MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA KIWANDA CHA KOROSHO CHA AMAMA NA KUHUTUBIA WANANCHI WA TANDAHIMBA

September 10, 2016

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Kitema I wilayani Tandahimba  waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili kwenye wilaya hiyo ikiwa sehemu ya ziara yake mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa kwa burudani ya ngoma wakati akiwasili kwenye makao makuu ya wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa wilaya ya Tandahimba  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kiwanda cha kubangua korosho cha AMAMA kilichopo wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi na Mdhibiti wa ubora wa bidhaa Bw. Karim Hassan (kushoto) ya hatua mbali mbali ambazo korosho hupitia wakati wa kubanguliwa kwenye kiwanda cha AMAMA kilichopo Tandahimba mkoani Mtwara.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

DKT. SHEIN AKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA (SMZ)

September 10, 2016

Baadhi ya Wakuu wa Vikosi vya SMZ wakiwa chini ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ wakiwa katika mkutano wa Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2015-2020 uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika mkutano wa Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2015-2020 uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
Baadhi ya Maafisa Tawala wa Mikoa ya Zanzibar katika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ wakiwa katika mkutano wa Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2015-2020 uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya wakiwa katika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ wakiwa katika mkutano wa Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2015-2020 uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika mkutano wa Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2015-2020 uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo wakati alipozungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika mkutano wa Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2015-2020 uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Radhiya Rashid Haroub (katikati) akisoma vifungu vya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 wakati mkutano wa mpango wa utekelezaji wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ,mkutano huo ulifanyika leo chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Idrisa Kitwana katika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, wakiwa katika mkutano wa Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2015-2020 uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.]

SWALA YA EID KUSWALIWA BAKWATA MAKAO MAKUU, KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

September 10, 2016
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

MKUU WA MKOA WA MWANZA AKABIDHI VYAKULA KWA NIABA YA RAIS MAGUFULI KWENYE KITUO CHA WAZEE BUKUMBI KWA AJILI YA IDD EL HAJJ

September 10, 2016
Katika kusherehekea Sikukuu ya Idd El Hajj siku ya Jumatatu Septemba 12, 2016, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, ametoa msaada wa vyakula wenye thamani ya shilingi laki saba na elfu themanini (780,000), kwa ajili ya Kituo cha kulelea Wazee na Walemavu wasiojiweza cha Bukumbi Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Akikabidhi msaada huo jana, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, aliuhimiza uongozi wa kituo hicho kusimamia vyema ugawaji wa vyakula hivyo li kuwafikia walengwa, ikizingatiwa kwamba kumekuwa kukiibuka malalamiko kutoka kwa wazee wanaoishi katika kituo hicho kwamba misaada ambayo imekuwa ikitolewa na serikali pamoja na wafadhili mbalimbali imekuwa haiwafikii yote.

Hata hivyo Kaimu Afisa Mfawidhi wa kituo hicho, Georgina Kwesigabo, alitanabaisha kwamba vyakula na misaana ambayo imekuwa ikitolewa na serikali pamoja na wafadhili mbalimbali kituoni hapo, yote imekuwa ikiwafikia walengwa wote isipokuwa kuna changamoto ya baadhi yao kuuza misaada wanayopatiwa ikiwemo vyakula, jambo ambalo linaulazimu uongozi wa kituo hicho kuandaa utaratibu wa kusimamia misaada hiyo hususani kuwapikia chakula wanaoishi kituoni hapo badala ya kuwagawia chakula ili wajipikie wenyewe.

Wazee wanaoishi kituoni hapo waliishukuru serikali kwa msaada huo ambapo walisema wanaendelea kumuombea Rais Magufuli na Serikali yake ili iendelee kuboresha kituo hicho ikiweo kuwekewa uzio ili kuondokana na hofu ya kiusalama waliyonayo kwani wakati mwingine wamekuwa wakiibiwa mali zao ikiwemo kuku ambazo wamekuwa wakizifuga.

Vyakula vilitolewa na Mhe.Rais Magufuli ni, mchele gunia sita (kila gunia kilo 50), mafuta ya kupikia madumu manne (kila dumu lita 20) pamoja na mbuzi wawili.
Baadhi ya wazee wanaoishi kwenye Kituo cha Bukumbi, wakifurahia mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza baada ya Rais Magufuli kuwapatia msaada wa vyakula kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Idd El Hajj, itakayofanyika kesho kutwa jumatatu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (mwenye kofia), akimsikiliza mmoja wa wazee katika Kituo cha Wazee Bukumbi.
Mmoja wa akina mama kwenye Kituo cha Bukumbi akiishukuru Serikali kwa msaada wa chakula ilioutoa kituoni hapo
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe.Juma Sweda (kulia), akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa chakula uliotolewa na Mhe.Rais Magufuli katika Kituo cha Wazee Bukumbi wilayani humo. Alisema Serikali inawajali Wazee wanaoishi katika kituo hicho na kwamba ina upendo kwao ndiyo maana inaendelea kuwahudumia.
Kaimu Afisa Mfawidhi wa kituo hicho, Georgina Kwesigabo, alitanabaisha kwamba vyakula na misaana ambayo imekuwa ikitolewa na serikali pamoja na wafadhiri mbalimbali kituoni hapo, yote imekuwa ikiwafikia walengwa wote isipokuwa kuna changamoto ya baadhi yao kuuza misaada wanayopatiwa ikiwemo vyakula, jambo ambalo linaulazimu uongozi wa kituo hicho kuandaa utaratibu wa kusimamia misaada hiyo hususani kuwapikia chakula wanaoishi kituoni hapo badala ya kuwagawia chakula ili wajipikie wenyewe.
Vyakula vilivyotolewa na Mhe.Rais Magufuli kwa ajili ya Makao ya Wazee na walemavu wasiojiweza Bukumbi, Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Huyu mbuzi, tehe tehe tehe!!
Makao ya Wazee na walemavu wasiojiweza Bukumbi, Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa BMG

KAMPUNI YA MIKAELA PROFESSIONAL TAILORS KULITAMBULISHA JIJI LA MWANZA KWENYE UBUNIFU WA MAVAZI.

September 10, 2016
Ofisi za Mikaela Professional Tailors zinapatikana Ghana Green View, barabara ya Airpot Jijini Mwanza. Wapigie kwa nambari 0767 68 28 88 ili wakuhudumie kwa wakati na kwa ubora.

Tofauti na ilivyo katika majiji mengine nchini kama vile Jijini Dar es salaam, Jiji la Mwanza halina mwamko mkubwa katika ubunifu wa mavazi.


Ni kutokana na hali hiyo, Wataalamu na Mabingwa wa Ushonaji wa mavazi ya aina mbalimbali (Kike na Kiume) Jijini Mwanza, Mikalela Professional Tailors, wameahidi kulitambulisha Jiji hilo katika ubunifu wa mavazi ili kuendana na kasi iliyopo katika majiji mengine.

"Awali nilikuwa nateseka sana. Nguo zangu nilikuwa nikishea Jijini Dar au Arusha na nikizivaa watu wengi wakawa wanauliza niliposhonea na kutamani niwapeleke. Nikaona kumbe Mwanza kuna uhitaji mkubwa wa ubunifu na ushonaji wa mavazi hivyo nikaamua kuanzisha kampuni ya ubunifu na ushonaji wa mavazi ya Mikaela Professional Tailor ili kukata kiu hiyo.