DAS CHINTIKA: WALIMU TUMIENI KONDOMU ILI KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

October 24, 2017

 Katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka akiwa kwenye mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa akizungumza na baadhi ya walimu walihudhuria mkutano huo. 
Baadhi ya walimu waliokuwa wanaimba wimbo wa walimu wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa uliofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.

Na Fredy Mgunda,iringa. 

Walimu wa halmashauri ya manispaa ya Iringa wametakiwa kutumia kinga ili kujikinga na magonjwa ya zinaa amboya yamekuwa yakipunguza nguvu kazi ya taifa.

Hayo yamesemwa na katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa.

Chintinka alisema kuwa kumekuwa na ongezeko la waathirika wa ugonjwa wa ukimwai kutokana na kufanya mapenzi bila kutumia kinga jambo ambalo ni hatari.

“Jamani hapa Iringa kuna tatizo kubwa la ugonjwa wa ukimwi hivyo niwaombe walimu wangu tutumie kondomu ili kujiepusha na gonjwa hili vinginevyo vizazi vyetu vyote vitaambukizwa ukimwi” alisema Chintinka

Chintinka alisema njia ya kuwa salaama kuepukana na gonjwa hili ni kujikinga kwa kutumia kondomu maana hata watoto wetu wameathirika kutokana na wazazi kutokuwa makini na matumizi ya kinga

“Naombeni tuwakinge hawa watoto wetu ambao wameathirika ili wasiwaambukize watoto wengine maana bila hivyo tutakuwa na kizazi kilichoathirika” alisema Chintinka

Aidha Chintinka aliwaomba walimu walioathirika kujitokeza ili kupewa lishe ambayo inatolewa na serikali bure hivyo walimu wametakiwa kujitokeza na kuweka wazi kwa mwagili wake ili aweze kupata mgao wa pesa za lishe.

“Jamani walimu fungu la lishe kwa walimu walioathirikia ni nono kweli naombeni walimu mjitokeze ili mfaidi fungu hili nono maana mimi nafahamu sisi ndio tunaotenga naombeni fikisheni ujumbe huu kwa walimu wengine ambao hawajafika hapa” alisema Chintinka

Chintinka aliwataka watumishi wanaotoa siri za watumishi walioathirika kuacha tabia hiyo mara moja ili kuwaweka huru waathirika na wengine waweze kujitokeza na wapate lishe iliyotengwa na wilaya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho manispaa ya Iringa MWL. Zawadi Mgongolwa alikiri kuwepo kwa viongozi wa sekta hiyo ambao wemekuwa wakitoa siri za walimu na watumishi walioathirika na ugonjwa wa ukimwi.

Kwa kweli mgeni rasmi umeongea ukweli kero kubwa kwa walimu ni kutolea siri nje kitu kinachowafanya walimu waathirika kujificha na maradhi yao” alisema Mgongolwa

Naye katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale alimpongeza mgeni rasmi kwa ujumbe wake ambao umekuwa faraja kwa walimu na kuwaongezea hali ya kwenda kufanya kazi ya uwalimu kwa kujituma na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wao.

TANGAZO KUTOKA TANGA UWASA KUTOKUWA NA HUDUMA YA MAJI

October 24, 2017

Kuna tatizo la Umeme Jiji lote l Tanga pamoja na  eneo la Mabayani na Mowe tangu saa 10:10 alfajiri ,hivyo pampu za kusukuma maji zimesimma na hakutakuwa na maji hadi umeme utakaporejea.

Shirika la Tanesco wanaendelea kushughulikia utatuzi wa tatizo hilo na Mtambo utaanza kufanya kazi umeme utakaporejea.

Huduma ya Maji itaimarika kwa awamu baada ya mtambo kuanza kufanya kazi hivyo tunaomba radhi kwa usumbufu unaoweza kujitokeza.

Imetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Kitengo cha Uhusiano Tanga UWASA.


Makubaliano ya mradi wa Rain Tanzania yasainiwa wilayani Serengeti ili kutatua kero ya maji

October 24, 2017
Binagi Media Group
Mkuu wa wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Nurdin Babu amewataka wananchi na watendaji wa serikali, kuhakikisha wanashiriki na kusimamia vyema utekelezaji wa miradi ya maji ili kutatua kero ya maji wilayani humo.

Babu ametoa kauli hiyo hii leo wakati akizungumza kwenye hafla ya kusaini makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa kutatua kero ya maji wilayani Serengeti, baina ya shirika la Amref Tanzania na halmashauri ya wilaya hiyo.

Mradi huo ujulikanao kama “Rain Tanzania” unatekelezwa wilayani humo kwa kipindi cha miaka miwili kupitia ufadhiri wa taasisi ya Cocacola Afrika katika Kata za Mosongo, Kenyamonta, Busawe pamoja na Nyansurura, ukilenga kusaidia upatikanaji wa majisafi na salama karibu na makazi ya wananchi ambapo hadi kukamilika kwake utagharimu dolla za Marekani sita.

Meneja wa mradi huo, Mhandisi Japhet Temu amesema pia utasaidia kuhamasisha usafi wa mazingira, ujengaji na utumiaji wa vyoo bora pamoja na kuwawezesha kiuchumi vijana na akina mama ambapo vikundi 50 vya vijana na 20 vya akina mama vitawezeshwa mafunzo na mitaji ya ujasiriamali.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Mkazi wa Amref Tanzania, Mturi James amewahimiza wananchi kushiriki vyema kwenye utekelezaji na utunzaji wa miundombinu ya mradi huo ili kuhakikisha unakuwa endelevu.

“Ndoa nyingi zinapata shida pale ambapo wanawake wanakwenda kuchota maji umbali mrefu na kuchelewa kurudi nyumbani”. Anasema Bi.Bwiru Elisha, mkazi wa Kijiji cha Gantamome wilayani Serengeti.

Wilaya ya Serengeti inakabiliwa na kero ya upatikanaji wa maji ambapo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Mhandisi Juma Hamis anasema kati ya miradi 10 ya maji katika halmashauri hiyo, ni miradi miwili pekee imekamilika na kutoa huduma ya maji kwa wananchi.

Mhandisi wa maji katika halmashauri ya wilaya ya Serengeti, Dickson Protas anasema wastani wa matumizi ya maji kwa kila mwananchi ni lita tano kwa siku ingawa uhitaji ni wastani wa lita 30 katika maeneo ya vijijini na lita 65 hadi 70 katika maeneo mjini.

Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kuanza utekelezaji wa mradi huo. Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa halmashauri ya Serengeti, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Mkazi Amref Tanzania.
Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kuanza utekelezaji wa mradi huo. Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa halmashauri ya Serengeti, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Mkazi Amref Tanzania.

BALOZI KAIRUKI AIPONGEZA KAMPUNI YA KILUWA INDUSTRIAL GROUP OF COMPANIES KWA KUANDAA KONGAMANO LA UWEKEZAJI WA VIWANDA MJINI BEIJING NCHINI CHINA

October 24, 2017
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa kairuki (tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe huo uliomtembelea ofisini kwake mapema leo .Picha na Ahmad Michuzi-China.
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies  ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Mohamed Kiluwa (pichani kulia) pamoja na viongozi Waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani wakiongozwa na Katibu Tawala mkoa wa Pwani Zuberi Semataba, mapema leo kwenye Ofisi za Ubalozi huo,Ujumbe huo umewasili mjini Beijing,nchini China kushiriki Kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda linalotarajiwa kufanyika mjini humo kesho Oktoba 25,2017 .

Kongamano hilo kubwa lenye uhamasishaji mkubwa wa uwekezaji wa Viwanda nchini Tanzania,limeandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies na litawashirikisha wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda na makampuni wapatao zaidi ya 200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China.

Balozi Kairuki amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies  Mohamed Kiluwa kwa kuonesha juhudi kubwa za kuwahamasisha na kutafuta washirika mbalimbali katika suala zima la uwekezaji wa viwanda nchini Tanzania.

Balozi Kairuki amesema kuwa,Kampuni ya Kiluwa kwa kufanya hivyo  wanaibeba dhana ya Tanzania ya Viwanda kwa utekelezaji kwa vitendo,na pia kuunga mkono dhamira ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya Viwanda,na kuongeza kuwa yuko tayari kutoa kutoa ushirikiano wa kutoka katika suala zima la kuwahamasisha wawekezaji kutoka nchini China na kwenda kuwekeza nchini tanzania katika suala zima la Viwanda.
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies, Mohamed Said Kiluwa (pichani kulia) pamoja na Muwakilishi wa baadhi ya viongozi waandamizi wa mkoa wa Pwani,Katibu Tawala mkoa wa Pwani Zuberi Semataba waliofika mjini Beijing,nchini China kushiriki Kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda linalotarajiwa kufanyika mjini humo kesho Oktoba 25,2017, Kongamano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,litajumuisha wafanyashabiashara, wamiliki wa viwanda na makampuni wapatao zaidi ya 200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China.
Katibu Tawala mkoa wa Pwani Zuberi Semataba akifafanua jambo mbele ya Balozi wa Tanzania nchini China,Mh. Mbelwa Kairuki mapema leo walipokwenda kumtembelea Ofisini kwake,pamoja na kupanga maandalizi ya Kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda linalotarajia kufanyika mjini Beijing hapo kesho Oktoba 25,2017. Kongamano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies na kuwaalika viongozi Waandamizi wa Serikali ya Mkoa wa Pwani,wafanyabiashara wakubwa ambao ni wamiliki wa viwanda na makampuni mbalimbali.

Mkurugezi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Naima Kiluwa akiandika kilichokuwa kikijiri kwenye mazungumzo hayo mafupi na Balozi Mh.Mbelwa Kairuki mara baada ya kuukaribisha ujumbe huo Ubalozini kwake na kuzungumza mambo mbalimbali yaliyohusu masuala ya uwekezaji kwa Tanzania,na baadae kupata chakula cha pamoja.
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa kairuki akimkabidhi zawadi mmoja wa watakaoshiriki Kongamano la Viwanda linalotarajia kufanyika kesho mjini Beijing,likatalojumuisha Wamiliki wa Viwanda,Wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali wapatao zaidi ya 200,anaeshuhudia kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Semataba
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa kairuki akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa 
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa kairuki akimkabidhi zawadi Mkurugezi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Naima Kiluwa 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa akiwatambulisha baadhi ya washirika wake mbele ya Balozi Kairuki (hayupo pichani),mapema leo mjini Beijing nchini China,wakiwa tayari kwa maandalizi ya Kongamano la Uwekezaji wa Viwanda linalotarajia kufanyika hapo kesho Octoba 25,2017 mjini humo.
Rais wa wanafunzi wasomao nchini China,Hussein Mtoro akiukaribisha Ujumbe kutoka Serikali ya Mkoa wa Pwani ikiongozwa na Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Semataba pamoja na uongozi wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies ukiongozwa na Mohamed Said Kiluwa (njano),walipofika Ofisini kwa Balozi wa Tanzania nchini China,Mh Mbelwa Kairuki,mapema leo mchana .Picha na Ahmad Michuzi-China.
NCHI ZILIZOENDELEA KITEKNOLOJIA ZISAIDIE KUBORESHA HARAKATI ZA UCHUMI WA VIWANDA-SAMIA

NCHI ZILIZOENDELEA KITEKNOLOJIA ZISAIDIE KUBORESHA HARAKATI ZA UCHUMI WA VIWANDA-SAMIA

October 24, 2017
Nchini zilizopiga hatua katika maendeleo ya Sayansi na Teknolojia zimetakiwa kuwa tayari kusaidia kuleta teknolojia hiyo ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza za kimazingira katika harakati za kufikia maendeleo ya uchumi wa viwanda. Akizungumza kwenye maadhimisho ya 72 ya Umoja wa Mataifa (UN) na wageni waalikwa kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassani amesema kwamba maendeleo ya viwanda yanakwenda sambamba na tishio la uharibifu wa mazingira na tabianchini ni muhimu kwa wadau wote wa maendeleo kujipanga. “Sote tunajua kwamba maendeleo ya viwanda yalikuja na uharibifu mkubwa wa mazingira na hali ya hewa katika kipindi cha mapinduzi ya viwanda kipindi kile cha karne ya 18th na 19th sasa ni muhimu kwa mataifa yaliyopiga hatua za kisayansi na teknolojia kuweza kuwa tayari kusaidia kwenye hili,” amesema Makamu wa Rais. Amesema nchini juhudi zinaendelea za kukuza uchumi na maendeleo ya watu lakini ni muhimu kwa wananchi kwa ujumla wao kuweza kulinda na kuhifadhi zaidi maliasili, hifadhi na rasilimali za taifa ili kuweza kufikia uchumi wa viwanda. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez mara baada ya kuwasili kwenye maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.[/caption] Aliongeza kwamba ofisi yake ambayo inashughulikia mambo ya tabianchini na mazingira wametunga sera, sheria na sera mpya ya mazingira na uendeshaji wa mambo ya mazingira pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2016 ambapo ni kuhakikisha juhudi za viwanda haziwezi kuathiri mazingira ya nchini. Awali akihutubia hadhara hiyo, Makamu wa Rais alifafanua kwamba kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya Umoja wa Mataifa (UN) ni kwamba “Maendeleo ya viwanda na utunzaji wa mazingira kwa maendeleo Endelevu” ni sahihi kwa wakati muafaka katika juhudi za kuibadilisha Tanzania kufikia uchumi wa viwanda. Amesema kwamba ni takribani miaka miwili tangu kuanzishwa kwa agenda za maendeleo endelevu 2030, ambapo malengo 17 yamewekwa na Tanzania imefanikiwa kuingia kwenye awamu ya pili ya maendeleo endelevu katika juhudi za kupambana na umasikini. “Katika kuhakikisha serikali inakuwa na fedha za kutosha kufikia malengo hayo ya maendeleo chini ya utawala wa Dkt John Joseph Pombe Magufuli mapambano dhidi ya rushwa, matumizi mabaya ya fedha za umma, ujangili na ubadhilifu yanadhibitiwa kikamilifu na mapambano yanaendelea,” alisisitiza. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki na Afisa Mwakilishi wa Unesco Dar, Ann Therese Ndong- Jatta mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee kushiriki maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa.[/caption] Kwa upande wake, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini (UN) Alvaro Rodriguez aamesema kwamba bado wanakabiliwa na changamoto nyingi hasa upande wa rasilimali ila wana matumaini kwamba kwa pamoja wanaweza kuwashawishi wadau wa maendeleo kusaidia katika vipaumbele vya nchini. “Wakati ambapo Tanzania inafanya mageuzi makubwa, inapoelekea kuwa nchini ya hadhi ya kipato cha kati, msaada wa Umoja wa Mataifa (UN) hauna budi kuendana na mahitaji na changamoto mpya,” amesema Rodriguez Aliongeza pia kwamba Umoja wa Mataifa (UN) wataendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na wadau wengine wa maendeleo ili kuweza kufikia malengo 17 ya maendeleo endelevu na aliishukuru Tanzania kuendelea kupokea wakimbizi pamoja na changamoto nyingi za kuhifadhi wakimbizi hao. Maadhimisho ya Umoja wa Mataifa (UN) kufanyika kila mwaka katika kukumbuka tangu umoja huo uanzishwe mwaka 1945 na Tanzania ilijiunga kwa mara ya kwanza mwaka 1961 mara tu baada ya uhuru na sherehe hizo za jana zilihudhuriwa na wageni mbalimbali mawaziri, mabalozi, viongozi wa dini na zilipambwa na bendi ya Jeshi la Watanzania wa Tanzania (JWTZ). Na Damas Makangale wa Thebeauty

WAZIRI MPINA AAGANA RASMI NA WATUMISHI WA NEMC.

October 24, 2017
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akitia saini katika kitabu cha wageni kwenye Ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC  alipoenda kuagana nao na kutoa neno baada ya kufanya nao kazi kama Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara Mpya ya Mifugo na Uvuvi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza wakati wa kuagana na watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, kulia ni mkaguzi wa Mazingira kanda ya Mashariki Bw. Jafari Chimgege na kushoto ni Dkt. Ruth Rugisha Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Baraza.
Katika Picha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina na Baadhi  ya viongozi katika Management ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC.
Picha ya Pamoja Waziri Mpina na Baadhi watumishi wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC.

Vyombo vya Habari vya Serikali vimetakiwa kufuata Maadili ya Uandishi wa Habari

October 24, 2017
Na: Genofeva Matemu –WHUSM
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amevitaka vyombo vya habari vya serikali kufuata maadali na miiko ya uandishi wa habari kwa kuzingatia weledi ili umma eweze kupata habari zilizokidhi vigezo vya uandishi wa habari.
Rai hiyo ameitoa jana jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) pamoja na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na kuzungumza na watendaji wa taasisi hizo.
“Vyombo vya habari vya serikali viwe mfano bora kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa watanzania wanapata taarifa sahihi na kwa wakati kwani vyombo hivi ni moja kati ya mhimili mkubwa wa nchi na kama vitatumika vibaya madhara yake ni makubwa sana” amesema Mhe. Shonza  
Aidha Mhe. Shonza amesema kuwa Serikali inathamini na kutambua mchango unaotolewa na vyombo vya habari vikiwemo vyombo vya serikali TBC katika kufikisha taarifa za ukweli na uhakika katika jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayob Rioba amemhakikishia Mhe. Shonza kuwa TBC itaendelea kuzingatia weledi na maadili katika kuhabarisha umma huku ikiendelea kubuni vipindi mbalimbali vitakavovutia jamii kuangalia televisheni hiyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa TSN imeendelea kuhakikisha kuwa taifa linahabarishwa kwa hakika kwa kutumia nyenzo mbalimbali na uzoefu tangu ilipoanzishwa miaka 88 iliyopita hivyo kuchangia katika maendeleo ya nchi yetu
“kwa sasa TSN ni zaidi ya magazeti, imejikita zaidi kuwa kampuni inayotoa huduma za habari kwa kutumia nyenzo mbalimbali za kiteknolojia ili kuweza kuendana na kasi ya maendeleo ya sayansi na taknolojia” amesema Dkt. Yonazi.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Bw. HAB Mkwizu (kulia) akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) alipofanya ziara katika Kampuni hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji TSN Dkt. Jim Yonazi
 Mkurugenzi Mtendaji TSN Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) katika Kampuni hiyo jana Jijini Dar es Salaam
 Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akizungumza na Menejimenti ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) alipofanya ziara katika Kampuni hiyo jana Jijini Dar es Salaam
 Mhariri wa gazeti la Daily News Bw. Leonard Mwakalebela (kushoto) akimwelezea Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) namna habari zinavopitiwa na kupangwa katika gazeti hilo alipofanya ziara katika kampuni ya TSN jana Jijini Dar es Salaam

MISA YA KUMUAGA ASKOFU MKUU WA JIMBO LA TUNDURU-MASASI MAREHEMU CASTOR PAUL MSEMWA YAFANYIKA KATIKA KANISA KATOLIKI LA BARAZA LA MAASKOFU JIJINI DAR ES SALAAM

October 24, 2017
Askofu Mkuu wa  Jimbo Kuu  Katoliki  la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akiaga  mwili wa Marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na  Masasi Castor Paul Msemwa mara baada ya Misa iliyofanyika katika Kanisa la Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Askofu Mkuu wa  Jimbo Kuu  Katoliki  Tabora Paul Ruzoka akiaga  mwili wa Marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na  Masasi Castor Paul Msemwa mara baada ya Misa iliyofanyika katika Kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na  Masasi Castor Paul Msemwa likiwa limebebwa na Mapadri wakielekea ndani ya Kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Askofu Mkuu wa  Jimbo Kuu  Katoliki  Tabora Paul Ruzoka akizungumza katika Misa ya kumuombea Marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na  Masasi Castor Paul Msemwa katika kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Waumini wa kanisa Katoliki wakiwa katika Ibada ya kumuombea Marehemu katika Kanisa hilo jijini dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Baraza la Maaskofu Tanzania Benard James akizungumza mara baada ya Misa hiyo. Picha na Mpiga Picha wetu.