MHANDISI KIJAZI APEWA JUKUMU LA SEFUE ILI KUHAKIKISHA MSANII RICH4D ANAONANA NA RAIS MAGUFULI.

March 11, 2016
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya kutoka Jijini Mwanza, Joseph Stanford, maarufu kwa jina la Rich4D akiwaonyesha wanahabari Jijini Mwanza (hawapo pichani) ramani ya Mkoa wa Dar es salaam aliyoitumia kutambua maeneo ya Mkoani huo.
 Hiyo ilikuwa baada ya kuwasili Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuonana na Rais John Pombe Magufuli ili kumpongeza kwa kuwajumuisha wasanii katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika baraza lake la Mawaziri. Rich4D alitembea kwa miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es salaam ili kutimiza adhma yake hiyo.

Msanii Joseph Starnford maarufu kwa jina la Rich4D alitembea kwa miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es salaam ili kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuwajumuisha Wasanii katika Baraza lake la Mawaziri, amesisitiza kuwa shauku yake ni kuonana na rais ili kutimiza adhma yake.
Zaidi Bonyeza HAPA

Semina ya Kuwanoa Wadau wa Sekta ya Sanaa, yafanyika jijini Dar es Salaam

March 11, 2016
Kwa mara ya kwanza, wadau wa Sanaa nchini wamepata fursa ya kukutana na Makampuni, Mashirika na Vyombo mbalimbali katika mafunzo yaliyofanyika hotel ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam. Semina hii iliongozwa na Maria Sarungi Tsehai, ambaye ni mdau mkubwa katika sekta hii
Mafunzo hayo yalifanywa na wataalam kutoka sekta mbalimbali kama Nyumba, Urembo, Saikolojia, Sanaa na Wasanii n.k
Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba, Arden Kitomari,akitoa mafunzo ya namna ya kuwekeza katika Sekta ya Nyumba nchini Tanzania,hususan kupitia miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa
Wadau wa Sanaa pia walipata mafuzo ya Namna ya kubalansi maisha yao ya Sanaa na yale ya Familia, kutoka kwa mwanasaikolojia maarufu, Aunt Sadaka Gandi.

Semina hii iliyopewa jina Celebrity Corporate Conference & Cocktail iliwahusisha pia COSOTA na BASATA ambao ni wasimamizi wakuu wa kazi za sanaa na taratibu zake
Ms Doreen Anthony Sinare, CEO wa COSOTA akitoa somo kuhusu usajili wa kazi, masharti ya kuzingatiwa na Sheria zinazomlinda Msanii aliyesajiliwa
Sekta lengwa katika semina hii ni wadau kutoka Filamu, Muziki, Urembo, Habari, na Wajasiriamali mashughuri
Bwana Aristides kutoka BASATA aliwaelekeza wadau kuhusu Taratibu mpya za kujisajili na chombo hiki, pamoja na faida zake.

Je, Unafahamu namna ya kuifanya Talanta yako kuwa Biashara? Hii ndio ilikuwa mada iliyoongozwa na Mjasiriamali mashughuri, Shekha Nasser wa Shear Illusions
Baada ya mada zote kukamilika, wadau walipata fursa ya kubadilishana mawazo na kujadili walichojifunza, kwa kushiriki Tafrija mchapalo iliyoandaliwa
Huu ukawa wakati muafaka wa wasanii kuuliza maswali na kutoa dukuduku zao kwa Makampuni, Mashirika na vyombo vinavyohusika na Sanaa na Wasanii. Mrembo na Mjasiriamali Jokate Mwegelo akiteta jambo na afisa kutoka BASATA
Mwanahabari Maimuna Kubegeya hakuwa nyuma kuuliza maswali na kufahamiana na CEO wa COSOTA, Ms Doreen Anthony Sinare
MwanaBlog maarufu John Bukuku akifurahia jambo na Meneja Masoko wa NHC, Arden Kitomari


Antu Mandoza akisisitiza jambo
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Popular Links ambao ndio waandaaji wa Semina hii akiwa katika pozi na Mkurugenzi Ruge Mutahaba kutoka Clouds Media
Warembo katika picha ya pamoja
Wasanii wa kutengeneza muonekano kutoka LuvTouch Manjano ya Shear Illusions, wakiwaonesha baadhi ya wageni, namna ya kupaka makeup
Mariam Ndabagenga, Mkurugenzi wa Popular Links akitoa neno la Shukran kwa wageni waalikwa wote na kuwakaribisha kwenye awamu ya pili ya Semina hii itakayofanyika mwezi Oktoba.

Semina hii ya Celebrity Corporate Conference & Cocktail imeandaliwa na Kampuni ya Popular Links kwa udhamini wa Heineken, The Guardian, Nipashe, Leteraha, Hyatt Regency hotel, Ndovu Special Malt, Cocacola, NHC, COSOTA, Jamii Media, BASATA, Shear Illusions, Clouds Media na Slide Visuals.
........................................................................................................ -- Popular Links Managing Director 0787 028 658 missiepopular@gmail.com Twitter: @MissiePopular Instagram: @MissiePopular FACEBOOK PAGE: Missie Popular www.missiepopular.blogspot.com

DUKA KUBWA LA KAMERA ZA KISASA LA DEO FILIKUNJOMBE LAZINDULIWA DAR

March 11, 2016
 Mkurugenzi wa Mauzo wa Kampuni ya Jumbo Camera House, Mathias Luoga akionesha vifaa mbalimbali vya kamera wakati wa uzinduzi wa duka jipya lililopo Jengo la NSSF Benjamin Mkapa, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Sara Filikunjombe,  mke wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ludewa, marehemu Deo Filikunjombe ambaye pia mmiliki wa kampuni hiyo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA: KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mke wa marehemu Filikunjombe, Sara  (wa pili kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Prodaction, Ritta Poulsen (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Jumbo Camera House, Paul Buckendahl (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo wa Kampuni hiyo, Mathias Luoga wakigongeana glasi zenye Champagn wakati wa hafla hiyo.
 Wageni waalikwa wakioneshwa moja ya kamera na vifaa vyake inayouzwa katika duka hilo kubwa la aina yake kwa Afrika Mashariki, Kati na Kusini.

 Paul akiwaongoza wageni waalikwa kusimama kwa dakika moja kumkumbuka marehemu Deo Filikunjombe
 Mgeni rasimi katika hafla hiyo, Ritta Poulsen akihutubia wakati wa uzinduzi wa duka hilo

 Kamera ya kisasa ya kupigia matukio kwa juu
 Baadhi ya wageni waalikwa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jumbo Camera Hose, Sara Filikunjombe akiwa na Ritta na mmoja wa wageni wakati wa hafla hiyo.
 Baadhi ya vifaa vya kamera
 Wageni walikwa wakiangalia vifaa mbalimbali vya kamera dukani humo
 Ssa ni wakati wa furaha





WAZIRI WA MAJI AIAGIZA BODI YA DAWASCO KUWASIMAMISHA WATUMISHI WAKE TISA KWA TUHUMA MBALIMBALI

March 11, 2016

 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge (katikati) akiongozana na Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Maji taka na Maji safi Dar es Salaam (DAWASCO) , Meja General (mstaafu), Samuel Kitundu (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Cyprian Luhemeja , wakati Waziri huyo alipoitembelea Dawasco jana na kisha kutangaza watumishi tisa ambao ameiagiza bodi kuwasimamisha kazi kupisha uchunguzi dhidi yao kufuatia tuhuma mbalimbali. Mhandisi Lwenge alitembelea leo. 

WATUMISHI AMBAO WAZIRI AMEAGIZA BODI IWASIMAMISHE KAZI NI:-
Meneja Rasilimali Watu, Mvano Mandawa, Meneja Ufuatiliaji na Tathmini, Reinary Kapera, Teresia Mlengu, Emmanuel Guluba, Peter Chacha, Fred Mapunda, Reginald Kessy, Jumanne Ngelela na Bernard  Nkenda. 

Aidha Waziri Lwenge aliagiza pia kuchunguzwa kwa CEO wa zamani Jackson Midala.

Miongoni mwa tuhuma zao ni pamoja na kufanya maunganisho ya maji yasiyofuata utaratibu kwa kampuni ya STRABAG inayotekeleza mradi wa mabasi yaendayo kasi na kusababisha kulikosesha shirika mapato yenye thamani ya sh Bilioni 2.8 (2,887,577,134/=). 
Mameneja wa Dawasco wakiwa katika mkutano huo.Baadhi yao  walisimamisha kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazo wakabili.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge (kulia) akizungumza na bodi pamoja na menejimenti ya Shirika la Maji taka na Maji safi Dar es Salaam (DAWASCO) wakati Waziri huyo alipotembelea makao makuu ya shirika hilo Dar es Salaam jana na kuiagiza bodi kusimamisha kazi watumishi tisa. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge (aliyesimama) akizungumza na bodi pamoja na menejimenti ya Shirika la Maji taka na Maji safi Dar es Salaam (DAWASCO) wakati Waziri huyo alipotembelea makao makuu ya shirika hilo Dar es Salaam jana na kuiagiza bodi kusimamisha kazi watumishi tisa.  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge (aliyesimama) akizungumza na bodi pamoja na menejimenti ya Shirika la Maji taka na Maji safi Dar es Salaam (DAWASCO) wakati Waziri huyo alipotembelea makao makuu ya shirika hilo Dar es Salaam jana na kuiagiza bodi kusimamisha kazi watumishi tisa.
 Mameneja wa Dawasco wakiwa katika mkutano huo.
 Mmoja wa mamena wa Dawasco akichukua dondoo za yake yaliyosema na Waziri Lwenge
  Mameneja wa Dawasco wakiwa katika mkutano huo.
  Mameneja wa Dawasco wakiwa katika mkutano huo.
 Mwenyekiti wa bodi ya Dawasco, Meja General (Mstaa) Samuel Kitundu (wapili kushoto) na baadhi ya wajumbe wa bodi wakitoka katiia mkutano huo. Ambapo pamoja na mambo mengine pia Waziri Lwenge aliiagiza bodi hiyo kuchunguza kampuni zote kubwa jijini Dar es Salaam kama zinalipia huduma ya maji.
Mameneja wakitoka katika mkutano huo.