MWENYEKITI
wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika kilele cha kuazimisha miaka 38 ya kuzaliwa chama hicho zitakazofanyika
kimkoa wilayani Handeni leo mwaka huu.
Sherehe
hizo kitaifa mwaka huu zinatarajiwa kufanyika Mkoani Ruvuma zinazoambatana na
shughuli za kimaendeleo kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.
Akizungumza
na Tanga Raha Blog, Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga, Shijja Othumani
alisema kuwa kabla ya kuelekea kilele hicho chama hicho kilianza kulifanya
mambo mbalimbali ikiwemo kuwakutanisha vijana kwenye Kongamano pamoja na kuwapa
uelewa juu ya umuhimu wa katiba inayopendekezwa.
Shijja
alisema kuwa shughuli nyengine za kijamii zilizofanyika ni pamoja na jumuiya ya
wazazi kutembelea wagonjwa kwenye vituo mbalimbali vya afya kwa lengo la
kuwafariji
Alisema
kuwa licha ya kufanya hivyo lakini Jumuiya ya Wanawake ya Chama hicho mkoa wa
Tanga(UWT) walifanya mikutano ya hadhara kuwaeleza wananchi masuala mbalimbali
ya kufanya ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Hata
hivyo alisema kuwa shughuli zilizofanywa zimeongeza uzalendo miongozi mwa
washiriki ambao wanaweza kuwa chachu ya maendeleo kwa wengine katika
kuhakikisha kazi za ujenzi wa taifa zinafanyika.
EmoticonEmoticon