KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI,MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA ENEO LENYE MGOGORO LA PORI TENGEFU LA LOLIONDO

March 09, 2017
Msafara wa Magari ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Malisili na Utaalii,yakpita katika maeneo mbalimbali ya Pori Tengefu la Loliono kwa ajili ya kujionea hai halisi ya mgogoro ulioo katika eneo hilo.
Mwenyekii wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi ,Maliasii na Utalii,Atashasta Ndetiye (katikati) akiongozana na wajumbe wengine wa kamati hiyo kutizama vyanzo vya maji vilivyoko katika Pori Tengefu la Loliondo.
Waziri wa Malisili na Utalii ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo,Prof Jumanne Maghembe akiongozana na wataalamu katika ziara ya kamati hiyo.
Mtafiti Mkuu wa Idara ya Ikolojia (TAWIRI) Dkt Edward Khoi akitoa maelezo ya kitaalamu kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Ardhi,Malisili na Utalii wakati wakitembela Pori tengefu la Loliondo.
Baadhi ya wajumbe wa kamato hiyo wakifuatilia maelezo kutoka kwa wataalamu wa Ikolojia na Uhifadhi.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,William Mwakilema akiwaeleza wajumbe w kamati hiyo madhara yatakayojitokea endapo eneo la Pori Tengefu la Loliondo halita hifadhiwa.
Wajumbe wa Kamati ya Maliasili na Utalii,wakitizama eneo linalotajwa kutengenezwa na wafugaji kwa ajili ya kunyweshea maji mifugo yao ndani ya Pori Tengefu la Loliondo.
Eneo linalouiwa na wafugaji unyweshea mifgo yao.
Sehemu ya Mabirik yanayotajwa kutengenezwa na jamii ya wafugaji kwa ajili ya kunywesha mifgo yao.
Mwenyekiti a Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii,Atashsta Ndetiye (kulia) pamoja na Waziri wa Malisili na Utalii,Prof ,Jumanne Maghembe wakitizama eneo ambalo i mapiio ya maji katik Pori Tengefu la Loliondo.
Moja ya Makundi ya Ng'ombe yaliyokutwa na Kamati hiyo katika Pori Tengefu la Loliondo.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakizungumza na mmoja wa wafugaji waliokutwa wakichunga Ngombe ndani ya Pori Tengefu la Loliondo. 
Kamati ilikutana pia na Changamoto ya uboovu wa Miundombinu ya barabara hali iliyolazimu magari kupita kwa tahadhari .
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakitizama moja kati ya vyanzo vy maji vinavyotiririsha maji yake katika mto Gurumeti uliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mbunge wa Jimbo la Sumve ambaye pia ni mjube wa kamati hiyo,Richard Ndasa akizungumza jambo mara baada ya kutizama moja ya vyanzo vya maji vilivyoko katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo.
Sehemu ya Makundi ya Mifugo pamoja na Mashamba yaliyopo katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazinia

WAFANYABIASHARA WA VILEO KATIKA MANISPAA YA UBUNGO WATAKIWA KUWASILISHA MAOMBI YA LESENI KABLA YA MACHI 15, 2017

March 09, 2017

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo anawatangazia wafanyabiashara wote wa vileo kuwa msimu wa kukata leseni za biashara za vileo kwa mujibu wa sheria ya vileo Na 28 ya Mwaka 1964 na marekebisho yake unaanza tarehe 1/04/2017.

Hivyo kila mfanyabiashara anapaswa kuwasilisha maombi ya leseni za vileo katika ofisi ya Biashara Manispaa ya Ubungo zilizopo eneo la Kibamba CCM Kabla ya tarehe 15/03/2017. (Maombi yaambatanishwe na Tax Clearence Certificate na Leseni iliyoisha)

Tigo yatangaza washindi wawili wa shindano la Digital Changemakers, yawazawadia dola 40,000 jijini Dar Es Salaam leo

March 09, 2017
 Mkurugenzi wa Kampuni ya simu za mkononi Tigo, Diego Gutierrez akiongoea na wanahabari. wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya dola elfu 20 za kimarekani kwa kila mmoja kwa washindi wawili wa shindano la Tigo Digital Changemakers leo, Tigo kushirikiana na taasisi ya Reach for change ndio waliondaa shindano hilo.Pembeni Meneja Programu  wa Reach for Change Tanzania Josephine Msambichaka na Meneja Huduma za jamii(CSR) Tigo , Halima Okash.


 Meneja wa Programu wa Reach For Change, Josephine Msambichaka akiongoea na wanahabari. wakati wa hafla ya kukabidhi hundi  kwa washindi wawili wa shindano la Tigo Digital Changemakers.

Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akiongea na wageni waalikwa kwenye hafla ya makabidhiano.


Mshindi wa  shindano la Tigo Digital Changemakers,Sophia Mbega akiongea na wanahabari mara baada kukabidhiwa hundi ya dola za kimarekani elfu 20 jijini Dar Es Salaam leo, Pichani nyuma ni Mshindi wa shindano hilo pia aliyejinyakulia pesa hizo, Nancy Sumari. Jumla ya washindi wawili walipata dola elfu 20 kila mmoja.

MKUU WA WILAYA YA KISARAWE AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE MKOA WA PWANI

March 09, 2017

 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness William Seneda (katikati), akihutubia kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Shule ya Msingi Chanzige wilayani  Kisarawe jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Khamis Dikupatile na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga'alo.
 Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Khamis Dikupatile, akipima shinikizo la damu katika maadhimisho hayo.
 Diwani wa Kata ya Kisarawe, Abel Mudo akipima afya.



 Ofisa Mikopo wa Benki ya Equity, Nelifyage Mbwilo (kulia), akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda (wa pili kushoto), wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya wajasiriamali katika maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga'alo na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Khamis Dikupatile.
 Wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Wilaya ya Kisarawe wakionesha kazi wazifanyazo.
 Wajasiriamali wakiwa na bidhaa zao mbalimbali wanazozalisha.
 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness (katikati), akiserebuka na wanawake katika maadhimisho hayo.
 DC Seneda akiserebuka na wanawake. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Winamwanga Caltural Heritage Association, Mwajuma Motto.
 Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mussa Gama (kulia), akimuelekeza jambo Mkuu wa Wilaya hiyo, Happyness Seneda.


 Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Wadau wa maendeleo kutoka Taasisi ya Jumuiya ya Miradi ya Maendeleo Kisarawe na Ilala(JUMIMAKI) wakiwa kwenye maadhimisho hayo. Katikati ni Katibu wa Hatibu Baruti.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneka (katikati kulia na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga'alo wakiwa katika picha ya pamoja na vijana wa Skauti wakati wa maadhimisho hayo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Ntela Mwampamba (kushoto), akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Madiwani wa Wilaya hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Maadhimisho yakiendelea.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Winamwanga Caltural Heritage Association, Mwajuma Motto akisoma risala kwa niaba ya wadau wa maendeleo wa wilaya hiyo.
Mdau wa maendeleo, Christina Lusian akisoma risala 
mbele ya mgeni rasmi.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga'alo, akihutubia kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Yusta Milinga akizungumzia ukatili wa kijinsia kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Seneda akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 61,550 kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali wilayani humo iliyotolewa na Benki ya NMB.
Wadau wa maendelea wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya hiyo baada ya kukabidhi msaada wa magodoro na vifaa vingine vyenye thamani ya sh.700,000.
Mkurugenzi wa Taasisi ya  Tanzania Kwanza Foundation, Hidaya Chomvi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya baada ya kumkabidhi zawadi.
Brass Bandi ya Magereza ikitumbuiza kwenye maadhimisho hayo.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameziagiza Halmshauri zote za mkoa huo kuhakikisha kuwa zinatenga asilimia tano ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya wanawake.

Agizo hilo lilitolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Shule ya Msingi Chanzige wilayani  humo jana. Ndikilo alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo.

"Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo hazitatekeleza wajibu wahakikishe wanajitahidi kufanya jukumu hilo muhimu kwa maendeleo ya wanawake wa mkoa huo" alisema Seneda.

Alisema katika kuwawezesha wanawake kiuchumi, Serikali imeanzisha Benki ya Wanawake Tanzania, mifuko mbalimbali ukiwemo  mfuko wa maendeleo ya wanawake (WDF) pamoja na kuhamasisha uanzishaji wa Saccos, vikundi vya uzalishaji mali na Vicoba na kwa kupitia fursa zilizopo kuwawezesha wanawake wajasiriamali kupata mikopo yenye masharti nafuu.

Alisema katika mkoa huo kuna jumla ya vikundi vya uzalishaji mali 1, 350 vyenye wanachama 5,411 lengo likiwa ni kumuwezesha mwanamke kushiriki katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi kuanzia ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla.

Seneda akizungumzia wilaya yake alihimiza suala zima la elimu na kuwataka wazazi kuwa mstari wa mbele kusimamia watoto wao na kupiga vita mimba za utotoni na kuwaoza watoto wao.

Alisema serikali haitamvumilia mzazi au mlezi yeyote atakayebainika kuozesha mtoto wake na mtu atakaye mpa mimba mwanafunzi.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)