ORXY GAS YASHIRIKIANA NA DORIS MOLLEL FOUNDATION KUKABIDHI MITUNGI 1000 KWA WAUGUZI

April 19, 2024

 NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

KAMPUNI ya Orxy Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation wamekabidhi mitungi ya gesi ya kupikia ya Orxy 50 kwa wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam kati ya mitungi  1000  inayotarajiwa kukabidhiwa kwa wauguzi na madaktari katika mikoa 10 nchini .

Akizungumza wakati wakisaini makubaliano ya ushirikiano yaliyofanyika katika hospitali ya rufaa ya Mwananyama, Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite amesema makubaliano walioingia baina ys kampuni hiyo na taasisi ya Doris Mollel ni kusaidia kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa watanzania.

Aidha amesema katika kampeni hiyo ya kuwezesha watanzania kuingia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia, mpaka sasa tayari wameshatoa mitungi kwa wananchi zaidi ya elfu 32 ili kusaidia lengo la kufikia asilimia 80 ya watumiaji wa nishati safi.

Amesema matumizi ya nishati safi ya kupikia inasaidia kuondoa hatari za kiafya kwa watumiaji wa kuni na mkaa kama nishati ya kupikia lakini pia hatari za kimazingira na ustawi wa jamii.

"Takribani watu 33,000 wanapoteza maisha nchini Tanzania kwa maradhi yanayotokana na kuvuta moshi unaotokana na mkaa au kuni hiyo ndio sababu ya Oryx gas kuja na suluhisho la kuwahamasisha wananchi kutumia gesi kwa matumizi ya kupikia", amesema Benoite

Ameeleza kuwa matumizi ya gesi yanaepusha wamama na watoto kuumika kubeba kuni hivyo kuepuka kujeuriwa na wanyama wakali wakiwa katika harakati za kutafuta kuni pia kuimarisha maisha ya wanawake na kuwalinda dhidi ya vitendo vya udhalilishaji.

“Kuanzia mwezi wa saba mwaka 2021 tumekuwa mstari wa mbele kuunga mkono utekelezaji wa mkakati wa serikali uliopewa nguvu na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania , Dk. Samia Suluhu Hassan kwa lengo kwamba ifikapo mwaka 2033 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia”, ameeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel amesema katika makubaliano waliosaini na oryxy watawafikia waguzi elfu moja ambapo watawapa mitungi na majiko ya gesi kama mabalozi kwa kina mama waweze kutumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni programu ya miaka miwili.

Amesema mitungi hiyo itakwenda kwa wauguzi walioko maeneo magumu ambapo watakuwa wanawatembelea kwenye vituo vya afya na zahanati ili kuweza kuwafikia wafanyakazi ambao ni wauguzi wanaofanya kazi kubwa ya kuokoa maisha hususani ya mama na mtoto.

Wakati huo huo Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala  Dk.Zavery Benela ameeleza kwamba hospitali hiyo  inakabiliwa na ongezeko la wagonjwa wa mifumo ya hewa.

Amefafanua kati ya wagonjwa wa nje 500 wanaofika kuonwa na madaktari bingwa asilimia 30 ya wagonjwa hao ni wa matatizo ya mfumo wa hali ya hewa unaosababishwa na hali ya hewa pamoja na mazingira ya kuandaa chakula kutokna na kuni na mkaa.

Aidha Dokta Benela amesema magonjwa ya mfumo wa hali wa hewa  yamekuwa changamoto hasa kwa watu wazima na watoto.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel akisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano na Kampuni ya Orxy Gas kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini na Taasisi ya Doris Mollel kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya makubalinao na Kampuni ya Orxy Gas kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel (katikati) akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya makubalinao na Kampuni ya Orxy Gas kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala mkoani Dar es Salaam  Dk.Zavery Benela
akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini na Taasisi ya Doris Mollel kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite na Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel wakionesha mkataba waliosaini  kwaajili ya kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite na Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel wakimkabidhi mtungi wa kupikia wa gesi ya Orxy mmoja wa wauguzi katika hospitali ya rufaa ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini makubalino kati ya kampuni ya Orxy Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite  akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mtungi wa kupikia wa gesi ya Orxy kwa wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala katika hafla ya utiaji saini kati ya kampuni ya Orxy Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.


Baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala wakifuatilia hafla ya utiaji saini kati ya kampuni ya Orxy Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Orxy Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

WAONGOZA NDEGE KUTOKA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA YA UGANDA (UCAA) WAHITIMU KATIKA CHO CHA CATC

April 19, 2024

 Wahitimu wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC), kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Uganda (UCAA) wamekumbushwa kwamba kusoma hakuishii darasani pekee, mengine wataendelea kujifunza maofisini mwao wakati wanafanya kazi husika kwa vitendo.


Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Idara ya Uongozaji ndege Bi Flora Alphonce aliyekuwa mgeni rasmi Aprili 19, 2024 wakati wa mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance). Na kuongeza kuwa anaishukuru UCAA kwa kuendelea kukiamini chuo cha CATC na kuendelea kuleta watalaam wake kwa mafunzo.

Bi Flora aliwafahamisha wahitimu hao kwamba chuo cha CATC ndani ya kipindi cha miaka mitatu ijayo kitakuwa na majengo na vifaa vya kisasa ambavyovitaongeza tija na kuleta utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazojitokeza hapa na pale kufuatia Serikali ya Tanzania kutenga Shilingi bilioni 78 kwa ajili ya mradi huo.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha CATC Bw.Aristid Kanje alisema amefurahishwa na kuwapongeza wahitimu hao wote kwa kumaliza kozi zao kwa ufaulu wa juu. Na kuongeza kuwa ni vugumu kumlazimisha mtu kupata maarifa, kwani maarifa yanapatikana kwa kuwa na hamu ya kuyapokea.

Wahitimu hao watano kutoka UCAA walifanya kozi mbili kwa muda wa wiki 12, awali kabla ya mahali wahitimu hao walipatiwa semina juu ya umuhimu wa masuala ya kiafya na namna yanavyoweza kuathiri waongoza ndege katika majukumu yao kutoka kwa Daktari Concethar Mushi.

Akitoa salamu za shukran kiongozi wa darasa hilo kwa niaba ya wenzake Bw. Erasmus Muhairwe aliishukuru CATC kwa ushirikiano iliyowapatia kwa muda wote wa kozi zao na kuwakumbusha wahitimu wenzake kwamba kwa kuhitimu kwao watu wana matarajio makubwa kwao hasa ya kutokufanya makosa.
Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce akizungumza na wahitimu wa  mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akizungumza jambo pamoja kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufunga mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce akiwakabidhi vyeti pamoja na zawadi kwa  wahitimu wa mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole akizungumza na wahitimu wa  
mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC). 
Dkt. Concethar Mushi akitoa mafunzo kuhusu umuhimu wa masuala ya kiafya na namna yanavyoweza kuathiri waongoza ndege katika majukumu yao wakati wa mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Kiongozi wa darasa hilo kwa niaba ya wenzake Bw. Erasmus Muhairwe akishukuru CATC kwa ushirikiano iliyowapatia kwa muda wote wa kozi zao na kuwakumbusha wahitimu wenzake wakati wa 
mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Wahitimu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Uganda (UCAA) wakiwa kwenye mahafali hayo


Picha ya Pamoja
DKT. NCHEMBA: TANZANIA IMEPIGA HATUA KIUCHUMI NA KIDEMOKRASIA

DKT. NCHEMBA: TANZANIA IMEPIGA HATUA KIUCHUMI NA KIDEMOKRASIA

April 19, 2024








SHARE


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Alice Albright, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo Makao Makuu ya Shirika hilo, jijini Washington D.C, kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea nchini Marekani, ambapo walijadiliana namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga kufanya mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi.


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa nne kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Alice Albright (wa sita kulia), Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Chidi Blyeden (wa tano kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa tatu kulia), Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Dkt. Juma Malik Akil (wa nne kushoto), Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Mafuru (wa kwanza kulia), Mratibu wa Tanzania wa Mradi wa MCC Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa pili kulia), Kiongozi wa Timu ya MCC nchini Tanzania Bw. Nilan Fernando (kushoto), Kamishna wa Idara Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade na Makamu wa Rais wa MCC anayeshughulikia Sera na ukaguzi, Bi. Alicia Mandaville, mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wao uliofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Washington D.C, ambapo walijadiliana ushirikiano wa shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga katika mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi, kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea nchini Marekani.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kulia), akiagana na Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Chidi Blyeden, baada ya kumalizika kwa Mkutano wao uliofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, jijini Washington DC, kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea jijini nchini Marekani, ambapo walijadiliana namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga kufanya mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kulia), ukiwa katika mkutano na Uongozi wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), ambapo walijadiliana masuala ya ushirikiano Shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga katika mageuzi ya kisera na kitaasisi aili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi, kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea jijini Washington D.C, nchini Marekani.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani) na Uongozi Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana kihusu ushirikiano wa Shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga kuleta mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi. Mkutano huo umefanyika kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea jijini Washington D.C, nchini Marekani.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Mafuru, akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani) na Uongozi Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana kihusu ushirikiano wa Shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga kuleta mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi. Mkutano huo umefanyika kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea jijini Washington D.C, nchini Marekani.


Uongozi wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), ukifuatilia kwa umakini majadiliano kati yake na Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), katika Mkutano wao uliofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Washington D.C, ambapo walijadiliana masuala ya ushirikiano na Shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga kuleta mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi, kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea jijini Washington D.C, nchini Marekani.


Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Chidi Blyeden (kushoto), akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Uongozi wa Shirika hilo na Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga kufanya mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi. Mkutano huo umefanyika kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea jijini Washington D.C, nchini Marekani.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Washington D.C.)
……..
Na Benny Mwaipaja, Washington D.C

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amelihakikishia Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation-MCC) kwamba Tanzania imepiga hatua kubwa katika masuala ya haki za binadamu, utawala bora, demokrasia na usimamizi imara wa uchumi wa nchi.

Dkt. Nchemba amesema hayo alipoongoza ujumbe wa Ta
nzani, kukutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa juu wa Shirika hilo, ukiongozwa na Makamu wake wa Rais Mhe. Alicia Mandaville, Jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo pande hizo mbili zilijadili namna ya kuharakisha utekelezaji wa mpango wa kusaidia mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kutatua vikwazo vya ukuaji uchumi, kupitia ruzuku itakayotolewa na Shirika hilo.

Alisema kuwa hatua hiyo si tu kwamba ni utekelezaji wa vigezo vilivyowekwa na Shirika hilo ili Tanzania iweze kunufaika na mpango huo unaolenga kutoa misaada ya kiufundi, bali ni nia ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kulinda uhuru wa watu.

Dkt. Nchemba aliihakikishia MCC kwamba Tanzania iko tayari kushirikiana na Serikali ya Marekani katika mpango huo na kuuomba uongozi huo kuuamini mchakato huo na ikiwezekana kuipatia nchi mradi mkubwa wa COMPACT II, utakao iwezesha nchi kupata fedha za kutekeleza miradi ya kimkakati katika sekta za usafirishaji, nishati, na maji..

Akizungumza kwa niaba ya Uongozi, Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Chidi Blyeden, aliahidi kuwa Shirika hilo liko tayari kuanzisha ushirikiano huo wa kimaendeleo kwa kuwa Serikali imepiga hatua kubwa kutimiza vigezo vilivyowekwa ili nchi iweze kunufaika na mpango huo.

Bi. Blyeden alieleza kuwa utekelezaji wa mpango huo ambao matokeo yake hapo baadae utaiwezesha Marekani kurejesha mradi wa Changamoto za Milenia (MCC-Compact) utakao kuwa na lengo la kusaidia nchi kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ya maendeleo.

Mwezi Desemba mwaka 2023, Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), ilizichagua Tanzania na Philippines, kama wabia wake katika kuandaa programu za awali (threshold programs) zitakazolenga kufanya mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Bodi hiyo ya MCC ilichukua uamuzi huo baada ya Tanzania na Philippines, kuonesha dhamira mpya ya kusukuma mbele mageuzi muhimu ya kuimarisha utawala wa kidemokrasia, kulinda haki za binadamu na kupambana na rushwa.

Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), ni shirika huru la Serikali ya Marekani linalojielekeza kupunguza umaskini duniani kupitia ukuaji wa kiuchumi, kwa kutoa ruzuku na misaada ya muda maalum kwa nchi zinazokidhi viwango na vigezo thabiti vya utawala bora, mapambano dhidi ya rushwa na kuheshimu haki za kidemokrasia.

Kupitia Mradi wa Changamoto za Milenia (COMPACT I) uliotekelezwa nchini Tanzania kwa muda wa miaka mitano kuanzia mwaka 2008 hadi 2013, uliiwezesha Tanzania kupata dola za Marekani milioni 698, zilizotumika kutekeleza miradi katika sekta za usafirishaji, nishati na maji.

Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara kutoka Tunduma – Sumbawanga, Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mafia, Ujezi wa barabara za Pemba, Tanga hadi Horohoro, Ukanda wa Mtwara, ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya usambazaji umeme ukiwemo Mradi wa Umeme Jua mkoani Kigoma pamoja kuyajengea uwezo mashirika ya umeme (TANESCO na ZECO).

Mradi mingine ni upanuzi wa mtambo wa kusukuma maji wa Ruvu Chini ulioongeza kiwango cha uzalishaji maji kutoka lita milioni 180 hadi lita milioni 270 kwa siku na mradi wa usambazaji maji wa mjini Morogoro ambao uliongeza kiwango cha uzalishaji maji kutoka lita milioni 18 hadi milioni 33 kwa siku.

SERIKALI KULIPA FIDIA ENEO LA IDEFU - MAKAMBAKO

April 19, 2024

 


Na. Saidina Msangi, WF, Dodoma.

Serikali imesema kuwa imeanza taratibu za tathmini ya eneo la makaburi ya Idefu - Makambako na taratibu za malipo zitaanza baada ya kuidhinishwa na Mthamini Mkuu wa Serikali.

Hayo yameelezwa bungeni, jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Makambako Mhe. Deo Kasenyenda Sanga, aliyetaka kujua ni lini Serikali italipa fidia eneo la Makaburi Idefu - Makambako ili kupisha ujenzi wa One Stop Centre.

 

Mhe. Chande alisema kuwa Serikali tayari imeshalipa fidia ya shilingi bilioni 4.6 kwa wananchi waliopisha eneo kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa One Stop Centre.

 

Aidha, baada ya kupata majibu hayo Mhe. Sanga alitaka kujua kama Serikali itaona umuhimu wa kulipa fidia hiyo haraka kwa kuwa kiasi kilichobakia si kikubwa, huku akitaka kujua wakati ambao Serikali italipa madai ya fidia kwa wananchi Kilolo waliopisha ujenzi wa makao makuu ya wilaya ambayo yameshawasilishwa muda mrefu.  

Mhe. Chande alisema kuwa tayari Serikali imeshalipa fidia kiasi cha Sh. bilioni 4.6 na kiasi kilicho baki ni Sh. milioni 100 na kumhakikishia Mhe. Mbunge huyo kuwa ndani ya mwaka huu wa fedha Serikali italipa fidia iliyobakia.

‘‘Kwa upande wa Kilolo Serikali iko tayari kulipa fidia hizo haraka inasubiri Mthamini Mkuu wa Serikali atoe idhini ili malipo yaweze kufanyika’’, alifafanua Mhe. Chande.