MWANALIBENEKE YUSKISS KISIBA ATIMIZA MIAKA KADHAA YA KUZALIWA KWAKE.

MWANALIBENEKE YUSKISS KISIBA ATIMIZA MIAKA KADHAA YA KUZALIWA KWAKE.

November 18, 2015

Anaitwa Yusuph Kisiba a.k.a Yuskiss Kisiba ambae ni Blogger @Lake Zone Media & Kisibasharesky Media, Graphics Desiner & Video Editor @Shafineys Film Production Jijini Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group
Tarehe kama ya leo (Nevemba 19) miaka kadhaa iliyopita alizaliwa hivyo hii leo anafurahia siku yake ya kuzaliwa na ndugu, jamaa na Marafiki. Nasi tunamtakia maisha mema katika kuzaliwa kwake.

"Novemba 19 ni tarehe ambayo Mwenyezi Mungu aliweza kuniruhusu kutoka katika tumbo la mama yangu kipenzi na kuuona ulimwengu huu. Na hapo ndipo safari yangu ilipoanzia na ikawa ndiyo chanzo cha kufahamiana na wewe hivi sasa. Novemba 19 ni siku ambayo huwa ya kipekee sana kwangu katika huzuni na furaha kutokana na kuishi mazingira haya ya ulimwengu uliojaa kila aina ya uzuri na ubaya wake.Ukiwa kama ndugu/rafiki yangu sina budi kukukumbusha kuungana nami kufanya ibada ikiwa na lengo moja la kumuomba  Mungu atusamehe makosa yetu. Kwa yeyote niliewahi kumkosea sina budi kukuomba radhi katika siku hii". Anasema Kisiba.

UPDATE: MSAADA WA WASAMARIA WEMA WA MATIBABU UNAHITAJIKA KWA DADA HUYU

November 18, 2015

Ndugu Wasamaria wema,

Napenda kutumia fursa hii kukushirikisha habari ya kusikitisha kuhusu dada Joyce Mwambepo (pichani akiwa na mwanaye wa miaka 4, na miguu yake iliyopooza) mkaazi wa Sinde jijini Mbeya. Dada huyu mwenye umri wa miaka 27 anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na huyo mwanaye.
Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana wa 2014 dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambayo haikusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa  Mbeya ambako inasemekana alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu, kwa kukosekana nyenzo za kumfanyia uchunguzi.
Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili,  hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa tena Mbeya baada ya kukosa shilingi 550,000/- za vipimo na matibabu.
Hadi nakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake (pichani kushoto) ambaye ni mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya wazazi wake wote wawili kufariki dunia. 
Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye huyp na bibi yake.  Inasikitisha.
Hivyo nimejitahidi kufuatialia ili kujua mahitaji halisi lakini ili kumsaidia Joyce inatakiwa aanze mchakato (process)  upya za matibabu kuanzia hapa Mbeya referral Hospital  hadi Muhimbili jijini Dar es salaam.
Gharama za matibabu ni kama ifuatavyo:
1. shilingi 300,000/- za kupima CT-SCAN
2. Shilingi 250,000/- za MRI
3. Usafiri wa kutoka Mbeya-Dar kwa gari maalum la kukodi 700,000/-
4. Gharama za msaidizi ambaye ni rafiki yake 300,000/-
5. Chakula 450,000/- (Endapo watakaa hospitali mwezi mzima)
6. Gharama za matibabu (CT-SCAN&MRI ni vipimo tu) 500,000/-
7. Na mahitaji mengineyo wakiendelea kupata tiba 500,000/-

Hivyo kwa kuanzia kiasi cha shilingi 3,000,000/- (milioni tatu) kinahitajika kumpunguzia mateso dada yetu huyu. Asante sana kwa moyo wako wa kujitoa na Mungu atakubariki.

Deo Kakuru Msimu
Msamaria mwema
+255769 512 420

Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.
--------------------------------------
UPDATES:
Wasamaria wema kadhaa wamejitokeza kumsaidia dada Joyce. Hatuna uhakika kwamba wote wanapenda majina yao yawekwe hadharani, Ila tunapenda hadi sasa kukiri upokeaji wa Tshs:
1. 505,000/-
2. 50,000/-
3.100,270/-
4. 10,000/-
5. 100,000/-
6. 500,000/- (ahadi ya uhakika)
7. 500,000/- (Michuzi Media Group)
7. 800,000/-  (Kulipia gharama za vipimo vya CT Scan Regency Hospital mgonjwa atapofikishwa Dar es salaam).

Hivyo ndiyo kusema jumla ya Tshs. 2,565,270/-  tayari zimekusanywa kumsaidia dada yetu huyu anayeteseka. Kwa niaba ya mgonjwa tunashukuru sana kwa msaada huo, hana cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mola mzidishiwe pale mlipopungukiwa.
Pamoja na yote hayo, kiasi cha Tshs. 3,000,000/- za ziada zinahitajika kwa ajili ya kuhitimisha zoezi lote hili. Hiyo ikiwa ni gharama za usafiri, malazi ya mgongwa na wasaidizi wawili kwa mwezi mmoja (atapopelekwa Dar es salaam kwa vipimo na matibabu) ili kumsaidia. Hivyo michango zaidi inahitajika kumuokoa dada Joyce. KUTOA NI MOYO.
Aidha, kwa kiasi kilichopatikan, mipango imeshafanywa kumpeleka dada Joyce katika hospitali ya rufaa ya Mbeya kwa uchunguzi mpya wa awali. Baada ya hapo tutawafahamisha nini kinachotakiwa kuendelea.


Deo Kakuru Msimu
Msamaria mwema
+255769 512 420

Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea sio tu kuchangia bali pia kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.



GAPCO KUDHAMINI KILIMANJARO MARATHON KILOMITA 10 KWA WALEMAVU 2016

November 18, 2015
Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (Wa pili kutoka kushoto) akishiriki katika uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo GAPCO ilitangaza kudhamini mbio za kilomita 10 kwa walemavu. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania Oscar Shelukindo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Pamela Kikuli, Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo katika Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni, Alex Nkenyenge na Meneja Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha.
Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (Wa tatu kutoka kushoto) akishiriki katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo GAPCO ilitangaza kudhamini mbio za kilomita 10 kwa walemavu. --- GAPCO, kampuni ya mafuta inayoongoza Tanzania imetangaza udhamini wake wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2016 kilomita 10 kwa walemavu. Akitangaza udhamini huo jana wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo ya Kilimanjaro Marathon, Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi alisema GAPCO inaona fahari kudhamini mbio hizo za kilomita 10 kwa walemavu. “Tumeshuhudia mbio hizi za Kilimanjaro Marathon zikikua tangu tuanze kudhamini mwaka 2011 na pia kufurahia faida wanayopata washiriki na jamii inayozunguka maeneo ambayo mbio hizi hufanyika kila mwaka. Tunayo furaha kufanya kazi na Wild Frontiers ambao ndio waandaaji wa mashindano haya,” alisema Kakwezi. “Kama sehemu ya kusaidia jamii ambayo tunafanya biashara, GAPCO Tanzania imeamua kusaidia wanariadha ambao ni walemavu kwa kudhamini mbio ambazo wanashiriki walemavu pekee,” alisema. Alisema udhamini wa GAPCO pia utahusisha usafiri, malazi na chakula kwa washiriki kutoka Dar es Salaam na pia zawadi za pesa kwa washindi wa mbio hizo za kilomita 10 ambazo zinafanyika pamoja na mbio nyingine za Kilimanjaro Marathon. Kakwezi aliendelea kusema kuwa Kilimanjaro Marathon limekua tukio kubwa linalovutia washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania na hivyo limesaidia sana kutangaza vivutio vya utalii kama vile Mlima Kilimanjaro na pia kuwaongezea kipato wafanyabiashara wa Moshi.”. ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

Kilimanjaro Marathon msimu wa 2016 yapigwa Tafu na Tigo zaidi ya milioni 200

November 18, 2015
   Meneja Mawasiliano ya Umma wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya kuzindua msimu mpya wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2016, ambapo Tigo wametoa zaidi ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya mbio hizo.  Hafla hiyo imefanyika leo asubuhi jijini Dar es Salaam.

Wadhamini wa mbio za Marathon msimu wa 2016 wakiwa katika picha ya pamoja.

Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi msaidizi wa Michezo tokaWizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Alex Nkenyenge akizungumza na wageni waalikwa pamoja na wanahabari. Kushoto kwake ni Meneja Mawasiliano ya Umma wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, John Wanyancha.

Wadhamini wa mbio za marathon msimu wa 2016, wakilipua baruti za makaratasi kuashiria kuzinduliwa kwa udhamini huo jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

  Wana habari wakiwa katika uchukuaji wa tukio hilo ili kuipasha jamii.

Wadau wa masuala ya riadha pamoja na wana habari mabalimbali wakifuatilia kwa karibu uzinduzi wa msimu wa mbio za marathoni za Kilimanjaro msimu wa 2016. 

photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"
NDUGA ALIPOAUKWAA USPIKA WA BUNGE JANA

NDUGA ALIPOAUKWAA USPIKA WA BUNGE JANA

November 18, 2015

nd1
Spika wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai akiongoza kikao cha kwanza cha Bunge hilo jana mara baada ya kuchaguliwa na wabunge.
nd2
Mgombea wa Uspika wa Bunge la Jamhuri kutoka Chama cha Wakulima Tanzania Peter Leonard Sarungi akiomba kura kwa wabunge.
nd3
Mgombea wa Uspika kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Goodluck le Medeye akiomba kura kwa wabunge
nd4
Watumishi wa Bunge wakionesha masanduku matupu ya kura za Spika
nd5
Baadhi ya watumishi wa Bunge wakigawa karatasi za kupigia kura ya Spika kwa wabunge.
nd7
Baadhi ya wabunge wakipiga kura ya Spika
nd10
Spika Mteule wa Bunge Job Ndugai akiongozwa na askari wa Bunge baada ya kutangazwa Mshindi na Mwenyekiti wa Bunge wa Muda Andrew Chenge baada ya kupata kura 254.
nd11
Mbunge Andrew Chenge akila kiapo cha Uaminifu cha Ubunge
nd12
Mbunge Richard Ndassa akila kiapo
nd13
Mbunge Mary Nagu akila kiapo
nd14
Mbunge wa Kuteuliwa Dkt. Tulia Ackson akila kiapo
nd15
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Upendo Peneza akila kiapo
Picha zote na Hussein Makame

Ujenzi wa eneo la hifadhi ya bahari wazua maswali

November 18, 2015
Kujengwa kwenye hifadhi ya Bahari Golden Tulip kwazua maswali ya sheria ya mita 60

Kumekuwa na sheria na kanuni mbalimbali zinazoundwa, ingawa wakati mwingine hushindwa kutekelezeka kwa wakati. Ukifika katika hoteli ya Golden Tulip utakuta jinsi eneo hilo linavyozidi kujengwa na kuendelezwa kama lilivyokutwa na mpiga picha wetu. Kujengwa kwa eneo hili lililokuwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi ni kinyume cha sheria ya Hifadhi ya Bahari. Tumeshuhudia maeneo mengi yakivunjwa kwa nyumba zao baada ya kubainika yamejengwa katika hifadhi ya bahari. Haijafahamikaa mara moja kama eneo hili limeruhusiwa kuendelezwa, ikiwa ni tofauti na jengo la Hoteli ya Golden Tulip
Sheria za Hifadhi ya bahari inasema ni marufuku kujenga nyumba mita 60 ilipokuwa bahari. Hali hii imeonekana kuwa tofauti baada ya kukuta hifadhi hii ikionekana kuanza kujengwa na kuanza kuzua maswali mengi kwa wadau wa maendeleo na Waanzania kwa ujumla wanaofuatilia mambo ya maliasili na utalii. Kibao hiki kinaonyesha jinsi eneo hilo lilivyotengwa kwa ajili ya kujenga jambo ambalo ni kinyume cha sheria za mita 60 za bahari.
Gari likipita katika barabara inayoelekea katika barabara ya Golden Tulip Hoteli, ambayo pia inaonekana eneo hilo lililowekwa mabati kwa ajili ya kuanza kulijenga kama lilivyokutwa na mpiga picha wetu. na chini mkazi wa jiji la Dar es Salaam akipita katika eneo hilo, huku ikionekana ramani mbalimbali za ujenzi huo.

KUELEKEA MSIMU WA SIKUKUU YA KRISMAS TIGO WAZINDUA KAULI MBIU MPYA, "LIVE IT, LOVE IT",

November 18, 2015
 Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyanja, akizungumza na waandishi wa habari wakati akimkaribisha Meneja Mkuu wa Tigo kuzungumza na wanahabari.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez  (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa uzinduzi wa  chapa mpya yenye kauli mbinu ya 'Live it, love it' itakayoimarisha nafasi ya mbunifu anayeongoza kwa ubunifu wa kidigiAali nchini. Kulia ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez, akionesha simu mpya zenye menyu ya Kiswahili wakati wa mkutano huo.
 Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Masoko wa Tigo, Olivier Prentout.
 Mkurugenzi wa Huduma za Masoko wa Tigo, Olivier Prentout (kulia), akizungumza na wanahabari kuhusu huduma mpya za Tigo kuelekea Sikukuu ya Krismas.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.

Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Tigo, imezindua chapa mpya yenye kauli mbinu ya 'Live it, love it' itakayoimarisha nafasi ya mbunifu anayeongoza kwa ubunifu wa kidigitali nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chapa hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Diego Gutierrez alisema chapa hiyo mpya itahakikisha inakuwa rafiki nzuri kwa Watanzania kuziona ndoto zao na kuzifikia.

Alisema kwa hapa nchini kama zilivyo nchi zingine intaneti imekuwa  nisehemu muhimu ya maisha ya watu kutokana na huduma za kidigitali kutumika katika biashara, elimu, kwa familia na kwa kujiburudisha.

"Tumejikita kwenye utoaji huduma katika matarajio hayo na rekodi ya mwenendo wa ubunifu wetu unatupa imani kuwa tunafanikiwa," alisema Gutierrez.

Katika hatua nyingine, kampuni hiyo imetoa ofa kwa wateja wake  kwa kuuza simu ya smartphone ya aina ya Tecno Y3 kwa sh. 99,000 kuelekea msimu wa Sikukuu ya Kristmass na Mwaka Mpya.

Gutierrez alisema simu hiyo itakuwa na 'menu' ya Kiswahili itakayomuwezesha mteja kuitumia kwa urahisi huku ikiwa na kamera mbele na nyuma, betri linalokaa kwa muda mrefu na vitu vingine.


A photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"
VIONGOZI WA KIMILA WAPITISHA AZIMIO LA KUMLINDA MTOTO WA KIKE

VIONGOZI WA KIMILA WAPITISHA AZIMIO LA KUMLINDA MTOTO WA KIKE

November 18, 2015
IMG_1623
Pichani juu na chini ni baadhi ya viongozi wa mila (Laigwanan na Laiboni) na akina mama mashuhuri (Ngaigwanan) wilayani Lolilondo wakisoma na kujadili azimio la pamoja la kumlinda mtoto wa kike kabla ya kulipitisha na kusaini wakati wa kongamano kubwa la siku mbili lililofanyika katika ofisi za halmashauri ya wilaya Ngorongoro, jijini Arusha.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
VIONGOZI wa kimila wa jamii ya Kimaasai na wanawake mashahuri wamepitisha Azimio la Loliondo lenye lengo la kumlinda mtoto wa kike na kuhakikisha maendeleo yake kiafya, kielimu na kitamaduni.
Azimio hilo ambalo limetiwa saini na viongozi hao mwishoni mwa kongamano kubwa la siku mbili lililofanyika, katika ofisi za halmashauri wilayani Ngorongoro, linapinga mila na desturi zinazomkandamiza mtoto wa kike. Mila na desturi ambazo zimepitwa na wakati.
Kabla ya kupitishwa na kusaini maazimio hayo viongozi hao wa kimila na mashuhuri walipatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili kuendeleza mijadala na uelewa na hatimae kuamini kwamba baadhi ya mila na desturi zinachangia na kuchochea athari za kiafya na kijamii hasa kwa watoto wa kike na kina mama.
Viongozi hao wamepitisha azimio hilo baada ya kupitia kifungu hadi kifungu na kuridhia yaliyomo kwa kuzingatia wajibu wao ndani ya jamii na uwezo mkubwa wa ushawishi kama viongozi wa mila (Laigwanan na Laiboni) na akina mama mashuhuri (Ngaigwanan) .
Aidha walisema kwamba watatumia nafasi zao kuelimisha jamii juu ya malezi bora ikiwa ni pamoja na mahali salama pa kulala watoto wa kike na kiume na kuelimisha jamii umuhimu wa elimu kwa kuwapeleka shuleni hasa kwa watoto wa kike.
“Naomba viongozi wenzangu twende tukaelimishe jamii juu ya madhara ya tohara kama tulivyoazimia na kuanzisha mchakato utakaosaidia kupunguza au kumaliza kabisa matendo ya tohara ndani ya jamii yetu,” alisema Mwenyekiti wa Baraza la Malaigwanan wilaya ya Ngorongoro, Joseph Oletiripai.
IMG_1611
Viongozi hao pia wamesema ni vyema jamii ya kifugaji kuacha kuendelea na vitendo vya kuwaoza watoto wa kike wakiwa bado wadogo na wakati mwingine kwa kuwakatisha masomo na kuwalazimisha kuolewa.
“Sisi kama viongozi tusiendelee kuwa chanzo cha kuendeleza matukio haya kwani ni ya ukatili kwa watoto wetu wa kike na tutumie nafasi hii kwenda kuwaelimisha viongozi wenzetu wengine mashuhuri ili kusambaza ujumbe na jamii ijue athari zinazotokana na ukeketaji pamoja na kuozesha watoto wetu wakiwa katika umri mdogo,” alisema Laanoi Munge.
Viongozi hao pia wamedhihirisha kuwa matukio ya vitendo vya ukeketaji na ndoa za utotoni vimechangia utoro nyumbani na kwenda kuishi kwa muda kwenye vituo maalum kwa kuogopa kufanyiwa tohara.
Watoto hao wamekuwa na hali ya kutoroka baada ya kugundua kwamba kuna matukio ya ulemavu na athari nyinginezo za kiafya zinazotokana na ukeketaji na salama yao ni kujitoa katika jamii hiyo na kutafuta hifadhi kwingine.
IMG_1627
Azimio hilo la Loliondo ambalo pia lilitiwa saini na waganga wa tiba asilia limetoa mwelekeo wa kuboresha afya ya uzazi, elimu na malezi kwa watoto wa kike katika jamii ya Kimaasai.
Aidha limetoa namna bora ya utekelezaji na kupitisha taratibu zitakazosaidia watoto wa kike wanaokimbia tishio la ukeketaji na kuhakikisha kwamba watasoma na kupata huduma zote za afya.
Katika maeneo yao baada ya kutia saini viongozi hao wameahidi kuonyesha ushirikiano wa karibu kwa viongozi wa serikali katika ngazi zote, viongozi wa dini, vyombo vya habari, walimu, wataalamu wa afya na wadau wa maendeleo katika maeneo yote ndani ya wilaya ili kuboresha afya ya uzazi, elimu na malezi bora kwa watoto.
Pamoja utiaji saini wa Azimio la Loliondo,viongozi hao wameliomba shirika la UNESCO na halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro kushirikisha viongozi wengi zaidi, kuendelea kutoa elimu kwa viongozi wa kimila na kuendelea kuwasaidia katika majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu na kuwasaidia uratibu wa shughuli zote za kupingana na unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.
IMG_1632
Katibu wa Baraza la Mila (W) Ngorongoro, Laanoi Munge akisoma azimio la kumlinda mtoto wake baada ya kulifanyia marekebisho ya pamoja mbele ya viongozi wa mila wa wilaya ya Ngorongoro.
Kongamano hilo lililozaa Azimio la Loliondo ni mwendelezo wa warsha zinazotolewa na UNESCO kwa ajili ya kutoa elimu ya kuwajengea uwezo na kugawa majukumu kwa viongozi wa kimila, wamama mashuhuri, viongozi wa dini, wakunga wa jadi pamoja na waandishi wa habari ili kutekeleza vizuri ufuatiliaji wa afya ya uzazi na malezi bora kwa watoto katika jamii ya Kimaasai.
Utiaji saini wa Azimio la Loliondo ulishuhudiwa na Katibu Tawala Wilaya ya Ngorongoro Bw. Lemuel Kileo, maafisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bw.Herman Mathias na Bi.Rose Haji Mwalimu.
Kongamano hilo la siku mbili lililofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro limeendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
IMG_1636
Katibu wa Baraza la Mila wilayani Ngorongoro, Laanoi Munge (kushoto aliyesimama) akimsomea baadhi ya maboresho ya vipengele vilivyomo ndani ya azimio hilo Ofisa Elimu ya Uzazi na UKIMWI kutoka UNESCO, Mathias Herman (kulia).
IMG_1643
Laigwanan wa kata ya Pinyinyi, Moses Mollel akiwasilisha maboresho ya azimio hilo baada ya kulijadili kabla ya kusaini.
IMG_1676
Ofisa Elimu ya Uzazi na UKIMWI kutoka UNESCO, Mathias Herman akifafanua jambo kwa viongozi hao baada ya kuridhishwa na maboresho ya azimio hilo katika kongamano kubwa la siku mbili lililofanyika katika ofisi za halmashauri ya wilaya Ngorongoro, jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Mkalimani wa kwenye kongamano hilo Mchungaji, Mark Murenga, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kileo, Mwenyekiti wa Baraza la Malaigwanan wilaya ya Ngorongoro, Joseph Oletiripai pamoja na Kiongozi wa Malaiboni wilaya ya Ngorongoro Bw. Sangau Naimodu.
IMG_1692
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka redio ya jamii Loliondo FM nao walikuwepo kuhudhuria tukio hilo la utiaji saini wa azimio la kumlinda mtoto wa kike.
IMG_1698
Baadhi ya maafisa wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro na waandishi wa habari waliokuwepo ukumbini kushuhudia tukio hilo.
IMG_1768
Mwenyekiti wa Baraza la Malaigwanan wilaya ya Ngorongoro, Joseph Oletiripai (kushoto), Kiongozi wa Malaiboni wilaya ya Ngorongoro Bw. Sangau Naimodu (wa pili kushoto) Laigwanan wa kata ya Pinyinyi, Moses Mollel (wa pili kulia) pamoja na Ngaigwanan wa Malambo, Miriam Lembirika wakisaini kwa niaba ya viongozi wengine wa mila wa Wilaya ya Ngorongoro, Azimio la Liliondo.Wanaoshuhudia (waliosimama) ni KatibuTawala wa Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kileo (kulia), Ofisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, Benezeth Bwikizo (wa pili kulia), Mtaalamu wa masuala ya vyombo vya habari vya kijamii na Mkufunzi kutoka UNESCO, Rose Haji Mwalimu (wa tatu kulia) pamoja na Ofisa Elimu ya Uzazi na UKIMWI wa UNESCO, Mathias Herman.
IMG_1772
Walioshuhudia tukio hilo wakipiga makofi baada ya zoezi hilo.
IMG_1701
Baadhi ya viongozi wa kimila na waandishi wa habari wakishuhudia tukio hilo la kusainiwa kwa azimio la kumlinda mtoto wa kike.
IMG_1782
Zoezi la utiaji saini likiendelea kwa kila kiongozi aliyeshiriki kongamano kubwa la siku mbili lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambalo limefanyika katika ofisi za halmashauri ya wilaya Ngorongoro, jijini Arusha.
IMG_1821
Picha ya pamoja baada ya zeozi kukamilika.
SERIKALI YAIPONGEZA JUHUDI ZINAZOFANYWA NA TAASISI YA DORIS MOLLEL FOUNDATION ZA KUSAIDIA WATOTO NJITI!

SERIKALI YAIPONGEZA JUHUDI ZINAZOFANYWA NA TAASISI YA DORIS MOLLEL FOUNDATION ZA KUSAIDIA WATOTO NJITI!

November 18, 2015
DSC_1839
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki akizungumza mbele ya wanahabari, madaktari na baadhi ya akina mama waliokuwa na watoto waliozaliwa kabla ya wakati maarufu kama Njiti (Hawapo pichani). Kushoto ni DoriS Mollel ambaye ni Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF) na wengine ni maafisa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[DAR ES SALAAM] Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongeza juhudi binafsi zinazofanywa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF) katika harakati zake za kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) na mambo ya elimu hapa nchini huku ikiahidi kuendelea kushirikiana nayo kufikia malengp yake.
Kauli hiyo imetolewa mapema leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki wakati wa kupokea vifaa maalum vya kusaidia watoto njiti vilivyotolewa na taasisi hiyo ya Doris Mollel Foundation tukio lililofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jengo la Watoto.
“Tunatambua mashine hizi ni bei kubwa na Serikali pekee yake haina pesa hivyo kwa kusaidiana na wadau kama hivi n faraja sana na tunapongeza juhudi hizi za taasisi ya DMF kwa kujitokeza kusaidia mashine kwa watoto njiti” ameeleza Mkuu wa Mkoa huyo.
Mkuu wa Mkoa huyo aliongeza kuwa, Mashirika mengine yaendelee kujitokeza kusaidia huduma za kijamii ikiwemo vifaa kama taasisi ya Doris Mollel kwani asilimia 100 ya wagonjwa na watu wengine wenye mahitaji katika tiba wanakimbilia Dar es Salaam hasa Hospitali ya Muhimbili.
“Tunaomba tena mukipata nyingine musisite kutiletea hapa maana Mkoa huu unapokea wagonjwa wengi kutoka maeneo mengi ya Tanzania na vifaa vya tiba mara nyingi vinakuwa ni vichache, Huko mikoani wanapewa rufaa waanakuja hapa pia hivyo DMF musisite kuja tena” alimalizia Mkuu wa Mkoa huyo.
Hata hivyo kwa upande wake Mwanzilishi na mtendaji Mkuu wa DMF, Doros Mollel amemweleza Mkuu wa Mkoa Meck Sadik kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali bega kwa bega katika juhudi za kusaidia watoto njiti nchini ikiwemo kutoa elimu, vifaa na usaidizi kwa jamii dhidi ya kukabiliana na watoto njiti nchini.
Katika tukio hilo, Mkuu wa Mkoa alishudia vifaa hivyo na kupokea kutoka DMF sambamba na kutembelea wote ya watoto njiti pamoja na ile ya Kangaroo ambayo wamama wenye watoto njiti wanakuwa wanapatiwa uangalizi maalum dhidi ya watoto wao ikiwemo kupata joto la Mama na baadae alipanda mti maalum mbele ya jengo hilo la Watoto kama kumbukumbu na juhudi za wadau katika kusaidia jamii dhidi ya watoto njiti.
DMF imeweza kusaidia vifaa katika wodi hiyo ya watoto Muhimbili vikiwemo (Suction machines, Oxygen Concentrators na Feeding tubes). Aidha Doris Mollel amebainisha kuwa baada ya hapo wanatarajia kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa kutoa vifaa kama hivyo huku lengo ikiwa ni kufika mikoa yote ya Tanzania.
DSC_1855
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili wakishuhudia tukio hilo maalum la taasisi ya DMF ilipotoa vifaa hivyo katika kitengo cha Jengo la Watoto.
DSC_1865
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadik akipata maelezo juu ya vifaa hivyo vilivyotolewa na Taasisi ya DMF.
DSC_1870
Msimamizi wa wodi ya akina mama wanaopatiwa huduma ya Kangaroo dhidi ya watoto wao ambao walizaliwa njiti, akimpatia maelezo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alipotembelea wodi hiyo leo.
DSC_1924
Picha ya juu na chini Mkuu wa Mkoa wa Dar e Salaam akiwafariji baadi ya wakinamama waliojifungua watoto kabla ya wakati maarufu njiti wakati alipotembelea wodi hiyo ya watoto mapema leo.
DSC_1929
DSC_1939
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akimpatia zawadi ambayo ni jozi ya soksi kwa ajili ya kusaidia watoto njiti kwa mmoja wa wamama waliokuwa katika wodi hiyo ya watoto njiti.
DSC_1873
Keki maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya siku maalum ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati maarufu njiti
DSC_1885
Mtoto Amne Salim (3) ambaye ni njiti akikata keki maalum kwa niaba ya watoto wenzake katika tukio hilo mapema leo.
DSC_1890
DSC_1891
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akimlisha keki mtoto Amne Salim katika tukio hilo.
DSC_1897
Mtoto Amne Salim akimlisha keki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadik katika tukio hilo.
DSC_1954
Baadhi ya akina mama waliokwenye mpango maalum wa kutunza watoto wao waliozaliwa njiti ujulikanao kama Kangaroo wakiwa wodini mapema leo wakati wa ugeni wa DMF na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam walipotembelea wodi hiyo.
DSC_1882
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaamm Meck Sadik akipokea na kukabidhi vifaa maalum kwa ajili ya kusaidia watoto njiti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili vilivyotolewa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation mapema leo.
DSC_1907
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadik akipanda mti maalum baada ya zoezi hilo la Taasisi ya Doris Mollel Foundation kutoa misaada ya vifaa vya watoto njiti.
DSC_1912
DSC_1921
DSC_1918
Shughuli hiyo ya upandaji mti wa kumbukumbu ikiendelea..
DSC_1900
Mama mzazi wa Doris Mollel akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.