DC KINONDONI AANZA MAPAMBANO DHIDI YA WATUMISHI HEWA

April 29, 2016

 
NA BASHIR NKOROMO Mkuu wa Wilaya a Kinondoni, Dar es Salaam,  Salum Hapi amesema, Serikali katika wilaya hiyo imebaini kuwa  imepoteza zaidi ya sh. bilioni 1.331 kwa kuwalipa wafanyakazi hewa wapatao 89.hadi sasa.
Amesema, baada ya kuapishwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo siku saba zilizopita, amesimamia maofisa wake kufanya uchunguzi na kubaini kuwa pamoja na wafanyakazi hao hewa ambao wameisababishia serikali kupoteza sh. 1, 331, 734, 881 pia wapo watumishi vivuli wapatao 8823 ambao wanalipwa mishahara wakati  hawafanyi kazi katika maeneo husika kutokana na sababu mbalimbali.
Hapi amesema wafanyakazi hao vivuli ni pamoja na waliohamia idara nyingine lakini wakati wanalipwa huko walikokwenda bado wanalipwa katika idara walizokuwepo mwanzo na kwamba wengi wao wapo katika Idara ya Elimu.
Akzungumza na waandshi wa habari Ofisini kwake, leo, Hapi amesema, amebaini hatua hiyo baada ya kufanya uchunguzi wa kinaa na kuwabinya wasimamizi katika idara mbalimbali za utumishi, na kwamba ameelekeza mwanasheria kuchukua hatua haraka ili wahusika wachukulie hatua za kisheria.
Katika hatua nyingine, Hapi amewataka wafanyabiashara ndogondogo maarufu kwa jina la machinga, kuwa kuanzia kesho ni marufuku kufanya shughuli zao katika maeneo yasiyo mahsusi kwa biashara katika wilaya ya Kinondoni.
Amesema, agizo hilo ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kutaka ifanyike hivyo kwa lengo la kulifanya jiji liwe safi kuunga mkono agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuhimiza usafi nchi nzima.
Hapi amesema, machinga wote kama wahanitaji kufanya biashara zao ni lazima waende katika maeneo yaliyopangwa, ambayo alisema, hapo mengi na bado yana nafasi za kutosha kwa ajili ya kutumika kufanyia biashara.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela afunga mafunzo ya PUBLIC PRIVATE DIALOGUE (PPD) na kutunuku vyeti kwa washiriki

April 29, 2016












JAJI MKUU MOHAMED CHANDE OHMAN KUWA MGENI RASMI KATIKA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

JAJI MKUU MOHAMED CHANDE OHMAN KUWA MGENI RASMI KATIKA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

April 29, 2016
DSC_0940
Mwenyekiti wa MISATAN, Simon Berege akizungumza na waandisshi wa habari kuhusu SIku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari. Kushoto ni Afisa Mafunzo wa TMF, Raziah Mawanga na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile.(Picha na Modewjiblog)
Siku za Uhuru wa Vyombo vya Habari ambayo hufanyika Mei 3 ya kila mwaka inataraji kufanyika jijini Mwanza kwa mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman na kuhudhuliwa na viongozi wengine nchini na wengine kutoka nje ya nchini ambapo kwa mwaka huu kaulimbiu ni KUPATA TAARIFA NI HAKI YAKO YA MSINGI.
Akizungumzia sherehe hizo katika mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa MISATAN, Simon Berege amesema sherehe za mwaka huu zinataraji kuwa na wageni zaidi ya 250 akiwepo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues.
Aidha Berege amesema kuwa siku ya uhuru wa vyombo vya habari kwa mwaka huu itafanyika kwa siku mbili, Mei, 2 kutakuwa na kongamano ambalo litatumika kujadili hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini na Mei, 3 ndiyo itakuwa siku husika ya maadhimisho.
“Kikawaida huwa kuna mambo tunafanya katika siku hiyo, tutawakumbuka waandishi wa habari waliopoteza maisha kazini, tutawakumbuka waandishi wa habari maveterani na waandishi wa habari waliopatwa na matatizo wakiwa kazini ... kwa mwaka huu tutakuwa na mambo ya kipekee tofauti na miaka iliyopita,” amesema Berege.
Pia ameongeza kuwa watapitia sheria zinazohusu uhuru wa vyombo vya habari kama Cyber Crime Act 2015 na Sheria ya Takwimu 2015 pia kuipitia miswada ya huduma ya vyombo vya habari na uhuru wa kupata taarifa.
DSC_0989
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la JAMHURI na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile akizungumzia hali ya uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata taarifa ilivyo nchini. Kulia ni Afisa Mafunzo wa TMF, Raziah Mawanga, Mwenyekiti wa MISATAN, Simon Berege na Ofisa Miradi katika Kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizelege.
DSC_0953
Afisa Mafunzo wa TMF, Raziah Mawanga akizungumza jinsi TMF inawasaidia waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa weledi. Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile. Kulia ni Mwenyekiti wa MISATAN, Simon Berege na Ofisa Miradi katika Kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizelege.
DSC_0963
Ofisa Miradi katika Kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizelege akizungumzia ushiriki wa UNESCO katika kuandaa Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ambapo kwa mwaka huu zinafanyika Mwanza. Kushoto ni Mwenyekiti wa MISATAN, Simon Berege na Afisa Mafunzo wa TMF, Raziah Mawanga.
DSC_0974
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma-Ledama akieleza kazi za Umoja wa Mataifa ili kuvisaidia vyombo vya habari kupata uhuru wa kufanya kazi bila kuingiliwa.
DSC_0942
Baadhi ya waandishi wa habari na watumishi waliohudhuria mkutano huo.

Tigo yatoa visima 12 vya maji kwa vijiji 12 Singida

April 29, 2016
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akikata utepe katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akifungua moja ya bomba katika kisima   katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi.
 Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia) akifungua bomba katika moja ya kisima katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo pembeni yake ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi.


Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mtinko  katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi. 

Singida, Aprili 27th 2016:  Kampuni ya simu ya Tigo leo imekabidhi visima 12 vya maji  vyenye thamani ya 174m/- kwa vijiji 12 mkoani  Singida  ikiwa ni kuchangia juhudi za serikali  za kupunguza  uhaba wa maji safi na salama uliopo nchini.

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano  iliyofanyika kwenye kijiji cha Mtinko wilayani Singida  mkoani Singida, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata  alisema ufadhili huo  umo kwenye mikakati ya kampuni ya kusaidia  jamii katika kunyanyua hali zao za maisha.
 Vijiji vitakavyonufaika kutokana na ufadhili huo pamoja na wilaya zake kwenye mabano ni Lulumba (Iramba), Kisana (Iramba), Kisonzo (Iramba), Songambele (Iramba), Kinyeto (Singida Vijijini) na  Damankia (Ikungi). Vingine ni  Muungano (Ikungi), Ighuka (Ikungi), Kamenyanga (Manyoni), Sasajila (Manyoni), Mtinko (Singida Vijijini) and Kinampanda (Kinampanda).
 “Msaada huu ni sehemu ya uwekezaji wa Tigo kwenye miradi ya kijamii  ambayo inaleta tija kubwa kwa jamii. Tuna imani kwamba kupitia visima hivi, Tigo inasaidia  kutatua uhaba mkubwa wa maji  katika eneo hili la mkoa wa Singida  ambalo kwa kiwango kikubwa  limekumbwa na uhaba mkubwa wa mvua katika kipindi cha miaka mine  iliyopita,” alisema Lugata.
 Aidha aliongeza kuwa uhaba wa maji  miongoni mwa  wilaya nyingi za Singida  umesababisha wakiazi wake  kupoteza muda mwinmgi kutafuta  bidhaa hiyo muhimu, jambo ambalo  Tigo inaamini  kuwa hivi sasa litafikia ukomo kutokana na upatikanaji wa visima hivyo.
 Makabidhiano ya visima hivyo yalihudhuriwa na kushuhudiwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge  ambaye aliishukuru Tigo kwa ufadhili huo uliopatikana kwa wakati mwafaka akisema kwamba visima hivyo vitapunguza kwa kiwango kikubwa  uhaba sugu wa maji  uliolikumba eneo hilo  na kuchangia kukua ustawi wa jamii  kijamii na kiuchumi.
 Hata hivyo, alitoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo  kuchangia kwenye juhudi kama hizo. Waziri Lwenge alisema, “Tunatoa shukrani za dhati kwa Tigo kwa kutuunga mkono kwenye juhudi zetu za kutatua  uhaba wa maji uliopo Singida na hata kwenye mikoa mingine nchini. Tuna imani visima hivi 12  vitasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo hili linaloikabili jamii kwa sasa”.


MWANAHABARI MTOTO NA MWANAMAZINGIRA WA UN, GETRUDE CLEMENT AWASILI JIJINI MWANZA.

April 29, 2016

Shujaa Wetu, Mwanahabari Mtoto, Mwanamazingira Balozi wa Umoja wa Mataifa UN kutoka Mwanza Tz, Getrude Clement (16) jana amewasili nyumbani Jijini Mwanza majira ya saa tatu usiku na kupokelewa kwa shangwe na ndugu, jamaa na marafiki katika Uwanja wa Ndege Mwanza.

Alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa nchini Marekani uliohusu Mabadiliko ya Tabia nchi (Climate Change) ambapo alihutubia õakiwakilisha kundi la Watoto na Vijana duniani.

Kutoka Kushoto Pichani ni Brightius Titus ambae ni Katibu wa Mtandao wa Watoto na Vijana Mkoani Mwanza MYCN, Katikati ni Getrude mmoja wa Watoto wa Mtandao huo na Kulia ni Shaban Magana ambae ni Mwenyekiti wa MYCN.

WANANCHI WA ITOBO, ITIRIMA - SIMIYU WAASWA KUZAA KWA KUFUATA UZAZI WA MPANGO

April 29, 2016
Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu mapema wiki iliyopita. Elimu hiyo ya uzazi wa mpango iliendana na huduma ya upimaji wa afya ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya uzazi wa mpango. Picha/Video na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. Wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wakipatiwa elimu ya uzazi wa mpango.
Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima.