NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, JAPHET HASUNGA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAMILIKI WA VIWANDA VYA MAZAO YAMISITU NCHINI

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, JAPHET HASUNGA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAMILIKI WA VIWANDA VYA MAZAO YAMISITU NCHINI

January 12, 2018

1m
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na  Rais wa Shirikisho la viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus  (kulia) wakati Rais  huyo  alipokuwa  akiwasilisha  taarifa  ya  wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu  wakati wa kikao   kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa  Wizara kukutana na wadau wa Wizara  kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa  
2m
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu  mara baada   kufungua kikao    kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa  Wizara kukutana na wadau wa Wizara  kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa
3m
Rais wa Shirikisho la viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus  akiwasilisha  taarifa  ya  wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga  wakati wa kikao   kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa  Wizara kukutana na wadau wa Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili.
4m
Baadhi ya  wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu  wakimsikiliza  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Japhet Hasunga  kwenye  kikao    kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa  Wizara kukutana na wadau wa Wizara  kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili
9m1
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza  kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga  kufungua  kikao cha  wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu  kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa  Wizara kukutana na wadau wa Wizara  kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili.
Picha na Lusungu Helela-MNRT
………………..
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewahakikishia wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu   nchini kuwapa ushirikiano wa kutosha pale inapohitajika kwa kuzishughulikia  changamoto mbalimbali zinazowakabili  ili kwenda sambamba na azma ya serikali ya awamu ya tano  ya Tanzania ya viwanda.
Amesema   Wizara ya Maliasili na Utalii  imedhamiria   kutatua changamoto zinazowakabili  ili kuwawezesha  wamiliki wa viwanda hivyo hasa  wazawa  kutoa  ajira nyingi kwa wananchi.
Amesema  Wizara hiyo haiwezi kufanya kazi pekee yake pasipo  kushirikiana  na sekta binafsi kwani  wao ndo wamiliki wa viwanda vinavyotoa ajira kwa wananchi ambao ndio walinzi wakubwa   misitu nchini.
Akizungumza kwenye kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, kati ya  viongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na  Wawakilishi wa Wamiliki wa Viwanda vya mazao ya misitu nchini,  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga aliwataka wadau hao  wasisite kuwasiliana nae pale wanapokuwa na jambo lolote linalohusu maendeleo ya viwanda vyao
‘’Nimechaguliwa na Mhe. Rais kuja katika Wizara hii kwa ajili ya kufanya kazi nanyi, tufanye kazi kwa ushirikiano’’ alisema Hasunga
Aidha, Naibu Waziri huyo, amelisema Serikali imeanzisha  utaratibu wa ugawaji wa vitalu   kwa njia  mnada na kwa njia  ya makubaliano binafsi  lengo lake  sio kuviua viwanda  wa mazao ya misitu vya vinavyomilikiwa wazawa bali ni kutaka kila mwenye sifa asiweze kukosa mgao huo.
Akifafanua kuhusiana na utaratibu huo mpya wa   ugawaji wa vitalu ulioanza mwaka jana , Hasunga alisema   asilimi 30 ya vitalu imekuwa ikifanyika  kwa njia ya mnada na asilimi 70 imekuwa ikifanyika kwa njia ya makubaliano binafsi hali iliyopelekea kupunguza malalamiko na pamoja na vitendo vya rushwa kwa wadau.
‘’Kila mmoja wetu hapa atakuwa shahidi hakuna hata mmoja mwenye kiwanda cha mazao ya misitu  aliyekosa mgao  kupitia  huu utaratibu mpya ulianza kutumika mwaka jana’’
Alisema kuwa licha ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa  wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu juu ya utaratibu huo mpya  ambao wengi ni wazawa kwa kushindwa kushindana na  matajiri lakini hata  hivyo utaratibu huo kwa njia ya mnada   umeisaidia  serikali k kupanga bei  stahiki ya soko katika njia ya makubaliano binafsi.
Hasunga alisema Serikali ipo tayari kupokea mawazo mapya kutoka kwa wamiliki wa viwanda hivyo kama wataona kuna umuhimu wa kuboresha utaratibu huo mpya wa ugawaji wa vitalu.
Wakati akijibu hoja za wadau hao, Hasunga aliwaagiza waandae ripoti itayoonesha changamoto zinazowakabili na kuiwasilisha ofisini kwake  ifikapo tarehe 10 mwezi ujao kwa ajili ya kufanyiwa kazi
Pia,  Aliwaagiza wamiliki wa viwandao hao kuunda  kitengo  kitakachokuwa na jukumu la  kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo  kujua masoko  pamoja na teknolojia rafiki ya  kuzalisha bidhaa zao zitakanazo na  mazao  ya misitu
Awali, Rais wa Shirikisho la viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus wakati akiwasilisha taarifa yake    ameiomba Wizara  iangalie namna ya kuwasaidia wamiliki wazawa viwanda vya mazao ya misitu  kwa vile  viwanda vilivyo vingi vimeshindwa kujiendesha kutokana na  kukosa malighafi  kwa kuwa wazao hao  wameshindwa kushindana na matajiri wakubwa wakati vitalu vinapouzwa kwa njia ya mnada.
Aliongeza kuwa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) iangalie uwezekano wa kupunguza bei za vitalu hivyo kwa kuwa viwanda vingi vimeshindwa kujiendesha kwa vile bei ya soko la mbao limeporomoka kutokana na  watu binafsi kuuza mbao kwa bei nafuu zilizotokana na miti iliyovunwa  ikiwa michanga.
Naye  Mwenyekiti wa  Chama cha  Umoja wa Wavunaji Sao Hill, Christian Ahiya, ameiomba Wizara kuona uwezekano wa kupunguza tozo 32 zinazotozwa  kwa wamiliki wa Viwanda vya mazao ya misitu kwa upande wa wilaya Mufundi  kwa kuwa hali hiyo imekuwa ukiwaumiza na kuwadidimiza.
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. MAGUFULI AHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 54 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. MAGUFULI AHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 54 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

January 12, 2018

1
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani humo.
2
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wakiwa wamesimama  wakati gwaride la heshma(halionekani pichani) lilipokuwa likipita katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani humo.
3
Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.
6
Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Mkapa akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na Rais mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.
9
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Saluti kutoka kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro mara baada ya kuhudhuria sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.
10
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wanachi mara baada ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.
11
Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akipungia mkono wakati akiwasili katika uwanja wa Amani.
12
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA wakipita mbele ya jukwaa kuu katika maandamano ya sherehe za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
13
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar.
14
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika uwanja wa Amani mara baada ya kuhudhuria sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
19.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amani kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
20
Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la Heshma katika  sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zolizofanyika katika uwanja wa Amani.
21
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zolizofanyika katika uwanja wa Amani.
PICHA NA IKULU


KAMPUNI YA PREMIUM AGRO CHEM LTD YASAMBAZA MBOLEA MASAA 24 KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS MAGUFULI

January 12, 2018
 Meneja Biashara na Masoko wa  Kampuni ya Premium Agro Chem Ltd, Brijesh Barot (kulia), akiangalia upakiaji mbolea uliofanyika katika maghala ya kampuni hiyo, Vingunguti jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Mbolea ikipakiwa katika malori tayari kwa safari ya kupelekwa mikoani.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Premium Agro Chem Ltd imeendelea kutekeleza agizo la Rais Dk.John Magufuli kwa kusambaza mbolea kwenda mikoani kwa masaa yote bila ya kujali mapumziko ya Sikukuu ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar inayofanyika leo nchini kote.

Akizungumza na waandishiwa habari wakati akisimamia upakiaji wa mbolea hiyo kwenye maghala ya kampuni hiyo yaliyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam leo, Meneja Biashara na Masoko wa kampuni hiyo, Brijesh Barot, alisema kwamba kwa jana wamesambaza mifuko 20,563,000 sawa na tani 1,028 na kuwa mbolea hiyo inasambazwa   kupitia kwa mawakala wao.

"Tunaendelea kusambaza mbolea kwa mikoa yote, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Rukwa, Songwe na Katavi, kupitia kwa mawakala pamoja na kuwatumia maafisa wetu walio katika vituo vya matawi yetu huko kwa ajili ya kuharakisha upatikanaji wa mbolea kwa wakulima vijijini," alisema Barot.

Barot alisema kuwa kwa leo watasambaza mifuko 1,200 sawa na tani 600 na hiyo ni kwa mbolea aina ya Urea ambapo alisema usambazaji unaendelea vizuri.

Alisema kampuni yao inafanyakazi kazi hizo kizalendo ndiyo maana wamekubali kuuza kwa bei elekezi mbolea ambayo wao walikuwa wameinunua muda mrefu kabla ya kutolewa kwa maagizo ya kununua kwa mfumo maalum wa serikali, na hili linafanywa kwa kumuunga mkono Rais Dkt Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa.


CCM HAKUNA SABABU YA KUFANYA KAMPENI 2020 TUNAHITAJI KUPITA BILA KUPINGWA: KHERI JAMES

January 12, 2018
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza na Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal

Wajumbe wa Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018. 
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James (Kulia) akieleza umuhimu wa wakazi wa Kata ya Kimandolu kumchagua Ndg Gaudence Limona kuwa diwani wao wakati akizungumza na Timu mbalimbali za kampeni kwenye kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018.
 Kikao kikiendelea
Wajumbe wa Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018. 

Na Mathias Canal, Arusha

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James amesema kuwa CCM haina sababu ya kufanya kampeni katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 badala yake kuna kila sababu ya kupita bila kupingwa kutokana na uimara wa CCM na serikali yake.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa ameyasema hayo Leo 12 Januari 2018 wakati akizungumza na Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu.

Kheri alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kutatua kero zote zisizo rafiki kwa wananchi kwa utekelezaji wa Mkataba wa wananchi na CCM kupitia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020.

Kheri aliwataka wananchi kujitokeza kwa mwingi kupiga kura hapo kesho 13 Januari 2018 kwani ni haki yao ya msingi kikatiba lakini pia aliwakumbusha kuwa katika uchaguzi huo wananchi wanapaswa kumchagua Diwani wa CCM kwa ajili ya maendeleo endelevu kwa ajili ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla wake.

Katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika kesho katika Kata ya Kimandolu Ndg Gaudence Limo ndiye mgombea wa CCM ambaye aliwahi kuwa Meya wa Jiji la Arusha.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti Kheri alivifananisha vyama vya upinzania nchini Tanzania na waharamia ambao kazi yao kubwa ni wizi na ujambazi, ujangili, udokozi, utapeli na uongo hivyo kupitia ulaghai wao haviwezi kufanikiwa kushika dola kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Aliwasihi vijana kukumbuka majukumu yao kama nguvu kazi ya Taifa kuwa ni pamoja na kusema ukweli, kuwajibika na kuwa watendaji na viongozi madhubuti sio viongozi biskuti.

Aidha, Kheri amewafikishia wakazi wa Arusha salamu za Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuwa anahitaji ushindi wa kishindo wa zaidi ya kura 12,000 na hiyo itakuwa zawadi pekee kwake.

“Ndugu zangu sisi wana CCM tunaweza kujadiliana harusi itafungwa vipi na wapi, tunaweza tukajadiliana aina ya magari ya kununua lakini hatuwezi kuwa na mjadala wa namna yoyote ile kwenye utafutaji wa dola ni lazima CCM ishinde” Alikaririwa Kheri

LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWA MDAU MUGANYIZI BISHEKO

January 12, 2018
 
Leo January 12, 2018 ni siku ya kuzaliwa kwa Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank of Africa Tanzania, Muganyizi Bisheko. Wote kwa pamoja tunapenda kukutakia heri na fanaka. Mwenyezi Mungu akujalie maisha marefu.


KAIMU MKURUGENZI UZALISHAJI MIFUGO NA MASOKO WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI DK. ASSIMWE RWIGUZA ASHIRIKI UPIGAJI CHAPA MIFUGO KATIKA MKOA WA SHINYANGA

January 12, 2018
 Kaimu Mkurugenzi wa uzalishaji  Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Dk. Assimwe Rwiguza akipigaji chapa ng’ombe katika Kijiji cha Idodoma Wilaya ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu 15 wa mifugo walioko katika mikoa 26 kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa linalotarajiwa kukamilika January 31 mwaka huu.
 Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Dk  Asimwe  Rwiguza akitoa ufafanuzi wa mahali sahihi panapotakiwa kupiga chapa kwa ng'ombe kwa wafugaji wa Kijiji cha Idodomya wilayani Shinyanga. kushoto ni Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya Shinyanga, Dk. Clement Batisiliko
Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Dk.  Asimwe  Rwiguza akitoa ufafanuzi kwa wafugaji wa Kijiji cha Idomya umuhimu wa kupiga chapa mifugo yao kabla ya muda wa nyongeza uliowekwa na Serikali kumalizika wa Januari 31 mwaka huu ambapo Dk. Assimwe ni miongoni mwa timu ya wataalamu 15 wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi walioko kwenye mikoa 26 ya Tanzania bara kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa.