ZAWADI DOTTO AIBUKA MSHINDI WA MASHINDANO YA URIMBWENDE YA "MISS ALBINISM 2016".

February 06, 2016
Mrimbwende Zawadi Dotto (Pichani) ameibuka kidedea katika Mashindano ya Miss Albinism Kanda ya Ziwa yaliyofanyika usiku wa Kuamkia leo Jijini Mwanza.

Miss Zawadi mwenye umri wa miaka 17 (mwanafunzi) ameibuka mshiki katika Mashindano hayo ambayo ni maalumu kwa ajili ya Watu wenye ulemavu wa ngozi kwa ajili kuonyesha umahiri wao katika tasnia ya urimbwene hii ikiwa pia ni ishara ya kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi wanaweza kushiriki katika shughuli na mashindano mbalimbali.

Mashindano hayo yanaandaliwa na Taasisi ya kusaidia Watu wanaoishi katika Mazingira hatarishi iitwayo SAVE VUNERABLE FOUNDATION ya Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Shirika hilo Alexander Exaud Mutowo ametanabaisha kwamba, baada ya mashindano hayo kukamilika kwa kanda zote nchini, Washindi wa Kanda hizo watashindanishwa Jijini Dar es salaam ili kumpata Mshindi wa Kitaifa wa MISS ALBINISM 2016.
Wshiriki Saba wa Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa na umri wao katika mabano ambapo kutoka Kushoto ni Hajra Sadru (22), Antonia Mathias William (17), Furaha Edward John (17), Pendo Faustine (15), Zabibu Abdallah (18), Zawadi Dotto (17) pamoja na Asteria Christopher.
Washiriki walioingia Nne bora ambapo kutoka kushoto Hajra Sadru, Furaha Edward, Zabibu Abdallah na Zawadi Dotto
Baada ya Mtifuano mkali hatimae majaji wakatangaza washini. Furaha Edward mshindi wa tatu (Kushoto), Hajru Sadru mshindi wa pili (katikati) na Zawadi Dotto akaibuka kuwa mshindi wa Kwanza (aliepiga magoti).
Mshindi wa Miss Albinism Kanda ya Ziwa akivikwa taji lake. Wa pili kulia ni Jalia Mtani ambae alikuwa Jaji Mkuu akitajana Majina ya washindi. Pembeni ni Mshereheshaji Emmanuel Shalali kutoka Sahara Media Group.
Mshindi wa Miss Albinism Kanda ya Ziwa akivikwa taji lake. Wa pili kulia ni Jalia Mtani ambae alikuwa Jaji Mkuu akitajana Majina ya washindi. Pembeni ni Mshereheshaji Emmanuel Shalali kutoka Sahara Media Group.
Katikati ni Mshindi wa Kwanza, Kulia Mshindi wa Pili na Kushoto Mshindi wa Tatu
Kampuni ya Visimbuzi (Ving'amuzi) ya StarTimes ilikuwa miongoni mwa makampuni yaliyosaidia kufanikisha mashindano hayo. Mwenye Kinasa sauti ni Erick Makonya ambae ni Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Kanda ya Ziwa akitaja zawadi zilizotolewa kwa washindi na Kampuni hiyo ambapo Mshindi wa Kwanza amejinyakulia Simu ya StarTimes  aina ya Solar5, Mshindi wa Pili simu aina ya P40 StarTimes na Mshindi wa tatu amejishindia simu aina ya B27 zote zikiwa ni android kutoka StarTimes.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakiongozwa na Marcella Mayala ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae alikuwa Mgeni Rasmi, wakiwa katika picha ya Pamoja na washindi.
Alexander Exaud Mutowo ambae ni Mratibu wa Shirika la VUNERABLE FOUNDATION  lililoandaa mashindano hayo akizungumza wakati wa mashindano hayo, ambapo amewasihi wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi ikiwemo kuunga mkono juhudi za shirika hilo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jiko katika katika kituo cha kuwahifadhi watu wenye ulemavu wa ngozi Buhangija kilichopo Mkoani Shinyanga.
Fredy Samwel Kaula ambae ni Mwenyekiti wa Shirika la VUNERABLE FOUNDATION akizungumza katika Mashindano hayo
Alfredy Kapole ambae ni Mwenyekiti wa Tanzania Albinism Sociaty TAS akizungumza wakati wa mashindano hayo
Mwenye kinasa sauti ni Marcella Mayala ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae alikuwa Mgeni Rasmi, akifungua mashindano hayo. 
Amesema ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza itaendeleza ushirikiano na Shirika la VUNERABLE FOUNDATION kwa ajili ya kupata wadau wa kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi.
Dickson Kiringo a.k.a Mr.White ambae ni Msanii chipukizi wa Muziki wa Kizazi kipya akitoa burudani. Msanii Barnaba Boy aliahidi kumsaidia Mr.White ili arekodi nyimbo mbili katika studio yake ikiwa ni bure kabisa.
Msanii Barnaba Boy akitoa burudani katika shindano la Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza.
Majaji ambapo kutoka Kushoto ni Jaji Angelina Chuma, Jaji Mkuu Jalia Mtani na Jaji Lilian Lambo
Wa pili kulia ni Alfredy Kapole ambae ni Mwenyekiti wa Tanzania Albinism Sociaty TAS pamoja na wadu wengine wakifuatilia mashindano hayo
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa BINAGI MEDIA GROUP
ZANZIBAR OCEAN VIEW YANUNUA MECHI ZA CAF

ZANZIBAR OCEAN VIEW YANUNUA MECHI ZA CAF

February 06, 2016

index 
MENEJA wa hoteli za Zanzibar Ocean View Jacob Makundi (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Idara ya Michezo wa Vyuo vya Mafunzo Khamis Ali Machenga, shilingi 5,000 zikiwa gharama za tiketi za mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya klabu ya Mafunzo na AS Vita ya DRC itakayochezwa Februaei 13, 2016, ambazo zilikwishachapishwa na kuanza kuuzwa. Kampuni ya hoteli za Zanzibar Ocean View imeamua kubeba gharama hizo pamoja na za mechi ya JKU na Gaborone United ya Botswana kuwania Kombe la Shirikisho.
(Picha na Ameir Khalid).
……………………………………………………………………………..
Na Salum Vuai, ZANZIBAR UONGOZI wa kampuni ya hoteli za Zanzibar Ocean View (ZGH), umeamua kubeba mzigo wa gharama za mechi za wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya klabu barani Afrika zitakazochezwa mwishoni mwa wiki ijayo. Mechi hizo za kwanza za raundi ya awali, ni ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Mafunzo wataikaribisha AS Vita kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, na JKU dhidi ya Gaborone United ya Botswana. Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 6, 2016 katika ukumbi wa Nyerere ulioko hoteli ya Zanzibar Ocean View mjini hapa, Meneja wa hoteli hizo Jacob Makundi, amesema hatua hiyo inalenga kuwafanya mashabiki wafike kwa wingi uwanjani siku ya mechi hizo. Alifahamisha kuwa, tayari kampuni yake imezinunua tiketi elfu kumi (elfu tano kwa kila mechi) zilizobaki baada ya nyengine kuuzwa, kwa gharama ya shilingi elfu kumi, na zitagaiwa kwa mashabiki watakaofika uwanja wa Amaan siku za michezo hiyo bila malipo yoyote. Makundi alifahamisha kuwa, kampuni yake pia itatoa fulana maalumu kwa wachezaji na viongozi wa klabu hizo, ambazo watavaa kabla ya mechi ya kwanza na watakaposafiri kwenda DRC na Botswana kwa ajili ya michezo ya marudiano. Meneja huyo amezitaja gharama nyengine ambazo kampuni hiyo itazibeba, ni kutoa punguzo la asilimia 75 kwa waamuzi, makamisaa, viongozi na wachezaji wa timu za wageni kwa huduma ya malazi na chakula kwenye hoteli zake. Ili kuwapa nguvu wachezaji wa Zanzibar, Makundi aliahidi kuwa kampuni hiyo itatoa zawadi ya shilingi milioni tano iwapo timu itashinda hapa nyumbani, na kuongeza kuwa ushindi huo utakuwa chachu kwao kufikiria motisha zaidi kwa mechi za ugenini. “Kwa kuwa sisi ni wadau wakubwa wa michezo, tumeona iko haja ya kuwashajiisha wawakilishi wetu hawa ili wafanye vizuri na kuinua jina la Zanzibar katika soka la kimataifa na tunatoa wito kwa taasisi nyengine zijitokeze kuongeza nguvu,” alieleza. Mapema, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ) Khamis Abdallah Said, aliushukuru uongozi wa kampuni hiyo, akisema unaonesha uzalendo kwa nchi katika kuunga mkono juhudi za kuendeleza michezo. Naye Abdallah Juma Mohammed, aliyemuwakilisha Mkurugenzi wa kampuni hiyo yenye hoteli tano kubwa Unguja na Pemba Amani Ibrahim Makungu, alisema Zanzibar Ocean imeanza lakini mlango uko wazi kwa wengine kuzisaidia timu hizo na pia michezo mingine. Akitoa shukuani kwa niaba ya timu zote mbuli, Mkuu wa Michezo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKU) Khamis Mohammed Suleiman, alisema ufadhili waliopata utawatia nguvu ya kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya Zanzibar kwenye michuano hiyo. Jumamosi Februari 13, Mafunzo wataikaribisha AS Vita katika mechi ya Ligi ya Mabingwa, wakati siku inayofuata JKU watakuwa wenyeji wa Gaborone United kutika Botswana kuwania Kombe la Shirikuso. Mechi zote hizo zitachezwa katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar kuanzia saa 10:00 jioni, na zile za marudiano zitapigwa wiki mbili baadae.

AFRICAN SPORTS,STAND UNITED HAKUNA MBABE ZATOKA BILA KUFUNGANA MKWAKWANI

February 06, 2016









DC MAKONDA ATOA SIKU 20 WENYEVITI WOTE WA SERIKALI ZA MITAA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM WAPEWE RAMANI ZA MITAA YAO

February 06, 2016
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza na Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wa wilaya hiyo kwenye mkutano uliofanyika Dar es Salaam leo kuhusu jinsi ya kutatua na kukomesha kero za ardhi
Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo, Paul Makonda (hayupo pichani)



Na Dotto Mwaibale

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ametoa siku 20 kwa Wenyeviti wote wa Serikali za Mitaa  Manispaa hiyo kuwa na ramani ya mitaa ili kuyatambua maeneo ya wazi.

Makonda amewataka watendaji wa Manispaa hiyo kwenda na kasi ya serikali ya kuwatendea haki wananchi katika kumaliza migogoro ya ardhi.

Akizungumza Dar es Salaam leo mchana na Wenyeviti zaidi ya 100 wa Serikali za Mitaa ya9 Manispaa ya Kinondoni ,Makonda alisema baadhi ya watendaji wanatanguliza maslahi mbele kuliko mahitaji ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.

Alisema migogoro ya ardhi ni kero kila sehemu  misibani, harusini na kwenye mazishi suala kubwa ni la ardhi na kuongeza kuwa mabaraza ya ardhi ya Kata hayana uhalali wa kuamua kesi hizo kwa kuwa baadhi yao hata uelewa wa masuala hayo hawana na yamekuwa  yakiongeza matatizo.

"Leo tumekutana hapa kwa sababu ya migogoro ya ardhi na kuanzia sasa ndani ya Wilaya ya Kinondoni nataka kurudisha heshima ya Wenyeviti wa Serikali za  Mitaa nawaagiza kuanzia sasa mtu yeyote kutoka Wizarani,Manispaa au hata mwekezaji lazima apitie kwanza kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mitaa,"alisema.

Alisema watendaji wengi Manispaa ndio chanzo cha migogoro ya ardhi kwa kutotimiza wajibu wao na wameshindwa kuonyesha dira ya kuwasaidia wananchi.

"Kibaya zaidi ili kujitengenezea mazingira ya ulaji wenyeviti hawashirikishwi katika hatua za awali wanahusika zaidi pale kunapotokea mgogoro,"alisema.

Aliongeza kuwa "Sina hofu wala uoga wala sina sifa ya kupendwa wala kutafuta kupendwa hivyo nitahakikisha ninatumia Mamlaka niliyopewa kufanya migogoro hii ya ardhi Kinondoni na kuwa historia na nikitaka jambo huwa sishindwi"alisema.

Alisema baada ya wenyeviti hao kupewa ramani atahakikisha anakutana na Wazi ri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilium  Lukuvi na maofisa wa ardhi.

"Hapo sasa watakaobainika kuhusika katika michezo michafu na kuchochea migogoro basi Waziri Lukuvi aondoke nao maana wameshindwa kazi"alisema

Makonda aliwataka wenyeviti hao kuonesha maeneo ya wazi na yale yaliyovamiwa ili kuchukua hatua kwani wenye dhamana wapo ofisini huku wananchi wakiwa wanateseka na migogoro hiyo.

Mkuu wa Idara ya Mipango Miji  Manispaa ya Kinondoni  Juliana Letara alisema Wenyeviti wote watapewa ramani za mitaa yao ndani ya wiki mbili kwa kuwa zipo kwenye kompyuta ofisini hivyo atawapatia ramani hizo.

Alisema kutokana na migogoro mingi ya ardhi anapendekeza kufanyike mapendekezo ya mabadiliko ya sheria kwa kuwa kesi zote za mabaraza ya kata zinaigharimu serikali zaidi ya  milioni tatu kwa siku.

Alizitaja kesi hizo kuwa ni za ardhi ya hifadhi,ardhi ya kawaida na ile ya kimila 

"Tulikopa benki ya TIB mkopo kwa  ajili ya kupima Viwanja likiwemo eneo la Mabwepande lakini kila siku tunatozwa riba ya sh.milioni tatu jambo ambalo ni gumu na ipo siku litashindikana na ndio maana tunauza Kiwanja hadi milioni 20 na 30,"alisema. 

Baadhi ya wenyeviti wa Serikali za Mitaa ambao walipata nafasi ya kuzungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo walimtaka Makonda kuondoa majipu sugu katika Manispaa hiyo likiwemo la maofisa mipango miji.


Alisema  wako tayari kufanyazi na Makonda lakini sio wafanyakazi hao kitengo cha ardhi kwa kuwa wamekuwa chanzo cha migogoro mikubwa ya ardhi.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

TAMASHA LA PASAKA MWAKA HUU KUFANYIKA MACHI 28 WILAYANI KAHAMA.

February 06, 2016

Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tamasha la Pasaka litakalofanyika  Mkoani Shinyanga Wilayani Kahama Machi 28 mwaka huu ambapo Tamasha la Pasaka mwaka huu halitafanyika jijini Dar es Salaam na baadala yake kufanyika mikoani. 

Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama wakati akizungumza nao leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

TAMASHA la Pasaka mwaka huu kufanyika Machi 28 Mkoani Shinyanga katika viwanja kahama wilaya ya Kahama, ambapo tamasha hilo limewapa kipaumbele waimbaji wa ndani ya nchi yetu.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Msama amesema kuwa Kauli mbiu ya Tamasha la Pasaka mwaka huu ni "UMOJA NA UPENDO HUDUMISHA AMANI KATIKA NCHI YETU". ambayo itatawala katika tamasha hilo hapa nchini.

Msama amesema kuwa Mwimbaji wa nyimbo za Injiri Bonfasi Mwaitege amethibisha kutumbuiza katika tamasha hilo pamoja na Mwimbaji wa nyimbo za Injiri Rose Mhando.

 Aidha Msama amelishukuru  Balaza la Sanaa Tanzinia(BASATA) kwa kuruhusu kufanyika Tamasha la Pasaka wilayani Kahama pia amewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika tamasha hilo mkoani humo.

MAADHIMISHO YA CCM YAFANA SINGIDA, JK AMMGIA SIFA LUKUKI RAIS MAGUFULI, YEYE AAGIZA VIONGOZI WASIOTEKELEZA ILANI YA CCM AONDOKE

February 06, 2016
 Rais John Magufuli akiwasalimia wananchi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa CCM Namfua, katika maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM ambayo kitaifa yamefanyika leo mkoani Singida. Kutoka kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana.
 Rais Magufuli akiwapungia mkono wananchi.
 Rais Magufuli akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu pamoja na Nape Nnauye.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete akilakiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana alipowasili kwenye Uwanja wa CCM Namfua, mjini singida kuongoza maadhimisho ya miaka 39 ya CCM.
 Rais John Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM, UJakaya Kikwete
 JK akisalimiana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan. Katikati ni Rais Magufuli.
 Mtoto Yusufu anayeandaliwa na babake kuwania urais 2050 akiwa kwenye baiskeli aliyotengenezewa na babake pichani.
 Mwanamuziki wa Bendi ya Yamoto Band akiwaimbisha wananchi wakati wa sherehe hizo.
 Bendi ya Yamoto ikitumbuiza wakati wa maadhimisho ya miaka 39 ya ccm kwenye Uwanja wa Namfua, Singida.
 Kikundi cha TOT kikitumbiza kwa wimbo maalumu wa maadhimisho ya miaka 39 ya CCM
 Watoto wakipiga mafataki kunogesha maashimisho hayo
 Rais Magufuli akimpongeza aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mashishanga kujiunga na CCM akitokea Chadema.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Cresto Haja aliihama Chadema na kujiunga na CCM
 Rais John Magufuli akimpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM, wakati wa maadhimisho yhayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa CCM Namfua, mjini Singida leo. Kutoka kushoto ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete na Samia Suluhu Hassan Makamu wa Rais.
Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa katika maadhimisho hayo.

MIAKA MINANE TANGU UTANGULIE MBELE ZA HAKI MZEE WETU MARWA BINAGI, BADO TUNAKUKUMBUKA.

February 06, 2016
"Yapo mengi ya kusema ila kwa leo nasema, pengo uliloliacha Mzee wetu Daniel Marwa Binagi tangu tarehe 06.02.2008 bado linaonekana na halitasahaulika kamwe. Mwenyezi Mungu Ailaze Roho yako Pahala Pema Peponi, Amina! Ni mimi mwanao Mpendwa
George Marwa Binagi (Pichani)".
Ilikuwa ni Sekunde, Dakika, Masaa, Siku, Wiki, Mwaka hatimae hivi sasa ni miaka Minane imepita tangu ututoke duniani Baba yetu Mpendwa, huku ukiacha kilio na majonzi kwa wanao tuliokuwa bado wachanga ambao hakika ulituacha ilihali tukihitaji malezi yako.

Ukiwa na Miaka 83 mwaka 2008, Mzee wetu Mzee Daniel Marwa Binagi Mzaliwa na Mkazi wa Kitongoji cha Chira Kata ya Turwa (Zamani), hivi sasa Kata ya Kenyamanyori Wilaya ya Tarime Mkoani Mara Mwenyezi Mungu alikupenda zaidi na kukuchukua ili ukapumzike baada ya kuteseka kwa maradhi katika kipindi cha muda mrefu.

Hakika uliipenda na kuiongoza Familia yako bila ubaguzi wa aina yoyote. Ulionyesha Mapenzi tele si tu kwa Wanao, Wajukuu zako, Wake zako bali kwa kila mmoja aliekuzunguka ambapo uliweza kuonyesha mapenzi tele kwake huku tabia yako ya kuchukia upuuzi na kuukumbatia ukweli ukikuongezea sifa rukuki kwa waliokufahamu.

Ukiwa na Elimu ya darasa la nne ambayo uliipata enzi za Mkoloni, uliweza kuleta mapinduzi ya ajabu katika Kijiji chako na hata Wilaya ya Tarime na kuwa mmoja wa Watu wenye Mafanikio makubwa Wilayani Tarime si tu kwa Kuwekeza katika Ujenzi wa nyumba na Biashara katika mji wa Tarime bali hata katika Uungwana wako.

Ulijizolea sifa ya kuhakikisha kila mtoto anapata elimu kadri apendavyo na hivyo ndivyo ilivyokuwa na ndiyo maana wakapatikana vijana mbalimbali kutoka katika uzao wako wakiwa nafasi mbalimbali za utumishi ikiwa ni pamoja na wale walioingia katika Sekta ya Elimu, Afya, Habari, Biashara, Urubani ikiwa ni miongoni mwa taaluma mbalimbimbali huku wewe mwenyewe ukiamini katika mfumo wa Biashara, Kilimo na Ufugaji.

Hakika wote waliopata malezi yako wanajivunia mpaka leo kuwa na Mzazi kama wewe Mzee wetu Daniel Marwa Binagi. Nakumbuka mambo mengi sana kutoka kwako ambayo ulikuwa ukiwatendea wakati huo mimi nikiwa mdogo. 

Nilitamani sana kupata malezi yako lakini Mwenyezi Mungu alikupenda zaidi. Nakumbuka namna ndugu zangu walivyosoma katika Shule na Vyuo vizuri tena kwa gharama kubwa. Naogopa kusema sana ili nisije nikakufuru ila nina kila sababu ya kusema kwamba pengine nami ningekuwa mmoja wa wanao ambao wangesoma katika shule na vyuo vizuri kama ulivyokuwa ukiniahidi wakati ukiwa kitandani unauguza maradhi yaliyokuwa yakikusibu.


Hakika Mzee wetu wetu Daniel Marwa Binagi tututaendelea kukukumbuka kwa kuyaendeleza yale yote mazuri uliyotuachia licha ya changamoto nyingi zinazojitokeza kutokana na pengo lako. Yapo mengi ya kusema ila kwa leo nasema kwamba pengo uliloliacha tangu tarehe 06.02.2008 bado linaonekana na halitasahaulika kamwe. Hakika safari uliyoianza hapa duniani tangu tarehe 25.02.1925 ilifikia tamati mwaka huo wa 2008. Mwenyezi Mungu Ailaze Roho yako Pahala Pema Peponi, Amina! 
Ni mimi mwanao Mpendwa 
George Marwa Binagi.