WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA 'BLACK FRIDAY

November 24, 2016
Watanzania watakiwa kuchangamkia ‘Black Friday’

Na Dotto Mwaibale

TUNAPOELEKEA mwisho wa mwaka wa 2016 huku sikukuu za krisimasi na Mwaka Mpya zikiwa zinakaribia, Watanzania wametakiwa kuchangamkia ofa za ‘Black Friday’ inayolenga kupunguza pakubwa bei ya kukaa kwenye hoteli nchini.

Rai hiyo imetolewa na kampuni inayotoa huduma za hoteli mtandaoni ya Jumia Travel ambapo inamuwezesha mtu kujionea hoteli mbalimbali, upatikanaji wa huduma, bei, mahali zilipo na pia fursa ya kuweza kulipia kabisa.

Mtandao huo umeingia makubaliano na hoteli kadhaa za Tanzania bara na visiwani Zanzibar katika kuhakikisha wateja wanaonja utamu wa huduma zao kwa punguzo kubwa ambalo limekuwa likiendelea kwa wiki mbili sasa na litafikia kilele mnamo Ijumaa tarehe 25 Novemba mwaka huu.

Akifafanua zaidi kuhusu siku hii ya Black Friday, Meneja Mkaazi wa Jumia Travel Tanzania Bi. Fatema Dharsee amesema kuwa hoteli ambazo zimetoa ofa hiyo ni pamoja na Africa House na Jaffreji House & Spa zilizoko katika Kisiwani Zanzibar pamoja na White Sands na Landmark Beach Resort & Conference Center zilizopo Tanzania Bara.

“Ninafahamu kuwa wengi wetu huwa tunatamani kutumia muda huu wa mapumziko katika sehemu nzuri yenye starehe zote tofauti na mazingira tuliyoyazoea. Hilo linawezakana kwani kupitia ushirikiano na hoteli tunazofanyakazi nazo tunawatangazia ofa ya punguzo kubwa la kwenda kujivinjari katika hoteli za nyota nne ambayo imeanza wiki iliyopita Novemba 14 na itadumu mpaka Novemba 25,” alifafanua.

“Kupitia ofa hii unaweza kuitumia pamoja na mpendwa wako, familia, ndugu, jamaa au marafiki. Kwa mfano, White Sands wanayo michezo ya kwenye maji, kituo cha kupiga mbizi chini ya maji na safari ya boti kwenda kisiwani. Tunawasihi watanzania kutumia fursa kama hizi ili kuweza kujionea huduma nzuri na hadhi ilizonazo hoteli za hapa nyumbani. Itakuwa ni jambo zuri sisi kwanza kuwa mabalozi wa vitu vyetu wenyewe na sio wageni wanaokuja kutembelea nchini.” Alimalizia Meneja huyo Mkazi wa Jumia Travel Tanzania

Kutokana na maendeleo ya teknolojia Jumia Travel (travel.jumia.com) inamuwezesha mteja kufanya huduma zote za hoteli kupitia programu inayoweza kupatikana kwenye kompyuta, tabiti na simu. Hivyo basi kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa njia rahisi na uhakika bila ya kumlazimu mtu mpaka kutembelea hoteli anayoitaka moja kwa moja.

Kuhusu Jumia Travel

Jumia Travel (travel.jumia.com) ni kampuni nambari moja unaongoza wa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao barani Afrika ambao humruhusu mteja kupata bei nzuri za hoteli zaidi ya 25,000 kwa nchi za Afrika na zaidi ya hoteli 200,000 duniani kote.

Dhumuni letu ni kuleta kila aina ya huduma za malazi kwenye mfumo wa mtandao na kutengeneza njia rahisi na nafuu zaidi kwa wateja kuzilipia.

Hapa Jumia Travel, tunao mamia ya wataalamu katika masuala ya utalii ambao huwasiliana na wateja wetu. Ofisi zetu zinapatikana katika miji na nchi zifuatazo Lagos (Naijeria), Accra (Ghana), Dakar (Senegali), Abidjan (Ivory Coast), Algiers (Algeria), Douala (Cameroon), Kampala (Uganda), Dar es Salaam (Tanzania), Nairobi (Kenya), Addis Ababa (Ethiopia), Porto (Ureno) na Paris (Ufaransa).

Kabla ya mwezi Juni 2016, Jumia Travel ilikuwa ikijulikana kama Jovago. Ilianzishwa mnamo mwaka 2013 na Jumia huku ikiendeshwa kwa ushirikiano wa karibu na makampuni kama vile MTN, Rocket Internet, Millicom, Orange na Axa.

BARAZA LA WAHITIMU WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE LAKUTANA KUJADILI MUSTAKABARI WA CHUO

November 24, 2016

 Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila (kushoto), akihutubia wakati akifungua Baraza la Wahitimu wa chuo hicho, Dar es Salaam leo.
 Katibu wa Baraza la Wahitimu wa chuo hicho, Jumanne Muruga (kushoto), akihutubia katika baraza hilo.
 Mwenyekiti wa Baraza hilo, Simon Simalenga (katikati), akiongoza baraza hilo. Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila na kushoto ni Katibu wa baraza hilo, Jumanne Muruga.

 Diwani wa Kata ya Mbezi, Humphrey Sambo ambaye aliwahi kuwa Rais wa Serikali ya chuo hicho (MASO), akichokoza mada katika baraza hilo.
 Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
 Meza kuu ikimba wimbo wa taifa.
 Wanachuo wakiimba wimbo wa taifa.
 Taswira ya mkutano huo.
 Baraza likiendelea.
Majadiliano yakiendelea.
 Wanafunzi wakisikiliza mada kwa makini.
 Taswira ya ukumbi.
Mwanahabari Suleiman Msuya ambaye ni muhitimu wa chuo hicho, akichangia mada katika baraza hilo.
Wanafunzi wakisikiliza mijadala.
Vyeti vikitolewa
Picha ya pamoja.



Na Dotto Mwaibale


MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila amesema chuo hicho kipo katika mpango wa kujenga miundombinu mizuri ili wanafunzi wapate elimu katika mazingira bora.


Profesa Mwakalila ameyasema hayo wakati akifunga Baraza la Wahitimu wa chuo hicho lililofanyika chuoni hapo Dar es Salaam leo kutokana na maombi ya wahitimu wa chuo hicho wanaounda baraza hilo kulalamikia miundombinu katika shule hiyo.


"Ni kweli tunachangamoto kubwa ya miundombinu hapa chuoni lakini tupo katika mpango wa kuijenga kwani tayari Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wameanza kuandaa michoro ya majengo na fedha tunategemea kupata kutoka kwa mifuko ya hifadhi ya jamii kwa ajili ya ujenzi na sasa tupo katika mazungumzo nao" alisema Mwakalila.


Alisema miundombinu  hasa madarasa na hosteli ni changamoto kubwa kwani kutokana na sifa ya chuo hicho wanafunzi wamekuwa wakiongezeka kila mwaka hivyo kusababisha changamoto hiyo ambayoitakwisha muda si mrefu.


Akizungumzia kuhusu la Baraza la Wahitimu alisema lilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya chuo na lipo chini yake na lengo kubwa ni kupata na kutunza orodha ya wahitimu pamoja na anuani zao, kuandaa mikutano na makongamano yenye mada zinazohusu maendeleo ya chuo pamoja na serikali na jamii kwa ujumla na kutafuta vyanzo vya mapato ya kusaidia maendeleo ya chuo.


Katibu wa baraza hilo John Muruga alisema kamati yao imebaini kuwa udahili wa wanafunzi umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo kwa mwaka 2016/ 2017 ni wanafunzi 2363 walidailiwa wanafunzi 553 wakiwa wa programu ya Astashahada, wanafunzi 471 wa programu ya Stashahada na wanafunzi 1339 wakiwa ni wa programu ya shahada ya kwanza.


"Idadi hii ya udahili inajumuisha pia wanafunzi waliodahiliwa katika Tawi la chuo cha Zanzibar ambao ni 354 " alisema Muruga.


(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)



MKURUGENZI WA ILEJE AWADHIBITI WAKWEPA KODI

November 24, 2016
 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ileje Haji Mnasi akiwa kwenye eneo husika la kukagua wakwepa kodi.
 
Hawa ni baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wialaya ya Ileje wakifutalia jambo lililokuwa likiongelewa na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ileje haji mnasi
Hili ni moja ya malori yaliyokuwa yakikwepa ushuru kwa kufanya biashara ya kushusha mizigo vichochoroni.
Hili ni moja kati ya gari linalobeba milunda bila kulipia ushuru na mkurugenzi Haji Mnasi kufanikiwa kulikamata wakati wa zoezi maalumu la kuwatafuta wakwepa kodi waliobobea kuikimbia serikali kulipa kodi

Na Daniel Mwambene, Songwe                           

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje wampongeza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Haji Mnasi kwa kukuza uchumi wa wilaya hiyo na kufanikiwa kuwadhibiti wafanyabiashara waliokuwa wakikwepa kodi.

Pongezi hizo zilitolewa na madiwani hivi karibuni wakati wa kikao cha Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.

Akizungumza na blog hii diwani wa kata ya Itumba Mohamed Mwala alisema kuwa wanatambua juhudi zilizofanywa na Mkurugenzi Haj Mnasi na wafanyakazi wa halmashauri kukusanya ushuru maeneo mbalimbali na kufanikiwa kuyakamata magari aina ya maroli yaliyokuwa yakikwepa ushuru.

Naye diwani wa kata ya Ibaba Tata Kibona alisema kuwa mkurugenzi na timu yake  wamekuwa wakitembea usiku kuwatafuta wakwepa kodi hasa kwenye kata yake ambapo mara kadhaa mkurugenzi huyo amekuwa akionekana nyakati za usiku.


"mimi sijawahi ona mkurugenzi kama huyu maana anaacha usingizi wake unamkuta kwenye kata nyakati za usiku akipambana nao wakwepa kodi na amefanikiwa kuwadhibiti wafanyabiashara wote wakwepa kodi na ndio maana sasa mapato yameanza kukua kwa kasi katika wilaya yetu"alisema Kibona 

Akielezea mafanikio hayo Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Godfrey Zimubiha alisema kuwa mafanikio hayo yanachangiwa na wadau mbalimbali ukiwemo uongozi ngazi ya wilaya,kata vijiji na wananchi kwa ujumla.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmahauri hiyo Haji Mnasi aliwapongeza wananchi,watumishi wa ngazi zote za wilaya na madiwani wote kwa kufanya kazi kwa weledi wao na kufanikisha malengo ya wilaya hiyo hata hivyo alimshukuru mkuu wa wilaya ya Ileje Joseph Mkude  kwa ushirikiano anaoutoa

 “Nashukuru mungu sasa madiwani wa wilaya yangu wameacha siasa na wanafanya kazi kwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuri kwa kile anachokifanya kuleta maendeleo ya nchi yetu na ndio maana unaona hata huku kwetu pato letu la wilaya limekuwa”alisema Mnasi

Aidha Mh Mnasi aliyataja baadhi ya maeneo yaliyokuwa korofi wakati wa ulipaji wa ushuru ni kama  kata ya Ngulilo ambako kulikuwa na utoroshaji wa mazao ya mbao pamoja na kata ya Mbebe na Isongole ambako nako kulikuwa na utoroshaji wa nafaka.

Mnasi aliwaonya wafanyabiashara wanaokwepa ushuru au kodi kwa kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu na elimu itaendelea kutolewa kuanzia ngazi ya kitongoji hadi wilaya ili kuwabaini wakwepaji wa ushuru ambao wanaathiri maendeleo ya wilaya hiyo.

“Nasema kuwa nitakula nao sahani moja wafanyabiashara wote wanakwepa ushuru hadi pale watakapo acha tabia hiyo na kusaidia uchumi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje kukua kwa kasi inayostahili”alisema Mnasi

Wilaya ya Ileje hutegemewa sana kwa uzalishaji wa mbao ambazo husafirishwa kwenda katika mkoa wa Songwe na Mbeya.

Ujumbe kutoka kwa Bi. Irina Bokova, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, kwa Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake, tarehe 25 Novemba, 2016.

November 24, 2016
-Usalama wa Wanawake kufuatia Mabadiliko ya Tabia Nchi
Ukatili dhidi ya wanawake ni uvunjaji mkubwa wa haki za msingi za binadamu na tishio kwa mamilioni ya wasichana na wanawake duniani kote. Takribani mwanamke mmoja kati ya wanawake watatu duniani amekuwa akipigwa, kulazimishwa kufanya ngono, au kunyanyaswa vinginevyo katika maisha yake. Jamii nzima imeathiriwa na ukatili ambao unaweza kuwa wa kimwili, kingono (unyanyasaji, kulazimishwa au kubaguliwa) na kisaikolojia (kunyanyaswa kwa maneno au kwa hisia, kama vile kuonewa au kutengwa).
Katika siku hii ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake, UNESCO inaangazia mabadiliko ya tabia nchi na uhaba wa rasilimali kama sababu za kuchochea ukatili dhidi ya wanawake – nyumbani, mitaani, wakati wa majanga asilia yanayosababishwa na tabia nchi.
Mabadiliko ya tabia nchi yanazidisha tishio - yanaweza kuongeza uhamaji na kukosa makazi kwa watu na kuchangia katika kutokuzalishwa kwa mazao au mafuriko, kuongeza msukumo nyumbani na katika utafutaji wa riziki.  Utafiti unaonyesha kwamba wanawake wanawajibika kwa asilimia 65 ya uzalishaji wa chakula katika kaya huko Asia, kwa asilimia 75 katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na kwa asilimia 45 huko Amerika ya Kusini. Mara nyingi, ni wajibu wa kiutamaduni wa wanawake unaowaweka katika hatari kubwa dhidi ya madhara ya mabadiliko ya tabia nchi – na kwa hiyo kujikuta wakiwa katika mazingira yenye uwezekano wa kufanyiwa ukatili wanavyotembea maili nyingi kila siku kutafuta chakula, maji na kuni au baada ya kukosa makazi au kupata umasikini kutokana na majanga. Kukosa njia za kujitafutia riziki na umasikini kunaweza pia kusababisha ukatili nyumbani kutokana na msukumo wa kiuchumi, pamoja na kuendelea kwa muda mrefu kwa mienendo ya ukeketaji wa wanawake na ndoa za utotoni.
UNESCO inashiriki kikamilifu katika kuimarisha ujasiri wa kukabili mabadiliko ya tabia nchi, ujumuishaji wa mkabala wa kijinsia katika utendaji wake wote. Kwa kutumia ushirikiano na mipango ya kibunifu, UNESCO inaendeleza fikra inayodai kuwa wanawake na wasichana ni muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, hasa, kwa mfano, mipango ya kusimamia maji na utayari wa kukabiliana na majanga.
Tunafahamu kwamba uzalishaji wa gesi ukaa unaiathiri sayari ya dunia. Tunapaswa pia tutambue kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanaathiri maisha ya wasichana na wanawake duniani kote. Tunapokuwa tupo tayari kuanza kutekeleza Mkataba wa Tabia Nchi wa Paris na kujiandaa kwa ajili ya mafanikio ya COP22 huko Marrekech, tusiisahau nusu ya idadi ya watu wetu na uwezo wao mkubwa wanaouwakilisha. Wanawake lazima wawe katika kiini cha utatuzi wote wa mabadiliko ya tabia nchi.


--
Zainul A. Mzige,
Operation Manager,
MO BLOG,