March 30, 2014

WANAFUNZI WA UDOM MWAKA WA MWISHO, WAAHIDI KUJIUNGA NA PPF

Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, akitoa mada kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo kwenye semina iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ambapo zaidi ya wanafunzi 500 walihudhuria semina hiyo Jumamosi Machi 29, 2014.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wakifuatilia mada kutoka kwa Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele.
March 30, 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AWASILI MKOANI RUKWA LEO TAYARI KWA KUANZA ZIARA YAKE YA SIKU 21

 Baadhi ya Wananchi na wanachama mbalimbali wakisubiri kumpokea katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Sumbawanga mkoani Rukwa mapema leo asubuhi. 
 Ndege iliyombeba Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ikiwasili katika uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa mchana huu. 
 Ndugu Kinana akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili mchana huu Sumbawanga mkoani Rukwa,tayari kwa kuanza ziara yake rasmi mkoni humu,ambapo ziara yake rasmi inaanzia Wilaya ya Nkasi,mkoani Rukwa.
March 30, 2014

VPL:YANGA SC YAPINGWA 2-1 MKWAKWANI AZAM FC AILAMBA SIMBA 2-1


Jumamosi Machi 29
Ashanti United 2 JKT Oljoro 1
Jumapili Machi 30
Azam FC 2 Simba 1
Mgambo JKT 2 Yanga 1
Mbeya City 1 Tanzania Prisons 0
Kagera Sugar 0 v Ruvu Shooting 0
Mtibwa Sugar 3 v Coastal Union 1
JKT Ruvu 3 v Rhino Rangers 1
MABINGWA Watetezi Yanga Leo huko katika dimba la Mkwakwani Tanga walifungwa Bao 2-1 na Mgambo JKT iliyokuwa ikicheza Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Mohamed Neto kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 30 kwa kile kilichodaiwa kukutwa na Hirizi na kipigo hicho inaelekea kinapeleka Ubingwa kwa Azam FC ambao Leo wameichapa Simba Bao 2-1.
Huko Mkwakwani, Mgambo JKT walipata Bao lao la Kwanza Dakika ya Kwanza tu Mfungaji akiwa Fully Maganga na Yanga kusawazisha katika Dakika ya 50 kwa Penati ya Nadir Haroub "Cannavaro" lakini Penati nyingine iliyopigwa na Malima Busungu katika Dakika ya 69 iliwapa ushindi Mgambo JKT.
Jijini Dar es Salaam, Azam FC waliichapa Simba Bao 2-1 kwa Bao za Hamisi Mcha, Dakika ya 16, na John Bocco, Dakika ya 56 wakati Bao la Simba lilifungwa na Joseph Owino katika Dakika ya 45.
Matokeo haya yanaifanya Azam FC izidi kupaa kileleni wakiwa na Pointi 53 kwa Mechi 23 na kubakiza Mechi 3 huku Yanga wakiwa Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 46 kwa Mechi 22 na kubakisha Mechi 4.