WATANZANIA WAHIMIZWA KUJIUNGA NA MTANDAO WA MITAJI

WATANZANIA WAHIMIZWA KUJIUNGA NA MTANDAO WA MITAJI

March 05, 2018

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora amewataka wafanyabiashara nchini kuhamasika kujiunga na mtandao wa mitaji ya ubia ili kuimarisha vitega uchumi vyao na pia kusaidia kuanzisha viwanda hapa nchini.
Profesa Kamuzora alisema hayo wakati akizindua Mtandao wa Mitaji ya Ubia Tanzania – Tanzania Venture Capital Network jijini Dar es salaam jana.
Aidha Katibu Mkuu huyo amesema uzinduzi wa mtandao huo umefanyika wakati mwafaka ambapo serikali ya awamu ya tano ipo katika mikakati ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda,
Aliwataka wananchi kuacha uoga katika ushiriki wa kuwawezesha kuwepo kwa mitaji ya kutosha kwa ajili ya uimarishaji wa uwekezaji nchini Tanzania.
Alisema serikali kwa sasa inafanya kila linalowezekana kuhakikisha mazingira ya biashara na uwekezaji yanakuwa bora, ndio maana wameanzisha mchakato wa kutengeneza sera ya maendeleo ya viwanda hasa katika sekta binafsi.
Alisema ni vyema wenye viwanda na wananchi wengine kushiriki katika mchakato huo ili kufanikisha nia ya kuipeleka Tanzania katika nchi ya viwanda. Alisema kwa kuwa na sera sheria nyingi zitabadilika na hivyo kupunguza urasimu na pia vikwazo vya kuwezesha kazi katika masuala ya viwanda na biashara.
Pia alitaka wamiliki wa Ubia huo kushirikiana na Costech katika kuhakikisha kwamba viwanda vinaanzishwa na kuendelezwa.
Alitaka kuwepo na elimu ya fedha na mitaji ili wananchi waweze kuthubutu na kufanikisha mitaji.
Mapema Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi amewataka wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa uwazi, kwa kuzingatia sheria za nchi, na kuwa tayari kujifunza maarifa mapya kila fursa inapojitokeza.
Akisitikishwa na mahudhurio duni ya wafanyabiashara katika hafla hiyo alisema kutofahamu undani wa soko la mitaji na fursa zake kunatokana na kutokuwa wazi na kufanya biashara kwa kufuata kanuni.
Akizungumzia kuhusu madai ya kuwapo kwa hali kuwa ngumu nchini Dr. Mengi pia amewataka Watanzania kuichukulia hali hiyo kama fursa ya kubuni biashara itakayowawezesha kupata faida kubwa.
Akiutambulisha Mtandao wa Tanzania Venture Capital kwa wadau, Muasisi wake Bw. Salum Awadh amesema Mtandao huo ni fursa kwa wawekezaji nchini kujipatia mitaji ya kuanzisha ama kuendeleza biashara zao kwa ubia kwa masharti rahisi.
Alisema kwamba wakati umefika kwa Tanzania kusonga mbele kutumia fursa zilizopo duniani za mitaji na kusema jirani zetu wa Kenya wamesonga mbele katika hilo.
Alisema kwamba kutokana na kutojua umuhimu na ushiriki katika mitaji yenye ubia, wananchi wengi wanakimbilia katika mabenki ya biashara ambako pia wanapambana na vikwazo vingine.
Alisema kwa kuwa na kampuni ya mitaji inayoweza kutafuta pia mtaji inayomilikiwa na wananchi wenyewe kupitia mitaji yao kutawezesha kuwapo na uimara wa viwanda na kuongeza idadi zake kwa kuwa mfumo wa fedha wa mitaji ni tofauti na kwenda benki.
Tanzania kwa sasa ina zaidi ya mabenki 50 ambayo yanajishughulisha na mambo mbalimbali yanayogusa biashara na hifadhi ya kawiada.
Alisema mazingira ya sasa yanahitaji mfumo mwingine wa ziada kusaidia upatikanaji wa mitaji nje ya mabenki na kuzinduliwa kwa mtandao wa ubia wa mitaji kutasaidia kuziba pengo lililopo.
Kwa sasa Tanzania kwa rekodi zilizopo inapata asilimia 17 ya mitaji ya ubia ya dola bilioni 2.4 iliyopo duniani huku Kenya ikiwa na nfasi nzuri zaidi.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta Binafsi nchini-TPSF Bw. Godfrey Simbeye, baadhi ya viongozi wa taasisi za serikali na wafanyabiashara mbalimbali.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi (kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Bw. Godfrey Simbeye (kulia) wakiwasili kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa Mtandao wa Mitaji ya Ubia Tanzania – Tanzania Venture Capital Network uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Bw. Godfrey Simbeye (kushoto) akifafanua jambo kabla ya kuanza kwa uzinduzi wa Mtandao wa Mitaji ya Ubia Tanzania – Tanzania Venture Capital Network uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Wanaomsikiliza ni Muasisi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital, Bw. Salum Awadh (wa pili kushoto aliyesimama), Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi (wa pili kulia) pamoja Mkurugenzi wa Uwekezaji na Maendeleo ya Viwanda –TPSF, Edward Furaha (kulia).
Muasisi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital, Bw. Salum Awadh akitoa maelezo kuhusu Mtandao wa Tanzania Venture Capital kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora (kushoto) kabla ya kuelekea kwenye hafla ya uzinduzi wa mtandao huo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Bw. Godfrey Simbeye (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi (kulia).
Muasisi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital, Bw. Salum Awadh akitoa neno la ukaribisho na kutambulisha mtandao huo ambapo amesema ni fursa kwa wawekezaji nchini kujipatia mitaji ya kuanzisha ama kuendeleza biashara zao kwa ubia kwa masharti rahisi wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mtandao huo ilyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi akitoa neno la ufunguzi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora kutoa hotuba ya uzinduzi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora akitoa hotuba ya uzinduzi rasmi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital ambapo amesema umefanyika wakati mwafaka ambapo serikali ya awamu ya tano ipo katika mikakati ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uwekezaji na Maendeleo ya Viwanda –TPSF, Bw. Edward Furaha na Aliyekuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Abdullah Mwinyi wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi akisalimiana na kubadilishana mawazo na wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi akibadilisha na mawazo na Afisa Mtendaji Mkuu wa DOB Equity, Brigit van Dijk-van de Reijt wakati wa hafla ya uzinduzi wa wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora (wa tatu kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta Binafsi nchini-TPSF Bw. Godfrey Simbeye (kushoto).
Tanzania Venture Capital Network-TVCN katika picha ya pamoja na mdau aliyewezesha kufanyika kwa uzinduzi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

MAKATIBU WAKUU 15 KUTAFUTA SULUHU ZA CHANGAMOTO ZINAZOKABILI ZIWA MANYARA NA TISHIO LA KUKAUKA KWAKE.

March 05, 2018
Lango Kuu la Kuingilia Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara ambapo Makatibu Wakuu zaidi ya 10 kutoka Wizara mbalimbali wametembelea kujionea hali ya tishio lililopo la Ziwa Manyara na Maeneo ya Shoroba .
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akitoa neno la ukaribisho kwa Makatibu Wakuu  kutoka Wizara mbalimbali katika kikao cha Mawasilisho ya Taarifa ya Tishio la kutoweka kwa Ziwa Manyara na Maeneo ya Shoroba .
Mwenyeji wa Ziara ya Makatibu Wakuu,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali ,Gaudence Milanzi akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.
Kaimu Meneja wa Ikolojia katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ,Yustina Kiwango akifanya Wasilisho la Taarifa kuhusu tishio la kutoweka kwa Ziwa Manyara,Maeneo ya Shoroba na Mitawanyiko ya Wanyama Tarangire -Manyara kwa Makatibu Wakuu hao.
Kaimu Meneja wa Ikolojia katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ,Yustina Kiwango akitoa maelezo kwa Makatibu Wakuu hao .
Miongoni mwa Majengo yaliyokuwa yakitumika kama Vyoo katika Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara likionekana kuharibika baada ya maji ya Mvua yaliyoambatana na Mawe zilizonyesha miaka michache iliyopita. 
Muonekana wa majengo mengine yaliyokuwa yakitumika kama vyo kwa wageni waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara baada ya kuharibika kutokana na Maji hayo ya Mvua.
Sehemu ya Ndege ambao ni kivutio kimojawapo kikubwa katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ambao hutegemea pia uwepo wa Maji katika maeneo hayo ambayo kwa sasa yameanza kukauka kutokana na Uharibifu wa Mazingira unaofanywa na Binadamu .
Mkuruenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi (Mwenye kofia) akiwaonesha Makatibu Wakuu waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara maeneo ya Ziwa Manyara ambayo yameanza kukauka.
Eneo moja wapo la Vivutio vya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara likionekana kuanza kukauka kutokana na Athari za kimazingira zinazosababishwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu zikiwemo ,Kilimo Uchimbaji wa Madini katika maene ya jirani na Ziwa hilo. 
Viabda vinavyotumiwa na Wachimbaji wa Madini katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara .
Moja ya Mtambo unaotumika katika shughuli za Uchimbaji wa madini katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ukiwa umehifadhiwa katika eneo mojawapo la Uchimbaji.
Maeneo ambayo shughuli za Uchimbaji wa Madini umekuwa ukifanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara .
Kijana akifanya shughuli ya uchekechaji wa Mchanga katika moja ya mito inayo peleka maji Ziwa Manyara ,shughuli hi imekuwa ikifanyika kwa lengo la kujipatia Madini ana ya Dhahabu ,Hata hivyo zoezi hili linatajwa kuwa moja ya Uharibifu wa Mazingira unaochangia kukauka kwa Ziwa Manyara.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali ,Gaudence Milanzi akiwanesha baadhi ya Makatibu Wakuu namna ambavyo athari za kimazingira zimeanza kuonekana katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara .
Baadhi ya Makatibu Wakuu wakitizama kwa mbali Ziwa Manyara.
Makatibu Wakuu wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) na wa serikali katika mikoa ya Arusha na Manyara mara baada ya kihitimisha ziara hiyo.

Na Dixo Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .

MNEC SALIM ASAS ATOA MILIONI 24 KWA AJILI YA MAENDELEO YA UWT WILAYA YA MUFINDI

March 05, 2018
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas ameendelea kuineemesha jumiya ya umoja wa wanawake mkoa wa Iringa (UWT) kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita (6,000,000) kwa jumuiya hiyo wilaya ya Mufindi kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita kwa ajili ya kuendeleza miradi ya umoja huo na kuondokana kuwa tegemezi. Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akikabidhiwa shati na umoja wa wanawake (UWT) wilaya ya Mufindi baada ya kukabidhiwa kofia ambayo ameifaa hapo
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akifurahia jambo na viongozi wa chama hicho pamoja na wabunge wa viti maalum mkoa wa Iringa.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas ameendelea kuineemesha jumiya ya umoja wa wanawake mkoa wa Iringa (UWT) kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita (6,000,000) kwa jumuiya hiyo wilaya ya Mufindi kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita kwa ajili ya kuendeleza miradi ya umoja huo na kuondokana kuwa tegemezi.
 
Pesa hizo zimetolewa wakati wa baraza la umoja wa wanawake wilaya ya Mufindi mkoani (UWT) lilofanyika katika ukumbi wa chama cha mapinduzi ulipo mjini Mafinga na kuhudhuriwa na wageni wengi wakiwepo wabunge wa viti maalum ambao ni Ritta Kabati,Rose Tweve na mama Mwamwindi.

Akizungumza katika baraza hilo MNEC Asas alisema kuwa amependezwa na mikakati ambayo imefanya na umoja huo wa wilaya ya mufindi kwa kuwa wanafanya kazi na viongozi pamoja na wananchi wa chini hivyo inakuwa rahisi kuendelea kukijenga chama hicho.

Nimeona kwenye hotuba yenu mmesema kuwa “mtahakikisha kuwa wanawake wanajiunga kwenye vikundi vya uzalishaji kama vile vikoba ,saccos na vikundi vingine ili waweze kupata mafunzo stahiki ya ujasiliamali kwa lengo la kupambana na hali ya kiuchumi na kuongeza kipato,”hakika kwa kufanya hivi mtawaokoa wanawake wengi sana kiuchumi. Alisema Asas 

Asas alisema kuwa nimesikia mnataka kujenga kipanda kwa ajili ya kuongeza ajira na kuongeza uchumi wa umoja huu,hilo ni jambo bora hivyo kwa kuona mikakati hiyo nawachangia kiasi cha shilingi milioni sita ili mfikie malengo yenu.

“Sijaona changamoto ila nimeona matarajio ambayo ni kuanzisha mradi wa kuuza sare za chama,kumalizia ujenzi wa vibanda vya umoja wenu,kutafuta eneo la ekar 5 kwa ajili ya kilimo cha viazi na kupanda miche ya miparachichi na kutafuta kiwanja kikubwa kwa ajili ya uwekezaji na ndio sababu iliyonifanya niwachangie kiasi hicho cha pesa” alisema Asas

Aidha Asas alimpongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Twelve  kwa jitihada alizozifanya za kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutoa mitaji kwenye kata kumi na saba  kwa kutoa kiasi cha silingi laki sita kwa kila kata,hivyo kwa kuliona hilo MNEC alisema kuwa atachangia kiasi cha shilingi laki tano kwa kila kata kwa kata zote 36 za wilaya ya Mufindi.

Kwa hili sipepesi macho nampongeza sana mbunge Rose Tweve kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha wanawake wanapata mafanikio kwa kuwawezesha kama alivyofanya kwa kufanya hivyo amefanikiwa kuwafikia wanawake walio na kipatao cha chini kabisa na nitaendelea kukusaidia mbunge kwa kazi unazozifanya kwa ajili ya maendeleo” alisema Asas

Kwa upande wake katibu wa UWT wilaya ya Mufindi Mwanaidi Kaleghela alimshikuru MNEC Salim Asas kwa kutoa msaada mkubwa kama huo ambao hata wao hawakutegemea kutokea kitu kama hicho,ukipiga mahesabu utagundua kuwa ametoa milioni ishirini na nne kwa UWT mufindi.

“Ametoa shilingi mioni sita kwa UWT na ametoa milioni kumi na nane kwa ajili ya kuongezea nguvu kwenye mfuko wa mbunge Rose Tweve hivyo lazima tujivunie kuwa na MNEC wa namna hii” alisema Kaleghela

Mbio za Tigo Kili Half Marathon zafana mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro

March 05, 2018
Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon upande wa wanaume,  Gefrey Kipchumba kutoka Kenya akimaliza mbio kwa kutumia saa 1:03 kwenye uwanja wa ushirika mjini Moshi jana.

Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathoni upande wa wanawake,  Grace Kimanzi kutoka Kenya akimaliza mbio kwa kutumia saa 1:13kwenye uwanja wa ushirika mjini Moshi jana

Washiriki  wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathoni wakiwa katika mashindano hayo mapema jana Mjini Moshi
Babu Joram Mollel katikati akiwa na wafanyakazi wa kampuni ya Tigo, pamoja na Mkurugenzi wao Simon Karikari kwa pamoja na kauli mbiu yao TUMETISHA KAMA BABU.


Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari akiwa na mzee Joram Mollel maarufu kama BABU, mara baada ya kumaliza mbio za kilomita 21 zijulikanazo kama Tigo Kili Half Marathon mapema jana.

Mshindi wa upande wa wanawake  mashindano ya kilomita 21 Tigo Kili Half Marathon toka Kenya Grace Kimanzi (katikati) akiwa na washindi wa pili toka Tanzania Fainuna Abdi na mshindi wa tatu, Pouline Nkehenya toka Kenya, wakinyanyua mfano wa Hundi juu mara baada ya kutangazwa kushinda mbio hizo. Kushoto ni waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari mapema jana.


Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kulia na Mkurugenzi Mkuu wa Tigo TaKarikari Simon Karikari wakimkabidhi mfano wa hundi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za Tigo Kili Half Marathon wanaume, Gefrey Kipchumba toka Kenya leo kwenye viwanja vya Chuo cha Ushirika mjini Moshi.

photo