January 01, 2014

UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA BENK ZA KIISLAM ZANZIBAR

DSC_0913 (1) 
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa Makao Makuu ya Benk ya Kiislamu ya PBZ na Tawi Jipya huko katika mtaa wa Mpirani Mjini Unguja ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.DSC_0915 (1)  
Mwananchi akipatiwa huduma katika Benki ya Kiislamu baada ya kuzinduliwa huko katika mtaa wa Mpirani Mjini Unguja ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.DSC_0928 (1)  
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi akitia saini baada ya Kujiunga katika Benki ya Kiislamu huko katika mtaa wa Mpirani Mjini Unguja ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.DSC_0974 (1)  
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Benki ya Kiislamu huko katika mtaa wa Mpirani Mjini Unguja ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.kulia yake ni Waziri wa Fedha wa Zanzibar Omar Yussuf Mzee na kushoto yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benk ya kiislam Juma Amour.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
January 01, 2014

BOBAN NI MCHEZAJI HALALI WA COASTAL UNION.

 Kikosi cha maangamizi cha CUSC....

 Hiki ni kipande cha gazeti la leo Jumatano Januari 1,2014 gazeti Mtanzania kuhusu habari za Boban.



Haruna Moshi, akimiliki mpira katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha wakati akiitumikia CUSC kwenye mechi yake ya kwanza ligi kuu na Wagosi wa Kaya. Ilikuwa ni mechi dhidi ya Oljoro JKT, ambapo CUSC iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
January 01, 2014

FM ACADEMIA WALIVYOUPOKEA MWAKA MPYA WA 2014 NA KUUAGA 2013

 Wanamuziki wa bendi ya Fm Academia, wakishambulia jukwaa kwa shoo kali ya pamoja wakati wa onesho lao maalum la kufunga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Business Park jana usiku.
 Mashabiki na wapenzi wa bendi hiyo, wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea jukwaani.

WAHAMIAJI HARAMU 590 WAKAMATWA MKOANI TANGA.

January 01, 2014


Na Oscar Assenga, Tanga.
JUMLA ya wahamiaji haramu 590 walikamatwa mkoani Tanga katika kipindi cha  kuanzia Januari 2012 hadi octoba 2013 kutokana sababu mbalimbali ikiwemo kuingia nchini bila kibali na kufanya kazi.

Takwimu hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya mkoa wa Tanga mwaka 2012 hadi Octoba 2013 kwa vyombo vya habari mwishoni mwa wiki.

January 01, 2014
WAZIRI WA FEDHA DK.WILLIAM MGIMWA AFARIKI DUNIA
Waziri wa Fedha, Dk. William Augustao Mgimwa (63) amefariki dunia.
Taarifa za hivi punde zinasema Waziri huyo wa fedha katika serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete amefariki dunia hii leo baada ya kuugua na kulazwa nchini Afrika Kusini.

Mgimwa aliyezaliowa January 20, 1950 na kuwa mbunge wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Binafsi ya Milpark ya nchini humo.

Dk. Mgimwa alikuwa mkufunzi katika Chuo cha Benki mkoani Mwanza, kabla ya kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Mkoa wa Iringa, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Hospitali hiyo ya Milpark ndiyo imekuwa ikitumiwa na Serikali ya Tanzania kupeleka watu wanaoumwa na mtu wa karibuni zaidi kuhudumiwa katika hospitali hiyo ni marehemu Dk. Sengondo Mvungi.

Tutawapa taarifa kamili ya Msiba huo mkubwa wakati wowote kuanzia sasa.