Tigo yafana Tamasha la Simu EXPO

June 15, 2016



 Baadhi ya Wateja wa Kampuni ya Simu Ya Tigo wakiwa katika foleni kwa ajili ya kuhakiki simu zao zoezi lililofanyika kwa ushirikiano baina ya makampuni ya simu na TCRA mapema mwisho wa wiki iliyopita katika viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam.



 Wateja wakipata maelezo kuhusu matumizi ya simu orijno zilizokuwa zinauzwa katika Banda la Tigo mapema mwisho wa wiki iliyopita katika viwanja vya Posta Kijitonyama,jijini Dar es salaam.


  Baadhi ya watoa huduma wa Tigo wakitoa huduma kwa wateja wao wakati wa kampeni ya kuhakiki simu kama ni Bandia au Orijino mapema mwisho wa wiki iliyopita katika viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam.


 Meneja Mauzo wa 4G kutoka Tigo Anthony Assenga akisikiliza maoni ya wateja waliotembelea banda la tigo wakati wa kampeni ya kuhakiki simu kama ni Bandia au Orijino mapema mwisho wa wiki iliyopita katika viwanja vya Posta  jijini Dar es Slaam.



Meneja Mauzo wa 4G kutoka Tigo Anthony Assenga akiongea na waandishi wa habari  (hawapo pichani) wakati wa kampeni ya kuhakiki simu kama ni Bandia au Orijino mapema mwisho wa wiki iliyopita katika viwanja vya Posta  jijini Dar es Slaam.


photo Krantz Mwantepele Founder & CEO , KONCEPT Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Website;www.koncept.co.tz
SERENGETI BOYS WAKIWA MAZOEZINI KARUME

SERENGETI BOYS WAKIWA MAZOEZINI KARUME

June 15, 2016

SER1 
Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Taifa ya vijana Tanzania – wenye umri wa chini ya miaka 17 (Serengeti Boys), Bakari Shime akisimamia mazoezi ya viungo  kwa wachezaji wa kikosi hicho kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijiji Dar es Salaam leo Juni 15, 2016. Serengeti Boys ipo kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Picha na Alfred Lucas wa TFF.
SER2 
Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Taifa ya vijana – Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 (Serengeti Boys), Sebastian Nkoma na Mshauri wa Ufundi wa TFF kwa maendeleo ya timu za Vijana, Kim Poulsen wakisimamia mazoezi ya viungo kwa wachezaji wa kikosi hicho kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijiji Dar es Salaam leo Juni 15, 2016. Serengeti Boys ipo kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Picha na Alfred Lucas wa TFF.
RAIS MAGUFULI AANDAA FUTARI YA PAMOJA YA VIONGOZI MBALIMBALI WA DINI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS MAGUFULI AANDAA FUTARI YA PAMOJA YA VIONGOZI MBALIMBALI WA DINI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

June 15, 2016

FUT1 
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika foleni na wageni wake kwenda kuchukua chakula wakati wa kufuturu katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016
FUT2Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndg. Ramadhani Madabida akifuatiwa na Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC)  Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ na wagemi wengine wakipakua chakula  katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli  Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016
FUT3 
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea machache baada ya futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016
FUT4 
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea machache baada ya futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016
FUT7 
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipongezwa na kaimu Mufti Sheikh Hamid Masoud Jongo baada ya kuongea machache  katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016
FUT8 
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Kadhi Mkuu wa Tanzania Sheikh Abdallah Mnyasi  katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016
FUT9 
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni mbalimbali  katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016
FUT10 
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Shamim Khan katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016. Kushoto ni Mke wa rais Mama Janeth Magufuli akifuatiwa na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa.
FUT11 
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Fr. Stephano Kaombwe katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016

MAANDALIZI YA TAMASHA KUBWA LA SHABANI ROBERT LITAKALOFANYIKA SEPTEMBA YAENDELEA

June 15, 2016
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Shabani Robert ,Mohamed Hariri akizuingumza jambo na wajumbe wakati wa kikao cha pili kilichofanyika leo ukumbi wa Tangamano mjini Tanga kushoto ni Katibu wa Kamati ya Maandalizi Madame Mkombo na kulia ni Bakari Nauma ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Timo
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Shabani Robert,Mohamed Hariri akizuingumza jambo na wajumbe wakati wa kikao cha pili kilichofanyika leo ukumbi wa Tangamano mjini Tanga wa kwanza kulia ni Mratibu wa Matukio wa Taasisi ya Timo,Bakari Kiwingu.
Afisa Sanaa wa Jiji la Tanga,Rose John Bendera akisisitiza jambo kwenye kikao cha pili cha maandalizi ya Tamasha la Shabani Robert litakalofanyika mwezi Septemba mwaka huu mjini Tanga.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)Mkoani Tanga,Ally Mwakababu akitoa elimu kwa washiriki wa kikao hicho namna ya kutumia huduma ya kikoa na toto kadi 
 Meza kuu wakifuatilia ndondo za tamasha hilo kwenye baadhi ya makabrasha leo wakati wa kikao hicho cha kwanza.

COCA-COLA KUENDELEA KUDHAMINI MASHINDANO YA UMISSETA NCHINI TANZANIA

June 15, 2016
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla akikagua wachezaji wakati wa Uzinduzi wa mashindano ya UMISETA ambayo mwaka huu yamedhaminiwa na kampuni ya Coca Cola. Uzinduzi huo ulifanyika May 10, 2016 katika uwanja wa Sokoine ambapo kulifanyika michezo na burudani mbali mbali. --- Mashindano kwa ajili ya fainali za kitaifa za Copa-UMISSETA ambayo yanadhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola, na ambayo yalipangwa kuanza kufanyika siku ya leo hadi hapo tarehe 24 Juni 2016 yametangazwa kuahirishwa. Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serikali iliyotolewa hapo jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), George Simbachawene, serikali imechukua uamuzi huo ili kupisha utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli la upatikanaji wa madawati, ambao kikomo chake ni mwisho wa mwezi huu. Mashindano haya ya fainali za Copa-UMISSETA yalilenga kuzikutanisha timu za mikoa mbalimbali nchini kwa pamoja Jijini Mwanza, zikiwa zimeundwa na wachezaji mbalimbali kutoka shule za sekondari ili wachuane kwenye michezo na sanaa.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke - Dar es Salaam, Sophia Mjema (kushoto), akisalimiana na wachezaji wa timu ya Makongo Sekondari katika Mashindano ya UMISETA ambapo kampuni ya Coca Cola ndiyo walikuwa ni wadhamini wakubwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2016. --- “Thamira yetu katika kudhamini mashindano haya na kushirikiana TAMISEMI iko pale pale, tukiwa tumejidhatiti kuendelea kuunga mkono jitihada za kutambua na kuinua vipaji vya vijana ambao watakuja kuifikisha Nyanja ya michezo nchini katika kiwango cha juu zaidi. Tutaendelea kuunga mkono na kusaidia kukua kwa sekta ya michezo nchini, hususani mashindano ya mpira wa miguu pamoja na mpira wa kikapu kwa vijana,” alisema David Karamagi, Mwakilishi Mkazi wa Coca-Cola Tanzania. Karamagi aliongeza kuwa kampuni ya Coca-Cola Tanzania inayo imani ya dhati na ikiamini ya kwamba mashindano ya michezo yanayoanzia ngazi ya chini kabisa ndiyo namna thabiti nay a kipekee katika kuibua vipaji vya wachezaji nchini. Pia Karamagi alisema kuwa, wakati wadau wakisubiri kwa hamu kutangazwa kwa tarehe mpya za kurejewa kwa fainali za mashindano haya nchini, Coca-Cola Tanzania ilishajipanga kudhihirisha ya kwamba michezo ni zaidi ya ushindani, kwa kuweza kuambatanisha mashindano haya na kujenga mshikamano wa timu shindani, urafiki na hata nidhamu kwa wachezaji na timu za mikoa inayoshiriki. Hivyo basi, kwa udhamini ulioingiwa mwaka huu, Coca-Cola Tanzania itaweza kupanua wigo wa ushirikishwaji wa michezo murua zaidi mbali ya mpira wa miguu, hasa kwa kuweza kujumuisha mpira wa kikapu. “Kampuni ya Coca-Cola nchini tutaendelea na dhamira yetu ya kuunga mkono jitihada ya vijana mbalimbali nchini kote katika kuwasaidia kudhihirisha vipaji vyao kupitia mashindano mbali mbali ya michezo, ikiwa ni pamoja na UMISSETA na Copa Coca-Cola’” alimalizia Karamagi.
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''