MHE HEMED ABDULLA ASEMA JUHUDI ZINAZOCHUKULIWA NA VIONGOZI WA MKOA KUSINI UNGUJA ZACHANGIA KUKUA KWA UFAULU

August 12, 2023

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amesema kukuwa kwa ufaulu Mkoa wa Kusini unguja kumetokana na juhudi zinazochukuliwa na Viongozi wa Mkoa huo kwa kuzingatia maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.


Mhe. Hemed ameyasema hayo wakati akiwasalimia wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Paje na Jimbo la Makunduchi katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua uhai wa Chama Mkoa wa Kusini Unguja.


Amesema kwa mwaka wa masomo 2022 Mkoa wa kusini Unguja umeongoza kwa ufaulu kutokana na juhudi za Makusudi zilizochukuliwa na Jumuiya ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechukua jitihada za kuanzia masomo ya Kidato cha Tano na kidato cha Sita Skuli ya Hasnuu Makame ili kupunguza masafa kwa wanafunzi kufuata elimu hiyo.


Aidha Mhe. Hemed amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza zaidi ya Bilioni 230 fedha za Mkopo wa Uviko 19 ambazo zimeelekezwa kwenye miradi mingi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Hospital za Wilaya na Mkoa, Skuli za Ghorofa pamoja na madarasa.


Aidha amewakumbusha wananchi na wanachama wa CCM kuendelea kudumisha Amani na Utulivu iliopo na kuwataka kuwa na umoja na mshikamano baina yao.


Nae Katibu wa Siasa na uhusiano wa Kimataifa Khadija Ali Salum amesema Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja wana kila sababu ya kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuelekeza miradi mingi ya Maendeleo Mkoani humo pamoja na kuwapongeza Wabunge, Wawakilishi na Madiwani kwa kuwatumikia wananchi wao.


Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadid ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi imeelekeza miradi mingi ya maendeleo Mkoa wa Kusini Unguja na tayari Serikali imeahidi kujenga Tenki kubwa la maji mkoani humo ambalo litamaliza changamoto ya upatikanaji wa huduma ya Maji safi na Salama Mkoani humo.


Katika ziara hiyo Mhe. Hemed ameweka Jiwe la Msingi ujenzi wa Ofisi ya Jumuiya ya Maendeleo na urekebishaji wa maadili Bwejuu (JUMAMABWE) ambapo ameipongeza Jumuiya hiyo kwa juhudi zake za kusaidia kurekebisha tabia katika jamii hiyo.


Aidha ameeleza kuwa eneo hilo limezungukwa na mahoteli ya Kitalii na kuwataka wana Jumuiya hiyo kuhakikisha wanatoa elimu ya kuzingatia Maadili, silka na tamaduni kwa wenyeji na wageni wanaofika maeneo hayo.


Akisoma taarifa ya ujenzi huo Katibu wa Jumuiya ya Maendeleo na urekebishaji wa maadili Bwejuu Bwana Hassan Simai Issa ameeleza kuwa Jumuiya hiyo imeanzishwa mwaka 2018 na kupatiwa usajili mwaka 2019 ambapo ujenzi huo unaendeshwa kwa nguvu za wananchi na wadau mbali mbali wa Maendeleo waliozunguka kijiji hicho.


Amefafanua kuwa kuwepo kwa Jumuiya hiyo kutazalisha fursa mbali mbali kwa vijana, kuweka jamii katika Mila, Silka na Tamaduni, pamoja na kuinua uchumi wa Zanzibar.


Katika ziara hiyo Mhe. Hemed ameshiriki Ujenzi wa Ofisi ya CCM Jimbo la Paje, ameweka Mawe la Msingi Tawi la CCM Bwejuu Kusini, Ujenzi wa Ofisi ya Jumuiya ya maendeleo na urekebishaji wa maadili Bwejuu, Tawi la CCM Sheba, na nyumba ya maendeleo Shehia ya Kajengwa.




DKT. KIKWETE ASISITIZA AMANI NCHI ZA SADC

August 12, 2023


Rais Mtaafu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati), akiwasilisha mada kwenye mhadhara wakati wa Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Luanda Angola. Kushoto ni Katibu Mkuu Mstaafu wa tatu wa SADC, Mhe. Tomaz Salomao na kulia ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Msumbiji, Mhe. Luisa Diogo.

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha, Bw. James Msina (wa pili kulia) na Wakili wa Serikali Mwandamizi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bi. Felista Lelo, wakifuatilia mada zilizotolewa wakati wa wa Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Luanda Angola.

Wajumbe kutoka Tanzania (mstari wa kwanza) wakifuatilia mada zilizoangazia maendeleo ya uchumi, zilizotolewa wakati wa wa Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Luanda Angola.

Rais Mtaafu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha, Bw. James Msina, katika viwanja vya Chuo cha Diplomasia Angola, wakati wa mikutano ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Luanda Angola.

Wajumbe kutoka nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa wakati wa Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Luanda Angola.


Rais Mtaafu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Tanzania katika viwanja vya Chuo cha Diplomasia Angola baada ya kuwasilisha mada kwa wajumbe wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na wanafunzi wa chuo hicho, jijini Luanda Angola.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano, WF, Luanda, Angola)

MBUNGE UMMY MWALIMU AFANYA ZIARA KATA YA DUGA JIJINI TANGA

August 12, 2023

.










*Atembelea Kituo Cha Afya Duga 
*Afungua Shina la Wakereketwa 
•Afungua Ofisi ya CCM  kata CCM ya duga .
     
Mbunge wa Tanga Mjini Mhe. Ummy Mwalimu leo tarehe 12/8/2023 amefanya ziara kata ya Duga. Katika ziara hii mbunge ametembelea kituo Cha Afya duga kukagua utoaji wa huduma ambapo amepongeza watumishi kwa kutokuwa na kifo hata kimoja cha mama mjamzito na watoto wachanga. Mhe Ummy amesema kuwa Rais Samia atatoa gari ya kubebea wagonjwa kwa ajili ya Kituo cha Afya Duga. 

Aidha Mh Ummy amemtaka Mganga Mkuu wa Jiji  kusimamia kwa karibu upatikanaji wa Dawa katika Kituo hicho. Mhe Ummy pia ameutaka Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kufanya ukarabati wa paa la Kituo hicho ili kuepusha madhara kwa wananchi. 
  
Pia Mhe Mbunge  alifungua shina la vijana wa CCM lililopo mtaa wa Magomeni Kirare na  kutoa shilingi milioni 1 kuwaunga mkono vijana hawa na kuahidi kuwatengenezea  turubai moja (tent) .

Pia Mhe Ummy amefungua Ofisi ya CCM kata ya Duga na   kusema ataendelea kujitolea kwa ajili ya Chama. Awali Mhe mbunge amenunua meza 3 na viti 7 kwa ajili ya ofisi hiyo.

Mwisho mbunge Ummy alitembelea makazi ya wazee duga ambayo ni kawaida yake kila mara kuenda eneo hilo au kutuma wasaidizi  wake kuwaona wazee hao na kuwapatia vyakula.

Katika ziara hiyo, Mhe mbunge aliambatana na viongozi wa chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Tanga wakiongozwa na Mwenyekiti Meja  mstaafu Hamisi Bakari Mkoba, Mkuu wa wilaya ya Tanga, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe Shillow na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Simon
 
Imetolewa na :
Ofisi ya Mbunge Jimbo la Tanga Mjini
12/8/2023