Kauli ya Chadema kuhusu kupotea Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Kwemtui Lushoto

May 19, 2013

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kanda ya kaskazini,Amani Golugwa akizungumza na waandishi wa habari mapema jana kuhusu kupotea kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kwekitui Lushoto kupitia chama hicho Miraji Kassimu ,kulia kwa katibu huyo ni Katibu wa Baraza la Vijana Chadema mkoa wa Tanga Jonathani Baweje na kushoto kwake ni Afisa kutoka chama hicho kanda hiyo Amina Thaguti "Aminata"

Chambo aahidi kuihamishia Mgambo Shooting uwanja wa Handeni msimu ujao

May 19, 2013

KIKOSI cha Mgambo wakiwa na Katibu wa Wizara ya Uchukuzi,Omari Chambo mara baada ya kumalizika mechi ya Ligi kuu Tanzania bara na timu hiyo kufanikiwa kubaki ligi kuu msimu ujao.




PAMBANO LA SIMBA, YANGA LAINGIZA MIL 500/-

PAMBANO LA SIMBA, YANGA LAINGIZA MIL 500/-

May 19, 2013
Na Boniface Wambura,Dar es Salaam.

Pambalo la watani wa jadi Simba na Yanga la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Mei 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa mabingwa wapya Yanga kushinda mabao 2-0 limeingiza sh. 500,390,000.

Mechi hiyo namba 180 ambayo ilikuwa kati ya saba la kuhitimisha ligi hiyo msimu wa 2012/2013 ilishuhudiwa na watazamaji 57,406 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,970,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,330,677.97.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 19,039 na kuingiza sh. 95,195,000 wakati kile cha sh. 7,000 kiliingiza watazamaji 17,647 na kupatikana sh. 123,515,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 63,036,064.81, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 37,821,638.88, Kamati ya Ligi sh. 37,821,638.88, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,910,819.44 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,708,415.12.
       
Mwisho.
Mradi wa kituo cha Kupoozea umeme Sahare ni juhudi za Serikali Kuu.

Mradi wa kituo cha Kupoozea umeme Sahare ni juhudi za Serikali Kuu.

May 19, 2013

Na Oscar Assenga, Tanga.
IMEELEZWA kuwa mradi wa kituo cha kupozea umeme kilichopo Sahare (33/11Kv,15MVA)ni muendeleo wa Juhudi za serikali kuu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hapa nchini kuendeleza usambazaji wa umeme wa uhakika katika maeneo yote hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa  na Mkurugenzi wa Millenium Challenge Tanzania,Mhandisi,Ipack Chanji wakati akitoa taarifa ya mradi wa kituo hicho kidogo cha kusambazia umeme Sahare kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2013 ambapo amesema mradi huo ulianza Juanri mwaka 2011 na unatarajiwa kukamilika Julai 2013.

Chanji amesema mradi huo ni utatumia kiasi cha (dola 1,541,408.95) ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania 2,508,643,066.12(Bilioni mbili milioni mia tano na nane,laki sita arobaini na tatu elfu sitini na sita na senti kumi na mbili) zilizopatikana kupitia akaunti ya changamoto za millennia ikiwa ni msaad wa watu wa marekani.

Amesema faida za mradi huo ni kuongeza nguvu ya umeme hasa kwa maeneo ya viwandani kitendo ambacho kitavutia wawekezaji ndani na nje pamoja na kupatikana  umeme wa uhakika kwa mahitaji ya nyumbani na maofisini na hivyo kuongeza tija kwenye uzalishaji mali hasa za viwandani ikiwemo kukua kwa pato la Taifa.

Mwenge huo umezindua miradi 7 yenye thamani ya bilioni 8 katika wilaya ya Tanga ambayo ni maabara katika shule ya sekondari st.christina,barabara ya viwandani,chama cha ushirika wafugaji maziwa kichangani,umeme,

  Mwisho.