WATEJA wa Tigo
waishio jijini Tanga wanatarajia kunufaika kwa kupata mtandano wa intaneti
wenye kasi kubwa zaidi kufuatia upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya 4GLTE hadi
kufikia kwenye jiji hili lililopo kaskazini mwa Tanzania.
Teknologia ya 4GLTE
ina kasi mara tano zaidi kuliko teknolojia ya 3G inayopatikana nchini kwa sasa.
Hayo yalisemwa na
Mkurugenzi wa Kanda ya Pwani, Goodluck Charles wakati wa mkutano wake na
waandishi wa habari kutangaza uzinduzi wa Upatikanaji wa Teknologia ya 4GLTE
jijini Tanga, uliofanyika kwenye ofisi za Kampuni hiyo Jijini hapa.
Alisema kuwa upanuzi
huo umetokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika majaribio ya awali ya
utoaji wa huduma ya 4G jijini Dar es Salaam kuanzia mapema mwaka huu ambayo ni
kielelezo cha jinsi ambayo Tigo imedhamiria kufanikisha kuleta mabadiliko ya
kidigital katika maisha ya watanzania na pia kuwa katika mstari wa mbele wa
kutumia teknologia ya kisasa na kibunifu nchini Tanzania.
Aidha alisema kuwa
mtandao wa 4G LTE una kazi kubwa zaidi katika kuperuzi na kupakua kwa rahisi
kutoka kwenye mtandano wa intaneti na pia katika kufanya mawasiliano kwa njia
ya Skype kwani huduma hiyo inaharakisha urushwaji wa picha za video na ubora wa
hali ya juu na kufanya mikutano kwa njia ya mtandao.
“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu waisio
Tanga kwamba sasa wanaweza kufurahia huduma bora zaidi za mawasiliano kutoka
Tigo na intaneti yenye kasi zaidi,Tanga ni makao makuu ya taasisi nyingi za
kimataifa ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki na kitovu cha Utalii nchini
“Alisema Goodluck.
…..Tunapenda
kuwatangazia wateja wetu wa Tigo kwamba bei ya vifurushi vyetu vya 4GLTE ni
sawa na bei ya vifurushi vya intaneti vya 3G kwa hivyo mteja haitaji kulipia
zaidi kwa ajili ya kutumia huduma ya 4GLTE na wateja wote wa Tigo 4GLTE
watanufaika na promosheni ,kila watakapoongeza salio la shilingi elfu
moja,atapata MB 500 za bure kama bonasi.
Alisema kuwa uzinduzi
wa upatikanaji wa huduma ya 4GLTE kwa ufanisi jijini Dar es Salaam na Arusha na
miji mingine katika mikoa sita ambapo huduma hiyo itaanza kupatikana hivi
karibuni kuwa ni Dodoma,Morogoro,Moshi
na Mwanza.
Mkurugenzi huyo
alisema kuwa jambo hilo linaifanya Tigo kuwa na mtandao mkubwa wa 4G LTE nchini
Tanzania ambapo lengo lao kuu ni kufanikisha huduma hiyo katika kila kona ya
nchi ifikapo mwaka ujao.