SHAMRA SHAMRA ZA SOKO LA SONI JANA.

April 12, 2015


 Wafanyabiashara wa matunda na mbogamboga mji mdogo wa Soni Wilayani Lushoto Mkoani Tanga wakisubiri wateja. Wafanyabiashara hao kwa muda mrefu wamekuwa wakiiomba halmashauri ya Wilaya kuwajengea vizimba kuepukana na kero nyakati za  mvua na jua,Picha zote na Salum Mohamed.




PICHA VURUGU KUBWA ZATOKEA MJINI IRINGA POLISI WALAZIMIKA KUTUMIA MABOMU,NI KATIKA ENEO LA IPOGOLO

April 12, 2015

 
Askari wa FFU wakiwa katika msako wa kuwasaka waliohusika na vurugu hizo eneo la Ipogolo mjini Iringa

MBOWE AKABIDHI AMBULANCE MBILI KWA HOSPITALI YA WILAYA YA HAI NA HOSPITALI YA MACHAME

April 12, 2015

Magari mawili ya kubebea wagonjwa(Ambulance) yaliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe yakiwasili katika viwanja vya soko la Kuni kwa ajili ya kukabidhiwa kwa viongozi wa hosptali ya wilaya ya Hai pamoja na hosptali ya Machame inayosimamiwa na kanisa la KKKT.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akiwa amembeba mtoto mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Kuni na kulakiwa na wananchi katika jimbo hilo.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini atembelea mgodi wa dhahabu bulyanhulu

April 12, 2015

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (kushoto) akipeana mkono na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, Brad Gordon, wakati alipowasili kutembelea mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, ulioko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga, Jumamosi Aprili 11, 2015.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (aliyesimama) akitoa hotuba yake mwanzoni mwa ziara yake ya kutembelea mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Jumamosi Aprili 11, 2015. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, Brad Gordon, na kulia ni makamu wa rais wa kampuni hiyo anayeshughulikia masuala ya kampuni hapa Tanzania, Deo Mwanyika.

Kaimu Meneja Mkuu mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Benedict Busunzu, akizungumza shughuli za uchimbaji madini za mgodi huo na huduma zitolewazo kwa jamii, wakati naibu waziri wa jishati na madini, Charles Kitwanga, alipofanya ziara ya kutembelea mgodi huo, Jumamosi Aprili 11, 2015.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, Brad Gordon, akizungumza wakati wa uwasilishaji shughuli mbalimbali zifanywazo na migodi inayomilikiwa na kampuni hiyo hapa nchini ya Bulyanhulu, North Mara na Buzwagi, wakati wa ziara ya naibu waziri wa nishati na madini, Charles Kitwanga, alipotembelea mgodi wa Bulyanhulu uliko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga, Jumamosi Aprili 11, 2015.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, Brad Gordon, (wapili kushoto), akimpa maelezo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, (watatu kushoto), alipotembelea eneo la chini ya ardhi la mgodiwa Bulyanhulu kiasi cha kilomita 1.5 chini ya bardhi, Jumamosi Aprili 11, 2015. Kushoto ni mwenyekiti wa kampiuni ya uchimbaji dhahabu ya Mlalo, Mohammed Hussein.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, Brad Gordon, (Kulia), akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 749.53, Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shjinyanga, Mophen Mwakajonga, ikiwa ni kodi ya huduma (service levy), huku Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (katikati) akishuhudia. Hafla hiyo ilifanyika kwenye mgodi wa Bulyanhulu ulioko wilayani humo April 11, 2015.
Sehemu ya Ujumbe ulioambatana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga katika ziara ya mgodi wa Bulyanhulu April 11, 2015.
Naibu waziri wa nishati na madini, Charles Kitwanga, (wakwanza kushoto) na ujumbe wake, wakipatiwa maelezo ya kiusalama muda mfupi kabla ya kuanza ziara ya kutembelea shughuli za uchimbaji madini chini ya ardhi kwenye mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu uliko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga Jumamosi Aprili 11, 2015.
Naibu waziri wa nishati na madini, Charles Kitwanga, (kushoto), na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, Brad Gordon, (kulia), wakimsikiliza mtaalam wa shughuli za uchimbaji madini ardhini, wa mgodi huo, wakati wa ziara ya naibu waziri Jumamosi Aprili 11, 2015.

IMETOSHA yaendeleza mkakati wake kimataifa kusafisha jina la nchi

April 12, 2015
Mkakati wa kutokomeza unyanyapaa na mauaji ya watu wenye ualbino nchini, uitwao IMETOSHA, jana ulianza rasmi kujitokeza kimataifa baada ya kushiriki katika pambano la kimataifa la kirafiki kati ya nyota wa zamani wa Barcelona na Veterani wa Afrika Mashariki.

Katika mpambano huo wa kimataifa uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mkangara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadick na maafisa kutoka katika mkakati huo walipata nafasi ya kuongea na wachezaji hao nyota wa Barcelona kuhusiana na dhana iliyoko katika nchi za nje ambako inaaminika Tanzania wanauana wenyewe kwa wenyewe kutokana na imani za kishirikina.
Akiongea baada ya mpambano huo ambapo Barcelona waliibuka washindi, Balozi na muasisi wa mkakati huo unaoelekea na sura ya kizalendo na kitaifa, Bw. Henry Mdimu alisema kulikuwa na haja wachezaji hawa warudi na ujumbe kwao wenye majibu ya maswali wanayojiuliza kuhusiana na mauaji ya albino na kukosa majibu.

"Maneno haya ya kwamba sisi tunauana kwa imani za kishirikina, ingawa matukio mengi yapo kanda ya Ziwa lakini nchi nzima inachafuka kwa hiyo haja ya kusafisha jina la nchi kwa mataifa ya nje ipo na sisi IMETOSHA tumeamua kuchukua jukumu", alisema Balozi huyo ambaye pia ana ualbino.

Mdimu alibainisha kwamba katika mkakati wa kimataifa wameanza kwa kuanzisha tovuti (imetosha.or.tz) ambayo itakuwa ikionesha matukio mbali mbali yanayopinga mauaji na unyanyapaa ili wanaoamini vingine waone kwamba unyanyapaa na mauaji kwa watu wenye ualbino si kitu ambacho watanzania kama taifa wanakifurahia.

Balozi huyo pia alitoa wito kwa kila mtanzania kuuunga mkono mkakati wa IMETOSHA ili katika miaka 20 ijayo  kizazi kijacho kiwe na jamii yenye watu wenye ualbino wanaoishi kwa amani katika nchi yao.
Wachezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania wakiongozwa na Patrick Kluivert (aliebeba mtoto) wakiingia uwanjani tayari kwa kukipiga na timu ya Tanzania Veterans katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. hadi mwisho wa mchezo, Barcelona ya Hispania ilishinda bao 2-1.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania, Patrick Kluivert akifurahia jambo na Mtoto Sharifa mwenye Ualbino kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Tanzania Veterans uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. 
 
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mkangara (wa pili kulia) akizungumza jambo na Mchezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania, Patrick Kluivert wakati akiwasalimia wachezaji hao kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Tanzania Veterans, uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jana.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadick.
Sehemu ya Wachezaji wa timu ya Tanzania Veterans na Barcelona wakiwa kwenye picha ya pamoja na Watoto wenye Ualbino mbele ya Bango la Mkakati wa kutokomeza unyanyapaa na mauaji ya watu wenye ualbino nchini, uitwao IMETOSHA.Habari/Picha na Othman Michuzi
-- Othman Michuzi Editorial Director & Chief Photographer CELL: +255 713 775869 /+255 789 103610 WEB: issamichuzi.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com michuzijr.blogspot.com EMAIL: othmanmichuzi@gmail.com Dar Es Salaam. Tanzania. East Africa.