zanchick yajipanga kushirikiana na wizara ya kilimo,maliasili,mifugo na uvuvi kuwasaidia wafugaji na wakulima wadogowadogo.
Uongozi wa Shamba la Kuku Maruhubi { Zanchick } umejipanga
kushirikiana na Wizara ya Kilimo,
Maliasili, Mifugo na Uvuvi katika kuwasaidia wafugaji na wakulima wadogo
wadogo Nchini ili waendeshe miradi yao ya uzalishaji katika misingi ya
kitaaluma.
Mkuu na muanzilishi wa Shamba hilo Dr. David Elua
akiuongoza ujumbe wa Viongozi watatu wa shamba hilo alieleza hayo wakati
akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini
kwake vuga Mjini Zanzibar.
Dr. David Elua alisema mpango huo uliolenga
kutekelezwa pande zote mbili za Muungano, Tanzania Bara na Zanzibar
utawanufaisha wanachi wa kipato cha chini zaidi ya 45,000 kwa kupata ajira
katika uendeshaji wa miradi ya ufugaji kuku kwa kutumia njia ya kisasa.Alisema katika hatua ya awali shamba hilo tayari
limeshatoa ajira zipatazo 300 katika kiwanda chake cha kutotoa vifaranga vya
Kuku kiliopo Maruhubi juhudi zikiwekwa zaidi katika kuunga mkono azma ya Serikali
Kuu katika uwekezaji wa viwanda vidogo vidogo.
Dr. David alimfahamisha Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar kwamba Sera hiyo iliyoanzishwa na Serikali na kuanza kukubalika kwa
baadhi ya mashirika na taasisi za uwekezaji ndani na nje ya nchi itawasaidia
zaidi vijana kupata ajira badala ya kusubiri ajira za serikali ambazo ni finyu
kwa miaka ya sasa.
Akizungumzia ugonjwa wa kuambukiza wa kipindupindu
ulioikumba Zanzibar katika Kipindi hichi Mkuu na Muanzilishi wa Shamba hilo la
Kuku Maruhubi Dr. David alisema Uongozi wake umepata mshtuko kutokana na janga
hilo linaloendelea kusumbua wananchi hasa Watoto wadogo.
Dr. David alisema Zanchick imeahidi kutoa mchango wa
shilingi Milioni 10,000,000/- ili zisaidie nguvu ya Serikali katika mapambano
yake dhidi ya maradhi hayo yaliyopoteza maisha ya watu wasiopungua 53 tokea
yavikumbe Visiwa vya Zanzibar mwezi septemba mwaka uliopita.
Akitoa shukrani zake kwa Uongozi wa Shamba hilo la
Kuku Maruhubi {Zanchick} Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kuzifanyia kazi
changamoto zote zinazoikumba Taasisi hiyo katika kuendesha miradi yake ya
uwekezaji hapa Nchini.
Balozi Seif alisema Serikali imeamua kuimarisha
miundombinu katika sekta mbali mbali za Uwekezaji ili kujenga mazingira bora
yatakayotoa fursa kwa Taasisi na Makampuni ndani na nje kuwekeza miradi yao ya
kiuchumi ili hatimae isaidie uchumi wa Taifa.
Shamba la Kuku Maruhubi ni miongoni mwa Taasisi za
uwekezaji zilizohamasika kuja kuwekeza miradi yao Nchini kufuatia ziara ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyoifanya Nchini Marekani mwezi
Oktoba mwaka 2011 kwa mualiko wa shirika la uwekezaji vitega uchumi Barani
Afrika la Nchini Marekani.
Ziara hiyo ya Balozi Seif ililenga kuitangaza
Zanzibar kwa taasisi na mashirika ya Marekani kuangalia uwezekano wa kuwekeza
miradi yao katika maeneo yaliyomo ndani ya Sekta za Utalii, Biashara, Elimu,
Kilimo, Afya, Miundombinu pamoja na Mazingira.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
6/5/2016.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Ujumbe wa Viongozi wa Shamba la Kuku
Maruhubi { Zanzchick } uliofika ofisini kwake kubadilishana mawazo juu ya sekta
ya uwekezaji.Aliyempa mkono ni Mkuu na muanzilishi wa shamba hilo
Dr. David Elua, wa kwanza kutoka kulia ni Meneja operesheni wa Shamba hilo Bw.
Christopher Kontonasios na wa kwanza kutoka kushoto ni Nd. Issa Kassim.
Balozi Seif akizungumza na Ujumbe
wa Viongozi wa Shamba la Kuku Maruhubi { Zanzchick } ukiongozwa na Mkuu na
muanzilishi wa Shamba hilo Dr. David Elua.
Balozi Seif akiwa katika picha ya
pamoja na Ujumbe wa Viongozi wa Shamba la Kuku Maruhubi { Zanzchick } mara
baada ya mazungumzo yao.Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu na muanzilishi wa
Shamba hilo Dr. David Elua, Bwana Michael Mantheakis, Nd. Issa Kassim na kushoto
ya Balozi Seif ni Meneja operesheni wa Shamba hilo Bw. Christopher Kontonasios.Picha na – OMPR – ZNZ.
RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANACHI ALIPOKUWA SAFARINI KUTOKEA DODOMA KUELEKEA ARUSHA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Babati Mkoani Manyara waliomsimamisha
sehemu mbalimbali wakati akitokea Dodoma kuelekea mjini Arusha kwa njia
ya barabara leo Mei 6, 2016. PICHA NA IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Babati Mkoani Manyara waliomsimamisha
wakati akitokea Dodoma kuelekea mjini Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Babati Mkoani Manyara waliomsimamisha
wakati akitokea Dodoma kuelekea mjini Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua
karanga kutoka kwa mjasiriamali mara baada ya kuwahutubia mamia ya
wakazi wa Babati mkoani Manyara waliojitokeza katika eneo la Stendi ya
Mabasi ya Babati Mkoani Manyara.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Magugu mkoani Manyara wakati
akielekea Mkoani Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na wafanyabiashara wa Stendi ya Mabasi ya Singida wakati alipokuwa
njiania kuelekea Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na wakazi wa Endasak mkoani Manyara wakati akitokea Dodoma kuelekea
Arusha kwa njia ya barabara.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na wananchi wa Dareda mkoani Manyara waliojitokeza kumsalimia wakati
akitokea Dodoma kuelekea mkoani Arusha. PICHA NA IKULU
Wizara ya Afya yapokea vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.4
Mkurugenzi
wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila (kushoto) akiongea na Waandishi wa
Habari leo 6 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam kuhusu msaada walioupokea
toka Shirika la Afya Duniani (WHO) wenye thamani ya shilingi bilioni
1.4.
Mkurugenzi
wa Huduma za Kinga,Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Neema Rusibimayila (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa
Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro
wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa tiba leo 6 Mei, 2016 jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi
wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa
Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro
wakikabidhiana hati za makabidhiano ya vifaa tiba leo 6 Mei, 2016 jijini
Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro
(kulia) akikabidhi jokofu kwa kwa jaili ya huduma za chanjo kwa
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila leo 6 Mei, 2016 jijini
Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro
(kulia) akikabidhi jokofu kwa kwa jaili ya huduma za chanjo kwa
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila leo 6 Mei, 2016 jijini
Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye
thamani ya shilingi bilioni 1.4 ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kutoa
chanjo kwa akina mama na watoto dhidi ya magonjwa mbalimbali nchini.
Akiongea na waandishi
wa habari Wizarani hapo, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila
ameeleza kuwa vifaa tiba hivyo vitasaidia uhifadhi wa chanjo katika
mikoa mbalimbali pamoja halmashauri nchini.
‘’Ni msaada mkubwa tulioupata
toka WHO na nina amini kuwa utatusaidia sana katika kufanikisha suala la
chanjo kwa akina mama na watoto nchini na pia tunaamini wataendela
kushirikiana na Wizara ili tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea’’,
alisema Dkt. Rusibimayila.
Ameongeza kuwa, kwa sasa vituo
vipya vinavyofunguliwa nchini vikiwemo vile ambavyo havikuwa na majokofu
vitakuwa na uwezo wa kupata vifaa hivyo kama vile majokofu na vifaa
vingine vya tiba ili huduma za chanjo ziweze kutolewa katika kila kituo
nchini.
Akikabidhi vifaa hivyo Wizarani
hapo, Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt.
Rufaro Chatoro amesema kuwa vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi
bilioni 1.4 ni pamoja na majokofu 200 pamoja na vifaa vitumikavyo kwa
ajili ya kutolea chanjo.
Kwa upande wake Mratibu Chanjo
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bwana
Emmanuel Yohana ameeleza kuwa, majokofu hayo pia yatapelekewa katika
wilaya ambayo yana upungufu wa majokofu pamoja na vituo vipya kwa ajili
ya kupunguza umbali kwa wagonjwa wa chanjo na pia ni moja ya kuweka
huduma karibu na wananchi nchini.
Aidha, ameongeza kuwa spesimeni
za polio na surua zilizotolewa na WHO zitapalekwa pia katika vituo kwa
jili ya kuchukua damu kwa ajili ya vipimo na kuletwa Dar es Salaam kwa
uchunguzi zaidi wa maabara.
‘’Wanufaika wa huu msaada
kutoka WHO ni wananchi wote wa Tanzania kwani utaenda katika vituo vyote
vya chini zikiwemo Zahanati’’, alisema Yohana.
Kupitia wadau mbalimbali Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea
kushirikiana na wadau hao katika kutafuta vifaa tiba mbalimbali kwa
lengo la kuhakikisha kuwa sekta ya afya nchini inaimarika kwani Tanzania
kwa sasa imeweza kudhibiti polio kwa kiasi kikubwa.
UN NA EU WAFURAHISHWA NA MIRADI WALIYOIFADHILI JIJINI MWANZA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) akisalimiana na kumkaribisha ofisini kwake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale (katikati) walipowasili jijini Mwanza kabla ya ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Ulaya.
MRATIBU Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale, wamesema wameridhishwa na miradi inayofadhili maeneo kadhaa jijini Mwanza.
Wakizungumza baada ya kutembelea Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Mwauwasa), Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC), Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) na Radio ya Kijamii (Saut), walisema utekelezaji wa miradi hiyo imewatia hamasa kubwa.
Awali akizungumza katika ofisi za Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo, Anthony Sanga, alisema mradi unaoendelea sasa wa kusambaza maji safi utakapokamilika utaweza kuwafikia wakazi 54,000 badala ya 23,000 wa sasa.
Sanga alisema mradi huo utakapokamilika Mei mwaka huu, utawafikia wakazi kwa asilimia 90 badala ya 68 za sasa.
“Mradi ukishakamilika utafanikisha makusanyo ya Sh. Bilioni 1.4 kwa mwezi badala ya kukusanya Sh. milioni 316 za sasa kwa mwezi, ukiwa na matanki ya ujazo wa lita 33,400,” alisema Sanga.
Akizungumzia hilo, Rodriguez alisema baada ya kushuhudia miradi hiyo ukiwamo wa maji taka chini ya ufadhili wa EU, amefurahishwa na hali ya miradi hiyo.
“Timu yetu imetembelea Mwauwasa na kushuhudia miradi hiyo inayofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya kwa ajili ya huduma ya maji kwa wananchi, pia tumeenda kuangalia chanzo cha maji na yanapowekwa maji taka,” alisema Rodriguez.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Prof. Kien Mteta, alishukuru UN na EU kwa miradi hiyo na kuja kushuhudia ufadhili wao.
“Ufadhili umelenga katika mambo matatu, moja kwenye maabara ambako vilinunuliwa vifaa vya mbalimbali vikiwamo vya kutambua kansa, pili vifaa vya mionzi kwa ajili kutambua vyanzo vya magonjwa,” alisema Prof. Mteta.
Aidha, alisema pia wafadhili hao walitembelea kitengo cha kutoa matibabu ya mionzi ya kansa, ambacho kinawafunza baadhi ya watumishi wake na upatikanaji wa mashine.
Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella mara baada ya kuwasili ofisini kwake mwishoni mwa wiki.
Hospitali ya Bungando yenye uwezo wa vitanda 950 iliyoanzishwa mwaka 1972 ni miongoni mwa hospitali nne kubwa nchini ambazo hutoa tiba maalumu ikihudumia watu milioni 16 katika mikoa minane ya kanda ya ziwa.
Hospitali hii inatoa tiba ya ugonjwa wa saratani kwa mifumo miwili. Moja kwa kutumia onkolojia au patholojia na tiba kwa kutumia mionzi.
Toka mwaka 2000 hospitali ya Bugando imekuwa ikifanyakazi kwa karibu na kampuni ya kitaliano ya TISSON ASSOCIATION ili kuboresha huduma zake patholiojia na pia kuanza kutibu kansa mwaka 2009.
Wataliano wamewezesha kufundishwa kwa wataalamu wa patholojia na onkolojia ya tiba, vifaa tiba, dawa na kuwezesha ziara za za kifundi za watu wa patholojia na utafiti.
Uangalizi wa wagonjwa wa kansa na matibabu yao ulianza mwaka 2009 na kuelezwa kuwa kwa mwaka wagonjwa 3500 wa kansa huangaliwa.
Huduma ya uangalizi ni pamoja na kufanya utambuzi, upasuaji na utoaji wa tiba ya kemo.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akitoa utambulisho wa ujumbe alioambatana nao kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Hata hivyo wagonjwa wanaohitaji huduma ya mionzi hukatiwa rufaa hospitali ya kansa ya Ocean (ORCI).
Kutokana na kuzidiwa kwa hospitali ya Ocean Road katika tiba ya mionzi, serikali iliamua kutanua huduma zake na kuzifikisha Bugando.
Ili kuwezesha haja ya serikali taasisi ya nguvu za atomiki duniani na ile ya hapa nchini kupitia mpango wa ushirikiano wa kiufundi walianzisha miradi kadha yenye lengo la kuwezesha huduma yenye tija kwa wagonjwa wa kansa.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo yanachangia miradi hiyo imekuwa ikisaidia serikali ya Tanzania kuwezesha tiba ya mionzi katika hospitali ya Bugando.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale katika ziara maalum ya kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na UN pamoja na EU jijini humo.
Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza CP. Clodwig Mtweve, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella pamoja na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale wakiwa wameshilikilia kuhamasisha utekelezaji wa malengo mapya ya maendeleo endelevu (SDGs) ambayo yamewafikia wakazi wa jiji la Mwanza.
Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa) mara baada ya kuwasili katika ofisi hizo jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mhandisi Anthony Sanga, akitoa 'power point presentation' ya maendeleo ya mradi wa maji unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya jijini Mwanza kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mhandisi Anthony Sanga akitoa maelezo ya mradi kwa ugeni ulioambata na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Maji yakiwa kwenye hatua ya kutakatishwa ili yawe salama kwa watumiaji.
Mhandisi wa ubora wa maji Mwauwasa, Godadi Mgwatu akitoa maelezo kwa mgeni ugeni huo ulioambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kukagua mradi wa maji wa Mwauwasa jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mhandisi Anthony Sanga akitoa maelezo kwa ugeni huo ya namna ya maji yanavyochujwa na kusafisha kwa kutumia mtambo maalum uliopo mbele yao. (Picha zaidi za ziara hii Bofya hapa)
Subscribe to:
Posts (Atom)