HALL: Aipigia saluti Coastal Union.

April 28, 2013
Oscar Assenga, Tanga.

KOCHA Mkuu wa Azam Fc,Stewart Hall amesifu kiwango cha timu ya Coastal Union ya Tanga kwa kueleza wachezaji wake wana uwezo mkubwa wa kuipa mafanikio timu hiyo siku zijazo.
Akizungumza na Blogi hii mara baada ya kumalizika mechi kati yao na Coastal Union ambapo timu zote zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 ,Hall alisema mechi hiyo ilikuwa ngumu na yenye ushindi kutokana na kila timu kuonekana kujipanga vema hasa katika mzunguko huo wa lala salama.
Hall alisema licha ya wao kujipanga vilivyo kuweza kuibuka na ushindi lakini hali haikuwa kama walivyotegemea kutokana na timu waliokuwa wakicheza nayo kuonekana kujipanga zaidi.
“Matarajio yetu ilikuwa tushinde ili kuweza kuongeza nafasi yetu ya kupata ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara na sio vyenginevyo “Alisema Hall.
Kwa upande wake,Kocha Mkuu wa Costal Union,Hemed Morroco alisema wanamshukuru mungu kwa kupata pointi moja muhimu na kueleza hivi sasa nguvu zao watazielekeza kwenye mechi yao na Yanga.
Mwisho

HAPA KAZI

April 28, 2013
Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga,Sixtus Nyaki akiwa ofisini kwake kama aliyokutwa na blog hii mwishoni mwa wiki,Picha na Oscar Assenga.
African Sports yapunguzwa kasi ya kusaka ubingwa na Small Prison

African Sports yapunguzwa kasi ya kusaka ubingwa na Small Prison

April 28, 2013
Na Oscar Assenga, Tanga.

BAO 1-0 walilofungwa timu ya African Sports “Wanakimanumanu”na Small Prison ya Tanga limewapunguzia mbio zao za kutaka kuwania ubingwa wa Ligi ya Mkoa wa Tanga kutokana na kuwa na idadi ya pointi sawa wakitofautiana mabao tu na timu hiyo.

Mchezo huo ambao ulianza kwa kasi ambapo kila timu ziliweza kuingia uwanjani hapo zikiwa na ari na nguvu ya kutaka kushinda kwa idadi kubwa ya mabao lakini hali ilikuwa ngumu kidogo kutokana na kuonekana kukamiana.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzie ambapo timu zote zilianza awamu ya pili kwa ushindani mkubwa ambapo kipindi hicho, Small Prison waliweza kufanya mabadiliko kwenye dakika ya 65 ambapo walimtoa Gerald Gasper na kuingia Said Mtupa.

Kuingia kwa mchezaji huo kuliweza kuwaongezea nguvu timu hiyo na kuanza kucheza kwa pamoja na kupeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa African Sports kwa dakika kadhaa na hatimaye kuweza kufanikiwa kuandika bao lao la kwanza na la ushindi kwenye dakika ya 74 kupitia Martin Mpanduzi baada ya kutokea piga ni kupige langoni mwa African Sports.

Baada ya kuingia bao hilo,African Sports waliweza kujipanga na kuanza kuliandama lango la Small Prison huku wachezaji wake wakipiga mashuti makali langoni mwa timu hiyo bila kuweza kwa mafanikio yoyote kutokana na uimara wa mlinda mlango wa timu hiyo,Frank Mutego.

Katika hatua nyengine baada ya mechi hiyo kumalizika wachezaji wa timu ya Small Prison waliweza kumbeba juu Kocha Mkuu wa timu hiyo, Raphael John wakimpongeza kwa ushindi ambao waliupata.

Kwenye mechi hiyo,African Sports iliwakilishwa na Mohamed Rashid,Abasi Peter,Rashid Hassani,Yusuph Ally,Said Abdallah,Pera Ramadhani,Mohamed Issa,Thabit Mgoha,Akrusus Jacim na Ramadhani Hamid.

Small Prison walikilishwa na Frank Mutego,Lazaro Nyato,John William,Mwaita Salehe,Mohamed Muya,Msafiri  Hassani,David Mwingira,Salim Mashaka,Juma Mohamed,Martin Peter na Gerald Gasper.

Mwisho.

Tusikate tamaa tuendelee kupambana.

April 28, 2013
MLEZI wa timu ya African Sports "Wanakimanumanu"Mr.Kilua akibadilishana mawazo na mmoja kati ya mashabiki wa timu hiyo mara baada ya kumalizika mechi yao na Small Prison ambapo African Sports ilikubali kichapo cha bao 1-0,mchezo uliochezwa uwanja wa Mkwakwani mjini hapa.

Shangwe za Small Prison hizo

April 28, 2013
Mashabiki wa Small Prison wakiwa wamembeba juu kocha wao Raphael John mara baada ya kumalizika kwa mechi yao na African Sports ambapo timu hiyo ilishinda bao 1-0,mchezo uliocheza uwanja wa Mwakwani.

Tunafuatilia

April 28, 2013

Mashabiki wa soka mkoa wa Tanga wakiufuatilia mchezo kati ya African Sports na Small prison mwishoni mwa wiki ambapo Small Prison ilishinda bao 1-0mchezo huo ulifanyika uwanja wa Mkwakwani