IPTL NA PAP WACHANGIA MILIONI 10 KUUNGA MKONO KAMPENI YA IMETOSHA

IPTL NA PAP WACHANGIA MILIONI 10 KUUNGA MKONO KAMPENI YA IMETOSHA

March 15, 2015
Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (kushoto) akimkabidhi balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 fedha waliyoitoa kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam. Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (kushoto) akimkabidhi balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 fedha waliyoitoa kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam.Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege. Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (wa pili kulia) akizungumza na wanahabari katika hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu. Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (wa pili kulia) akizungumza na wanahabari katika hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu.Baadhi ya viongozi na wajumbe wa kamati ya utendaji ya Imetosha Foundation wakipiga picha na hundi ya shilingi milioni 10 fedha iliyotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Wa kwanza kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege. Baadhi ya viongozi na wajumbe wa kamati ya utendaji ya Imetosha Foundation wakipiga picha na hundi ya shilingi milioni 10 fedha iliyotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Wa kwanza kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.
Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege

 Na Mwandishi Wetu  
KAMPENI maalumu za kupinga mauaji ya watu wenye u-albino nchini inayojulikana kama 'Imetosha' iliyoanzishwa na balozi wa kujitolea, Henry Mdimu, chini ya Imetosha Foundation zimezidi kushika asi baada ya makampuni ya IPTL na PAP kutoa shs milioni 10 kusaidia kampeni hizo. 

 Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege jana alimkabidhi balozi Mdimu mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 kama ishara ya kuunga mkono kampeni hizo za kutoa elimu kutokomeza imani potofu zilizojengeka kwa baadhi ya wanajamii juu ya watu wenye albino.

 Akizungumza katika hafla hiyo fupi Bw. Makandege alisema matukio ya mauaji au kukatwa viungo kwa watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino yamefika hatua ya kutisha nchini Tanzania, hususani katika kanda ya ziwa hivyo kuna kila sababu kila mmoja bila ubaguzi kushiriki kusaidia mapambano hayo. 

 Alisema ulemavu wa ngozi waliyonao watu wenye albino ni mapungufu ya kibaiolojia ambayo ni mapenzi ya Mungu hivyo imani potofu zinazoendelea hazina budi kupigwa vita kwa nguvu zote. "...Kuna minongono mitaaani kwamba watu wanatenda matukio hayo wana imani potofu kwamba ukitumia kiungo cha mtu mwenye albinism, ndipo utafanikiwa. 

Kama kweli viungo vyao vingekuwa vinaleta utajiri, basi watu wenye albinism wangekuwa matajiri namba moja duniani," alisema Makandege akizungumza.

 "...Sisi IPTL na PAP tumeguswa sana na jambo hili. Kwa wote wanaofanya matendo haya, mnapaswa kuwa na hofu ya Mungu mkijua kuwa siku ya kihama, kila mtu atajibu na kuhukumiwa kwa matendo yake. 

Tunakubaliana kabisa na wenzetu IMETOSHA Foundation kwamba, imefika wakati kila Mtanzania, na hata wageni waishio Tanzania, kusema IMETOSHA na kusimama kidete kuwalinda hawa ndugu zetu," alisisitiza kiongozi huyo wa IPTL. 

Aidha kampuni za IPTL na PAP zimeyataka makampuni mengine nchini na watu binafsi kuungana kwa kuchangia harakati hizi za imetosha ili kusaidia kampeni ya imetosha kupita mikoa ya kanda ya ziwa kupaza sauti na kuielimisha jamii juu ya uwepo wa imani potofu zinazoendeleza mauaji ya watu wenye u-albino. 

Kwa upande wake Balozi wa Imetosha, Mdimu aliishukuru kampuni za IPTL na PAP kwa moyo wauliouonesha wa kusaidia harakati hizo na kumtaka kila Mtanzania kwa nafasi yake kusaidia kupaza sauti kwamba imetosha mauaji na unyanyasaji wanaoupata watu wenye ualbino. 

Alisema mauaji haya yanamgusa kila Mtanzania na kuendelea kuichafua nchi yetu hivyo kumtaka kila mmoja kupaza sauti yake kupinga vitendo hivyo. 

Machi 28, 2015 Imetosha Foundation inatarajia kufanya matembezi ya hisani kuchangisha fedha zaidi ili kusaidia kampeni za kukomesha mauaji ya watu wenye u-albino kabla ya kuanza rasmi safari za kuzunguka katika mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na wasanii waliojitolea kueneza elimu hiyo kwa jamii moja kwa moja.
Chakula cha usiku kuchangia fedha za ujenzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, tawi la Dar Es Salaam, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa Ijumaa, Machi 12, 2015

Chakula cha usiku kuchangia fedha za ujenzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, tawi la Dar Es Salaam, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa Ijumaa, Machi 12, 2015

March 15, 2015


1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  na viongozi wengine meza kuu wakati wa  sala ya Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani la Kanisa hilo, Askofu Alex Malasusa pamoja na wachungaji wengine wa KKKT wakati wa chakula cha usiku kuchangia fedha za ujenzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, tawi la Dar Es Salaam, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa Ijumaa, Machi 12, 2015. Katika uchangiaji huo, Rais Kikwete aliwezesha kupatikana kwa sh. bilioni 1.6 mbali na ahadi na fedha zitakazopatikana kutokana na bidhaa zilizouzwa kwa njia ya mnada.
2
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani la Kanisa hilo, Askofu Alex Malasusa pamoja na wachungaji wengine wa KKKT wakati wa chakula cha usiku kuchangia fedha za ujenzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, tawi la Dar Es Salaam, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa Ijumaa, Machi 12, 2015. Katika uchangiaji huo, Rais Kikwete aliwezesha kupatikana kwa sh. bilioni 1.6 mbali na ahadi na fedha zitakazopatikana kutokana na bidhaa zilizouzwa kwa njia ya mnada.
PICHA NA IKULU

ZIARA YA KINANA NGORONGORO

March 15, 2015


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wanakijiji cha Ngaresero kilichopo kata ya Loliondo
  • Wananchi wamuelezea matatizo yao ya ardhi ,maji,barabara na mawasiliano ya simu
  • Aahidi kuwakutanisha wananchi na Waziri wa Ardhi na Waziri wa Maliasili
  • Awapongeza wananchi hao kwa umoja na mshikamano wao

Zakayo Sironga Oloidimaye mkazi wa kata ya Ngaresero
,Ngorongoro ,akiuliza swali linaluhusu mipango ya kuwaletea hudumaza mtandao
ili waweze kupiga simu kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye
mkutano wa mapokezi uliofanyika Ngarasaoo ikiwa sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu
wa CCM kupita jimbo kwa jimbo , wilaya kwa wilaya nchini lengo likiwa
kuimarisha Chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.

 Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Ngaresero kilichopo Loliondo wilaya ya Ngorongoro.


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Elias Ngorisa ambaye pia ni diwani ya kata ya Malambo akizungumzia mipango ya halmashauri kusaidia kushuriki ujenzi wa madara katika shule ya sekondari Samunge
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Samunge kabla ya kushiriki ujenzi wa shule ya sekondari Samunge wilayani Ngorongoro
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi  wa madarasa ya kidato cha tano na cha sita katika shule ya sekondari ya Samunge kulia ni Mbunge wa Ngorongoro, Saning’o Ole Telele
 Watoto wa kimasai wa kijiji cha Mdito wakiwa juu ya kichuguu wakiangalia msafara wa Katibu Mkuu wa CCM (haupo pichani)ukipita kijijini kwao .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Loliondo Sakala.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa tank la maji katika kijiji cha Loliondo Sakala.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM kijiji cha Wasso Ndugu Revocatus William Parapara.Awali ndugu Revocatus Willim Parapara alikuwa Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Ngorongoro kwa takribani miaka 15.
 Wananchi wa Kata ya Wasso wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Wasso wilaya ya Ngorongoro.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wanakijiji cha Ngaresero kilichopo kata ya Loliondo

OBRIGADO KUTUA TAMASHA LA PASAKA 2015

March 15, 2015

Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki kuhusiana na ujio wa mwimbaji nyota kutoka Afrika Kusini Thori Mahlangu (Obrigado). (Picha Francis Dande)
 Msama akifafanua jambo.
…………………………………………………. 
Na Loveness Mboje
RAIA  wa Afrika Kusini
ambaye ni Mwanamziki wa nyimbo za injili, Thori Mahlangu (Obrigado),
amethibitisha kuwa mmoja wa waimbaji wa kimataifa watakaotumbuiza katika
Tamasha Pasaka litakalofanyika Aprili 5.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha
hilo, Alex Msama alisema kuwa sambamba na mwimbaji huyo ataambatana na waimbaji
wengine 16 kutoka nchini humo huku Faustine Munishi maarufu kwa jina la Malebo na
Solomon Mukubwa  kutoka nchini Kenya nao watakuwepo.
Msama alisema kuwa viingilio vya tamasha hilo kwa watoto vitakuwa shs. 2,000 viti vya kawaida shs.5,000 VIP B, shs. 10000 VIP A shs. 20,000 kwa watu wakubwa na kuongeza kuwa mara baada
ya tamasha hilo, Aprili 12 itakuwa ni zamu ya wakazi wa jiji la Mwanza katika Uwanja wa  CCM Kirumba.
Aidha kwa upande wa waimbaji wazawa  Msama amesema kuwa mwimbaji Joshua Mlelwa ambaye alikuwa
mwimbaji wa Upendo Group  naye atapamba tamasha hilo ambalo linasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki.
Tamasha hilo linatimiza
miaka 15 tangu lianzishe na linatarajiwa kihudhuriwa na watu mbalimbali kutoka
nchi za Kenya, Uganda,Rwanda, Afrika Kusini Uingereza na
wenyeji Tanzania.

MASHINDANO YA NSSF MEDIA CUP 2015 YAFUNGULIWA

March 15, 2015
 Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa mashindano ya NSSF Media Cup 2015, yaliyoanza kulindima katika viwanja vya Sigara, Chang’ombe Dar es Salaam leo asubuhi.
  Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akihutubia baada ya kufungua mashindano hayo.
 Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (katikati), akiwa meza kuu na viongozi mbalimbali waliohudhuria ufunguzi wa mashindano hayo. Kutoka kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,Ludovick Mrosso, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini NSSF, Abubakar Rajab, Mkurugenzi Rasilimali Watu, Chiku Matessa na Mkurugenzi wa Uthamini na Usimamizi wa Hadhara, Sadi Shemliwa.
 Kikosi cha Timu ya Free Media kilichofungua mashindano hayo kwa kucheza na Shirika la Utangazaji Tanzania TBC.
 Kikosi cha Shirika la Utangazaji Tanzania TBC kilichomenyana na Free Media na kuibuka washindi wa bao 1-0 na kuendelea na mashindano hayo.
 wadau wa michezo wakifuatilia mashindano hayo.
 Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (katikati), akiwasalimia wachezaji wa timu ya Netball ya NSSF.
 Wachezaji wa timu ya Netball ya NSSF wakimsikiliza mgeni rasmi Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga.
Mchezaji wa timu ya Free Media, Moses Magwai (kushoto), akimtoka Shaban Kassim wa TBC wakati wakimenyana leo viwanja vya Sigara jijini Dar es Salaam.
Mkutano Mkuu wa TASWA umepangwa kufanyika Julai 25 na 26 mwaka huu mkoani Morogoro

Mkutano Mkuu wa TASWA umepangwa kufanyika Julai 25 na 26 mwaka huu mkoani Morogoro

March 15, 2015

images 
KAMATI YA Utendaji y Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ilikutana Dar es Salaam jana na kujadili masuala mbalimbali.     
A; MAFUNZO
Kikao kilikubaliana watafutwe wataalamu wa kuendesha mafunzo kwa kada mbalimbali za waandishi wa habari za michezo nchini ili kuongeza ufanisi katika namna ya kuripoti habari za michezo michezo mbalimbali.
Kundi la kwanza litakuwa la waandishi chipukizi ambao wapo chini ya miaka mitano katika taaluma, ambapo mafunzo yao yatafanyika Machi 25 mwaka huu Dar es Salaam yakishirikisha waandishi wa habari chipukizi 30 na wa kada ya kati 10.
Tayari TASWA imepata mdhamini wa mafunzo hayo na kinachofanyika hivi sasa ni uteuzi wa washiriki, ambapo wahariri wa habari za michezo watahusishwa kupendekeza washiriki kutoka katika vyombo vyao.
Wakufunzi wa semina hiyo watakuwa waandishi wa habari wakongwe, walimu wa uandishi wa habari na wataalamu wa michezo mbalimbali nchini. Jumatano Machi 18 TASWA itatangaza mdhamini wa mafunzo ya Dar es Salaam pamoja na majina ya washiriki.
 Awamu ya pili pia itafanyika Dar es Salaamwaandamizi ikihusisha waandishi wa habari za michezo wa kada ya kati 30 na waandishi wa habari waandamizi 10 na itafanyika mwanzoni mwa Mei mwaka huu.
Awamu ya tatu itahusisha waandishi wa habari za michezo waandamizi na wahariri wa habari za michezo na jumla yao itakuwa 40 na  itafanyika mkoani Mtwara Mei 29, 30 na 31 mwaka huu. TASWA ipo hatua za mwisho za mazungumzo na wadhamini wa mafunzo hayo ya Mtwara.
     B; MKUTANO MKUU
Mkutano Mkuu wa TASWA umepangwa kufanyika Julai 25 na 26 mwaka huu mkoani Morogoro, ambapo pamoja na mambo mengine utajadili Rasimu ya Katiba mpya ya chama hicho.
 
Kamati ya Utendaji ya TASWA imeteua kamati maalum ya kushughulikia katiba hiyo, ambapo hivi sasa Katibu Mkuu anawasiliana na wajumbe walioteuliwa katika kamati hiyo na baada ya wote kupewa barua na kukubali uteuzi atatangaza majina hayo.
 
C: Kamati ya Faraja
 
Kikao kilikubaliana kuwa iundwe Kamati ya Faraja kwa ajili ya kuwafariji wanachama wake kutokana na matukio mbalimbali yanayowakuta ikiwemo ugonjwa.
Uamuzi huo umechukuliwa kwa nia ya kuhakikisha waandishi wa habari za michezo wanakuwa wamoja kwa shida na raha kwa vile wamekuwa kama ndugu.
Kwa kuanzia TASWA inawaomba wadau wote kushirikiana na kamati hiyo ambayo jukumu lake la kwanza itakuwa kumsaidia mwandishi mkongwe nchini, Masoud Sanani, ambaye waandishi wengi kwa namna mbalimbali wamepita mikononi mwake.
Sanan hivi sasa ni mgonjwa kwa zaidi ya mwaka mmoja na yupo kwao Zanzibar, ambapo juzi niliwasiliana naye na amesema afya yake inazidi kuimarika siku hadi siku.
Kutokana na hali hiyo TASWA kwa kushirikiana na kamati hiyo imepanga kwenda kumjulia hali Jumapili Machi 22 mwaka huu.Tunaomba wadau waipe ushirikiano kamati yetu.
Walioteuliwa katika kamati hiyo na nafasi zao kwenye mabano ni Angela Msangi (Mwenyekiti), Majuto Omary (Katibu), Zena Chande (Mhazini),  Asha Kigundula, Isakwisa Mwaifuge  na Elias Kambili (Wajumbe).
 
D;MEDIA DAY
Maandalizi kuhusiana na bonanza kwa wanahabari yanaendelea na matumaini ni kuwa litafanyika Aprili 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam kama ilivyopangwa.
 
E;MSIBA WA KOCHA MARSH
TASWA imepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha aliyepata kuwa Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Sylivestre Marsh, hivyo inatoa pole kwa familia na wanamichezo wote hapa nchini katika kuomboleza kifo cha kocha huyo.
 Marsh atakumbukwa na waandishi wa habari za michezo kutokana na ukaribu wake na alikuwa na ushirikiano wa kutosha pale alipoombwa kufanya hivyo.

27 WAITWA STARS KUWAVAA MALAWI

March 15, 2015

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars ) Mart Nooj, ametangaza kikosi cha wachezaji 27 watakaoingia kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi utakaofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijin Mwanza Machi 29, 2015.

Taifa Stars inayotarajia kucheza na The Flames mwishoni mwa mwezi huu, itaingia kambini machi 22 machi  katika hotel ya Tansoma kujiandaa na mchezo huo kabla ya kuelekea jijini Mwanza machi 24 kwa maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo.

Wachezaji walioitwa kuingia kambini kujiandaa na mchezo huo ni; Magolikipa,  Deogratius Munish (Yanga), Aishi Manula na Mwadini Ali (Azam FC), walinzi ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris (Azam FC), Mwinyi Haji (KMKM), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Oscar Joshua (Yanga), Abdi Banda na Hassan Isihaka (Simba SC).

Viungo ni Frank Domayo, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Mcha Khamis (Azam FC), Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo (Stand United), washambuliaji Mwinyi Kazimoto (Al Markhiry - Qatar),

Saimon Msuva , Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta (Tp Mazembe - Congo DR), John Bocco (Azam FC), na Juma Luizio (Zesco United - Zambia)

Timu ya Taifa ya Malawi inatarajiwa kuwasili jijini Mwanza machi 27, 2015 ikiwa na kikosi kamili, wakiwemo wachezaji nane wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini, Msumbuji, Congo DR na Zimbambwe.

Malawi inashika nafasi ya 91 katika viwango vipya vya FIFA Duniani vilivyotolewa mwezi huu, huku Tanzania ikipanda kwa nafasi saba na kushika nafasi ya 100.

TFF YAMALIZA MKUTANO MKUU

March 15, 2015
   
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) jana limefanya Mkutano Mkuu wa Mwaka katika ukumbi wa Morogoro hoteli ya mjini Morogoro ambapo mgeni Rasmi alikua ni mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr Rajabu Rutengwe.

Katika hotuba yake kwa wajumbe wa mkutano huo, Dr Rutengwe aliushukuru uongozi wa TFF nchini kwa kuweza kuandaa mkutano mkuu mzuri na wa kisasa ambao pia ulifanyikia katika mkoa wake wa Morogoro.

Akiongea na wajumbe wa mkutano mkuu Dr Rutengwe alisema, TFF ina changamoto ambazo inapaswa kuzifanyia kazi kwa kushirikiana na wadau wa mpira wa miguu nchini kwa ujumla, changamoto hizo ni kukosekana kwa wataalamu wa vyakula, wataalamu wa tiba na wataalamu wa saikolojia.

Dr Rutengwe aliomba TFF kwa kushirikiana na serikali inapaswa kuandaa wataalamu wengi wa masuala hayo ili kuweza kuendana na mahitaji ya kuwaanda wanamichezo bora ambao watakua tayari kwa ushindani na sio ushiriki.

Aidha mkuu wa mkoa huyo aliipongeza Kamati ya Utendaji ya TFF kwa kuupa mkoa wa Morogoro uenyeji wa mkutano mkuu ambapo pia umefanyika na  malengo kufanikiwa kwa asilimia mia moja, na kusema kwa niaba ya serikali ya mkoa wapo tayari kupokea tena mwaliko wa uenyeji wa mikutano mbalimbali ya TFF.

Mkutano ulijadili Ajenda za kawaida ambazo ni Kufungua Mkutano ni Uhakiki wa Wajumbe,  Kuthibitisha Muhtsari wa Mkutano Mkuu uliopita, Yatokanayo na Mkutano uliopita, Hotuba ya Rais, ripoti kutoka kwa Wanachama,  Kuthibitisha ripoti ya utekelezaji wa Kamati ya Utendaji.
Zingine ni Kuthibitisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu 2013, Kuthibitisha ripoti ya Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu, Kupitisha bajeti ya 2015, Marekebisho ya Katiba,  Mengineyo na  Kufunga Mkutano.
Kwa mara ya kwanza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limepata bendera yake ambayo ilipitishwa na mkutano mkuu na asubuhi ya jumapili Machi 15 mwaka huu, imepandishwa kwa mara ya kwanza Morogoro hoteli.
Aidha wajumbe wa mkutano mkuu pia wamepitisha azimio la kuanzishwa kwa mfuko wa maendeleo ya mpira wa miguu nchini (FDF), ambapo kutaundwa kamisheni maalum itakayoshugulikia suala hilo.
Lengo la kamisheni hiyo ni kuisaidia TFF kuandaa na kuratibu mipango ya maendeleo ya soka la watoto, vijana, wanawake nchini na kuviwezesha vyama vya soka vya mikoa (FA), vyama shiriki vya TFF kujiendesha katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya soka la vijana.
Pia mkutano mkuu huo ulitoa azimio la kuitaka serikali itoe msamaha wa kodi kwa vifaa vya michezo hasa vinavyotumika kufundishia watoto michezo.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe 125 na kati yao wajumbe watano ni wanawake.
Kikao kijacho cha mkutano mkuu kitafanyika kati ya mwezi Novemba na Disemba mwaka huu.

MWANDISHI KAMBI MBWANA AWASHUKURU KWA KUMUUNGA MKONO

March 15, 2015
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Jana ilikuwa ni Machi 14 mwaka 2015. Machi 14 ni siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwangu baada ya kutimiza miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwangu. Ingawa nafurahia kuzaliwa huko, lakini hudhuni inamea nifikiriapo kila ninachokifanya leo au nitakachofanya kesho nikiwa na uhai, hakitaaweza kuonwa na baba yangu, mzee Mbwana Hemed Masoud, maarufu kama Mzee Kajembe.

Kambi Mbwana, pichani
Mzee huyo aliyefanikisha uwapo wangu duniani akishirikiana na mwanamke jasiri na mkarimu na mwenye upendo kwa familia yake na jamii kwa ujumla, Bi Fatuma Omary, alifariki mwaka 2012 katika Hospitali ya Wilaya Korogwe (Magunga) na kuzikwa kijijini kwake Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Lala pema peponi baba yangu. Baada ya kusema hayo, nachukua fursa hii kuwatakia kheri wote walionitakia kheri ya kuzaliwa hiyo jana. Nimekuwa mwenye furaha kubwa nionapo jamaii yangu inaniheshimu na kunithamini. Kila nionapo mtu anayeguswa na mwenendo wangu, hakika nafarijika kupita kiasi.
Mdau wa Maendeleo na mmiliki wa mtandao wa Handeni Kwetu, akizungumza jambo katika moja ya matukio aliyoandaa likiwamo la NSSF Handeni Kwetu lilofanyika mwishoni mwa mwaka jana, wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Nimekuwa nikifanya mambo mengi kwa ajili ya kuitumikia jamii na Tanzania kwa ujumla. Kama ilivyokuwa kawaida ya mambo mazuri hayakosi changamoto, nimekuwa nikitatizwa na baadhi ya mambo ambayo mwisho wa siku yanakuwa kama funzo kwangu.

Funzo hilo ni kuona naendelea kuishi kwa kufanya juhudi zote kama nilivyopanga bila kuona wangapi wananikubali na wangapi wananichukia. Nimeamua pia kukaza msuri kuanzisha vitu ambavyo ni active vyenye mchango na jamii yangu.

Mwaka 2013 nilianzisha tamasha la Handeni Kwetu linalofanyika kila mwisho wa mwaka, yani Desemba. Mwaka huu likifanyika litakuwa ni mara ya tatu mfululizo. Aidha, sehemu ya bajeti ya tamasha hilo kwa mwaka jana, pia lilitumika kugharamia safari vijijini na baadhi ya viongozi wa taasisi ya Handeni Kwetu Foundation, ambayo ni miongoni mwa waasisi kwa nia ya kuikomboa jamii ya Handeni na Tanzania kwa ujumla.

Nashukuru kwa ushirikiano mkubwa ninaopata kutoka kwa wana jamii yangu, wakiwamo wa wilayani Handeni, mkoani Tanga, bila kusahau Watanzania wote. Nawashukuru viongozi wa serikali wanaoshirikiana na mimi. Nawashukuru pia viongozi wa vyama vya siasa, mashirika na taasisi zote za serikali na zisizokuwa za kiserikali.

Kwa heshima ya kipekee niwashukuru Mfuko wa Hifadhi ya jamii (NSSF) na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services kwa kuniunga mkono katika mambo mengi, hususan tamasha la NSSF Handeni Kwetu 2015.

Nawashukuru pia ndugu zangu waandishi wa habari, vyombo vya habari kama vile radio, magazeti, televisheni na bloggers ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakinisaidia mno kutangaza kile ninachofanya au ninachokusudia kukifanya.

Wakati naendelea kusema hayo, naomba Watanzania wenzangu tujiandikishe kwa wingi kwenye daftari la kudumu la kupiga kura ili tupate haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu ujao utakaofanyika Oktoba mwaka huu. Kujiandikisha kwetu pia kutatupa nafasi ya kushiriki katika kuipigia kura Katiba Pendekezwa.

Mchakato huo wa kura ni muhimu kwa mustakabali wan chi yetu. Kamwe asitokee mtu wa kutuhadaa kwamba tuache kuipigia kura Katiba wala kuacha kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu ujao. Kupiga kura ni haki ya msingi kwa wananchi wote.

Hata kama huitaki Katiba hiyo au mgombea wa udiwani, mbunge na urais, ila dawa si kususa bali kupiga kura ya kukataa kama sheria zinavyosema. Najua wapo baadhi ya wanasiasa wanapita pita kutupumbaza kwamba Katiba haina tija, kwamba haijakamilika na kuongea kila wapendacho wao. Mimi nasema Katiba yetu pendekezwa ni nzuri na imezingatia mambo yote yenye tija kwa Watanzania wote.

Kwa wale ambao hawajafanikiwa kuisoma, watafute namna ya kuisoma ili wajiridhishe kabla ya kuipigia kura ya ndio au hapana. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete atakumbukwa kwa kitendo cha kufanya bidii kubwa kuhakikisha kwamba mchakato huo wa Katiba mpya unafanyika kwa mafanikio.

Pia atakumbukwa kwa kufanikisha mambo mengi mazuri ndani ya utawala wake kama vile shule za Kata kuendelezwa na kujengwa maabara, barabara, vituo vya afya na Hospitali nyingi kujengwa bila kusahau miradi mikubwa kuanzishwa itakayokuwa na tija kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naamini mambo mengi yaliyoanzia kwenye kipindi cha uongozi wake yataendelezwa hata pale atakapofikia mwisho wa utawala wake. Namaliza kwa kuwaomba tena ushirikiano ndugu zangu Watanzania juu ya mambo yote nifanyayo na nitakayopenda kuyafanya siku hadi siku kwa kipindi cha mwaka huu na miaka mingine ijayo.

Najua ninayo nafasi kubwa ya kuifanyia mambo mema nchi hii. Najua pia ninayo kiu na shauku ya kuona akili yangu, kichwa change na mikono yangu inachangia kwa kiasi kikubwa kuwapatia nuru wengine walionizunguuka.

Itakapotokea napatwa na tatizo, naomba ndugu zangu tuendelee kushirikiana kwa kuniombea, kunisaidia na sio kunililia kwa naamna yoyote ile. Pamoja na changamoto kadhaa ninazokutana nazo hususan za baadhi ya viongozi wasiopenda kuona nafanya mambo makubwa kwenye nchi hii, lakini kwa dua zenu, utu wenu, ushirikiano wenu naamini kwa pamoja tutaweza kumpiga adui yetu huyo na kuambulia aibu. Nawashukuru wote mlionitakia heri ya kuzaliwa kwangu na hata wale walioshindwa kufanya hivyo mmewakilishwa na wengine. Nitashindwa kuwataja kwa majina yenu wote, maana ni wengi mlionitumia ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu yangu na kwenye mitandao ya kijamii kuonyesha mapenzi yenu kwangu. Asanteni sana. Sina cha kuwalipa, ila Mungu pekee ndiye wa kuwalipa.

Mwisho kabisa naomba tufanye kazi kwa bidii kujenga uchumi wa nchi yetu. Tuache kulalamika bila sababu za msingi. Tutumie fursa yoyote hata kama iwe ndogo kwa ajili ya kufanikisha maendeleo yetu na ya nchi yetu Tanzania. Tukifanya hivyo, hakika tutapiga hatua na kujimudu kiuchumi jambo litakalotufanya tushindwe kutumika vibaya kwa wanasiasa wanao

Mungu naomba unisaidie; tusaidie pia kwa kuilinda nchi yetu iwe ya amani na utulivu. Mpe afya njema rais wetu ili amalize kipindi chake kwa amani.
+255712053949
+255753806087