JULIO:COASTAL UNION TUTAKUTANA KWENYE LIGI KUU.

July 31, 2013
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
KOCHA Msaidizi timu ya Simba,Jamhuri Kiwelu "Julio"ameipiga vijembe timu ya Coastal Union ya Tanga kwa kusema yenye ni miongoni mwa makocha waliotoa mchango mkubwa kwenye timu hiyo na kuiambia kuwa watakutana kwenye ligi.

Julio alitoa kauli hiyo hivi karibuni mara baada ya kumalizika kwa mechi ya kirafiki kati ya timu hiyo na Coastal Union,mchezo uliomalizika kwa Simba kukubali kichapo cha bao 1-0 bao ambalo lilifungwa na Chrispian Udula aliyetumia uzembe wa mabeki wa Simba kupachika wavuni bao hilo.

Alisema mchezo huo ulikuwa mzuri na wenye upinzani mkubwa kutokana na timu zote kucheza vema lakini pia ushindi huo wa wapinzani wao umewapa hasira ya kutaka kulipiza kisasi kwao kwenye mechi ya ligi kuu kwani huo ndio mpango wao ni kucheza ligi kwa mafanikio msimu ujao.

Kocha huyo alisema walifurahi kucheza mechi hiyo ambayo ilikuwa kipimo cha kuangalia aina ya uchezaji inaoucheza timu yao huku akitolea visingizio kuwa mwamuzi wa mchezo huo,Isihaka Shirikisho kuwa alichangia wao kukosa ushindi kwenye mchezo huo.

Kwa upande wake,Kocha Mkuu wa Coastal Union,Hemed Morroco alisema huo ni mwanzo mzuri kwa timu hiyo kwani malengo yao makubwa ni kuhakikisha wanazifunga timu zote zitakazocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani na ugenini ili kuweza kurudisha heshima ya mwaka 1988 ya kuchukua ubingwa wa ligi hiyo.

VIKUNDI VINNE VYA KILIMO WILAYA YA KILINDI KUWEKA KAMBI MAONYESHO YA WAKULIMA MOROGORO.

July 31, 2013
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
VIKUNDI vinne vya kilimo kutoka wilayani Kilindi mkoani Tanga, vinatarajiwa kuweka kambi ya siku nane katika maonyesho ya Wakulima mkoani Morogoro na kwenda kuwa mfano bora wilayani kwao.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, DC Selemani Liwowa, alipozungumzia faida zinazoweza kupatikana katika maonyesho hayo ya wakulima yanayofanyika Morogoro kwa Kanda ya Mashariki.

Akizungumza zaidi, Liwowa alisema kuwa maonyesho ya kilimo yamekuwa na tija kwa kiasi kikubwa, hivyo anaamini kwa vikundi vyao vilivyopata nafasi hiyo vitakuwa kwenye mazingira mazuri.

Alisema wao wilaya wametoa ofa ya vikundi viwili, ambapo wadau wao wakuu, Shirika la  World Vision nao wametoa ofa ya vikundi vingine viwili kwa ajili ya kujumuika na wakulima wenzao.

“Katika maonyesho haya ya wakulima, sisi tunaamini kuwa mpango huu utakuwa na mafanikio makubwa, hivyo kinachotakiwa kufanywa kwa sasa ni kuongeza umakini kwenye kujifunza.

“Nane Nane imepangwa kwa makundi, hivyo wilaya Kilindi inayotokea mkoani Tanga ipo katika Kanda ya Mashariki, ambapo shughuli mbalimbali zitaonyeshwa na kujifunza kwa wakulima wetu,” alisema.

Wilaya ya Kilindi inatokea katika wilaya Handeni kabla ya kugawanywa na kuwa wilaya mbili, ambapo zote zipo mkoani Tanga, chini ya Mkuu wa Mkoa wake, Chiku Gallawa.

Serikali yatangaza kutambua mchango wa blogs Tanzania, huku ikizundua Kampeni ya kuhamasisha matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii

July 31, 2013
Msanii wa muziki wa asili Tanzania ambaye pia ni msanii wa maigizo na filamu, Mrisho Mpoto akizungumza jambo mbele ya waaandishi wa habari na wamiliki wa blogs mbalimbali katika uzinduzi wa matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii. Mrisho alisimama kuzungumza dakika chache baada ya wimbo alioimba na Banana Zoro kuzinduliwa, unaojulikana kama 'Futa, Delete Kabisa'. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),John Nkomo katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkomo, akizungumza mbele ya wamiliki wa blogs mbalimbali Tanzania, waandishi wa habari katika warsha ya kampeni ya kuzindua matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuhamasisha suala zima la maendeleo.

Afisa Uhusiano wa TCRA,Innocent Mungi akiwakaribisha wadau mbalimbali

wa mambo ya habari za kwenye mitandao,kuhusiana na uzinduzi wa kampeni ya

kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano,Warsha hiyo

imefanyika leo Makao makuu ya Ofisi hizo,zilizopo barabara ya Sam Nujoma

jijini Dar.

Wadau wa mawasiliano wa mitandao ya kijamii, blogs, wakisikiliza hoja mbalimbali zilizotolewa na viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA katika uzinduzi wao wa matumizi mazuri ya mitandao kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo ya Taifa.

Picha kwa hisani ya handenikwetu.blogspot.com

KASSIM MGANGA AIPIGIA SALUTI "I LOVE YOU'

July 31, 2013
Na Oscar Assenga,Tanga.

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva hapa nchini,Kassim Mganga amesema wimbo wake wa "I Love You" ambao aliuachia mwezi uliopita anaamini utafanya vizuri na kuweza kumpa mafanikio makubwa kama zilivyokuwa zilizopita.

Mganga ambaye anatamba na wimbo wake wa "Ndoa Ndowano"ambao uliweza kuutikisha anga ya bongo fleva hapa nchini kutokana na aina ya mashairi aliyoyatumia kwani amepania kuutangaza mziki wake kitaifa na kimataifa zaidi.

Akizungumza na Blog hii ,Msanii huyo alisema wimbo huo unazungumzia upendo kwa ujumla hasa ukihusisha watu wawili wanaokuwa wakipendana kwa thati na kuelezea mikakati ya video yake upo mbioni kuiachia.

Aliongeza kuwa wimbo huo umetayarishwa na studio za Mazuu ambapo pia aliitaka serikali kutekeleza kwa vitendo ahadi zake za kuwasaidia wasanii wa mziki huo kwani wengi wao wanashindwa kupata haki zao za msingi kutokana na mifumo iliyopo.

Mganga alitoa ushauri kwa wasanii chipukizi kuwa makini kwa sababu mziki hivi sasa ni biashara hivyo wanapotaka kufanya mziki wajipange vilivyo na sio kukurupuka pamoja na kuwataka wasanii wakubwa kuacha kuwabagua wasanii hao bali washirikiane ili kuweza kusukuma mbele guruduma la maendeleo yao.

STARS ILIYOFUNGWA UGANDA SIO YENYEWE BALI NI MZIZIMA UNITED.

July 31, 2013
KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA (TAIFA STARS).
Na Oscar Assenga, Tanga.
KATIBU Mkuu wa Zamani wa Coastal Union,Salim Bawazir amesema timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars”iliyofungwa na Uganda katika mashindano ya Chan ni Mzizima United na sio timu ya Taifa kwani timu hiyo bado haijachaguliwa.

Bawazir ambaye pia ni mdau wa soka mwenye heshima kubwa sana katika klabu ya Coastal Union ya Tanga alisema ili tuweze kuwa na timu bora ya Taifa lazima kuwe na mashindano yatakayojumuisha mikoa yote ya Tanzania kama ilivyokuwa Taifa Cup.

Aliongeza kuwa mashindano hayo yachezwe katika kituo kimoja kwenye mkoa wa Dar es Salaam ili kuweza kumpa urahisi Kocha Mkuu wa timu ya Taifa aweze kuchagua timu bora ambayo italeta mafanikio kwenye mashindao mbalimbali ndani ya nchini na nje.

Katibu huyo aliongeza alishauri pia kuwepo kwa mashindano ya Jimbo Cup ambayo yatahusisha timu kutoka wilaya mbalimbali kwenye mikoa na kupata timu nzuri itakayopata ridhaa ya kucheza mashindano ya Taifa Cup kwa mafanikio ili kumpa urahisi kocha mkuu

kuangalia wachezaji wazuri kwa ajili ya timu za Taifa za Vijana na wakubwa.

Alisema kutokana na muundo wa sasa wakuchagua timu ya Taifa kupitia mashindano ya Ligi kuu inakuwa ni vigumu sana kupata wachezaji wenye vipaji vizuri kwani wachezaji wanaotegemewa sana ni kutoka vilabu vya Yanga na Simba aambapo kwa mtindo huo wachezaji wengi wanatoka mkoa mmoja wa Dar es Salaam wakati nchi ya Tanzania ina mikoa 26.

Kwa mtindo wa kutegemea kupata timu ya Taifa kupitia mashindano ya Ligi kuu haitoshi lazima shirikisho la soka libuni mashindano mbalimbali ambayo yatashirikisha mikoa yote ya Tanzania kama FA Cup na vile vile wayatilie mkazo mashindano ya ligi daraja la kwanza kwa kuangalia wachezaji kwani ligi hiyo imepuuzwa kwa kutokupelekwa mwalimu mkuu wa timu ya Taifa kuangalia vipaji vipya.

Akizungumzia suala la Yanga kugoma kuingia mkataba  wa kuonyeshwa michezo yao na Kampuni Television ya Azam alisena Yanga wao wajitoe  lakini timu zingine  zikubali kuwa na mkataba na kampuni hiyo.

Alisema kama Yanga wana mikataba ya ufadhili na makampuni mengine na mara nyingi sana kusalimu kwa kuwakubalia baadhi ya  maamuzi yao ndio tatizo, Kampuniya Azam na TFF wakubali ufadhili huo na waitoe Yanga michezo yao isionyweshwe katika kituo cha Televison ya Azam, timu zote zilizobaki zinahitaji ufadhili zaidi ni vyema makampuni mengi ya ndani na nje yakatoa ufadhili ili kuondoa matabaka katika ligi kuu.

MECHI YA SIMBA YAACHA PIGO COASTAL UNION.

July 31, 2013
Na Mwandishi Wetu,Tanga.
KATIBU Mkuu wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga,Kassim El Siagi (aliyekaa pichani juu)amesema mechi yao na Simba SC imewaachia pigo licha ya kuibuka na ushindi kutokana na kuwasababishia majeraha washambuliaji wawili mahiri katika timu hiyo baada ya kuumia kwenye mchezo huo.

Akizungumza na Blog hii,El Siagi alisema mechi hiyo ilikuwa nzuri kutokana na wao kuibuka na ushindi lakini wakajikuta pia wachezaji wake hao wakipata majeraha madogo madogo ambayo watalazimika kuyatibu kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu hapa nchini.

El Siagi aliwataja washambuliaji hao kuwa ni Crispian Udulla na Keneth Masumbuko ambao kila mmoja kwa wakati wake waliweza kutoa mchango mkubwa sana ambapo masumbuko aliifungia Coastal Union bao la ushindi kwenye mechi yao na URA wakati Crispian Udulla aliweza kuwa mwiba kwenye mecho ya na Simba kwa kuifungia timu hiyo bao.

Aliongeza kuwa malengo yao makubwa ni kucheza mechi nyengine ya kirafiki Iddi Mosi na timu nyengine ambayo wataitangaza baadae baada ya kumalizia mazungumzo yao ambapo yakienda vizuri watacheza na Yanga.

"Malengo yetu msimu ujao ni kuhakikisha tunacheza ligi kwa mafanikio makubwa ikiwemo kuchukua ubingwa wa ligi hiyo kwani hilo linawezakana kutokana na uimara wa kikosi hicho na mshikamano uliopo miongoni mwao "Alisema El Siagi.

Katibu huyo alisema timu hiyo msimu ujao itakuwa tofauti na vile inavyofikiriwa na wadau wa soka hapa nchini kwani usajili ambao wameufanya na wanaotarajiwa kuufanya utakuwa kielelezo tosha cha timu hiyo kuelekea maandalizi yao.

UHURU SELEMAN HUYO AKICHEZA KWA STAIL WAKATI WA MAZOEZI LEO.

MAZOEZI SIO MCHEZO.

KIKOSI CHA COASTAL UNION KIKIWA MAZOEZINI JANA UWANJA WA MKWAKWANI.