RAIS MAGUFULI AIAGIZA BOT KUHARAKISHA SERA YA RIBA

December 13, 2017
Na: Beatrice Lyimo,MAELEZO-DODOMA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameihimiza Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuharakisha uandaaji wa Sera ya Riba ambayo zitaifanya taasisi za kifedha kuwa na riba zinazowiana na nafuu.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Mjini Dodoma wakati wa akizundua tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo jengo la LAPF Makole ambalo ni tawi kubwa kwa mkoa wa Dodoma.

“Serikali imechukua hatua mbalimbali za kukabiliana na changamoto za mabenki kutolipwa na wakopaji kwa kuanzisha mfumo wa kuhifadhi taarifa za mkopaji ambazo zitawezesha benki zote kuwatambua wakopaji na kuweza kuchukua tahadhari stahiki, pia itaendelea kutoa vitambulishio vya Taifa ambavyo kwa sasa vina taarifa zote muhimu za mwananchi,” amefafanua Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli ametoa wito kwa BOT kudhibiti matumizi ya dola na fedha nyingine za kigeni hapa nchini kutokana na kuharibu uchumi wa nchi. Dkt. Magufuli ametolea mfano wa fedha zilizoshikiliwa Airport ya Dar es Salaam ambazo ni zaidi ya Dola Bilioni Moja zikiwa hazijulikani zilipokuwa zikipelekwa.

Vile vile ameiagiza BOT kufungia mabenki na makampuni ya simu ambayo hayatajiunga na kituo cha kuhifadhia taarifa ambacho kina mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali kuhakikisha yamejiunga kufikia mwisho wa mwaka vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Rais Magufuli ametoa wito kwa mabenki yote nchini kupeleka huduma za kibenki hadi vijijini kupitia njia mbalimbali kama vile mabenki yanayotembea, mitandao ya simu pamoja na kutumia mawakala ili kuongeza ukwasi kwa mabenki hayo.

Mbali na hayo Dkt. Magufuli ameitaka Benki ya CRDB kuandaa utaratibu wa kujenga Makao Makuu ya Benki hiyo mjini Dodoma kwani Dodoma ndio Makao Makuu ya nchi na tayari Serikali imeshaanza kuhamia.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amewakaribisha wawekezaji mbalimbali kuwekeza katika Mkoa wa Dodoma na kuahidi kutoa ushirikiano kwa wawekezaji hao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei ameipongeza Serikali kwa uamuzi wa ukusanyaji wa kodi kwa kutumia mifumo ya kielektroniki.

Pia Dkt. Kimei amemkabidhi Rais Magufuli Hundi ya Shilingi Milioni 100 kwa ajili ya ufadhili wa miradi mbalimbali ya kijamii ambapo Rais Magufuli ameikabidhi hundi hiyo kwa uongozi wa Mkoa na kuagiza uongozi huo kujenga Wodi ya wagonjwa katika Hospital ya Mkoa wa Dodoma.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB Ali Laay amesema kuwa CRDB imefanikiwa kulipa gawio la shilingi Bilioni 19.5 ambalo lilielekezwa katika uboreshaji wa sekta ya afya nchini.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE AZINDUA JUKWAA LA WANAWAKE WILAYANI HUMO

December 13, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Temeke
Felix Lyaniva azindua jukwaa la wanawake Kiwilaya katika viwanja vya Mwembe Yanga. Katika uzinduzi huo DC Lyaniva asisitiza wanawake kupendana,kuwa na umoja ili kujiletea maendeleo ya kweli,hata kufikia uchumi wa kati.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akiwa akishuhudia wakina mama wakipiga na mabanho yenye ujumbe tofauti katika uzinduzi wa jukwaa la wanawake Wilaya ya Temeke.

Wanawake hao ambao wamejitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo, huku sherehe hizo zikipambwa na shamrashamra za maandamano ya vikundi mbalimbali vya wanawake wajasiriamali.
Pia wanawake wajasiriamali walionesha kazi za mikono na ubunifu ufanywao na vikundi vyao.
Katika uzinduzi huo ulifanyika uchaguzi wa mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Kiwilaya ambapo Johari Maulid Mkonde alichaguliwa rasmi kuwa mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilayani Temeke.
Hata hivyo wanawake wa Temeke wamepewa fursa kushiriki uchumi wa viwanda ili waweze kufika malengo ya maendeleo endelevu ya 50/50 ya dunia kufikia mwaka 2030.
Jukwa la wanawake liliundwa ili kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuondoa pengo kubwa ambalo limejengeka duniani na kuongeza ushiriki wa wanawake katika uchumi duniani kote. Majukwaa haya yatazinduliwa katika Mikoa yote nchini na Halmashauri zote. Katika Mkoa wa Dare Es Salaam Wilaya ya Temeke ni Wilaya ya kwanza kuzindua jukwaa la wanawake.
Kauli mbiu katika uzinduzi huu ni ''Mwanamke Tumia Fursa Kushiriki Uchumi wa Viwanda''

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA NYUMBA ZA MAKAZI ZA NHC IYUMBU DODOMA LEO

December 13, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisaidiwa na viongozi wengine kufunua kitambaa kuashiria kufunguliwa kwa nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisaidiwa na viongozi wengine kukata utepe kuashiria kufunguliwa kwa nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyuma la Taifa (NHC) Mama Blandina Nyoni, Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu wakikagua moja ya nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na NHC eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017
Muonekano wa baadhi za nyumba nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na NHC na kufunguliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi wa dini na wananchi wakati wa sherehe za ufunguzi wa nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza mshereheshaji Ephraim Kibonde wakati wa ufunguzi wa nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wafanyakazi wa NHC wakati wa sherehe za ufunguzi wa nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongozana na Spika Job Ndugai, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi,Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu wakati wa sherehe ya ufunguzi wa nyumba 150 mpya za makazi zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Iyumbu nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Desemba 13, 2017. PICHA NA IKULU

MBUNGE WA JIMBO LA NZEGA VIJIJINI DKT KIGWANGALLA AKABIDHI PIKI PIKI 19 MBELE YA KATIBU MKUU WA CCM DNUGU KINANA KWA WATENDAJI NA VIONGOZI WA KATA WA JIMBO HILO

December 13, 2017


Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla leo amekabidhi piki piki 19 kwa Viongozi na Watendaji wa kata 19 ndani ya jimbo hilo,makabidhiano hayo yalifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Check Pointi mara baada ya mkutano Mkuu wa jimbo kufanyika.Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana (Wa tatu kushoto) na kulia ni Katibu wa CCM wilaya Nzega Ndugu Janath Kayanda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nzega,Mh.Godfrey Ngapula . Picha na Michuzi Jr-Nzega.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpongeza mmoja wa Watendaji Kata kwa kukabidhiwa Piki Piki na Mbunge wao wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla,jioni ya leo katika ukumbi wa Checki Point,mjini humo mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa cha cha Mapinduzi (CCM ) Ndugu Abdulrahaman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa jimbo la Nzega vijijini mapema jioni ya leo katika ukumbi wa mikutano wa Check Point,wilayani humo mkoani Tabora.Ndugu kinana amewapongeza Wana CCM wa jimbo la Nzega kwa kushinda uchaguzi wa marudio wa madiwani,viongozi mbalimbali walioshinda nafasi mbalimbali za uongozi kwa ngazi ya Wilaya na kuwataka kuwa wamoja sambamaba na kushirikana katika kuhakikisha wanawaletea maendeleo wananchi na sii kulumbana tena.
Picha na Michuzi Jr-Nzega.
Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla akizungumza mbele ya Viongozi na wajumbe mbalimbali wa jimbo hilo waliojitokeza kwa wingi,katika Mkutano wao Mkuu wa jimbo ambao mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana .Dkt Kigwangalla amekabidhi piki piki 19 kwa Viongozi na Watendaji wa kata 19 ndani ya jimbo hilo. Mkuu wa Wilaya ya Nzega,Mh.Godfrey Ngapula kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Tabora,akitoa salamu mbele ya Viongozi na wajumbe mbalimbali wa jimbo la Nzega Vijijini kabla ya Mkutano Mkuu wa jimbo hilo kuanza.
Viongozi na wajumbe mbalimbali wa jimbo la Nzega Vijijini wakishangilia jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwasalimia kabla ya kuanza rasmi mkutano mkuu wa jimbo hilo,ambapo Mbunge wa jimbo hilo Dkt Hamisi Kigwangalla amekabidhi piki piki 19 kwa Viongozi wa Kata na Watendaji ili kuwasaidia kupambana na chanagamoto za usafri wakati wakiendelea kusikiliza na kutatua matatizo ya Wananchi wa jimbo hilo.
Viongozi na wajumbe mbalimbali wa jimbo la Nzega Vijijini wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia mapema leo katika ukumbi wa Checki Point,mjini humo wakati wa mkutano mkuu wa jimbo hilo,ambapo Mbunge wa jimbo hilo Dkt Hamisi Kigwangalla amekabidhi piki piki 19 kwa Viongozi wa Kata na Watendaji ili kuwasaidia kupambana na chanagamoto za usafri wakati wakiendelea kusikiliza na kutatua matatizo ya Wananchi wa jimbo hilo.
-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.
PROF. MBARAWA ATAKA UJENZI RELI YA KISASA KUHARAKISHWA

PROF. MBARAWA ATAKA UJENZI RELI YA KISASA KUHARAKISHWA

December 13, 2017
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali ya Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa (kushoto), kuhusu kusimamia kwa karibu mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge), wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo katika kijiji cha Soga Mkoani Pwani na Ngerengere mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali ya Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa (kulia), alipomweleza hatua za ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge), wakati Waziri huyo alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo Mkoani Pwani.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akichanganya zege katika moja ya Makalvati yanayojengwa katika mradi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge), katika eneo la Kisarawe alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo Mkoani Pwani.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), akibonyeza kitufe cha kuruhusu zege kwenda kwenye kalvati linalojengwa kwenye Reli ya Kisasa (Standard Gauge), wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo Mkoani Pwani.
Muonekano wa moja ya kalvati linalojengwa kwenye Reli ya Kisasa (Standard Gauge), katika eneo la Kisarawe Mkoani Pwani. Mradi huo unajengwa kwa awamu mbili ambapo sehemu ya kwanza inajengwa kutoka Dar es Salaaam mpaka Morogoro ambapo sehemu ya pili itajengwa kutokea Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma.
Mafundi wa Kampuni ya Yapi Merkezi wakiendelea na kazi ya kujaza zege kwenye moja ya kalvati linalojengwa kwenye Reli ya Kisasa (Standard Gauge), katika eneo la Kisarawe Mkoani Pwani.
Tingatinga likiendelea na kazi ya kuchenjua tabaka la chini la Reli ya Kisasa (Standard Gauge), katika eneo la Soga, Mkoani Pwani.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa wito kwa mkandarasi Yapi Merkezi na Motaengil Africa wanaojenga reli ya kisasa (Standard Gauge Railway), kufanya kazi kwa uadilifu, kulingana na vipimo vilivyo kwenye mkataba ili kuwezesha mradi huo kukamilika kwa wakati.

Aidha, ameitaka Kampuni Hodhi ya Rasilimali za reli (RAHCO), kuhakikisha kuwa inafuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo kwani wananchi wamekuwa wakisubiri kukamilika kwake na kuanza kupata huduma za usafiri wa treni zitakazorahisisha shughuli zao za kibiashara na kijamii.

Akizungumza leo mara baada ya kukagua mradi huo katika kijiji cha Soga mkoani Pwani, Waziri Mbarawa amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya wakandarasi hao na kuagiza kuongeza spidi zaidi ili ifikapo mwaka 2020 mradi huo uwe umekamilika.“Kasi mnayoenda nayo sio mbaya, ila naomba RAHCO mhakikishe mnasimamia kwa karibu kuhakikisha spidi inaongezwa ili kazi ikamilishwe haraka na kwa viwango”, amesema Profesa Mbarawa.

Akiwa katika kijiji hicho, Waziri Mbarawa amemwagiza Kaimu Mtendaji Mkuu wa RAHCO, Masanja Kadogosa, kukutana na uongozi wa kampuni hizo kujadili na kuangalia fursa za upatikanaji wa ajira kwa watanzania hususan wakazi wa eneo inapopita reli hiyo.

Kwa upande wake, Kaimu Mtendaji Mkuu wa RAHCO, Masanja Kadogosa, amesema mpaka sasa mradi huo upo ndani ya muda na kumhakikishia Waziri Mbarawa kuwa mradi utakamilka kwa wakati kwani kazi inayofanyika sasa ni kuweka zege kwa ajili ya ujenzi wa boksi kalvati ambapo kazi hiyo inaendelea vizuri.

Ameongeza kuwa katika kipindi hiki mradi ulisuasua kutokana na changamoto za mvua za vuli, hivyo amefafanua kuwa wana mpango wa kuongeza kambi nyengine nane upande wa Soga na nane upande wa Ngerengere ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.

Mradi wa SGR unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza unahusisha ujenzi wa reli kutoka Dar es salaam – Morogoro na ya pili itahusisha sehemu ya Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma pamoja na njia za kupishana ambapo kwa pamoja itakuwa na urefu wa kilometa 722 na itajengwa kwa gharama ya shilingi Trilioni 7.1.

WAZIRI KALEMANI AKAGUA MIRADI YA UMEME REA III KONGWA NA KONDOA

December 13, 2017
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (aliyeshika kipaza sauti) akiwasalimu wananchi wa Kijiji cha Pembamoto, Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma, alipofanya ziara kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III)
Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (kushoto), akimpokea Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia) alipowasili jimboni kwake Kongwa kukagua Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto), akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bilinith Mahenge (kulia), alipofika ofisini kwake hivi karibuni, kabla ya kutembelea Wilaya za Kongwa na Kondoa kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III). Kushoto kwa Waziri ni Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga. Wengine ni watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na wakandarasi wanaotekeleza Mradi husika katika Wilaya hizo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akimkabidhi Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, kifaa kinachotumika kuunganisha umeme katika nyumba pasipo kutandaza nyaya, kijulikanacho kama UMETA. Waziri alitoa kifaa hicho kama zawadi kwa baadhi ya wazee katika Kijiji cha Makole, Wilaya ya Kongwa, wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA III) pamoja na kuzungumza na wananchi.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kulia), akifafanua jambo kwa Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (kushoto), alipokuwa katika ziara ya kazi jimboni humo kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III). Wengine pichani ni viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wataalam kutoka wizarani, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Diwani wa Kata ya Nhumbi, Wilaya ya Kongwa, Sina Mude akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Wilaya ya Kongwa, Seif Shabani (kulia), akiorodhesha jina la mmojawapo wa wazee waliopatiwa zawadi ya kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III)

Sehemu ya umati wa wananchi katika Vijiji vya Makole, Pembamoto na Bereko wilayani Kongwa na Kondoa, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (aliyeshika kipaza sauti), akiwatambulisha wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika Wilaya ya Kongwa, wakati wa ziara yake kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi huo. 
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota (kulia) akiwa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo wakimpokea Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kutoka kulia) alipowasili wilayani humo kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III). Kulia kwa Waziri ni Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (aliyeshika kipaza sauti), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Bereko, Wilaya ya Kondoa wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni Mbunge wa Kondoa, Ashatu Kijaji, akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati – mbele) wilayani humo kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III)
Kazi ya kuunganisha umeme katika Kijiji cha Bereko, Wilaya ya Kondoa ikiwa katika hatua za mwisho, kama mafundi hawa walivyokutwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).

Na Veronica Simba – Dodoma
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amekagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika Wilaya za Kongwa na Kondoa mkoani Dodoma.

Katika ziara hiyo ya siku moja iliyofanyika Jumatatu Desemba 11, 2017, Waziri Kalemani aliwasisitiza viongozi wa Halmashauri ambako Mradi wa REA III unapita, kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kuunganisha umeme hususan katika Taasisi mbalimbali za umma.

“Siyo vema Taasisi muhimu za umma zikaendelea kukosa umeme kwa kutokuwa na fedha hivyo kuwatesa wananchi. Hakikisheni mnatenga fedha kwa shughuli hiyo muhimu.”

Aidha, alibainisha kuwa, maeneo yanayopewa kipaumbele katika Mradi wa REA III ni Taasisi zote za umma ili kuhakikisha zinatoa huduma bora kwa wananchi.

Pia, aliwataka wakandarasi wanaotekeleza Mradi huo katika maeneo mbalimbali nchini, kukutana na viongozi wa maeneo husika wakiwemo wabunge ili wapewe mwongozo wa sehemu muhimu za kipaumbele zinazotakiwa kuunganishiwa umeme.

Kwa upande wake, Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, akizungumza wakati wa ziara ya Waziri jimboni kwake, aliwaasa watendaji katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuongeza uwajibikaji kwa wateja wao ili kuboresha utoaji huduma ya umeme kwa wananchi.

“Bado zipo changamoto kadhaa katika utoaji wa huduma ya umeme kwa wananchi. Tanesco ongezeni uwajibikaji ili wananchi wanufaishwe na huduma hiyo muhimu kama Serikali ilivyodhamiria.”

Naye Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni Mbunge wa Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji, alitoa pongezi na shukrani kwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati kwa kupanga kuviunganishia umeme vijiji 24 vya Wilaya hiyo, kupitia REA III.

“Kwa niaba ya wananchi wa Kondoa, natoa pongezi za dhati kwa Serikali na kuiomba iendeleze jitihada hizi za kuwaletea wananchi wake maendeleo kupitia upatikanaji wa nishati muhimu ya umeme,” alisema.

Katika ziara hiyo, Waziri Kalemani alifuatana na viongozi na wataalam mbalimbali kutoka wizarani, Tanesco na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), akiwemo Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga.

WADAU WA TAKWIMU WAKUTANA KUJADILI NA KUTATHMINI UTEKELEZAJI WA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU NA MPANGO WA PILI WA MAENDELEO WA TAIFA

December 13, 2017
Na Emmanuel Ghula
WADAU wa Takwimu nchini wamekutana ili kujadili upatikanaji wa Takwimu za msingi na uzalishaji wa takwimu na mapungufu yaliyopo katika kupima na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa.

Akizungumza wakati akifungua warsha ya siku mbili ya wadau hao, Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango Mhandisi Happiness Mgalula amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Maendeleo pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)  wameandaa warsha hiyo ili kujadili namna bora ya upatikanaji wa takwimu zitakazosaidia kufanikisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo.

“Leo tumekutana hapa kwa pamoja ili kujadili namna bora ya upatikanaji wa takwimu kwa ajili ya kupima na kutathmini utekelezaji wa viashiria vya Malengo ya Maendeleo Endelevu na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa katika sekta ya Ukuaji Uchumi, Ajira na Ushindani wa Kiuchumi,” amesema Mhandisi Mgalula.

Amesema Serikali itaendelea kuratibu upatikanaji wa takwimu rasmi nchini kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu pamoja na wadau wengine ili kufanikisha utekelezaji wa seti za malengo ya ulimwengu katika muda maalumu na ambayo mkazo wake ni kuondoa aina zote za umaskini pamoja na njaa. 

Amesema Serikali imepiga hatua kubwa katika kuweka mikakati ya utekelezaji wa Malengo ya Mandeleo Endelevu (SDGs) tangu mwaka 2015 ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano mikubwa miwili ya Kitaifa kwa ajili ya kuwajengea wananchi uelewa mzuri kuhusu SDGs na utekelezaji wake. 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya amesema NBS itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhak  takwimu rasmi zinapatikana kwa wakati ili ziweze kutumika na Serikali pamoja na wadau wengine wa maendeleo katika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Aidha, Ruyobya amesema washiriki watajadili namna bora zaidi ambayo wadau wanaweza kushiriki katika kuchangia mapungufu ya upatikanaji na uzalishaji wa takwimu pamoja na ubunifu na ujuzi wa teknologia katika uzalishaji na upatikanaji wa takwimu.
 Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango Mhandisi Happiness Mgalula akizungumza wakati akifungua warsha ya siku mbili ya wadau wa takwimu waliokutana kuanzia leo jijini Dr es Salaam katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere.
 Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa hafla ya ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya wadau wa takwimu waliokutana leo jijini Dr es Salaam katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere.
Baadhi ya wadau wa takwimu waliokutana leo jijini Dar es Salaam katika warsha ya siku mbili ili kujadili namna bora ya upatikanaji wa takwimu kwa ajili ya kupima na kutathmini utekelezaji wa viashiria vya Malengo ya Maendeleo Endelevu na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa.