JESHI LA MAGEREZA KUINGIA USHIRIKIANO RASMI NA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA

JESHI LA MAGEREZA KUINGIA USHIRIKIANO RASMI NA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA

June 02, 2014


PIX 1 (2)Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara alipowasilishwa katika ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwete (kulia).
PIX 2 (3)Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (wa pili kulia) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwete (wa tatu)  wakisani hati za makubariano ya ushirikiano kati ya Taasisi hizo mbili.  Wakwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Malewa na wa nne kulia ni Naibu wa Tatu wa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Modest Valisango anayeshughulikia Teknolojia na Huduma za Kujifunzia Chuoni hapo.
PIX 3 (3)Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Malewa(wa kwanza kulia) na Prof. Modest Valisango (wa kwanza kushoto) wakisaini hati za makubaliano ya ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
PIX 6 (2) Baadhi wa washiriki wa hafla ya utiwaji sahini makubaliano kati ya Jeshi la Magereza na Chuo Kikuu cha Huria cha Tanzania wakifuatilia kwa karibu simulizi za  aliyewahi kuwa mfungwa Bw. Haruna Pembe (hayupo pichani) alivyosoma na kumaliza shahada yake ya sharia na hivi sasa anasoma shahada ya uzamili chuoni hapo.
Na Insp Deodatus Kazinja, PHQ
Jeshi la Magereza nchini limeingia katika Makubaliano rasmi na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) katika kuboresha na kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili.
Makubaliano hayo yamefanyika leo Jumatatu 02 Juni, 2014 katika  Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Chuo hicho kilichoko eneo la Biafra Kinondoni Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na wajumbe mbalimbali kutoka Chuoni hapo, Jeshi la Magereza pamoja na wanahabari Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Tolly Mbwete amesema kuwa ushirikiano kati ya Magereza na OUT umekuwepo kwa muda mrefu ila hivi sasa ni kuuimarisha zaidi kwa kufanya mapitio kwenye maeneo ya ushirikiano kwa lengo kujumuisha maeneo mengi zaidi.
Ametaja maeneo yanayokusuduiwa katika makubaliano hayo kuwa ni Mafunzo na shughuli za utafiti, uandaaji wa mitaala na vifaa vya mafunzo hususani ni katika suala la urekiebishaji wa wahalifu, utoaji wa elimu kwa umma kuhusu shughuli zinazofanywa na taasisi hizi mbili, ubadilishanaji wa nyaraka, vitabu vya rejea na vifaa muhimu vya maktaba, maendelea ya kitaaluma kwa watumishi wa Jeshi la Magereza na wafungwa nakadhalika.
Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja amesema kwa muda wote Jeshi la Magereza limekuwa tayari kushirikiana na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa kutoa vibali mbalimbali kwa wanafunzi na wakufunzi wanaotaka kufanya tafiti katika maeneo ya Magereza, kutoa vibali kwa watumishi wa Jeshi la Magereza kusoma katika chuo hicho na kutoa ushirikiano wa dhati kwa wafungwa wanaotaka kusoma kwa kutumia chuo hicho wakiwa gerezani.
Makubaliano haya ya leo yatakuwa ya msaada sana kwa Jeshi la Magereza katika kulifanya liwe la kisasa na kulipunguzia matumizi” Alisema Kamishna Minja.
Katika hafla ushuhuda wa wafungwa kusoma na kufanikiwa wakiwa gerezani ulitolewa na ex-mfungwa Haruna Pembe aliyepata shahada ya sheria (LLB) akiwa gerezani na sasa yuko nje baada ya kushinda rufaa yake akiwa sasa anafanya shahada ya pili ya sheria katika Chuo Kikuu hicho. (Picha zote na Insp. Deodatus Kazinja, PHQ)

BAKARI MTAMA AHAIDI MAKUBWA COASTAL UNION

June 02, 2014
BEKI wa kati mpya wa Klabu ya Coastal Union, Bakari Mtama amehaidi kutoa mchango mkubwa kwa  timu hiyo kwenye msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara lengo likiwa kuipa mafanikio.

Mtama alitoa kauli hiyo hivi karibuni mara baada ya kusaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo yenye makazi yake barabara kumi na moja jijini Tanga  akitokea klabu ya Mgambo Shooting.
Alisema michuano ya ligi kuu Tanzania bara siku zote inakuwa na ushindani lakini atakaikisha anashirikiana vizuri na wachezaji wenzake ambao watakuwa wamesajiliwa ili kuweza kuipa maendeleo timu hiyo kongwe hapa nchini.
    “Nimefurahi sana kusajiliwa Coastal Union..naahaidi sitawaangusha nitatoa mchango wangu mkubwa kuhakikisha tunafikia malengo yaliyowekwa kwenye timu yetu hasa tukizingatia ushirikiano “Alisema Mtama.
Beki huyo ni miongoni mwa wachezaji waliongara sana msimu uliopita na hivyo kuhaidi kuendeleza jitihada zake kuifikisha kucheza kwa umakini mkubwa ili kuweza kuipa fursa timu hiyo ya kushiriki mashindano makubwa ikiwemo kombe la Shirikisho.
Wachezaji wengine waliosajiliwa ni pamoja na Nigeria Ike Bright Obina ambaye alisaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo.

Mchezaji huyo msimu uliopita alikuwa akiichezea Ashanti United kwa mkopo kwa kipindi cha miezi sita akitokea Klabu ya Azam FC

Mchezaji mwengine mpya aliyesaini mkataba huo ni mshambuliaji wa Ashanti United Hussein Sued wakati mchezaji wa zamani aliyesaini mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo ni Razack Khalfani baada ya ule wa awali kumalizika.

STARS KUWASILI LEO, PONGEZI ZAMIMINIKA

June 02, 2014
NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Kikosi cha Taifa Stars ambacho jana (Juni 1 mwaka huu) kiliitupa Zimbabwe (Mighty Warriors) nje ya michuano ya Afrika baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 kinarejea nchini leo (Juni 2 mwaka huu) kutoka Harare.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam saa 12.30 jioni kwa ndege ya Kenya Airways ikitokea Harare kupitia Nairobi.

Stars imefuzu kucheza raundi inayofuata kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2, kwani awali (Mei 18 mwaka huu) iliifunga Zimbabwe bao 1-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika raundi ya pili, Taifa Stars itacheza na Msumbiji ambapo itaanzia nyumbani kati ya Julai 19 na 20 mwaka huu, wakati mechi ya marudiano itafanyika Msumbiji kati ya Agosti 2 na 3 mwaka huu.

Wakati huo huo, Taifa Stars imeendelea kupokea salamu za pongezi kutoka kwa wadau mbalimbali baada ya kufanikiwa kuvuka kikwazo hicho cha kwanza katika harakati zake za kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.

Salamu hizo zimetoka kwa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Manyara (MARFA), mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) akiwakilisha Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA), John Kadutu, na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ahmed Idd Mgoyi.

U15 TANZANIA YATUA MEDALI VIFUANI
Timu ya Tanzania ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 15 iliyoshika nafasi ya pili katika Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) iliyofanyika Gaborone, Botswana inawasili leo (Juni 2 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

U15 ambayo imeshinda mechi tatu, sare moja na kufungwa moja inawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12.30 jioni kwa ndege ya Kenya Airways ikitokea Gaborone kupitia Nairobi.
Tanzania ambayo imepata medali za fedha kwa kushika nafasi hiyo ikiwa chini yaKocha Abel Mtweve ilizifunga Afrika Kusini 2-0, Botswana 2-0, Swaziland 3-0 na ikatoka sare ya bao 1-1 na Mali. Ilifungwa mabao 2-0 na Nigeria ambao ndiyo walioibuka mabingwa.

Wachezaji 16 waliounda kikosi cha Tanzania ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli, Amri Nyuki, Amede Amani, Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove Mdumule, Hance Msonga, Kelvin Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro Shaban, Rajab Mohamed na Thomas Chindeka.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
GARI LA NICE & amp; LOVELY MISS TANGA LATUA MKONGE HOTEL

GARI LA NICE & amp; LOVELY MISS TANGA LATUA MKONGE HOTEL

June 02, 2014

20140531_095629 
Gari ambalo atakabidhiwa mshindi wa shindano kubwa nala kipekee linalosubiriwa kwa hamu na wakazi wa mkoa wa Tanga, Nice & Lovely Miss Tanga 2014 tayari limepelekwa mkoani humo na sasa lipo katika maegesho ya magari katika hotel ya Mkonge. 

Mkurugenzi wa kampuni ya Mac D Promotion ambao ndio waandaaji wa shindano hilo, Irene Rweyunga amesema mwaka huu wampaniakuhakikisha wanapata washiriki wenye sifa na viwango lengo likiwa ni kuhakikisha mshindi anakuja kutwaa taji la Redds Miss Tanzania mwaka huu.  
 
Irene amesema mwish wa kuchukua na kurudisha fomu za kuhiriki shindano hilo ni jumampili hii ya tarehe 08 June 2014, na kambi rasmi itaanza jumatatu ya tarehe 09 June 2014 katika hotel ya Tanga Beach Resort.
 
Shindano la Nice & Lovely Miss Tanga litafanyika June 21′ 2014 katika Hotel ya Mkonge. Wadamini waliodhamini shindano hili ni Nice & Lovely, Eatv, Redds, Breeze Fm, Tanga Beach Resort, Mwambao Fm na Rweyunga Blog
NBC TANZANIA ILIVYOMKARIBISHA NCHINI MTENDAJI MKUU WA BARCLAYS PLC, ANTHOY JENKINS

NBC TANZANIA ILIVYOMKARIBISHA NCHINI MTENDAJI MKUU WA BARCLAYS PLC, ANTHOY JENKINS

June 02, 2014


01 (7)  
Mtendaji Mkuu wa Barclays PLC, Anthony Jenkins akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC Tanzania wakati wa ziara yake nchini jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Bi. Mizinga Melu.
02 (1)  
Mtendaji Mkuu wa Barclays PLC, Anthony Jenkins (kulia) akipozi kwa picha na Rachel Mwalukasa mmoja wa wafanyakazi aliyemkabidhi tuzo kwa kuwa mfano wa kuigwa katika suala la kujitolea binafsi katika kuisaidia jamii. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji nwa NBC Tanzania, Mizinga Melu.
03 (2)  
Wafanyakazi wa NBC Tanzania wakionyesha sura ya matumaini wakati wakimsikiliza bosi wao, Antony Jenkins alipokuwa akizungumza kuhusu mikakati ya kimaendeleo ndani ya benki hiyo nchini.
04  
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC wakishangilia hotuba ya Mtendaji Mkuu wa Barclays PLC, Anthony Jenkins wakati wa ziara yake nchini Tanzania.
05  
Mtendaji Mkuu wa Barclays PLC, Anthony Jenkins (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bytrade Tanzania Managing Director, Harish Dhutia katika hafla iliyoandaliwa na NBC kwa ajili ya wateja wa makampuni  wakati wa ziara yake nchini Tanzania mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Mizinga Melu.
06 
Wafanyakazi wa NBC Tanzania wafuatilia kwa makini hotuba ya Mtendaji Mkuju wa Barclays PLC, Anthony Jenkins wakati wa ziara yake nchini   ambapo alifanya mikutano na wafanyakazi, wateja wa NBC na wadau wengine wa benki hiyo.