RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA MASHIRIKA YA KIPAPA –VATICAN BABA ASKOFU PROTAS RUGAMBWA, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

August 10, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Sanamu ya  Bikira Maria wa Fatima kutoka kwa Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Rozali aliyopewa na Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa wapili kutoka kushoto Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza na kumuaga mgeni wake Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU



Wagombea sita wa Urais TFF uso kwa uso kwenye kipindi maalum leo Ijumaa saa 3 usiku, mbashara ndani ya TBC 1 na TSN online.

August 10, 2017
KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN) pamoja na Shirika la Utangazaji nchini (TBC) kesho Ijumaa (Agosti 11, 2017)wameandaa kipindi maalum kwa wagombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kitakachofanyika mjini Dodoma kuanzia majira ya saa 3 usiku.

Kipindi hicho maalumu kitarushwa mubashara kupitia TBC pamoja na ‘TSN Online’ kitawakutanisha wagombea urais; Ally Mayay, Fredrick Mwakalebela, Wallece Karia, Shija Richard, Iman Madega na Emmanuel Kimbe ikiwa ni saa chache kabla ya siku ya uchaguzi yaani kesho kutwa Jumamosi.

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya kipindi hicho, Enock Bwigane alisema kuwa ili mpira wa miguu uendelee kukua nchini TBC na TSN iliona ni vyema ikawakutanisha wagombea kwenye jukwaa moja ili waweze kuwaambia wananchi ni kwa njia gani wataweza kuinua soka la Tanzania kama wakipewa dhamana hiyo.

Alisema, “Kuna takribani wapiga kura 130, wagombea urais ni sita lakini mmoja ndiye atakayeshinda na kuongoza shirikisho hilo kwa miaka minne kabla ya uchaguzi mwingine hivyo tumeona haja ya kuwakutanisha na kuwawezesha wananchi waweze kuwafahamu...

“…Naamini fursa ya kuwakutanisha na kuwapa nafasi ya kuwaeleza watanzania sera na mipango yao ya kuboresha soka ni jambo la msingi na ni haki yao ukizingatia kuwa leo ndiyo siku ya mwisho ya kampeni,” alisema Bwigane.

Naye Katibu wa kamati hiyo, Alfred Lasteck alisema kuwa TSN ikishirikiana na TBC inatambua nini watanzania wanataka kufahamu kuhusu mpira wa miguu na ndiyo maana imepanga kuwakutanisha wagombea ili waweze kuzungumza na umma kabla ya uchaguzi hapo kesho.

 “Kuna zaidi ya Watanzania milioni 50 ambao wangependa kufahamu ni nini kitasaidia soka la Tanzania ili liweze kuendelea kutoka lilipo sasa hadi kufikia mafanikio.

MAMBO TISA YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUUPANDA MLIMA KILIMANJARO

August 10, 2017

Na Jumia Travel Tanzania

Hivi unajua kwamba binti wa miaka nane, Roxy Getter, kutokea Florida nchini Marekani amekuwa ni mwanamke wa kwanza mwenye umri mdogo zaidi kupanda mlima Kilimanjaro mpaka kileleni mnamo mwezi Julai mwaka 2017? Kama hiyo haitoshi, Mmarekani Kyle Maynard, ambaye hana mikono wala miguu mwaka 2012 aliweza kuupanda Mlima Kilimanjaro mpaka kileleni mwenyewe bila ya msaada wowote? Licha ya kuupanda mlima huu wengine wamekuwa wakijiwekea nia  ya kufanya mambo mbalimbali kwa mara ya kwanza wakiwa kileleni kama vile kundi la wachezaji wa kike 30 wa mpira wa miguu kutokea mataifa 20 walivyofanikisha azma yao ya kucheza mechi kwa dakika zote 90 kwenye urefu wa mita 4000 mwezi Julai mwaka huu!   
Kuupanda Mlima Kilimanjaro ambao ndio unashikilia rekodi ya kuwa mrefu zaidi barani Afrika ukiwa na urefu wa mita 5,895 (sawa na futi 19,341) na unaoweza kupandika kwa urahisi zaidi duniani ni miongoni mwa malengo wanayojiwekea watu mbalimbali katika maisha yao kutoka kila kona ya dunia.

Tanzania Women of Achievement (TWA) yazindua jukwaa la mwongozo, ushauri na kujifunza kidijitali kwa ajili ya wasichana na wanawake Afrika

August 10, 2017
Rais taasisi isiyo ya serikali ya wanawake wenye mafanikio Tanzania (Tanzania Women of Achievement….TWA) Irene Kiwia (Kulia) akiongea na hadhara wakati wa kuzindua zana ya taasisi hiyo itakayotumika kiubunifu kufundisha wasichana na wanawake nchini, uzinduzi huo umefanyika sambamba na mkutano wa taasisi ya Graca Machel Trust unaoendelea jijini Dar es Salaam.

Rais taasisi isiyo ya serikali ya wanawake wenye mafanikio Tanzania (Tanzania Women of Achievement….TWA) Irene Kiwia (Kulia) akiongea na hadhara wakati wa kuzindua zana ya taasisi hiyo itakayotumika kiubunifu kufundisha wasichana na wanawake nchini, uzinduzi huo umefanyika sambamba na mkutano wa taasisi ya Graca Machel Trust unaoendelea jijini Dar es Salaam.

VIPINDI VYA KILIMO KATIKA VYOMBO VYA HABARI VITASAIDIA KUINUA KILIMO NCHINI

August 10, 2017
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani wa wilaya hiyo mjini hapa leo. Mafunzo hayo yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB). Kutoka kushoto ni Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa Wilaya ya Mtwara, Joseph Tesha, Kaimu Katibu Tawala, Francis Mkuti na Mshauri wa Kilimo Mkoa wa Mtwara, Ally Linjenje.

DKT TIZEBA: SEKTA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI ITAENDELEA KUWA KICHOCHEO KATIKA KUJENGA UCHUMI WA VIWANDA

August 10, 2017
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akisisitiza jambo kabla ya kufungwa kwa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.
- Hide quoted text -

Na Mathias Canal, Lindi

Serikali imesema kuwa  Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi itaendelea kuwa muhimili na kichocheo katika kujenga uchumi wa viwanda ambao ndio kipaumbele cha Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli. 

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Dkt Charles Tizeba  wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, nane nane kitaifa, katika viwanja vya ngongo katika manispaa ya lindi jana tarehe 8/8/2017.

Dkt Tizeba alisema kuwa kwa ushirikiano na Watumishi wote katika Wizara, amejipanga kuhakikisha kuwa, Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inaendelea kukua sawa sawa na mahitaji ya Wananchi. 

Alisema kuwa jambo hilo linawezekana ambapo inawezekana kwa kiasi kikubwa kuzalisha malighafi za kutosha za kuwezesha viwanda kuzalisha bidhaa mbalimbali, ambazo zitauzwa ndani na nje ya nchi kwa bei nzuri na ya ushindani. 

Alisema kuwa kupitia mbinu hiyo wizara itakuwa imefanikisha kuongeza mchango wa Sekta hizo katika uchumi wa Taifa na pia katika kuondoa umaskini kwa Watanzania wengi.

Sambamba na hayo pia Mhe Dt Tizeba alisema kuwa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo, mabadiliko ya tabianchi, ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangia kupungua kwa uzalishaji na tija ya mazao, uhaba wa malisho ya mifugo na rasilimali maji.  

Katika kukabiliana na jambo hilo Mheshimiwa Dkt Tizeba alisema kuwa Wizara yake imejipanga kuendelea, kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni pamoja na kuzalisha mbegu bora zinazovumilia ukame, magonjwa na kutoa mavuno mengi. 

Alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na Wabia wa Maendeleo, wamekamilisha Mpango wa Kilimo Kinachohimili Mabaliliko ya Tabianchi na Miongozi ya uzalishaji mazao, ufugaji na uvuvi. Muongozo wa kilimo umetolewa kulingana na Kanda za Kilimo za Kiteknolojia. Miongozo hiyo, imezinduliwa na kuanza kusambazwa kwa Maafisa Ugani wa Kilimo Mifugo na Uvuvi na kwa wananchi, kuanzia Mwezi, Mei na Juni, 2017. 

Alisema Mikakati mingine, inayoendelea ni pamoja na kuhakikisha kuwa mbolea bora, inapatikana kwa wingi na kwa bei nafuu zaidi, sawasawa na agizo la Makamu wa Rais la kuwasaidia Wakulima, Wafugaji na Wavuvi kupunguza gharama za uzalishaji ili waweze kufaidika na matunda ya juhudi zao.   

Sambamba na hilo aliongeza kuwa wizara yake imejipanga ili kuhakikisha kuwa inaendelea kuwaelimisha na kuwasaidia Wafugaji wa Tanzania, kufuga kitaalamu zaidi ili kuepuka hali ya kuhamahama kwa ajili ya kutafuta malisho na maji. 

Alisema kuwa jambo hilo litawezesha kufuga kwa tija na pia kupunguza migogoro ya Wakulima na Wafugaji.

MWISHO

NMB yaendelea kung'ara Maonesho ya Nane Nane, Arusha na Morogoro

August 10, 2017

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto - Dr. Hamisi Kigwangala akikabidhi kikombe cha ushindi kwa Meneja wa NMB kanda ya Mashariki – Aikansia Muro baada ya benki hiyo kuibuka mshindi wa kwanza kwenye Maonyesho ya Nane Nane Mjini Morogoro. Kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano wa NMB kwa serikali – Aneth Kwayu na kulia ni Meneja wa tawi la NMB Wami – William Kaitara.

Meneja Mikopo wa NMB mkoa wa Arusha, Oscar Rwechungura (kushoto) akipokea kombe la ushindi wa kwanza kwa taasisi za fedha kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenesta Mhagama wakati wa kilele cha maonesho ya wakulima Nanenane uwanja wa Themi mkoa wa Arusha.

Naibu Waziri wa TAMISEMI – Suleiman Jafo akimkabidhi cheti cha ushindi Meneja wa NMB Tawi la Dodoma – Harold Lambileki baada ya benki ya NMB kuibuka mshindi wa Tatu katika sekta ya fedha kwenye maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini Dodoma. NMB inashiriki maonesho ya Nane Nane katika kanda saba na kutoa elimu juu ya huduma za mikopo kwenye sekta ya kilimo.

Baadhi ya wafanakazi wa Benki ya NMB wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi.

Picha ya kumbukumbu baada ya ushindi.

BENKI ya NMB imeendelea kufanya vizuri kwenye maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika kanda mbalimbali nchini. NMB Imeshika Nafasi ya kwanza kati ya taasisi za kifedha kwenye mikoa ya Arusha na Morogoro huku ikishika Nafasi ya tatu katika mkoa wa Dodoma.
Benki ya NMB inashiriki katika maonesho ya Nane Nane maarufu kwa wakulima kwenye mikoa sita ya Lindi, Mbeya, Dodoma, Morogoro, Arusha na Mwanza. Miongoni mwa malengo ya NMB ni kuhakikisha inarahisisha zaidi na kuchochea maendeleo ya kilimo na kuwaendeleza wakulima nchini.

Wafanyakazi wa benki ya NMB wakifurahia kombe lao walilokabidhiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenesta Mhagama wakati wa kilele cha maonesho ya wakulima Nanenane uwanja wa Themi mkoa wa Arusha.

Naibu Waziri wa TAMISEMI – Suleiman Jafo akimkabidhi cheti cha ushindi Meneja wa NMB Tawi la Dodoma – Harold Lambileki baada ya benki ya NMB kuibuka mshindi wa Tatu katika sekta ya fedha kwenye maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini Dodoma. NMB inashiriki maonesho ya Nane Nane katika kanda saba na kutoa elimu juu ya huduma za mikopo kwenye sekta ya kilimo.

Mgeni rasmi katika kilele cha Maonesho ya Nane Nane mkoani Mbeya, Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, MHE. George Simbachawene akimkabidhi zawadi mmoja wa waliotembelea banda la NMB katika maonesho hayo.




--
___________________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.


Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470


          http://joemushi.blogspot.com