MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA AZUNGUMZA NA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA WERUWERU.

April 25, 2016
Wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Weruweru wakiimba wakati wakielekea ukumbini kwa ajili ya kuanza rasmi kwa sherehe ya kuwaaga.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru Rosemery Tarimo akimuongoza mgeni rasmi katika mahafali ya 31 ya kidato cha sita ,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania ,Joel Raulant (kulia) wakati wakielekea ukumbini kwa ajili ya sherehe za mahafali hayo.
Mgeni rasmi katika mahafali ya 31 katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Weruweru ,Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,Joel Raulant akiingia ukumbini pamoja na Mkuu wa shule hiyo Rosemery Tarimo.
Mgeni rasmi ,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,Joel Raulant na wageni wengine wakiwa wamesimama wakifuatilia wimbo wa shule hiyo wakati ukiimbwa na wanafunzi katika mahafali hayo.
Wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Weruweru wakiimba wimbo wa shule.
Walimu na watumishi wengine wa shule hiyo wakifuatilia sherehe ya mahafali hayo.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru,Rosemery Tarimo akitoa taarifa ya shule hiyo kwa mgeni rasmi wakati wa mahafali hayo ya 31 ambapo jumla ya wanafunzi 390 wamehitimu.
Wahitimu wakifuatilia taarifa ya shule hiyo iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa shule hiyo ,Rosemery Tarimo.
Wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita katika shule hiyo wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi.
Mzazi mualikwa ,Jaji Amir Mruma akizungumza kwa niaba ya wazazi wenye watoto wanaosoma katika shule hiyo.
Mgeni rasmi katika mahafali ya 31 ya kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Weruweru ,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania ,Joel Raulent akitoa hotuba yake wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,Joel Raulent akitunuku vyeti kwa wahitimu 390 wa kidato cha sita katika shule hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

WAZEE WASIOJIWEZA KITUO CHA BUKUMBI MWANZA WAIOMBA SERIKALI KUIMALISHA HUDUMA ZA AFYA KITUONI KWAO

April 25, 2016
Wauguzi wa zahanati ya kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakiwaongoza waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliofika kuwatembelea wazee wanaoishi katika kituo hicho kujua jinsi wanavyoishi na kuwa kutambua suala la uzazi wa mpango. Ziara hiyo ya waandishi wa habari iliyofanyika wiki iliyopita iliratibiwa na taasisi inayojishuhulisha na ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango (TCDAA) wakishirikiana na Marie Stopes Tanzania. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Wazee wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakiendelea na kazi za mikono.
Mmiliki wa Blog ya Kajunason akimsaidia kusuka kikapu mmoja ya wazee anayelelewa katika kituo hicho.
Moja ya nyumba wanayoishi wazee hao.
Waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliotembelea Wazee wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi wakifanya mahojiano ili kujua changamoto mbali mbali zinazowakabili ambapo wazee hao walisema jambo kubwa linalowaumiza kicha ni upatikanaji wa matibabu katika zahanati yao jambo linalowafanya wengine kuishi na maradhi kwa muda mrefu.
Waaandishi wakiendelea kufanya mahojiano na Wazee wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi.
Ofisa Mfawizi wa Makao ya wazee wasiojiweza, Michael Bundala akifanya mahojiano na waandishi wa habari ambapo katika mahojiano hayo alielezea kuwa kuna changamoto nyingi za kuishi na wazee hawa kama kiongozi kwa vile wazee wamekuwa wakorofi mno na kuona siwatendei haki katika maamuzi ambayo nimekuwa nikiyatoa ikiwemo katika ugawaji wa vyakula. 
--- Na Cathbert Kajuna - Mwanza. Wazee wanaoishi katika kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wanaiomba Serikali kuwapatia huduma za afya katika Zahanati ya kituo chao.   Wazee hao wanaeleza kwamba changamoto hizo katika ziara ya waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliounganishwa pamoja na kuratibiwa na taasisi inayojishuhulisha na ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango (TCDAA) na Marie Stopes Tanzania.   Wakizungumza kwa nyakati tofauti wazee hao wanasema katika zahanati hiyo hakuna dawa na wanapoumwa wanalazimika kununua dawa.   Mwenyekiti wa kambi hiyo, Helen Emmanuel anasema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za huduma ya afya pamoja na wenzao wasiojiweza kufukuzwa kambini.   "Tunapofika katika zahanati hii daktari anatupima vizuri lakini hakuna dawa hivyo anatuandikia kwenye karatasi anatuambia tukanunue.   "Kwakweli hii ni changamoto kubwa sana kwetu kwasababu wakati mwingine tunapoandikiwa dawa hela ya kununulia tunakosa hali inayosababisha tunaendelea kuumia kutokana na kwamba afya zetu ndio hizi na hatuna sehemu ya kujipatia kipato" alisema Heleni.   Pia alisema kwa sasa wapo wazee 78 katika kambi hiyo lakini wapo walemavu wenzao saba ambao wameambiwa wahame kambini waende vijijini wakati hawana uwezo.   "Kwakweli inaumiza sana kwasababu hawana uwezo wa kujitafutia pia mimi sina uwezo wa kuwasaidia kwasababu mimi mwenyewe ni mlemavu ,"alisema.   Ofisa Mfawizi wa Makao ya wazee wasiojiweza,Michael Bundala alisema hapa kambini tuna watoto 17 ambao wazazi wao wako humu kambini na wengine waliotimiza miaka 18 tuliwapunguza na kuwatengea eneo kwa ajili ya makazi na tusingefanya hivyo tungekuwa zaidi ya 800 kwasababu wengine wanapeana mimba wenyewe kwa wenyewe.   Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Kigongo Kata ya Idetemya, Sebastian Kisumu alisema ipo changamoto ya vijana wa nje kuwapa mimba wasichana wa kambi hiyo.   Alisema wapo wataalamu mbalimbali mambo wanafika katika kambi hiyo kutoa elimu ya uzazi wa mpango lakini wengi wao hawaipokei hali inayosababisha kuwa na idadi kubwa ya watoto ambao hawana baba.
DC HAPI AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA YA ALI HASSAN MWINYI

DC HAPI AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA YA ALI HASSAN MWINYI

April 25, 2016

H1
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akikagua matengenezo ya  barabara ya Ali Hassan Mwinyi leo tarehe 25 Aprili 2016 jijini Dar  es Salaam
H2
 Mkuu wa wilaya Kinondoni Ally Salum Hapi wa kwanza kulia akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa ujenzi wa barabara ya Ali Hassani Mwinyi Halipo tembelea leo kuona maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo
H3
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akiwa na wafanyakazi wa MS ESTIM CONSTRUCTION CO.LTD
H4
Mkuu wa wilaya Mhe.Ally Hapi akiongea na msimamizi wa ujenzi.
H5
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi kushoto akiwa na meneja wa Tanroad katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi leo tarehe 25 Aprili 2016
Balozi Amina Salum Ali awataka watendaji Wizarani kuleta mabadiliko katika utendaji wa kazi

Balozi Amina Salum Ali awataka watendaji Wizarani kuleta mabadiliko katika utendaji wa kazi

April 25, 2016


ainaMasanja Mabula – Pemba
 
WAZIRI wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar,  Balozi Amina Salum Ali amewataka watendaji wa Wizara hiyo kuleta mabadiliko katika utendaji wa kazi, ili kuifanya Zanzibar iweze kufikia katika uchumi wa kati.
 
Alisema kuwa, Wizara imeandaa sera  mbali mbali ambazo zinaweza kuifanya Zanzibar kufikia uchumi wa kati, ikiwa ni pamoja na sera ya biashara, viwanda na sera ya mpangokazi ambao utekelezaji wake utaanza leo (jana).
 
Akizuzungumza na watendaji wa Wizara hiyo pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo tofauti katika ukumbi wa Makonyo Chake Chake, alisema ipo haja kwa watendaji wake kujibadilisha kwa kuwa na sera madhubuti ya  kuwa na viwanda vikubwa, ambavyo vitaifanya Zanzibar kufikia uchumi wa kati.
 
Alieleza suala la kukuza viwanda Zanzibar kuwa, Wizara inataka kukiendeleza kiwanada cha sukari Mahonda, kujenga kiwanda cha maziwa, kiwanda cha Zanzibar Milin na kiwanda cha makonyo ambacho hutoa mafuta ya karafuu, makonyo na mafuta mengine ya mimea.
 
 ”Kuna mambo lazima tuyabadilishe, kwanza utendaji wa kazi wa silka ya kawaida ambapo wanataraji matokeo yatakayobadilisha maisha ya wananchi, utendaji utakaotuletea mapato na maendeleo, hii ndio itakayoifanya Zanzibar kufikia uchumi wa kati”, alisema Balozi huyo.
 
Balozi Amina aliwataka watendaji hao kufanya kazi ya ziada katika kubadilisha Zanzibar  na kuwa ya maendeleo zaidi kwa kutumia bidhaa zinazotokana na kilimo.
 
Alisema kuwa, asilimia 85 ya viwanda Zanzibar ni vya wananchi, hivyo ni vyema juhudi zikatendeka katika kuvibadilisha na kufikia viwanda vikubwa, kwani Zanzibar inayo nafasi kubwa ya kuzalisha na kuuza bidhaa zinazotokana na kilimo.
 
”Tunatakiwa tufanye kazi ya kuibadilisha Zanzibar kwa kutumia bidhaa zinazotokana na mimea, kwani uzalishaji unataka bidii kubwa, hivyo ipo haja ya kuwashirikisha wa Zanzibar na nje yake kwa kutembeleanaili kuona wenzetu wanafanya nini na sisi tuweze kufuata”, alieleza Waziri huyo.
 
Waziri huyo alisema, ipo haja ya kutolewa elimu kwa wajasiriamali na kuwezeshwa kwa kupitia sehemu za nje zenye maeneo ya kiuchumi ili kujifunza mambo mbali mbali ambayo wataiga kutoka huko.
 
”Ili tufikie huo uchumi wa kati ni lazima Serikali ijipange kuwawezesha wajasiriamali na wawekeze kupitia sehemu za wenzao ka kuwatembeza, kupatiwa elimu na soko, jambo ambalo ni changamoto kubwa kwetu”, alieleza.
 
Akizungumzia suala la karafuu alieleza kuwa, Zanzibar imefanya vizuri kwa miaka mitano iliyopita kwa uzalishali wa zao hilo, ambapo Serikali imenunua tani elfu 20 kutoka kwa wananchi, ikiwa na thamani ya shilingi billioni 285.89.
 
”Serikali imejiandaa vizuri na bei itaendelea kuwa ile ile kama alivyoahidi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe: Dk Ali Mohamed Shein, lengo ni kuivusha Zanzibar kwenda katika uchumi wa kati”, alisema.
 
Alisema bei ya ununuzi wa zao la karafuu haijashushwa kama baadhi ya wananchi wanavyodai, kwani hiyo ni ahadi ya serikali katika kustawisha maisha ya wakulima wa zao hilo.
 
Aliwataka wananchi kuacha kabisa uuzaji wa karafuu kwa njia ya magendo na waendelee kuuza hapa Zanzibar, kwani fedha zinapoingia serikalini huwafaa wananchi wenyewe kutokana na huduma za kijamii.
 
”Pia tufanye biashara inayokubalika kimataifa, karafuu zetu tusuzichanganye na makonyo kwa sababu kuna ushindani mkubwa wa soko, hivyo ni vyema tukazianika sehemu sahihi na kuwa kavu kabisa”, alifahamisha.
 
Aidha alisema kuwa, Wizara itakuwa na utaratibu wa kuangalia bei ya vyakula na kuhakikisha kwamba vyakula vinavyoingia vinakuwa na viwango vya kimataifa pamoja na usafi.
 
”Tuko tayari kuingia katika mapambano, kwa nini tusiwe na viwango vya vyakula vinavyoingia wakati nchi nyengine wanavyo, tutahakikisha zinaingia bidha zenye ubora na viwango”, alisisitiza.
 
Mwandishi wa habari Salim Ali Mselem kutoka redio Istiqama akiuliza swali, alisema serikali itapanga sera ipi ambayo itawawezesha wananchi wote wakati wanapoimarisha upande huu, wananchi hukwama kwa upande wapili.
 
”Zao la karafuu limeongezwa bei lakini na kodi inaongezeka kwa wafanyabiashara siku hadi siku, jambo ambalo wenye kipato cha chini wanaumia, kwa mfano wafanyabiashara wa sokoni hapa Chake Chake wanatozwa kodi elfu 60 badala ya elfu 30, kweli wananchi wanawezeshwa hivi”, alihoji Salim.
 
Nae Nasra Mohamedi kutoka ZBC televisheni akitoa hoja yake kuwa, kama iliyoelezwa wajasiriamali wapo asilimia  85, hivyo serikali itafute njia mbadala ya kuwawezesha ili kutumia njia ya digital katika kufanya kazi zao ili kufikia maendeleo zaidi.
 
Waziri Amina alikuwa kwenye ziara ya kutembelea vitengo mbali mbali vya Wizara, ambapo aliona jitihada mbali mbali zinazofanywa na wajsiriamali na kujionea mambo mbali mbali ambayo hufanywa katika kiwanda cha makonyo Wawi Chake Chake, ikiwa ni pamoja na mafuta yanayotengenezwa kwa karafuu na makonyo

NSSF YAWAKWAMUA WANANCHI WA KIGAMBONI.

April 25, 2016


 Hivi juzi tumeshuhudia ufunguzi wa daraja la Kigamboni ambalo Mh. Rais Dr. John Pombe Mgufuli alilipa jina la daraja la Nyerere. Daraja hili ni matunda ya uwekezaji wenye tija unaofanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii la NSSF.

Shirika hilo kwa kushirikiana na serikali limeweza kujenga daraja lenye urefu wa mita 680 likiwa na barabara sita; tatu zikielekea Kigamboni na tatu zikitokea Kigamboni.  Daraja hili lina njia ya watembea kwa miguu yenye upana wa mita 2.5 kila upande.

Daraja hilo limejengwa kisasa na kampuni ya  China Railway Construction Engineering Group iliyotekeleza mradi huo kwa kushirikiana na kampuni ya China Railway Major Bridge Group kutoka nchini China.


 Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hili, kumejumuisha barabara za kufika katika daraja hili zenye jumla ya urefu wa kilomita 2.5. Katika ujenzi wa daraja hili, Shirika la NSSF limetoa asilimia 60 ya gharama za Ujenzi na Serikali asilimia 40 ya gharama hizo.

 Akizungumza na waandishi wa habari waliotembela daraja hilo hivi karibuni, Meneja wa Mradi huo kutoka NSSF, Muhandisi Karim Mattaka alisema daraja la Kigamboni limejengwa ili kuondoa kero ya siku nyingi ya usafiri kwa wakazi wa Kigamboni na wakazi wa Dar es Salaam kwa ujumla, kuimarisha hali ya uchumi wa Mkoa huu wa Dar es Salaam, mikoa ya jirani na nchi kwa ujumla pamoja na kuimarisha hali ya uchumi wa shirika, kuliwezesha shirika kuboresha na kulipa mafao kwa kutunza thamani ya fedha kupitia kitega uchumi hiki.

Faida zitokanazo na uwekezaji huo kwa mujibu wa Muhandisi Mattaka ni faida ya moja kwa moja kwa wanachama kwani huingizwa katika akaunti zao pindi wanapochukua mafao yao pamoja na kulipia matibabu yatolewayo bure kwa wanachama.

“Daraja hili linadhihirisha uwezo wa shirika katika nyanja za uwekezaje na kuwapa wanachama uhakika kuwa pesa zao ziko salama,’’.

 “Ni dhahiri kuwa daraja litaondoa usumbufu mkubwa ambao wananchi walikuwa wanaupata na hata wakati mwingine kupoteza maisha, kwani vivuko vya Kigamboni vikiwa vimeharibika wananchi walikuwa wanatumia mitumbwi ambayo wakati mwingine sio salama,.’’ Alisema  

> Kukamilika kwa daraja hilo kunaelezwa kuwa kutachangia sana katika kusukuma maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Kigamboni, Jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

 Inaelezwa kuwa daraja hilo sasa limefungua fursa  kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kukamilisha utaratibu wa kujenga mji wa kisasa (Kigamboni Elite City) utakaokuwa na nyumba za kisasa,   kuongeza  ufanisi katika utalii kwa kujenga mahoteli ya kitalii katika fukwe zilizopo eneo la Kigamboni, kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoa ya kusini mwa nchi yetu na hata nchi jirani zetu, kupanua kilimo cha matunda, mboga na mazao mengineyo yanayozalishwa  katika eneo hili.

 “Wakulima sasa wataweza kufikisha bidhaa zao sokoni kwa urahisi zaidi na hivyo kuongeza kipato chao,’’ aliongeza.

 Kwa mujibu wa Muhandisi Mattaka daraja hilo vilevile  litarahisisha uwezekano wa upanuzi wa bandari upande wa Kigamboni.

 “Kwa ujumla Daraja la Kigamboni litaboresha sana usafiri ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na kupunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa magari unaolikabili Jiji la Dar es Salaam hasa baada ya ujenzi wa barabara ya Dar es Salaam – Chalinze kwa kiwango cha “Expressway” ambayo itaunganishwa na Bandari ya Dar es Salaam kupitia Daraja la Kigamboni.,’’ alisema

 Muhandisi Mattaka alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wadau wa shirika hilo kuhusu usalama wa fedha zao na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa kiwango cha kimataifa.

 Kwa upande Muhandisi wa Mradi huo kutoka kampuni ya  China Railway Construction Engineering Group iliyotekeleza mradi huo kwa kushirikiana na kampuni ya China Railway Major Bridge Group kutoka nchini China, Muhandisi Jamal Mruma alitumia fursa hiyo kuwatoa hofu watumiaji wa daraja hilo kwa kuwa limetengenezwa katika ubora na teknolojia ya hali juu kabisa.

 “Ni aina ya mradi bora kabisa kuwezeshwa na NSSF pamoja serikali na hatimaye kutekelezwa kampuni bora katika masuala ya ujenzi kutoka China.Niwatoe hofu watumiaji wa daraja pamoja na wanachama wa NSSF kuwa wajivunie mradi huu unafaida kubwa sana kwao na taifa kwa ujumla...waulinde na wajivunie haya ni matunda ya pesa zao,’’ alisema.

 Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa daraja, Naibu waziri wa kazi, ajira, vijana na walemavu aliwaasa waajiri wasiopeleka michango yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii kutekeleza sheria kwa kuchangia kwa wakati ili kuepuka usumbufu wakati wanachama watakapokua wanahitaji mafao yao.
UCHAGUZI MKUU YANGA JUNI 05, 2016

UCHAGUZI MKUU YANGA JUNI 05, 2016

April 25, 2016
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo imetangaza Juni 05, 2016 kuwa siku ya Uchaguzi Mkuu wa viongozi ndani ya klabu ya Young Africans SC ya jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Wakili Aloyce Komba amesema mchakato mzima wa uchaguzi wa klabu ya Young Africans utakuwa ndani ya siku 33, ambapo mchakato unatarajiwa kuanza rasmi Mei 03, 2016.
Komba amesema jukumu lao Kamati ya Uchaguzi TFF  ni kusimamia na kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo unafanyika katika hali ya demokrasia.
Ifuatayo ni kalenda ya mchakato wa Uchaguzi katika klabu ya Young Africans SC:
Mei 03, 2016 Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, atatangaza mchakato wa kulabu ya Young Africans, nafasi zinazogombewa na kubandika kwenye mbao za matangazo.
Mei 04-9, 2016 – Kuanza kuchukua fomu za kugombea na mwisho wa kurudisha fomu kwa wagombea.
Mei 10, 2016 Kamati ya Uchaguzi TFF itakaa kikao cha mchujo wa awali  wa wagombea na kuandika barua za kuwajulisha wagombea juu ya mchujo wa awali.
Mei 11, 2016 Kamati ya Uchaguzi TFF itachapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo orodha ya awali ya wagombea.
Mei 12-13, 2016 Kipindi cha kupokea na kuweka pingamizi kwa wagombea wote.
Mei 14-15, 2016 Kamagi ya Uchaguzi TFF itapitia pingamizi zote na kufanya usajili wa wagombea.
Mei 16, 2016 Kamati ya Uchaguzi TFF itatangaza na kubandika kwenye mbao za matangazo matokeo ya awali ya usahili.
Mei 17, 2016 Sekretarieti kuwasilisha masuala ya kimaadili kwenye Kamati ya Maadili ya TFF.
Mei 18-19, 2016 Kamati ya Maadili TFF itapokea, kusikiliza na kutolea maamuzi ya kamati ya maadili.
Mei 20, 2016 Kamati ya Maadili ya TFF itatangaza maamuzi ya kamati.
Mei 21-22, 2016 Kipindi cha kukata Rufaa kwa maamuzi ya masuala ya Kimaadili kwenye kamati ya Rufaa ya Maadili TFF.
Mei 23, 2016 Kamati ya Maadili tff itasikiliza rufaa za kimaadili.
Mei 24, 2016 Kamati ya Rufaa ya Maadili itatoa maamuzi ya Rufaa.
Mei 25-26, 2016 Kipindi cha kukata Rufaa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi kwenye kamati ya Rufaa ya Uchaguzi TFF.
Mei 27-28, 2016 Rufaa kusikilizwa na kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Mei 29, 2016 Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi TFF kutangaza maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Mei 30, 2016 Kamati ya Uchaguzi TFF kuchapisha orodha ya mwisho ya wagombea na kutangazwa na kubandikwa kwenye mbao za matangazo.
Mei 31 – Juni 04, Kipindi cha kampeni kwa wagombea.
Juni 05, 2016 siku ya Uchaguzi Mkuu wa klabu ya Young Africans.
Wakati huo huo Kamati ya Rufaa ya TFF Jumamosi, itasikiliza pia rufaa ya klabu ya Geita Gold pamoja na rufaa ya kocha msaidizi wa Toto Africans Choke Abeid,

KILOMBERO SUGAR YAWEKEZA ZAIDI YA MILIONI 200 MWAKA JANA KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KIJAMII

April 25, 2016

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kilombero Sugar Mark Bainbridge akiwaongoza Wazazi na wafanyakazi wa Kilombero Sugar kukagua darasa katika shule ya msingi Muungano lililojengwa kwa ufadhili wa chama cha kusaidia jamii cha Kilombero Community Charitable Trust (KCCT). Hafla hiyo ilifanyika Kilombero mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi mtendaji wa Kilombero Sugar Mark Bainbridge akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi ya Muungano mbele ya darasa la awali lililojengwa kwa ufadhili wa chama cha kusaidia jamii cha Kilombero Community Charitable Trust (KCCT) Hafla hiyo ilifanyika Kilombero mwishoni mwa wiki.
Mwakilishi wa Kilombero Sugar Joseph Rugaimukamu akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Muungano baada ya kukabidhiwa madawati na chama cha kusaidia jamii cha Kilombero Community Charitable Trust (KCCT), hafla hiyo ya kukabidhi ilifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro. 
******************
Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kimewekeza zaidi ya shilingi milioni 200 katika kipindi cha mwaka jana kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii katika nyanja za afya na elimu, ikiwa ni kurudisha sehemu ya pato lake kwa jamii ambapo kiwanda kinaendesha shughuli zake.

Meneja wa Mfuko wa kusaidia Jamii (Kilombero Community Charitable Trust (KCCT) Mary Elizabeth alisema jana kuwa miradi iliyotekelezwa mwaka jana ni pamoja na ujenzi wa madarasa miwili katika shule za msingi Kalunga na Muungano kwa jumla ya shilingi milioni 38.5.

Alisema kabla ya utekelezaji wa mradi huu, wanafunzi wa chekechea walikuwa wakisomea chini ya mti wa mwembe ambapo masomo yamekuwa yakiahirishwa mara kwa mara kutokana na mvua na wakati mwingine ilibidi kufyeka majani marefu ili kuandaa sehemu ya kusomea.

Mradi mwingine uliotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Mang’ula and Mgudeni wenye thamani ya shilingi milioni 30. Kila choo kina mashimo sita na sehemu ya kujisaidia haja ndogo na pia kwa ajili ya watu wenye ulemavu.

 “Pamoja na kuwa Mmoja wa wazalishaji wakubwa wa Sukari nchini, pia Kiwanda cha Sukari Kilombero kimekuwa mstari wa mbele kusaidia miradi mbalimbali ya afya na Elimu ili kuweza kuboresha mazingira ya kusomea and afya za Watoto wa wilaya za Kilombero na Kilosa,” alisema.

Aliitaja miradi mingine ya kijamii iliyotekelezwa ikiwa ni Pamoja na ujenzi wa bweni la wasichana katika shulie ya sekondari ya Ruhembe kwa thamani ya shilingi milioni 90 ambalo litaweza kupokea wanafunzi 48. Hii itaondoa usumbufu wa kutembea kwa zaidi ya kilomita 40 kila siku kwa wasichana hawa.

Kwa upande wa afya, Kiwanda cha Sukari Kilombero kinaendelea na ujenzi wa Nyumba ya wafanyakazi wa afya katika hospitali ya Nyandeo wenye thamani ya shilingi milioni 43. Pia katika kuendeleza mashirikiano kati ya Mfuko wa Kusaidia Jamii na Kiwanda cha Sukari wamewekeza zaidi ya shilingi milioni 700.

Akishukuru katika hafla ya makabidhiano, mkuu wa shule ya sekondari ya Ruhembe Bw Johannes Ruekulamu alishukuru Kiwanda cha Sukari Cha Kilombero kwa ujenzi wa bweni ambalo litaongeza ufaulu, nidhamu na kupunguza mimba kwa Watoto wa shule.

Naye mwenyekiti wa kamati ya Wazazi shule ya msingi Muungano Bw Denis Athanas alisema ujenzi wa madarasa utamaliza kabisa tatizo la muda wa zaidi ya miaka sita ambapo wanafunzi wamekuwa wakisomea chini ya mti na mara nyingi wakinyeshewa na mvua au jua kali.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI LEO TAREHE 25 APRILI, 2016 AMEFANYA UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA 26 YA TANZANIA BARA.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI LEO TAREHE 25 APRILI, 2016 AMEFANYA UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA 26 YA TANZANIA BARA.

April 25, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Aprili, 2016 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara. Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, 2 wamebadilishiwa vituo vya kazi na 13 wamebakisha katika vituo vyao vya sasa.  Makatibu Tawala wapya walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
  1. Arusha -                     Richard Kwitega
  2. Geita –                         Selestine Muhochi Gesimba
  3. Kagera –                      Armatus C. Msole
  4. Kilimanjaro -            Eng. Aisha Amour
  5. Pwani –                       Zuberi Mhina Samataba
  6. Shinyanga –                Albert Gabriel Msovela
  7. Singida -                     Dr. Angelina Mageni Lutambi
  8. Simiyu -                      Jumanne Abdallah Sagini
  9. Tabora -                     Dkt. Thea Medard Ntara
  10. Tanga -                       Eng. Zena Said
Makatibu Tawala waliobadilishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo;
  1. Kigoma -                     Charles Amos Pallangyo (Kutoka Mkoa wa Geita)
  2. Morogoro -                Dkt. John S. Ndunguru (Kutoka Mkoa wa Kigoma)
Makatibu Tawala waliobakishwa katika vituo vyao vya sasa vya kazi ni kama ifuatavyo;
  1. Dar es salaam -         Theresia Louis Mbando
  2. Dodoma -                  Rehema Hussein Madenge
  3. Iringa –                        Wamoja Ayubu Dickolagwa
  4. Katavi –                       CP Paul Chagonja
  5. Lindi –                         Ramadhan Habibu Kaswa
  6. Mara –                        Benedict Richard Ole Kuyan
  7. Manyara –                  Eliakimu Chacha Maswi
  8. Mbeya-                       Mariam Amri Mjunguja
  9. Mtwara –                     Alfred Cosmas Luanda
  10. Mwanza -                   CP. Clodwing Mathew Mtweve
  11. Njombe –                    Jackson Lesika Saitabau
  12. Rukwa –                      Symthies Emmanuel Pangisa
  13. Ruvuma -                    Hassan Mpali Bendeyeko
Makatibu Tawala wa Mikoa 10 ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza, wataapishwa siku ya Jumatano tarehe 27 Aprili, 2016 saa tatu asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam. Gerson Msigwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU Dar es salaam 25 Aprili, 2016

ST CHRISTINA YAFUNIKA MAHAFALI TANGA

April 25, 2016




Tangakumekuchablog
Tanga, WAZAZI na Walezi Tanga wametakiwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni na kupiga vita michezo mitaani  wakati wa masomo lengo likiwa nikuondosha wimbi la watoto mitaani.
Akizungumza wakati wa mahafali ya 14 shule ya ST, Christina Girls Secondary School ya Tanga juzi, Afisa Elimu Mkoa, Mayasa Hashimu, alisema kuna wimbi kubwa la watoto  ambao wako na umri wa kwenda shule wanashinda mitaani.
Aliwataka kuhakikisha kila mzazi na walezi watoto wao wanashiriki kikamilifu masomo darasani na kupiga vita mchezo wa pool wakati wa kazi masomo  lengo likiwa nikuwajenga kielimu na kuwa msaada maishani mwao ya baadae.
“Hapa tupo wazazi walezi pamoja rika mbalimbali, kupitia hadhara hii ya kuwaaga watoto wetu, tuhakikishe kila mmoja anakuwa na wajibu wa kutambua kijana wake anaenda shule” alisema Mayasa na kuongeza
“Ofisi yangu niko na utaratibu wa kufanya ziara shuleni kuona mahudhuria ya wanafunzi darasani, sitakuwa tayari kuona idadi ya wanafunzi wa darasani inapungua na niko tayari kwenda hadi kwa mzazi” alisema
Alisema ili kulifanikisha lengo la mtoto kupata haki yake ya kupata elimu ni wajibu wa wazazi kuhakikisha wanashiriki masomo kikamilifu na kuacha kuwatumikisha kazi ambazo hawastahili kuzifanya.
Kwa upande wake, Afisa Taaluma Taasisi ya Counfusion Chuo Kikuu Dar es Salaam, Isaac Mbata, alisema kwa mara ya kwanza wataanza kufundisha lugha ya Kichina katiba baadhi ya shule nchini na kuanzia wataanza na ST Christina ya Tanga.
Alisema uamuzi wa kufundisha lugha hiyo ni kuona umuhimu mfumo wa utandawazi katika biashara  na kupendelea kuanza shule ya ST Christina na nyengine kutajwa mbeleni.
“Umuhimu wa kufundisha kichina kwa baadhi ya shule ni uamuzi tuliooa utakuwa sahihi kwanza kibishara na mahusiano ya wenzeti ambao tumekuwa tukienda kwao mara kwa mara na wao pia wapo wengi hapa nchini” alisema Mbata
Mbata aliwataka wanafunzi hao kulipokea wazo hilo la lugha ya kichina ambalo amesema mbali ya kujua lakini pia ni moja ya sehemu ya lugha za kigeni ambayo inaweza kumpatia mtu ajira mbele ya safari katika maisha.


 Wanafunzi wa kidato cha sita shule ya Srkondari ya ST Christina ya Tanga, wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kutunukiwa vyeti wakati wa mahafali ya 14 shuleni hapo juzi. Jumla ya wanafunzi 121 walimaliza masomo yao.




Wahitimu wa kidato cha sita shule ya Sekondari ya ST, Christina  Tanga, wakiingia ukumbini wakati wa mahafali ya 14 shuleni hapo juzi, Jumla ya wahitimu 121 walimaliza masomo ya kidato cha sita juzi.