete akiagana na mmoja wa wazee mashuhuri wa Mkowa wa Dar es salaam

 Rais Kikwete akisalimiana na mchora katuni maarufu Ali Masoud ‘Kipanya’ huku Mrisho Mpoto akisubiri zamu yake

 
 Rais Kikwete akiongea na Mwana FA



Mkono wa mwisho ni wa mtoto huyu aliyepata bahati ya kuagana na Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali baada ya futari

TAMKO LA JUKWAA KUHUSU BUNGE MAALUM LA KATIBA LINALOANZA DODOMA AGOSTI 5, 2014

July 27, 2014

 Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitoa tamko kuhusu Bunge la Katiba litakaloanza Agosti 5, 2014 ambapo walishauri Bunge hilo likae wiki mbili badala ya miezi miwili kama ilivyopangwa ili kupunguza matumizi makubwa ya fedha za Umma. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Kamati na Uongozi Jukata Omar Ali Omar,  Meneja Habari na Mawasiliano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Kenny Ngomuo, Makamu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda na  Mratibu wa Jukata, Diana Kidara.
 Makamu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda, akisoma tamko hilo.
 Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini.