SERIKALI IMESEMA INATAMBUA VICOBA KAMA MKOMBOZI WA WANYONGE NCHINI.

November 28, 2014

Eleuteri Mangi- Dodoma
28/11/2014.
 
Serikali imesema kuwa VICOBA ni taasisi binafsi inayomilikiwa na wananchi wenyewe vikiwa ni miongoni mwa tasisi ndogo za kifedha ambazo ni za kibinafsi na huanzishwa, kuendeshwa na kusimamiwa ama kijijini, kitongojini na hata kwenye kata.

Hayo yamebainishwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Rungwe Magharibi Prof. David Mwakyusa (CCM) ambaye alitaka kujua kama Serikali inatambua VICOBA  kama mkombozi wa wanyonge.

Mwigulu amefafanua kuwa taasisi hizo zimo kwenye sekta ya fedha isiyorasmi na zinatoa huduma za kifedha mijini na vijijini.

 “Uwepo wa taasisi hizi, umewezesha kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi waliombali na huduma za sekta rasmi ya fedha na hivyo kuwa mkombozi wa wanyonge” alisema mwigulu.

Aidha, kwa kutambua suala hilo, ili kusaidia na kuimarisha taasisi hizo, Mwigulu amesema kuwa Serikali baada ya kupata ushauri kutoka kwa Mshauri Mwelekezi wa masuala ya uchumi na tafiti za kijamii, inafanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Taasisi ndogo za huduma ya fedha ya mwaka 2000 ili kuihuisha iweze kukabili na kuzingatia mabadiliko na maendeleo yanayojitokeza katika sekta hiyo.

Vilevile Mwigulu amesema kuwa Serikali inakamilisha uhuishaji wa sera ya taasisi ndogo ndogo za kifedha ambapo hatua inayofuata ni kuandaa mapendekezo ya muswada ambayo yatapelekwa Baraza la Mawaziri mara baada ya kupata idhini na maelekezo ya Baraza hilo na muswada huo utafikishwa bungeni.

Taasisi ya VICOBA ilianzishwa nchini mwanzoni mwa miaka ya 2000, ambapo imekuwa na manufaa kwa wananchi wengi wenye kipato cha chini hususan wanawake waishio vijijini wamefanikiwa kuboresha kipato chao na maisha yao kwa ujumla kwa kujiunga na taasisi hiyo.
RAIS KIKWETE AMTUMIA MKUU WA MKOA WA TANGA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

RAIS KIKWETE AMTUMIA MKUU WA MKOA WA TANGA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

November 28, 2014


Jakaya-Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Rajabu Rutengwe kuomboleza vifo vya watu 11 ambapo wengine kadhaa walijeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea tarehe 27 Novemba, 2014.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Mkanyageni Mkoani Tanga baada ya basi dogo aina ya Toyota Coaster Na. T 410 BJD iliyokuwa ikitoka Tanga Mjini kuelekea Lushoto kugongana na Lori aina ya Scania Na. T 605 ABJO.
 “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kupotea ghafla kwa maisha ya watu 11 na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea katika Mkoa wako wa Tanga”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake na kuongeza:
 “Naomba upokee salamu zangu za rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kutokana na vifo hivyo, na kupitia kwako, naomba salamu za pole ziwafikie watu wote waliopotelewa na ndugu na jamaa zao kwenye ajali hiyo”.
Rais Kikwete amesema anawaomba wote waliopoteza ndugu na jamaa zao kwenye ajali hiyo wawe watulivu na wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, na amewahakikishia kuwa yuko pamoja nao katika kipindi chote cha maombolezo.

“Kwa wote waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo, namwomba Mungu awajalie ahueni na wapone haraka, ili warejee tena katika hali zao za kawaida. Namwomba Mola azipokee na kuzilaza mahala pema peponi Roho za Marehemu wote, Amina”, amemalizia kusema Rais Kikwete katika Salamu zake.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
27 Novemba, 2014

KINANA ATAKA BAADHI YA SHERIA ZINAZOHUSU WAKULIMA WA KOROSHO ZIANGALIWE UPYA

November 28, 2014


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumpokea wakati akiwasili wilaya ya Mtwara kijijini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Mtwara vijijini ,Katibu Mkuu wa CCM anazunguka nchi nzima kufuatilia utekelezaji wa ilani na kuimarisha chama chetu.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akisisitiza wananchi wa kata ya Nanyamba kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kata ya Nanyamba ,Mtwara vijijini ikiwa sehemu ya ziara yake ya kujenga na kuimarisha Chama.
Ujenzi wa  Wodi za wagonjwa kituo cha afya kata ya Nanguruwe wilaya ya Mtwara vijijini ukiwa unaendelea kwa kasi nzuri.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa wodi ya wagonjwa ya kituo cha afya cha Nanguruwe kutoka kwa Mganga Mfawidhi Dk.Issa Lipupu,Katibu Mkuu wa CCM anaendelea kukijenga chama kwa kukagua ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kata ya Nanguruwe wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM kwenye wilaya ya Mtwara Vijijini,tarehe 20 Novemba 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kata ya Nanguruwe ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kuna sheria zinazomkandamiza mkulima inabidi zitazamwe upya kwani zisipobadilishwa mkulima atakuwa anakandamizwa kila siku na kutoona faida ya kuwa mkulima wa korosho.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye mnara wa shujaa Ahamad Mzee aliyepambana na Wareno waliokuwa wanataka kuivamia Tanzania mwaka 1972 mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.


  Wananchi wa kijiji cha Kitaya mkoani Mtwara wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye kijiji hicho kinachopakana na nchi ya Msumbiji.
 Wasanii wa kikundi cha ngoma cha Kitaya wakitumbuiza kwenye uwanja wa mikutano ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyefika kijijini hapo kujionea uhai wa chama na kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa ilani.
 Wageni kutoka nchi jirani ya Msumbiji wakisimama wakati wa utambulisho.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Kitaya wilaya ya Mtwara Vijijini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kitaya kilichopo mpakani na nchi ya Msumbiji ikiwa sehemu ya ziara yake mkoani Mtwara ambapo anakagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi pamoja na kujenga na kuimarisha chama.
 Wananchi wa kijiji cha Kitaya wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa anawahutubia wakazi wao ikiwa sehemu ya ziara yake ya kujenga na kuimarisha chama.
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile akihutubia wananchi wa Kitaya ambapo aliwaambia mipango ya maendeleo na utekelezaji wake unaendelea vizuri kwenye miradi yote ambayo iliahidiwa na serikali.
SHIRIKA LISILOKUWA LA KISERIKALI LINALOJIHUSISHA NA UHIFADHI WA MAZINGIRA NA WANYAMA PORI WORLD WIDE FUND FOR NATURE WWF KUPAMBANA NA UJANGILI NCHINI.

SHIRIKA LISILOKUWA LA KISERIKALI LINALOJIHUSISHA NA UHIFADHI WA MAZINGIRA NA WANYAMA PORI WORLD WIDE FUND FOR NATURE WWF KUPAMBANA NA UJANGILI NCHINI.

November 28, 2014
DR. SHEIN AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA NA MAKATIBU ZANZIBAR LEO

DR. SHEIN AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA NA MAKATIBU ZANZIBAR LEO

November 28, 2014

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha  Bw.Khamis Jabir Makame  kuwa  Mkuu  wa Wilaya ya Kusini Unguja  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo kabla alikuwa Mkuu wa Wilaya Kaskazini B Unguja.[Picha na Ikulu.]unnamed1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha  Bw.Haji Makungu Mgongo  kuwa  Mkuu  wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo kabla alikuwa Mkuu wa Wilaya Kusini Unguja.[Picha na Ikulu.]unnamed2 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha  Bw.Hassan Khatib Hassan kuwa  Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]unnamed3 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bi Madina  Mjaka Mwinyi kuwa Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]unnamed4 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dkt. Said Seif Mzee kuwa Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]unnamed5 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dkt. Juma Yakout Juma kuwa Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bibi Khadija Bakari Juma kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]unnamed10 
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (katikati)akiwa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa wakifuatilia kwa makini Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akiwwapisha Manaibu Katibu Wakuu Wizara mbali mbali za Serikali na Wakuu wa Wilaya mbali mbali za Unguja na Pemba  katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo, [Picha na Ikulu.] unnamed9 
Mawaziri waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Wakuu wa Wilaya mbali mbali za Unguja na Pemba pamoja na Manaibu Katibu Wakuu Wizara mbali mbali za Serikali wakifuatilia kwa makini walipokuwa wakiapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar, [Picha na Ikulu.] unnamed8 Mwanasheria Mkuu wa Serkali ya Mapinduzi ya Zanzibar Said Hassan Said(kulia) akiwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria  katika Viapo mbali mbali vya Wakuu wa Wilaya za Zanzibar na Katibu Mkuu na Manaibu Katibu wakuu wa Serikali waliapishwa leo na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, [Picha na Ikulu.] unnamed7 
MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA

MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA

November 28, 2014

unnamedWaziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 27, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
unnamed3Spika wa Bunge Anne Makinda akizungumza, Bungeni Mjini Dodoma Novemba 27, 2014. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
unnamed5Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 27, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

unnamed8
unnamed9Waziri  Mizengo Pinda  akizungumza na Mbunge wa Maswa Magaribi, John Cheyo, kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Novemba 27, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)unnamed10Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole- Sendeka kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Novemba 27, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)unnamed11Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (katikati) na Mbunge wa Lshoto, Henry Shekifu kwenye jengo la Utawala la  Bunge mjini Dodoma Novemba 27, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BILEKU MPASI KUTOKA CONGO (DRC) NA MASHUJAA BAND KUFANYA ONESHO LA PAMOJA DISEMBA 12-2014

November 28, 2014


 Rais wa Band ya Mashujaa, Chalz  Baba (kushoto), akitoa burudani mbele ya wanahabari Dar es Salaam leo, kuhusu onesho hilo litakalofanyika katika ukumbi huo.. Kutoka kulia ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Mabibo, Joseph Emanuel na Ofisa Uhusiano wa Band ya Mashujaa, King Dodo la Buche. 
 Ofisa Uhusiano wa Band ya Mashujaa, King Dodo la Buche (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu onesho hilo. Kulia ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Mabibo, Joseph Emanuel na Rais wa Band ya Mashujaa, Chalz Baba
 Meneja Matangazo wa Band ya Mashujaa, Maxmilian Luhanga (katikati), akizungumza katika mkutano huo.  
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Mabibo, Joseph Emanuel (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kampuni ya Bia ya Mabibo imedhamini onesho hilo. Kulia ni Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Mabibo, Salumu Kabanda.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.



Na Mwandishi Wetu

MWANAMUZIKI mkongwe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Bileku Mpasi, atafanya onesho maalum katika utambulisho wa nyimbo mbili mpya za bendi ya Mashujaa 

utakaofanyika Desemba 12 mwaka huu kwenye ukumbi wa Ten Lounge zamani Business Park.


Akizungumza Dar es Salaam leo  mratibu wa onesho hilo, King Dodoo la Buche, alisema kuwa Mpasi ambaye alitamba katika tasnia ya muziki wa dansi alipokuwa na gwiji, marehemu, Pepe Kale, atakuja na wasanii wengine ili kutoa burudani ya kiwango cha juu.

Dodoo alitaja nyimbo hizo mbili ambazo zitatambulishwa ni pamoja na Rafiki Sokoni na My Queen.
Aliwataka mashabiki wa muziki wa dansi nchini kujiandaa kushuhudia onyesho hilo linalotarajiwa kuwa la kihistoria hapa nchini.
Rais wa Mashujaa Musica, Chalz Baba, alisema kuwa wamejiandaa kutoa burudani nzuri na kuendeleza heshima yao ya bendi bora kwa mwaka wa pili mfululizo.


" Napenda kuwahakikishia wapenzi wa bendi yetu tutafanya kazi ya ubora wa juu, ni kawaida yetu kufanya kazi nzuri, tuna usongo,"  alisema Chalz.

Mashujaa pia itatumbuiza nyimbo zake zilizotamba katika albamu zake za Risasi Kidole na Ushamba Mzigo.

Katika onesho hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Mabibo  kupitikia kinywaji chake cha  Windhoek.

Akizungumza kwa niaba ya kampuni hiyo meneja biashara wa kampuni hiyo Joseph Emmanuel, alisema wameamua kudhamini utambulisho huo ili kuendeleza muziki wa dansi nchini kufikia hadhi ya kimataifa.

Alisema kuwa wapenzi 100 wa kwanza watakaoingia kwenye onesho hilo watapewa bia moja ya Windhoek Draught bure.

Naye Rais wa Mashujaa Chalz Baba amewataka wapenzi wajiandae kupata burudani ya aina yake katika uzinduzi. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE NDANI YA WILAYA YA TANDAHIMBA.

November 28, 2014


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Tandahimba ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa zao la korosho lina hadithi nyingi sana na njia pekee ya kuleta ukombozi kwa mkulima ni kujenga kwa viwanda vya kutosha vya kubangulia Korosho nchini.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Tandahimba ambapo aliwaambia wasihadaike na wapinzani ambao muda wao wa ujana wameutumia wakiwa CCM na uzeeni kuingia upinzani na kuanza kuhadaa watu walioishi kwa amani kwa muda mrefu.
 Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Juma Njwayo akihutubia wakazi wa Tandahimba mjini ambapo alielezea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 unavyoendelea jimboni kwake.
 Wanakwaya wa kikundi cha Nia Moja cha Tandahimba wakiimba wakati wa mkutano wa CCM uliofanyika Tandahimba ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kuimarisha na kukijenga Chama.
 Wananchi wa Tandahimba mkoani Mtwara wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye anazunguka nchi nzima kukagua na kuimarisha uhai wa Chama.
Mjumbe wa kuteuliwa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Tandahimba Jaffary Hassan Mwadili almrufu Mwarobaini akiwasalimu wananchi .
Mwarobaini alikuwa  Katibu wa  Chadema wilaya ya Tandahimba baadae akajiunga na CCM
 Wananchi wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi kwenye mkutano wa CCM Tandahimba
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaidia kubeba gunia la korosho kwenye ghala la korosho la TANECU ,Tandahimba mkoani Mtwara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipita juu ya magunia ya Korosho alipotembelea ghala la korosho la TANECU ikiwa sehemu ya ziara yake ya kujenga na kuimarisha Chama mkoani Mtwara .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia moja ya nyumbailiyoezuliwa paa na mvua yenye upepo mkali iliyonyesha jana jioni katika Kata ya Nanyanga Ndugu Saidi Mnambenga ambaye  ni mlemavu wa macho.
 Paa la nyumba ya Ndugu Abdala Athumani Mwatama likiwa chini baada ya kuezuliwa na upepo mkali jana jioni katika kata ya Nanyanga.

 Moja ya nyumba iliyoathirika na mvua za upepo katika kata ya Nanyanga wilaya ya Tandahimba ambapo nyumba zaidi ya arobaini zimeathirika na mvua hiyo

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha lundo la kadi zilizorudishwa kutoka vyama vya upinzani katika kata ya Mahuta wakati wa uzinduzi wa shina la wakereketwa Chingongola.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Mndimba wakati waujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mdimba wilayani Tandahimba.
 Katibu wa NEC itikadi na Uenezi CCM akiwataka wananchi wa kata ya Mdimba wilaya ya Tandahimba kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kwani kura ndio haki yao ya msingi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mdimba.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Mahuta huku akiwa ameshikilia kadi za wanachama wa upinzani waliorejea CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Mahuta baada ya kufungua shuna la wakereketwa waendesha boda boda Mahuta wilaya ya Tandahimba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wajumbe wa kikao cha halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tandahimba, uliofanyika Mahuta wilayani Tandahimba,Mtwara.