ESRF YATAFUTA SULUHU YA UTENGENEZAJI MIJI I

ESRF YATAFUTA SULUHU YA UTENGENEZAJI MIJI I

November 19, 2017
MANUFAA ya uchumi unaokua kwa kasi kuelekea uchumi wa kati wa viwanda hayataonekana kama taifa litakuwa na changamoto katika utengenezaji wa miji yake na hivyo kuvuna tija ya miji iliyopangwa vyema. Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka Paul Kessy wakati akifungua mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF). Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuangalia mada tatu zilizokubaliwa kufanywa kama sehemu ya kutengeneza mwongozo wa namna ya kuendesha mpango huo ili kuisaidia serikali katika kutengeneza miji salama na yenye tija. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho wakati wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Mada hizo tatu ni pamoja na kuangalia miundombinu ya miji na huduma za kifedha katika utengenezaji wa miji, mahusiano ya serikali kuu na ya mitaa ; na mada ya tatu ni namna ya kupata taarifa sahihi ili kuimarisha uwekezaji. Kessy alisema wakati serikali inatekeleza malengo ya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano (FYDP) ll , wenye lengo la kuweka mazingira sawa kwa uchumi wa viwanda na maendeleo, mpango huo wa ESRF umekuja muda muafaka kwani utasaidia kutafuta na kutoa majawabu halisi na sahihi. Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka Paul Kessy akifungua mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
Alisema kwamba kama nchi itataka kuwa na maendeleo yenye kujali binadamu ni vyema kuwa na maamuzi ya miongo yenye kuakisi uhalisia na mahali pekee kwa sasa kupata huo uhalisia ni wa kutumia mpango huo wa ESRF ambapo wanazuoni watakutana kujadili uhalisia wa mambo na kutoa mapendekezo ya kukabili changamoto. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk Tausi Kida alisema mkutano huo ambao ni wa kwanza tangu alipoamua kuwa na Tanzania Urbanisation Laboratory, Agosti mwaka huu umelenga kusaidia kutengeneza njia ya kusaidia utengenezaji wa miji salama yenye tija nchini. Alisema kwa kuwa mwenyekiti wa mpango huo ni Tume ya Mipango wao wakiratibu tu, ni dhahiri mawazo na mapendekezo yatakayokuwa yanatolewa kulingaana na utafiti yatasaidia sana kuwa na miji salama. Pichani juu na chini ni Bw. Anton Cartwright kutoka Taasisi ya Miji ya Afrika iliyopo Afrika Kusini, akitoa mada ya utangulizi wakati wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. [ Mtafiti kutoka ESRF, Jires Tunguhole (kulia) akiwasilisha mada kuhusu kuwelewa upangaji wa miji na namna fedha zinavyopatikana wakati mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dr. Wilfred Lameck, akiwasilisha mada Utafiti kuhusu mahusiano ya serikali kuu na serikali za mitaa Tanzania wakati wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Dr. Nathalie Jean-Baptiste kutoka Taasisi inayoshughulikia makazi ya watu katika Chuo Kikuu cha Ardhi, akiwasilisha mada kuhusu maisha ya kila siku ya watanzania katika miji wakati wa wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Pichani juu na chini ni washiriki wakitoa maoni wakati wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. [ Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka Paul Kessy akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida. Mtafiti Mwandamizi wa ESRF, Prof. Haidari Amani akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Dr Kate Owens kutoka World Resources Institute ya Marekani akitoa neno wakati wa kufunga mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Pichani juu na chini ni washiriki wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. [ Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto) akibadilishana mawazo na Bw. Anton Cartwright (katikati) kutoka Taasisi ya Miji ya Afrika iliyopo Afrika Kusini pamoja Dr. Kate Owens kutoka World Resources Institute wakati wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

NLUPC YAANZA KUREJEA MWONGOZO WA UPANGAJI MATUMIZI YA ARDHI YA WILAYA

November 19, 2017
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi akielezea kwa ufupi malengo ya warsha kwa ajili ya kurejea mwongozo wa upangaji,utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi ya Wilaya, Mjini Morogoro
 Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu,Sera na Mawasiliano wa Tume Bi. Albina Burra akitoa maelezo mafupi kwa Mkurugenzi wa NLUPC Dkt. Stephen Nindi kuhusiana na kazi ya kurejea mwongozo wa upangaji,utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi ya Wilaya.
 Makundi mbalimbali ya wana kikao kazi wakiwa wana rejea mwongozo wa upangaji,utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi ya Wilaya kabla ya kutoa mrejesho
 Bw. Eugine Cylio Mtaalam kutoka NLUPC akitoa mawasilisho kwa niaba kundi lake.
 Bw. Paulo Tarimo kutoka Wizara ya Kilimo akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa kusikiliza mrejesho wa majadiliano yaliyokuwa yanaendelea kutoka katika makundi mbalimbali.
 Afisa Programu kutoka Haki Ardhi Bw. Joseph Chiombola akitoa mawasilisho kwa niaba kundi lake.
 Bw. Angolile Rayson kutoka PELUM Tanzania akitoa mawasilisho kwa niaba kundi lake.
Afisa Miradi kutoka TNRF Bw. Daniel Ouma akichangia jambo kuhusu matumizi ya Ardhi na maendeleo endelevu.
 Afisa Sheria wa NLUPC Bi. Devotha Selukele akichangia jambo juu ya 'Participatory Land use Management'  (PLUM)
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Ufugaji Tanzania Bw. Joshua Lugaso (wa pilikulia) akichangia jambo kuhusu wafugaji wakati wa kikao kazi.
 Afisa Takwimu kutoka NLUPC Bi. Blandina Mahudi akichangia jambo kuhusiana na maswala ya Takwimu.
 Baadhi ya watumishi kutoka NLUPC, kuanzia kushoto ni Afisa Mipango Bw. Gerald Mwakipesile, Afisa Sheria Bi. Devotha Selukele, Afisa Tawala Bi. Nakivona Rajabu na Afisa Habari Bw. Geofrey Sima wakati wa Kikao kazi

Tume na wadau mbalimbali  kutoka Serikalini,Asasi za kiraia wamekutana Morogoro kwa ajili ya kutengeneza urejewa mwongozo wa upangaji,utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya Ardhi ya Wilaya.

Akizungumza wakati wa mchakato huo Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya mipango na Matumizi ya Ardhi(NLUPC) Dkt. Stephen Nindi alisema kuwa NLUPC  ikishirikiana na Haki Ardhi pamoja na wadau mbalimbali wanaojihusisha na upangaji, utekelezaji  wa usimamizi wa mipango ya ardhi wamekutana kwa ajili ya kuanza kupitia namna ya upangaji wa matumizi ya Ardhi ya Wilaya ambapo mwongozo huo uliandaliwa tangu mwaka 2006.

“Kutokana na mambo mengi  kutokea kwa muda wa miaka kumi na moja (11), ambayo tungependa  yawepo katika muongozo huu wa namna ya kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya Wilaya, mambo hayo yaliyojitokeza ni kama mabadiliko ya tabianchi na athari zake kuwa kubwa inayopelekea mabadiliko ya hali ya kimazingira, ushirikishwaji wa jinsia pamoja na makundi mengine madogo madogo mfano watu wanaotegemea mizizi na wanaohama hama toka sehemu moja kwenda sehemu nyengine” Alisema Dkt. Nindi.

Aliongeza kuwa  Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Magufuli anayesisitiza kuwa  Nchi iwe  ya viwanda na uchumi wa kati, na katika muongozo wa kuandaa mpango wa  matumizi ya ardhi ya Wilaya haukuupa msukumo wa viwanda. Mwongozo huu utaangalia utaratibu wa  namna gani  viwanda vitaendelea katika ardhi ya Wilaya na vijiji.

Kutokana na mabadiliko mbalimbali yaliyotokea nchini yakiwomo ya kiuchumi,kisiasa,kijamii,na ndani ya miaka hii kumi na moja kumekuwa na ukuaji wa mashamba ya saizi ya kati ekali 100 hadi 150 umeongezeka ambapo unahitaji muongozo mpya na namna ya kusimamia katika ngazi ya Wilaya,Miji mingi  watu wamezidi kuongezeka ambapo ukuaji huo unaonekana haukutiliwa mkazo wakati wa mwongozo wa awali ulio andaliwa miaka 11 iliyopita,ambapo sasa kuna kasi ya ongezeko ya ukuaji wa miji na vijiji, mwongozo huu utaangalia  namna gani mambo haya yote yataendelezwa vizuri.

Kwa upande wake Afisa Programu kutoka Haki Ardhi Bw. Joseph Chiombola ambao wanajihusisha na utafiti pamoja na utetezi wa maswala ya ardhi alisema kuwa Haki Ardhi ni jukwaa ambalo limekuwa likiendesha mijadala mbalimbali inayohusiana na maswala ya ardhi nchini Tanzania, na kwamba maswala ya matumizi ya ardhi yanahitaji mjadala mpana unaotakiwa kuwahusisha wananchi kwa ujumla.

“Moja ya malengo yetu ni pamoja na kuhakikisha kwamba kunafanyika mabadiliko ya Sera,Sheria,kanuni na miongozo mbalimbali, na hili swala la mipango na matumizi ya ardhi ni sehemu moja tunayo iangalia kwa sababu kama ikiendelezwa ipasavyo itasaidia kuweka ulinzi wa ardhi na wazalishaji wadogo ambayo ndio jukwaa tulilokuwa tukizungumzia sana kwa ajili ya haki zao kwa kipindi chote cha uwepo wetu” alisema Chiombola.

Aliongeza kuwa mipango hii ni muhimu kwa sababu inawagusa wazalishaji wa kila siku wakiwemo wakulima,wafugaji, waokota matunda,warina asali na wavuvi kwa kuwa wamekuwa wanahusika na ardhi kwa namna moja au nyengine. Hivyo mipango itakayokuwa kwa manufaa ya jamii hizo itakuwa na manufaa makubwa katika kuongeza kipato chao na kubadilisha hali ya maisha yao. 

Nae Naibu Katibu Mkuu wa wa Chama cha Wafugaji Tanzania Bw. Joshua Lugaso alisema kuwa kutengeneza urejewa mwongozo wa upangaji,utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya Ardhi ya Wilaya utakuwa ni mkombozi kwa mfugaji kutambulika katika maswala ya ardhi Tanzania jambo ambalo halijawahi kutokea kwa miaka mingi.

“Katika mwongozo huu mfugaji ameonekana sana na kuondoa dhana ya kila wakati wakulima kuonekana, tunaamini kwamba ni mpango unaoenda kufanya kazi  kwenye Wilaya tunaamini kwamba ikisimamiwa vizuri, migogoro ya wafugaji na wakulima itakwisha” alisema Lugaso.

Katika mwongozo  uliopita kulikuwa na mapungufu ambayo ni  pamoja na mkazo wa namna ya jamii zinavyokabiliana na mabadiliko ya Tabianchi haukuwa na mkazo mkubwa,hakukuwa na mkazo wa namna ya ardhi za Wilaya zinavyopangwa ili kuhakikisha kwamba kunakuwa kuna ukuwaji wa viwanda katika ardhi ya wilaya au ya vijiji, pia swala la ushirikishwaji katika upande wa jinsia na makundi madogo madogo wanaotumia ardhi ambao katika jamii hawana nguvu ya kisiasa,kiuchumi  kwa kuwa na wao wanatakiwa watambuliwe.

KABURI LAFUKULIWA MOSHI KUONDOA UTATA WA MWILI WA MTU ALIYEZIKWA BAADA YA KUOKOTWA MTON

November 19, 2017
Jeshi la Polisi likiwa limezungushia utepe eneo ambalo kuna kaburi ulimozikwa mwili ambao familia ya Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo aliyepotea ,Humphrey Makundi ulitilia shaka.
Kaburi ulimozikwa mwili wa mtu aliyezikwa na Manispaa ya Moshi baada ya kuokotwa Mto Ghona jirani na ilipo shule ya Sekondari .
Askari Polisi wakishirikiana na ndugu wa Mwanafunzi aliyepotea Humphrey Makundi wakifukua Kaburi ulimozikwa mwili wa mtu aliyeokotwa Mto Ghona katika wilaya ya Moshi.
Kaburi likifukuliwa.
Baba mzazi wa Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Scolastica aliyepotea,Jackson Makundi (Katkati) akijadili jambo na wanandugu wakati zoezi la kufukua kaburi likiendelea.
Baba mzazi wa Mwanafunzi Humphrey ,Jackson Makundi (Mwenye suti nyeupe) akitizama mwili (haupo pichani) baada ya kaburi kufukuliwa.
Baba mzazi wa Mwanafunzi Humphrey ,Jackson Makundi (Mwenye suti nyeupe) akionekana akiwa amekaa chini baada ya kutizama mwili uliofukuliwa katika kaburi .
Askari Polisi na Wanandugu wa kijana aliyepotea wakijaribu kusaidia kumnyanyua mzazi wa Mwanafunzi huyo kutoka katika eneo lilipo kaburi lililofukuliwa .
Baba mzazi wa Mwanafunzi Humphrey ,Jackson Makundi (Mwenye suti nyeupe) akisindikizwa kutoka katika eneo la Makaburi ya Karanga katika manispaa ya Moshi.
Mwili uliofukulia katika Makaburi hayo ukiwekwa katika gari la Polisi kwa ajili ya kwenda kuhifadhiwa katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC.
Gari la Polisi likiwa na mwili uliofukuliwa katika Makaburi ya Karanga.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

 UTATA umeighubika familia ya Jackson Makundi ambayo kijana wake aliyetambulika kwa jina la Humphrey Makundi,Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo kupotea katika mazingira tatanishi.

 Utata wa kupotea kwa mwanafunzi huyo unatiliwa shaka zaidi na familia hiyo baada ya kufukuliwa kwa kaburi ulimozikwa mwili uliookotwa mto Ghona mita 300 ,jirani na shule hiyo ukidaiwa kushabihiana na wa mwanafunzi huyo

  Humphrey Makundi, mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Scolastica anatajwa kupotea tangu Novemba 7 mwaka huu akiwa shuleni hapo huku wanafunzi wenzake wakiendelea na mitihani ya kidato cha Pili ya upimaji ya kitaifa .

 Familia ya kijana huyo yenye makazi yake mkoani Dodoma ikalazimika kutumia mitandao ya kijamii kutoa taarifa za kupotea kwake ikidai mazingira ya kutoweka kwake ni ya kutatanisha na baadae kuwasilisha taarifa katika kituo cha Polisi cha Himo .

Kutokana na kuwepo kwa taarifa za kuokotwa kwa mwili huo ,familia iliwasilisha maombi katika mahakama ya Hakimu Mkazi, Moshi na mahakama ikaamuru kufukuliwa kwa Kaburi hilo zoezi lililoanza majira ya saa 8:30 mchana na kudumu kwa zaidi ya saa moja.

Jeshi la Polisi liliongoza zoezi hilo katika makaburi ya Karanga huku likishuhudiwa na ndugu wa mtoto aliyepotea ambapo baada ya mwili kutolewa kaburini hali ya simanzi ilionekana katika nyuso za baadhi ya ndugu wa Mwanafunzi huyo akiwemo baba mzazi wa kijana huyo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issa akathibitisha uwepo wa tukio hilo huku akieleza kuwa tayari jeshi la Polisi linawashikilia wati 11 akiwemo mmiliki wa shule hiyo Edward Shayo huku likifanya uchunguzi wa kina kuhusu matukio hayo mawili.

Mwili uliofukuliwa katika makaburi ya Karanga upande wa marehemu wasiokuwa na ndugu ulipelekewa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya KCMC kwa uchunguzi zaidi chini ya uangalizi wa jeshi la Polisi wakishirikiana na madaktari kutoka  KCMC.

UTAFITI MAPATO NA MATUMIZI KAYA BINAFSI WAANZA TANZANIA BARA

November 19, 2017
Benny Mwaipaja

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amezindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, utakaogharimu shilingi bilioni 10 zilizotolewa na Benki ya Dunia.

Lengo la utafiti huo utakaofanywa na Ofisi Kuu ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni kupata takwimu zinazohusu shughuli za kijamii na kiuchumi, mapato na matumizi, hali ya makazi na umiliki wa rasilimali katika ngazi ya kaya.

Dkt. Mpango alisema kuwa Utafiti huo utaiwezesha Serikali kupima kiwango cha hali ya umaskini wa kipato, chakula na pengo baina ya matajiri  na maskini kuanzia kipindi cha mwaka 2013 hadi sasa.

“Takwimu zilizopo hivi sasa zinaonesha kwamba kiwango cha umasikini wa kipato ulipungua kutoka asilimia 34 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 28.2 mwaka 2012” Alisema Dkt. Mpango.

Alisema pamoja na takwimu hizo, bado kiwango cha umasikini ni kikubwa na kwamba Serikali kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali inahakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma za msingi za kijamii kwa kadri uchumi unavyokua hivyo kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo la umasikini.

“Nimefurahi kuelezwa kuwa utafiti huu utakusanya takwimu katika kaya binafsi 10,460 kwa Tanzania Bara kuanzia Novemba 2017 hadi Novemba 2018 na kwamba kupitia zoezi hili, Serikali ya Awamu ya Tano imetoa ajira kwa vijana wapata 620 katika maeneo ya vijijini na mijini” alieleza Dkt. Mpango.

Aliwaasa wadadisi hao kufanyakazi zao kwa umakini na weredi mkubwa ili takwimu zitakazopatikana ziwe sahihi na kuonya kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaojaribu kuvuruga zoezi hili.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa alieleza kuwa ukusanyaji wa Takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi utafanyika katika maeneo 754 yaliyochaguliwa kitaalamu kwa kutumia takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012.

“Utafiti huu utakuwa wa saba tangu Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961, ambapo tafuti nyngine zilifanyika 1969, 1991/92, 2001, 20117 na mwaka 2011/12” aliongeza Dkt. Chuwa.

Alisema kuwa utafiti huo mpya utafanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa ijulikanayo kama Survey Solution (CAPI) na kwamba matokeo ya awali ya utafiti huo yanatarajiwa kutolewa ndani ya miezi sita ijayo ili nchi iweze kufahamu kiwango cha umasikini uliopo katika jamii hivi sasa baada ya kufanyika kwa utafiti kama huo miaka mitano iliyopita.

“Utafiti wa mwisho uliofanyika mwaka 2011/2012 uliotumia karatasi uligharimu shilingi bilioni 20 lakini kwa kutumia teknolojia mpya, utafiti huu utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 10 pekee” alisisitiza Dkt. Chuwa.

Dkt. Chuwa alisema kuwa anaamini matokeo ya utafiti huo yatakuwa chachu ya kupata takwimu za msingi kwa ajili ya kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa program mbalimbali za kitaifa na kimataifa zenye kulenga kupunguza kiwango cha umasikini nchini.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia miundombinu ya TEHAMA Bw. Baltazar Kibola alisema kuwa watatoa ushirikiano wakutosha kwa wadadisi hao katika ngazi zote kuanzia Mikoa, Wilaya, Halmashauri, Kata, Vijiji na Vitongoji ikiwemo kufanyia marekebisho vitendeakazi vya kukusanyia takwimu hizo vikipata hitililafu ili azma ya Serikali ya kupata takwimu sahihi itimie kama ilivyopangwa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu  (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo kuhusu namna utafiti  wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi utakavyotekelezwa wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi na uzinduzi wa wa zoezi la ukusanyaji takwimu za utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi, Mjini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akimkaribisha  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kufunga mafunzo ya Wadadisi, na kuzindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za Utafiti wa Mapato na Matumizi wa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, Mjini Dodoma.

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza jambo wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi na kuzindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za Utafiti wa Mapato na Matumizi wa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, mjini Dodoma, utakaohusisha kaya binafsi 10,460.