Bi. Samia Suluhu Ahaidi Umeme Kila Kijiji Ruvuma, Viwanda vya Mahindi, Kahawa

September 08, 2015

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (katikati) akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini, Martin Mtonda (kushoto) na mgombea udiwani wa CCM.


MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu ameanza ziara yake mkoani Ruvuma akiinadi ilani ya chama hicho huku akiahidi neema kwa wakulima wa kahawa na mahindi wa mkoa huo.

Bi. Samia Suluhu ambaye amehutubia mikutano mitatu katika majimbo mawili ya mkoa wa Ruvuma yaani Jimbo la Nyasa na Mbiga Vijijini, akizungumza katika mikutano yake amesema serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda itahakikisha inashusha umeme katika vijiji vyote vya mkoa huo kwa awamu ili kuchochea maendeleo ya wananchi.

Alisema kwa kuwa mkoa huo unazalisha mazao ya mahindi na kahawa serikali itahakikisha inaanzisha viwanda eneo hilo vya kusaga na kuandaa unga wa mahindi kwa wakulima na kuwawezesha ili wauze unga na kunufaika zaidi tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo wamekuwa wakilanguliwa.

Alisema viwanda vingine ambavyo Serikali ya CCM itavianzisha ni pamoja na viwanda vya kubangua kahawa na kuiandaa kikamilifu tayari kwa kutumika, jambo ambalo alisema licha ya kuongeza thamani ya zao hilo itaongeza ajira kwa vijana na kuchochea uchumi wa wakulima eneo hilo.
Akizungumzia miundombinu ya barabara ambayo bado ni changamoto kwa mkoa huo hasa vijijini alisema serikali itakayoundwa na CCM chini ya uongozi wa Dk. John Pombe Magufuli pamoja na yeye watahakikisha wanajenga na kuboresha barabara za maeneo hayo ili ziweze kupitika kwa uhakika.

Hata hivyo kiongozi huyo amesema Serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015 imejipanga kuboresha vizuri huduma za afya kuondoa ukiritimba na rushwa, elimu kwa kutoa elimu bure toka darasa la kwanza hadi kidato cha nne pamoja na ujenzi wa mabweni na uwezeshaji vijana na akinamama kiuchumi popote walipo mjini na vijijini.

Ziara ya mikutano ya kampeni ya mgombea mwenza huyo wa urais tiketi ya CCM, inaendelea leo katika Mkoa wa Ruvuma na ataingia Jimbo la Tunduru kuendelea kuinadi ilaya ya chama hicho kuomba ridhaa kwa wananchi ili waweze kurejeshwa madarakani na kuunda dola.

Pichani juu ni baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamefurika katika kiwanja cha Kijiji cha Maguu Wilaya ya Mbinga kumsikiliza mgombea mwenza wa urais kupitia tiketi ya CCM alipokuwa akiinadi ilani ya chama hicho.


Pichani juu ni baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamefurika katika kiwanja cha Kijiji cha Maguu Wilaya ya Mbinga kumsikiliza mgombea mwenza wa urais kupitia tiketi ya CCM alipokuwa akiinadi ilani ya chama hicho.
Baadhi ya wananchi na wanaCCM wa Kijiji cha Maguu wilayani Mbinga wakimsubiri mgombea mwenza wa urais, CCM, Bi. Samia Suluhu. 


Pichani juu ni baadhi ya pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda zilizompokea mgombea mwenza wa CCM urais, Bi. Samia Suluhu mara baada ya kuingia Wilaya ya Mbinga zikiwa zimeegeshwa pembeni huku mkutano wa hadhara ukiendelea. 

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya kampeni ya mgombea mwenza, Bi. Asumpta Mshama akizungumza na wanaCCM na wananchi (hawapo pichani) katika Kijiji cha Maguu, Wilaya ya Mbinga. 
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (kulia) akizungumza na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu, kabla ya kuanza kuhutubia katika mikutano wake wa kampeni.  

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM ambao ni wenyeji wake mkoa wa Ruvuma.

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (katikati) akizungumza na mmoja wa vijana walemavu waliohudhuria mkutano wake wa hadhara Kijiji cha Maguu. Bi. Suluhu alimsaidia fedha kijana huyo. 

*Imeandaliwa na www.thehabari.com

MAGUFULI AHIDI KUFUFUA VIWANDA MKOANI TANGA,KUONGEZA AJIRA KWA VIJANA

September 08, 2015
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akifafanua jambo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Tanga waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika katika viwanja vya Tangamano jioni ya leo mjini Tanga. 
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tanga kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya angamano,jioni ya leo ambapo aliahidi kuboresha Bandari ya Tanga, kujenga Viwanda vya matunda na samaki ili kuweza kupunguza tatizo kubwa la ajira kwa vijana.
 Naibu Waziri wa Sheria na Katiba,ambaye pia ni mgombea Ubunge viti maalum upande wa akina Mama mkoa wa Tanga (UWT),Mh Ummy Mwalimu akimuombea Kura za kutosha mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ili aweze kuibuka mshindi na kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano.
 Wakazi wa mji wa Tanga waliofika kwenye mkutano huo wakishangilia jambo. 
 Nyomi la watu . 
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akisalimiana na  Naibu Waziri wa Fedha na mgombea ubunge wa Jimbo la Iramba  Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba
  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba akihutubia wakazi wa mji wa Tanga kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Tanga na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya Tangamano kwenye mkutano wa kampeni za CCM,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aliwahutubia wananchi hao.


 Dkt Magufuli akisisitiza jambo mbele ya maelfu ya wananchi (hawapo pichani) jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika uwanja wa Tangamano.
  Naibu Waziri wa Fedha na mgombea ubunge wa Jimbo la Iramba  Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akihutubia wakazi wa Tanga mjini kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Tangamano. 
  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba na Naibu Waziri wa Fedha na mgombea ubunge wa Jimbo la Iramba  Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa kampeni jioni ya leo katika uwanja wa Tangamano,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alihutubia na Kumwaga sera zake kwa wananchi,ikiweno na kuomba ridhaa ya kuwaongoza katika miaka mitano ijayo.
 Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Mzee Yusuph Makamba akihutubia wakazi wa Tanga mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika ndani ya viwanja vya Tangamano.
 Maelfu ya Wananchi wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kuwaomba wananchi hao wajitokeze kwa wingi Oktoba 25 na kumpigia kura ya ndio ili aibuke mshindi na kupewa ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa mji wa Tanga waliofika kwenye mkutano hadhara wa kampeni,uliofanyika jioni ya leo katika viwanja vya Tangamano mjini humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.

PICHA NA MICHUZI JR-TANGA

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAARIFA KUHUSU MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WA MWEZI AGOSTI, 2015

September 08, 2015

 Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim Kwesigabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana kuhusu mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Agosti, 2015. Kulia ni Kaimu Meneja wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

UWEZO wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 62 na senti 97 mwezi Agosti, 2015 kutoka mwezi Septemba, 2010 ikilinganishwa na shilingi 62 na senti 98 iliyokuwa mwezi Julai, 2015.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim Kwesigabo wakati akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Agosti, 2015 kwa waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo.

Kwesigabo alisema mfumuko wa bei wa mwezi Agosti 2015 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.02 ikilinganishwa na asilimia 0.41 iliyokuwa mwezi Julai, 2015.

"Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 158.81 mwezi Agosti, 2015 kutoka 158.78 mwezi Julai, 2015.

Alisema kuongezeka kwa fahirisi za bei kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula, baadhi ya bei za bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na gesi kwa asilimia 2.0, mafuta ya taa kwa asilimia 2.3, mazulia kwa asilimia 1.4, dizeli kwa asilimia 3.8 na petroli kwa asilimia 8.3.

Gwesigabo alisema kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinatumiwa na kaya binafsi.

Alisema mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Agosti, 2015 umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi Julai 2015.

Aliongeza kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2015.

Alisema Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 158.81 kwa mwezi Agosti, 2015 kutoka 149.31 mwezi Agosti, 2014.

Alisema Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Agosti 2015 umepungua hadi asilimia 10.2 kutoka asilimia 10.6 ilivyokuwa mwezi Julai 2015.

Alisema mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaokaribiana na baadhi ya nchi nyingine za Afrioka Mashariki ambapo mfumuko wa bei kwa mwezi Agosti 2015 nchini Kenya umefikia asilimia 5.84 kutoka asilimia 6.62 mwezi Julai, 2015 na Uganda umefikia asilimia 4.80 kutoka asilimia 5.4 mwezi Julai, 2015.