January 07, 2014

ZITTO KIDEDEA, AIBWAGA CHADEMA MBELE YA TUNDULISU MAHAKAMA KUU LEO

 HONGERA: Wakili wa CHADEMA Tundu Lisu (kulia) akilazimika kumpongeza aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe baada ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, John Mkamwa, kuridhia zuio la Zitto asijadiliwe na ngazi yoyote ya maamuzi ya Chadema, hadi kesi ya msingi aliyofungua dhidi ya chama hicho itakapomalizika. Jaji huyo amekubali kesi ya msingi iungurume na itaanza kusikilizwa Februari 13, mwaka huu. (PICHA NA THENKOROMOBLOG)
 Zitto akitoka kwa msaada wa mabaunsa wake katika chumba cha mahakama kuu baada ya uamuzi huo wa  Mahakama kuu leo jioni.
Tundu Lisu na wapambe wake wakionekana kutoka kwa aibu Mahakamani baada ya kubwagwa

 Tundulisu aklizungumza na waandishi nje ya mahakama
 Wakili wa Zitto akizungumza na waandishi nje ya mahakama kuu
 Wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono Zitto wakishangilia abaada ya ushindi wa kiongozi huyo

CHADEMA KANDA YA KASKAZI:TUTAPITISHA WAGOMBEA WANAOKUBALIKA.

January 07, 2014
Na Oscar Assenga,Tanga.
KATIBU wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa amesema chama hicho kitahakikisha kinawapitisha wagombea wanaokubali kwenye chaguzi za udiwani na wenyeviti wa serikali za vijiji ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibuni katika mikoa ya Tanga ,Kilimanjaro na Arusha kuziba nafasi zilizoachwa wazi lengo likiwa ni kushika hatamu ya uongozi kwenye chaguzi hizo.
 
Golugwa alisema hayo leo wakati akizungumza na TANGA RAHA ambapo alisema mikakati hiyo itakwenda sambamba na ufanyaji wa kampeni za kiustarabu kwa kueleza sera makini ambazo zitawapa hamasa wananchi kuweza kukichagua chama hicho lengo likiwa kuwapa maendeleo pamoja na kuzipatia ufumbuzi kero zinazowakabili.
 
Alisema umuhimu wa kuwaweka wagombea wanaokubali kwenye chaguzi hizo ni mkubwa sana kutokana na kutaka kutengeza historia ya kipekee kwa kuwa na madiwani wawili kwenye jimbo la Tanga ambao wataweza kuleta mabadiliko ya kiutendaji kwa viongozi wengine waliopo.
 
     “Chama chetu kitaingia kwenye mchakato wa kuangalia nani anaweza kuipeperusha bendera kwenye chaguzi hizo na ambaye atakuwa akikubalika kwa asilimia kubwa na wananchi wa mahala husika na sio vyenginevyo “Alisema Bolugwa.
 
Alisema kuelekea uchaguzi huo lazima wanachama na wapenzi wa chama hicho kuachana na makundi ambayo hayana tija kwao badala yake kuwa na mshikamano ambao utawawezesha kupata mafanikio ambayo yanapeleka kushika nyazifa za uongozi kwenye kata na vijiji hivyo.
 
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika kutokana kata mbili mkoani Tanga ambazo ni Kiomoni na Mtae Jimbo la Mlalo wilayani Lushoto viongozi wao kutokuwepo kwa kufariki na kujiuzulu na hivyo kupelekea nafasi zao kubaki wazi.
 
Aliyataja maeneo mengine yaliyowazi ambapo uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika ni kata ya Sombeni Jimbo la Arusha,Kata ya Kiboroloni Jimbo la Moshi na Karachimbi Jimbo la Kiteto Manyara
 

COASTAL UNION YAMPAGIA SIFA CHIPO.

January 07, 2014
Na Oscar Assenga,Tanga.
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umemwagia sifa Kocha mkuu wa timu hiyo Yusuph Chipo kutokana na uwezo wake kiutendaji alioufanya kwa kipindi kifupi ambacho amekabidhiwa timu hiyo ambacho  kinaonyesha mafanikio makubwa kwao siku za mbeleni.
 
Akizungumza jana,Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga,Hemed Aurora “Mpiganaji”alisema uwezo wa mwalimu huo umeweza kuchangia kwa kiasi kikubwa timu yao ya pili kuweza kuchukua ubingwa wa kombe la uhai Cup na kuweza kuipa heshima timu hiyo na mkoa wa Tanga kwa ujumla.

MASHUJAA BENDI KUTUMBUIZA TANGA

January 07, 2014
Na Oscar Assenga,Tanga.
BENDI ya mziki wa Dansi nchini ya Mashujaa Music Band chini ya Rais wao Charles Baba wanatarajiwa kufanya maonyesho mawili mkoani Tanga ambapo moja litafanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Nyumbani Tanga mjini Januari 11mwaka huu.
Akizungumza na TANGA RAHA BLOG,Mratibu wa Onyesho hilo,Steven Ngonyani “Maji Marefu”alisema onyesho hilo linatarajiwa kuwa la aina yake hasa ukizingatia umahiri wa bendi hiyo mpaka ikafanikiwa chukua tuzo tano za Kilimanjaro music award hapa nchini.
Maji Marefu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) alisema kabla ya kufanyika onyesho hilo bendi hiyo itafanya onyesho lake la kwanza wilayani Korogwe Januari 10 mwaka huu ambapo watatumbuiza kwenye ukumbi wake wa Mamba Club.
  “Ninachoweza kusema maandalizi ya maonyesho yote mawili yanaendelea vizuri na ninaamini wakazi wa wilaya ya Korogwe na jiji la Tanga watapata burudani ya aina yake “Alisema Maji Marefu.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Mashujaa Group Limited,Maximilian Luhanga alisema baada ya bendi hiyo kupata tuzo tano za Kilimanjaro Music Award wakaona wakati huu wafanya maonyesho kwa wapenzi wao ili kuweza kuwapa shukrani.
Alisema bendi hiyo baada ya kumaliza maonyesho yao mkoani Tanga itazunguka nchi nzima ili kuweza kuwapa wapenzi wao ila kitu roho inapenda kwa kuwapa burudani isiyo na kifani.
Aidha alisema wasanii wa bendi hiyo watatua mkoani Tanga wakiongoza na Rais wao Charles Baba,Rapa mahiri wao Furgeson ambaye ni pia alipata tuzo kutokana na umahiri wake.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

January 07, 2014
Release No. 002
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Januari 7, 2014

SEMINA YA WAAMUZI, MAKAMISHNA JAN 13
Semina ya waamuzi na makamishna wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inafanyika Januari 13 na 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ndiye anayetarajiwa kufungua semina hiyo.

Wakati huo huo, Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kimemwalika Rais Malinzi kuwa mgeni rasmi kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Simba na Chuoni itakayochezwa kesho (Januari 8 mwaka huu) saa 2 usiku Uwanja wa Amaan.

MAKOCHA WA LESENI B WAKABIDHIWA VYETI
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine amekabidhi leseni B kwa makocha walioshiriki kozi iliyofanyika mjini Zanzibar mwaka jana.

Jamhuri Kihwelo alipokea leseni hiyo inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa niaba ya washiriki wengine tisa waliofuzu mafunzo hayo.

Makocha wengine waliofuzu kozi hiyo iliyoendeshwa na mkufunzi Bhekisisa Boy Mkhonta kutoka Swaziland ni Abdulghan Msoma, Hafidh Badru, Nasra Juma Mohamed, Gulam Abdallah Rashid, Mohamed Ayoub Suleiman, Shaaban Ramadhan, John Simkoko na Hemed Suleiman Ali.


Hivi sasa Tanzania ina makocha 40 wenye leseni B za CAF baada ya wengine 31 kufuzu katika mafunzo yaliyofanyika mapema mwaka juzi jijini Dar es Salaam chini ya mkufunzi Honor Janza kutoka Zambia.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

CCM TANGA YAWAONYA WATENDAJI WA SERIKALI.

January 07, 2014
Na Oscar Assenga, Tanga
HALMASHAURI Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga (CCM) imekemea vikali tabia ya watendaji wa serikali wanaojifanya miungu watu na kuzitaka mamlaka husika kuhakikisha wanawachukulia hatua kali ili kukomesha vitendo vya aina hiyo.

Uamuzi huo ulifikiwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga (CCM)kilichofanyika mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka wilaya mbalimbali mkoani hapa ambapo mambo mawili makubwa yaliyotawala kikao hicho ni migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji na mgogoro kati ya wakulima wa chai, chama cha wakulima wa chai (Utega) pamoja na mwekazaji.

BUMBULI YARIDHISHA NA SHABAHA YA SHIRIKA LA MAENDELEO (TAYODEA)

January 07, 2014
HALMASHAURI  ya  Wilaya ya Bumbuli Mkoa wa Tanga imeridhishwa na shabaha ya Shirika la Maendeleo la Vijana Mkoa wa Tanga (TAYODEA)  ya kuhamasisha vijana na kwamba limekuwa kichocheo cha maendeleo Wilayani humo.

Hayo yalielezwa na watendaji wa kata za Halmashauri hiyo  wakati wa mkutano wa wadau wa mradi wa uwajibikaji kijamii katika halmashauri ya  Bumbuli  uliyofanyika kwenye ukumbi wa Kimalube mjini Soni.

 Mkutano huo ambao pia uliwashirikisha baadhi ya wataalamu wa idara mbalimbali, walisema kuwa Tayodea  limekuwa mstali wa mbele katika kutoa elimu kwa jamii na viongozi wa ngazi zote kuhusu wajibu na haki na hivyo kuleta muamko mkubwa wa kimaendeleo.

Wamedai kuwa mbali na elimu hiyo lakini shirika hilo limekuwa mfano wa kuigwa kwa kuchangia na kushiriki katika shughuli za maendeleo ikiwemo kuibua changamoto na jinsi ya kukabiliana nazo.

WILAYA YA TANGA YAFANIKIWA KWA KIASI KIKUBWA KWENYE SEKTA YA ELIMU.

January 07, 2014
Na Mbaruku Yusuph,Tanga

WILAYA ya Tanga katika mwaka huu wa 2013 mefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika sekta ya elimu kwa ufaulu wa wanafunzi wa  darasa la saba ambao walifanya mtihani wao wa Taifa mwezi wa kumi  ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana.

Akizungumza ofisini kwake kaimu Afisa elimu Jiji, Damas Kifanga alisema kuwa ufaulu huo uliojumuisha shule 93 za Tanga mjini na Vijijini  umeongezeka mwaka huu ingawa sekta hiyo ya elimu inakabiliwa na changamoto nyingi.

Aidha alisema katika sekta hiyo ya elimu Wilaya ya Tanga mwaka huu imefanikiwa kutoa wanafunzi 4266 kati ya wanafunzi 6261 sawa na 40% ya ufaulu wa matokeo ya darasa la saba ambapo ni tofauti na mwaka jana kitu ambacho kinaleta hamasa katika sekta hiyo muhimu katika maisha ya kila siku.

Hata hivyo Kifanga alisema kuwa ili kukabiliana na idadi ndogo ya wanafunzi waliokosa nafasi za kujiunga na shule za serikali,ni lazima kuunganisha nguvu kutoka serikalini,wazazi na taasisi zisizo za kiserikali ili kuweza kuinua sekta hiyo ya elimu katika Wilaya ya Tanga Mjini.