TAIFA STARS KWENDA AFRIKA KUSINI KESHO

TAIFA STARS KWENDA AFRIKA KUSINI KESHO

July 29, 2014

images
Release No. 132
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Julai 29, 2014
TAIFA STARS KWENDA AFRIKA KUSINI KESHO
Msafara wa watu 27 wa kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kinaondoka kesho (Julai 30 mwaka huu) saa 10 jioni kwa ndege ya Air Tanzania kwenda Afrika Kusini ambapo kitapiga kambi ya siku mbili kabla ya kuingia Maputo kuikabili Msumbiji (Mambas).
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itawasili saa 9 asubuhi kesho (Julai 30 mwaka huu) kwa ndege ya Fastjet, na baadaye jioni kuunganisha safari ya Afrika Kusini.
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itachezwa Agosti 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa uliopo Zimpeto nje kidogo ya Jiji la Maputo.
Msafara huo wa Taifa Stars kwenda Afrika Kusini unajumuisha wachezaji 19 na waliobaki ni maofisa wa Benchi la Ufundi lililo chini ya Kocha Mkuu Mart Nooij kutoka Uholanzi.
Wakati kiungo Mwinyi Kazimoto ametua leo (Julai 29 mwaka huu) nchini kuungana na wenzake, washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wao wataungana na wenzao kesho (Julai 30 mwaka huu) jijini Johannesburg wakitokea Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Wakati huo huo, Serengeti Boys imewasili salama jana (Julai 28 mwaka huu) jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 dhidi Afrika Kusini (Amajimbos).
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili itachezwa Jumamosi, Agosti 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto kuanzia saa 9 kamili mchana kwa saa za Afrika Kusini.
Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyofanyika Julai 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Serengeti Boys inahitaji ushindi kwenye mechi hiyo au aina yoyote ya sare ya mabao ili ifuzu kwa raundi ya tatu.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
WAZIRI WA UCHUKUZI DK.HARRISON MWAKYEMBE AFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA MAKAO MAKUU YA OFISI ZA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (TCAA) KWA AJILI YA KUJIONEA SHUGHULI MBALIMBALI NA KUONGEA NA WAFANYAKAZI ULIOMBATANA NA UZINDUZI WA BODI

WAZIRI WA UCHUKUZI DK.HARRISON MWAKYEMBE AFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA MAKAO MAKUU YA OFISI ZA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (TCAA) KWA AJILI YA KUJIONEA SHUGHULI MBALIMBALI NA KUONGEA NA WAFANYAKAZI ULIOMBATANA NA UZINDUZI WA BODI

July 29, 2014

01
Waziri wa Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (kulia)akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Ndege wa Mamlaka Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Nuis Kasambala alivyokuwa akimuelezea na kumuonyesha jinsi wanavyofanya mitihani kwa wanafunzi wa ndege  wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wanafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA. Waliosimama nyuma ni Kamati ya bodi ya Mamlaka hiyo wakifuatilia kwa makini.   
03
Waziri wa Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (kulia)akisisitiza jambo kwa  Mkurugenzi wa Ndege wa Mamlaka Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Nuis Kasambala alivyokuwa akimuelezea na kumuonyesha jinsi wanavyofanya mitihani kwa wanafunzi wa ndege  wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wanafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA. Waliosimama nyuma ni Kamati ya bodi ya Mamlaka hiyo wakifuatilia kwa makini 04
Waziri wa  Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akikabidhiwa  na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha moja ya tuzo waliyotunukiwa Tanzania na Baraza la Usafiri wa Anga Duniani kwa kutambua mchango wa TCAA.anayeshuhudia katikati ni Makamu Mweneyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka hiyo Weggoro Nyamajeje,  wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wanafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA. 05
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Mbwana Mbwana akitoa shukrani kwa niaba ya bodi na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kwa Waziri wa  Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe, (wa pili kutoka kulia)wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wanafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi Weggoro  Nyamajeje na Kaimu Mkurugenzi wa TCAA ,Charles Chacha. 06
Waziri wa  Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akijibu maswali ya wafanyakazi wa  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wanafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo Mbwana Mbwana, wengine ni  Makamu Mwenyekiti Weggoro Nyamajeje na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Charles Chacha. 07
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wakimsikiliza kwa makini Waziri wa  Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani)  wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wanafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA. 08
09
Mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, akiuliza swali kwa   Waziri wa  Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe  swali (hayupo pichani)  wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wanafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA. 10,
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa anga Tanzania TCAA,(kushoto) wakati alipfanya ziara ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wanafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA.

EID MUBARRAK WDAU WOTE WA MTANDAO HUU

July 29, 2014


Eid Mubarrak!, Mmiliki wa mtandao wa TANGA RAHA BLOG, ndugu Oscar Assenga, anapenda kuwatakia waislamu wote heri ya Sikukuu ya Eid El Fitri.

Tunaungana nanyi kati siku hii muhimu katika kalenda ya Dini ya Kiislamu...Eid El Fitri....Eid Mubarrak!!!