RAIS MAGUFULI ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KATIKA UBALOZI WA UFARANSA NCHINI

RAIS MAGUFULI ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KATIKA UBALOZI WA UFARANSA NCHINI

November 17, 2015

po1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa nchini kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
po2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
po3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Malika Berak Tanzania mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo na kutoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande kufuatia vifo vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
po4
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi huo mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
po5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak mara baada ya kusaini kitabu cha Maombolezo Ubalozini hapo.
………………………………………………………………………………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo vya watu zaidi 130 vilivyotokea November 15, 2015 kutokana na mashambulizi ya ugaidi mjini Paris, Ufaransa. Pamoja na kutia saini kitabu cha maombolezo, Mheshimiwa Dr. Magufuli ametoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande na kumuombea uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu Dokta Magufuli ambaye amepokelewa na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bibi Malika Berak amesema Tanzania imeguswa na vifo hivyo na inaungana na Ufaransa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Aidha Rais Magufuli amewaombea majeruhi wote wa tukio hilo wapone haraka ili waweze kuungan a na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amewasili Mjini Dodoma jioni hii kwa shughuli mbalimbali za kikazi. Mheshimiwa Magufuli amesafiri kwa gari kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na taarifa ya shughuli atakazozifanya mtaarifiwa baadaye.
Imetolewa na; Gerson Msigwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, IKULU November 17, 2015
Tigo yadhamini Tamasha Kubwa la Mtikisiko Mjini Songea

Tigo yadhamini Tamasha Kubwa la Mtikisiko Mjini Songea

November 17, 2015

ti1
Wasanii chipukizi wa Songea, Mary na Mwana King Nizo wakitumbuiza kwenye Tamasha la Mtikisiko lililofanyika uwanja wa Majimaji Mjini Songea . Tamasha liliodhmaniwa na Tigo lenye lengo la kupiga vita maambukizi ya virusi vya Ukimwi
TI2
Kikundi cha Ruvuma Kings toka songea kikitumbuiza kwenye Tamasha la Mtikisiko lililofanyika uwanja wa Majimaji Mjini Songea . Tamasha hilo liliodhmaniwa na Tigo lenye lengo la kupiga vita maambukizi ya virusi vya Ukimwi
TI3
 Kikundi cha Ruvuma Kings toka songea kikitumbuiza kwenye Tamasha la Mtikisiko lililofanyika uwanja wa Majimaji Mjini Songea . Tamasha hilo liliodhmaniwa na Tigo lenye lengo la kupiga vita maambukizi ya virusi vya Ukimwi
TI4
Wacheza shoo wa bendi ya FM Academia wakifanya yao kwenye Tamasha la Mtikisiko lililofanyika uwanja wa Majimaji Mjini Songea . Tamasha hilo liliodhmaniwa na Tigo lenye lengo la kupiga vita maambukizi ya virusi vya Ukimwi
TI5
Mc Edo wa Ebony fm akifanya yake kwenye Tamasha la Mtikisiko liliofanyika mwishoni mwa wiki uwanja wa Majimaji mjini Songea. Tigo ndio wadhaminiwa tamasha hilo.
TI6
Kiongozi wa bendi ya Fm Academia, Nyoshi El Saadat akiwaongoza wacheza shoo wake kwenye Tamasha la Mtikisiko lililofanyika uwanja wa Majimaji Mjini Songea . Tamasha hilo liliodhmaniwa na Tigo lenye lengo la kupiga vita maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU).
TI7
Sehemu ya wateja wa tigo wakipata burudani  kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea.

KOBE 201 WALIOKUWA WAKISAFIRSHWA NJE YA NCHI WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA J.K NYERERE

November 17, 2015

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.
Adelhelm Meru akikagua mabegi matano yenye Kobe 201 yaliyokamatwa usiku wa
kuamkia leo na askari wanyamapori kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na
usalama katika uwanja wa Kimataifa wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.  
 
Watuhumiwa
hao wa usafirishaji wa wanyamapori wametajwa kuwa ni David Mungi mkazi wa
Muheza Mkoani Tanga na Mohammed Suleiman (43) mkazi wa Zanzibar ambao katika
tukio hilo walishafanikiwa kupita kwenye mitambo ya ukaguzi lakini mbwa maalum
(sniffer dogs) wakasaidia kugundua uhalifu huo. Kwa pamoja watuhumiwa hao
walikamatwa na tiketi za kusafiria kuelekea nchini Malaysia. 
 
Kobe wapatao 201 waliokamatwa na askari wanyamapori kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutumia mbwa maalum (sniffer dogs).   
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Dorina Makaya kulia na Mmoja wa Askari wanyamapori wakiangalia kobe 103 waliotelekezwa eneo la Tabata hivi karibuni
baada wahalifu waliohusika kuhofia kukamatwa na vyombo vya dola. 
(Picha na Hamza Temba – Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii)

SIKU YA WATOTO NJITI

November 17, 2015

 Mwanzilishi wa Mfuko wa Doris Mollel, Doris Mollel akizungumza katika kilele cha maazimisho ya siku ya watoto waliozaliwa kabla ya siku (njiti) katika mkutano ambao umefanyika leo kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Kulia ni mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akizungumza kwenye maadhimisho hayo leo.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha akifuatilia mkutano huo leo pamoja na wauguzi waandamizi wa hospitali hiyo.
 Mmoja wa kinamama akiwa na mtoto wake ambaye alizaliwa kabla ya kutimiza siku akishiriki maadhimisho hay oleo katika hospitali hiyo.
 Mashine iliyotolewa kwa ajili ya kuwatunza watoto wanaozaliwa kabla ya muda. Mashine hiyo imetolewa leo na mfuko wa Doris Mollel kwa ajili ya kutunza watoto hao.
 Mmoja wa kinamama, Lipina Lyimo akizungumza katika kilele cha maazimisho ya siku ya watoto waliozaliwa kabla ya siku (njiti). Katika mkutano na waandishi wa habari Mama Lyimo amesema alijifungua mtoto kabla ya kutimiza muda na kwamba madaktari na wauguzi walimwelekeza jinsi ya kumtunza mtoto wake, Emmanuel Mgumba hadi amekuwa mkubwa na kuwa na afya bora.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akiwa amembeba mtoto, Emmanuel Mgumba  ambaye alizaliwa kabla siku. Mama wa mtoto huyo Lipina Lyimo ameleza jinsi alivyopewa huduma nzuri na wauguzi na madaktari wa ‘Huduma ya Mama Kangaroo’ baada ya kujifungua mtoto kabla ya muda (njiti).
MKURUGENZI WA TUME YA UCHAGUZI ATANGAZA MAJINA NA MADIWANI WA VITI MAALUM

MKURUGENZI WA TUME YA UCHAGUZI ATANGAZA MAJINA NA MADIWANI WA VITI MAALUM

November 17, 2015

kai1
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu Ramadhan Kailima akitangaza majina ya Madiwani wa Viti Maalum walioteuliwa na tume ya uchaguzi kutoka vyamba mbalimbali vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu nchini kote  kutokana na idadi ya ushindi wa viti vya wabunge na madiwani kwa Chama husika.
Bw. Kailima ametanganza majina hayo wakati alipokutana na waandishi wa habari leo kwenye ofisi za Tume hiyo zilizopo jengo la Posta mkabala na Wizara ya Mambo ya Ndani.
…………………………………………………………………………..
NA SHAMIMU NYAKI- MAELEZO
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania ( NEC) leo imetangaza  majina ya Madiwani wa viti maalum walioteuliwa na vyama vyao vya siasa kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa  habari katika ofisi za Tume hiyo, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Bw. Ramadhani Kailima amesema jumla ya viti maalum vilivyopo ni 1407 kutoka Kata 3923 cha Uchaguzi, ambapo viti 1393 ndivyo vilivyogawiwa kwa vyama vya siasa vilivyoshiriki Uchaguzi na kutimiza vigezo vya kupata Madiwani wa viti maalum.
Aidha katika mgawanyo huo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepata viti 1,022 kikifatiwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) viti 280 huku Chama Cha Wananchi CUF kikipata viti 79,ACT Wazalendo na NCCR-Mageuzi wakipata viti 6 kwa kila chama.
Ameongeza kuwa idadi kamili ya viti maalum  itakamilika pale Uchaguzi katika Kata ambazo hazikufanya uchaguzi kukamilika  na pia ameviagiza vyama vya siasa kukamilisha uwasilishaji wa majina ya waliowateuwa kuwakilisha Kata zao katika Uchaguzi Mkuu uliopita  ili waweze kusajiliwa.
“ Waandishi muache malumbano ya mambo ya vyama vya siasa bali muhimize wananchi kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi unaoendelea nchini ili kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba” alisema Bw Kailima.
Uchaguzi kwa majimbo ambayo hayakuweza kuwapata wawakilishi wao yanatarajiwa kufanya uchaguzi hivi karibuni. Majimbo hayo  ni Lushoto, na  Ulanga Mashariki ambao utafanyika tarehe 22 Novemba,mengine ni Ludewa na Masasi mjini utakaofanyika tarehe 20 Desemba na jimbo la Kijitoupele huko Zanzibar utafanyika hapo baadae.
Serikali Kuboresha Huduma ya Maji kwa Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

Serikali Kuboresha Huduma ya Maji kwa Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

November 17, 2015

index 
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Maji Bw. Athumani Sharif akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mikakati ya Serikali kutatua tatizo la upatikanaji wa maji jijini Dar es Salaam mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa. (Picha na Fatma Salum.)
…………………………………………………………………………………………..
Na. Georgina Misama – Maelezo Serikali inatarajia kuzalisha maji lita milioni 270 kwa siku baada ya kukamilika kwa mradi wa upanuzi wa Chanzo cha Maji cha Ruvu Chini na upanuzi wa mtambo wa kusafishia maji. Mradi huo unaotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Kimarekani la Millenium Challenge Co-operation umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 66.24 na unatarajiwa kukamilika wakati wowote baada ya kukamilika kwa kazi ya kulaza bomba linalosafirisha maji toka Ruvu chini kuja Jijini Dar es Salaam. Akiongea na waandishi wa habari, leo Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Maji, Bw. Shariff Athumani amesema kwamba mradi wa upanuzi wa mtambo wa ujenzi wa bomba la Ruvu Chini utapunguza kero ya maji kwa wakazi wote wanaotumia maji kutoka Ruvu Chini. Akiyataja maeneo yatakayofaidika na kukamilika kwa mradi huo ni pamoja na Bagamoyo na vitongoji vyake, Bunju, Mabwepande, Boko, Tegeta Kunduchi na Mbezi Beach. Maeneo mengine ni pamoja na Mbezi Juu, Salasala, Kawe, Makongo, Chuo Kikuu, Mikocheni, Msasani, Masaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Sinza, Manzese, Ubungo, Mabibo, Kigogo, Buguruni, Ilala, Kurasini, Bandarini na maeneo yote ya katikati ya jiji la Dar es Salaam.

NAMNA MBUNGE MTEULE WA JIMBO LA TANGA,MUSSA MBARUKU ALIVYOFANYA ZIARA KWENYE MAENEO YALIYOAPATWA MA MAFURIKO YA MVUA

November 17, 2015



MBUNGE Mteule wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku amewataka watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kuacha kukaa ofisini badala yake waende kwenye maeneo ya wananchi waliokumbana na mafuriko kutokana na mvua zinazonyesha juzi jijini Tanga na kusababisha maji kutuama katika makazi yao.

Mbaruku alitoa wito huo jana wakati alipofanya ziara ya kushtukiza
katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa iliyonjesha hivi karibuni jijini Tanga na kuathiri baadhi ya maeneo yalisiyokuwa na miundombinu imara ya kupitisha maji.

 
Maeneo ambayo alitembelea ni Kwanjeka, Shule ya Msingi Mnyanjani na eneo la Jengo la Hospitali la Kata ya Mnyanjani na shule ya Msingi Magaoni Kata ya Magaoni ambapo katika ziara hiyo alibaini kuwepo changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la kutokuwepo miundombinu imara inayosababisha maji kujaa maeneo ya watu nyakati za mvua.
 
Alisema kuwa kimsingi watendaji wa halmashauri hawawezi kuendelea kukaa ofisini wakati wananchi wa maeneo hayo wanateseka na tatizo la maj kujaa kwenye maeneo yao bila kupatiwa ufumbuzi wa kina hali iliyopelekea kushindwa kutambua wafanye nini.
 
Aidha akiwa kwenye eneo lililoathirikana mafuriko hayo alijaribu
kuwasiliana na Mhandisi wa Jiji la Tanga ambapo alimtaka kufika kwenye maeneo yote yaliyoathirika na tatizo hilo ili kuangalia namna ya kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.

  “Hali hii sio nzuri kabisa kwa sababu ikiendelea hivi bila kuwepo
kwa utatuzi wake wananchi wanaweza kukumbana na magonjwa mbalimbali ya milipuko ikiwemo Kipindupindu na mengineyo hivyo niwatake watendaji wa Halmashauri hasa ofisi ya Mhandisi wa Jiji la Tanga kuhakikisha wanalishughulikia tatizo hili haraka “Alisema Mbunge huyo.

Aliongeza kuwa afya za wananchi ni muhimu sana kwa ajili ya ukuaji wa maendeleo yao ya kila siku na kuchangia ukuaji wa uchumi hivyo ni muhimu wao kuweza kuwekewa miundombinu imara itakayowezesha maji yanayofika kwenye maeneo yao nyakati za mvua yaweze kupita kuelekea baharini ili kuondoa adha hiyo kwao.

Hata hivyo alisema suala kubwa atakalokwenda kulifanyia kazi ni
kuhakikisha maeneo hayo yanayoathiriki na tatizo la kuwepo kwa
mafuriko mara kwa mara nyakati za mvua atahakikisha anaweka
miundombinu imara kwa kujenga mifereji itakayoweza kupitisha maji yatakayoweza kuungana na mingine kwa ajili ya kupeleka maji hayo baharini.

 
Akiwa shule ya msingi Mnyanjani alibaini kuwepo kwa changamoto kubwa ya wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo hasa kipindi cha mvua kubwa zinapokuwa zikinyesha kutokana na kuwepo mrefeji mkubwa ambao unapofurika maji yake huwa ni hatari kwa wanafunzi wanaosoma shule hiyo.  

Akizungumza wakati alipomkaribisha Mbunge huyo alipoingia shuleni hapo,Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Edna Sariko alimueleza mbunge huyo kuwa tatizo la kutokuwepo mifereji kwenye maeneo hayo kumesababisha maji kujaa kwenye daraja lililopo karibu na eneo la shule hiyo na kusababisha wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo pindi mvua zinapokuwa zikinyesha.
 
Hata hivyo Mbunge huyo alihaidia kuzichukua changamoto hizo na kwenda kuzifanyia kazi kwa upana ili walimu na wanafunzi waweze kuondokana na kero hiyo ambayo imekuwa ikimwamisha juhudi za kuinua kiwango cha elimu shuleni hapo.

Mashindano ya Uvuvi ya Wazi Slipway yaliyodhaminiwa na Tigo yafana

November 17, 2015
Wasimamizi wa shindano la wazi la uvuvi la Slipway wakipima mmoja kati ya samaki walioshindanishwa kwenye shindano hilo lililodhaminiwa na Tigo jana


Sehemu ya muonekano ambapo mashabiki walikuwa wakisubiria wavuvi kutoka baharini.



Washindi wa kwanza shindano  la wazi la uvuvi Slipway ambao walijishindia mashine ya Yamaha, kutoka kushoto,  Akida Hamad, Ali Mwinshehe na simon Aloyce wakiwa na zawadi yao, shindano hilo lilidhaminiwa na Tigo.


Washindi wa pili shindano  la wazi la uvuvi Slipway ambao walijishindia solar power, kutoka kushoto,  Stamili Seleman na Jumaa Halfan wakiwa na zawadi yao, shindano hilo lilidhaminiwa na Tigo.


Sehemu ya wateja wa Tigo wakipata huduma toka kwa watoa huduma wa Tigo ikiwa ni sehemu mojawapo ya  huduma zilizokuwa zinapatikana kwenye shindano hilo.
Sehemu ya wateja wa Tigo wakipata huduma toka kwa watoa huduma wa Tigo ikiwa ni sehemu mojawapo ya  huduma zilizokuwa zinapatikana kwenye shindano hilo.

photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"
Kampuni ya LETSHEGO/Faidika yapata asilimia 75 ya hisa katika benki ya Advans Tanzania

Kampuni ya LETSHEGO/Faidika yapata asilimia 75 ya hisa katika benki ya Advans Tanzania

November 17, 2015

DSC_1794
Mtendaji Mkuu wa Afrika Mashariki wa kampuni ya Letshego, Bwana Tom Kocsis akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho mpya wa kununua hisa asilimia 75 za benki ya Advans Tanzania. wengine ni maafisa waandamizi wa kampuni hiyo (Picha zote na Andrew Chale).

Na Andrew Chale, Modewjiblog

Kampuni ya LETSHEGO Holding Limited yenye makao yake makuu nchini Botswana ambayo kwa Tanzania ikijulikana kama taasisi ya Mikopo ya Faidika, imetangaz kupata asilimia 75 ya hisa kutoka katika benki ya Advans ya Tanzania kwa kununua hisa moya kwa shilingi Bilioni 15.5 ambazo ni sawa na dola za Kimarekani Milioni 7.

Wakizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema jana jijini Dar es Salaam, viongozi wakuu wa Faidika na Advans Tanzania wamebainisha kuwa sasa huduma za kifedha nchini zimeongezeka maradufu hivyo ni fursa za kipekee kwa watanzania wakiwemo wajasiriamali kujitokeza kwa wingi kuchangamkia huduma katika benki hiyo ya Advans.

"Kufanikiwa kwa Faidika, kunaongeza uwekaji wa akiba, malipo, mikopo ya biashara ambayo ni moja ya mikakati yetu kwa wateja wetu. Hii pia itaruhusu benki ya Advans kutoa mchango mkubwa kwa Serikali ya Tanzania" ameeleza Mkurugenzi Mkuu wa Letshego Group, Chris Low katika tukio hilo.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa, Benki kuu ya Tanzania (BOT) imeipatia kibali taasisi hiyo ya Faidika kuwa wakala wa benki ya Advans wa kutoa huduma za kibenki kwa niaba ya benki hiyo, katika vituo takribani 105.

Hata hivyo Letshego inaamini kuwa mafanikio hayo ni ishara tosha ya kutoa huduma bora kwa watu wote ikiwemo wale wa kipato cha chini, kati katika jamii ambao kihistoria hawajaweza kupata huduma stahiki katika benki za biashara hivyo mfumo mzuri wa kuwezesha jamii kupata huduma za kifedha, Letshego imekuja wakati muafaka wa kusaidia Serikali kuinua uchumi.

Letshego/Faidika kwa Tanzania inatoa huduma zaidi ya Watanzania 44,000 kupitia taasisi yake hiyo ya mikopo ya Faidika huku bidhaa na huduma zake pia zikipatikana kupitia mitandao wenye matawi zaidi ya 105 na ofisi za Satelaiti huku ikiwa na timu ya maafisa mauzo wapatao 230.
DSC_1778
Mkurugenzi Mtendaji wa Advans Tanzania, Bwana Tanguy Gravot (wa kwanza kulia) akizungumza kwenye mkutano mkutano huo. Wengine ni maafisa kutoka kampuni ya Letshego ambao wamenunua hisa asilimia 75 kwa benki hiyo ya Advans Tanzania.

Kwa upande wao benki ya Advans Tanzania wamepongeza kampuni ya Letshego kuwa mbia mkuu wa benki hiyo kwa njia ya uuzwaji wa hisa. Kwa hatua hiyo Letshego atakuwa mwanahisa mkuu huku wale wanahisa waanzilishi wa benki hiyo wakiwemo Advans SA na FMO watabaki kuwa wanahisa wadogo wa kampuni.

"Umoja ulioundwa kati ya kampuni hizi mbili utaiwezesha benki ya Advans Tanzania kutoa huduma zilizo bora kwa wateja wote wakiwemo wale wadogo, wa kati na wakubwa kwa maeneo yote huku pia kuongeza wigo wa kijiografia za huduma." alieleza Mkurugenzi Mtendaji wa Advans SA, Bw. Claude Falgon.

Kwa hatua hiyo, Advans inaamini kuwa wajasiriamali waadogo na wa kati ni wakati wa kuchangamkia fursa zaidi katika benki hiyo.

Advans ya Afrika Kusini (Advans SA) ni kampuni iliyoundwa tokea mwaka 2005 na Developement Finance 9Horus) pamoja na Eid,KfW, FMO, CDC Group plc, AFD group na IFC huku shughuli yake kubwa ikiwa ni kutengeneza mtandao wa taasisi ndogo ndogo za kifedha (MFIs) katika nchi zinazoendelea na zinazoinukia ilikutoa huduma za kifedha kwa wajasiliamali wadogo na wa kati.

Mtandao wa Advans umesambaa karibu dunia nzima ambapo pia waweza kutembelea mtandao wa : www.advansgroup.com
DSC_1807
Mkurugenzi Mkuu wa Letshego Group, Chris Low (katikati) akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati wa shughuli hiyo ya kutangaza kuingia ubia na benki ya Advans Tanzania.
DSC_1801
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia shughuli hiyo.
DSC_1826
Mmoja wa wajumbe wa Bodi wa Taasisi ya mikopo nchini ya Faidika, Dk.Ellen Otaru Okoedion akielezea fursa za mikopo inayotolewa na Faidika huku akitumia wasaha huo kuwaomba wajasiriamali kujitokeza kwa wingi kuchangamkia huduma za kibenki na mikopo zinazotolewa na Faidika pamoja na benki ya Advans Tanzania.
TFF YATANGAZA TENDA YA MSHAURI WA ELEKTRONIKI

TFF YATANGAZA TENDA YA MSHAURI WA ELEKTRONIKI

November 17, 2015
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), kwa kushirikiana na mzabuni wa tenda ya elektroniki benki ya CRDB, leo limetangaza tenda ya kumsaka mshauri wa mfumo wa Elektroniki (Consultant) kwa ajili ya  kupitia mapungufu yaliyopo katika mfumo wa uuzaji tiketi wa elektroniki katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania.

TFF imetangaza tenda hiyo ili kumpata mshauri wa mfumo huo wa tiketi za elektroniki, ambao ulisamishwa na serikali mapema mwaka huu mwezi Aprili.

Maombi ya tenda yawasilishwe katika ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam, kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 10 jioni siku za kazi Jumatatu mpaka Ijumaa.

Gharama ya fomu ya kuombea tenda ni shilingi laki moja (100,000), na mwisho wa maombi ni Disemba 17, 2015.
STARS VS ALGERIA LEO BILDA

STARS VS ALGERIA LEO BILDA

November 17, 2015
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager leo usiku saa 1:15 kwa saa za Algeria, (sawa na saa 3:15 kwa saa za Afrika Mashariki) itashuka dimbani kuwakabili wenyeji Algeria katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Stars inashuka dimbani kusaka ushindi katika mchezo wa leo, utakaoipelekea kuweza kusonga mbele kwa hatua ya makundi, kufuatia kutoka sare y amabao 2-2 katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.
Jana jioni Taifa Stars ilifanya mazoezi jioni katika uwanja wa Mustapher Tchaker uliopo mjini Bilda utakaotumika kwa mchezo wa leo, ambapo wachezaji wote wapo katika hali nzuri na morali ni ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo.
Akiongea kuelekea kwenye mchezo wa leo, kocha mkuu wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa amesema anashukru vijana wake wote wapo salama, hakuna majeruhi kikubwa anachosubiri ni jioni kushuka uwanjani kusaka ushindi katika mchezo huo.
Mapema leo asubuhi, benchi la ufundi la Taifa Stars pamoja na wachezaji wake, wamefanya matembezi ya miguu kwa dakika 30 katika viunga vya mji wa Bilda, kuweka miili tayari kwa mechi ya jioni dhdi ya Mbweha wa Jangwani.

JIJI LA MBEYA HATARI KUKUMBWA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

November 17, 2015

Wafanyabiashara ndogo ndogo katika eneo la Makunguru jijini Mbeya wakiendelea na shughuli zao kama kawaida .

Na Mwandishi wetu,Mbeya

Halmashauri ya jiji la Mbeya limewataka wafanyabiashara ndogondogo hususani wa chakula  kujijengea tabia ya kuchoma taka nyakati za jioni mara wamalizapo kuuza biashara zao na si kusubili gari ya taka kuja kuzoa.

Aidha imewataka  wakazi hao kuondokana na fikra duni  ya kuamini kuwa kazi ya uzoaji wa taka na kusafisha mazingira ni ya halmashauri ya Jiji na sio mali ya mtu.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dkt. Samweli Lazaro, amesema, wananchi wanatakiwa kujenga tabia ya usafi na sio kusubili kupigizana kelele na serikali kwa kuwahimiza kufanya usafi kwani adui mkubwa wa afya ni uchafu hivyo kila mmoja anapaswa kuwa mlinzi wa mwezake katika kutunza mazingira.

Hali hiyo imesababisha kuwepo kwa malimbikizo mengi ya taka  kwenye sehemu zisizorasmi  ndani ya JIji la Mbeya na kupelekea jiji hilo kuwa chafu hususani katika maeneo ya  sokoni.

Amesema, hivi sasa halmashauri ilianzisha mpango wa uzoaji wa taka barabarani ambapo mpango huo umeonekana  kupokelewa na wananchi kwa asilimia 100 changamoto inakuja kwa upande wa halmashauri kuonekana kuzidiwa kutokana na ukosefu wa vitendea kazi.

“Halmashauri ilianzisha zoezi la kupitia taka zinazozalishwa na wananchi ambazo huziweka barabarani na magari yanapitia lakini mapango huu umeonekana kuzaa matunda kwa jamii kuupokea lakini tatizo ni uhaba wa vitendea kazi,”alisema.

Alisema, ili zoezi hilo lifanikiwe halmashauri inahitaji zaidi ya gari saba za ubebaji taka na kontena 80 lakini mpaka sasa magari yaliyopo ni manne na kontena 30 .

Hata hivyo kutokana na changamoto hiyo, Lazaro anawasihi wananchi kujenga tabia ya kuweka mazingira safi hasa kipindi hiki cha mvua kwani ndipo magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu yanapoibuka na kusababisha vifo vya watu.

Mwisho.

JAMIIMOJABLOG MBEYA
Vijana nchini kuendelea kunufaika na Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha Dar es Salaam (YEID)

Vijana nchini kuendelea kunufaika na Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha Dar es Salaam (YEID)

November 17, 2015

z2
Afisa mwelekezi wa wa Programu ya kukuza Ajira zenye staha kwa Vijana Dar es Salaam,kupitia Elimu ya Biashara na Ujasiriamali. Bi. Emiliana Muchu akiwasilisha mada kuhusu mafanikio ya program hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Kamati inayokutanisha wadau wa program hiyo.Picha na Frank Shija, WHVUM
z3
Meneja wa Programu ya kukuza Ajira zenye staha kwa Vijana Dar es Salaam Bibi. Maria Fustiniano ( wapili kutoka kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kamati ya wadau wa program hiyo uliofanyika mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.
z4
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya True Maisha Bw. Erick Crispin akiwasilisha mada namna taasisi yake inavyofanya shughuli zake katika kutoa mafunzo kwa Vijana hivi karibuni jijini Dar es Salaam

BREAKING NYUZZZ.......: JOB NDUGAI NDIYE SPIKA MPYA WA BUNGE LA 11 LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

November 17, 2015
Hatimaye Job Yustino Ndugai CCM amechaguliwa kuwa Spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchaguliwa kwa kura 254 sawa na
asilimia 70% ya kura zilizopigwa akifuatiwa na mgombea wa CHADEMA Goodluck Ole Medeye ambaye amepata kura 109.


Hata hivyo wagombea   hao ambao walikuwa 7 kati ya 8 wameweza kutoa shukrani na pongezi kwa  Ndugai wakisema anastahili na ndio maana akachaguliwa na kumtaka aongoze
vyema bunge hilo.


Job Ndugai ameibuka mshindi wa kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupata kura 254 sawa na asilimia 70 ya kura zote ambapo jumla ya kura zilizopigwa ni 365

Matokeo ya kura za Spika.

A: Job Ndugai (CCM)- 254
B: Goodluck Ole Medeye (CHADEMA) - 109
C: Hashimu Rungwe (CHAUMA)- 0
D: Peter Sarungi (AFP) -0
E: Dkt Godfrey Malisa (CCK)- 0
F: Richard Lymo (T.L.P) -0
G: Robert Kisinini (DP) -0


Kura zilizoharibika ni 2

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YAZINDUA CHAPA MPYA LIVE IT, LOVE IT KUELEKEA MSIMU WA SIKUKUU YA KRISMAS

November 17, 2015

 Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyanja, akizungumza na waandishi wa habari wakati akimkaribisha Meneja Mkuu wa Tigo kuzungumza na wanahabari.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez  (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa uzinduzi wa  chapa mpya yenye kauli mbinu ya ‘Live it, love it’ itakayoimarisha nafasi ya mbunifu anayeongoza kwa ubunifu wa kidigitali nchini. Kulia ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez, akionesha simu mpya zenye menyu ya Kiswahili wakati wa mkutano huo.
 Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Masoko wa Tigo, Olivier Prentout.
 Mkurugenzi wa Huduma za Masoko wa Tigo, Olivier Prentout (kulia), akizungumza na wanahabari kuhusu huduma mpya za Tigo kuelekea Sikukuu ya Krismas.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.
……………………………………………………………………….
Mwandishi Wetu
 
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Tigo, imezindua chapa mpya yenye kauli mbinu ya ‘Live it, love it’ itakayoimarisha nafasi ya mbunifu anayeongoza kwa ubunifu wa kidigitali nchini.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chapa hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Diego Gutierrez alisema chapa hiyo mpya itahakikisha inakuwa rafiki nzuri kwa Watanzania kuziona ndoto zao na kuzifikia.
 
Alisema kwa hapa nchini kama zilivyo nchi zingine intaneti imekuwa  nisehemu muhimu ya maisha ya watu kutokana na huduma za kidigitali kutumika katika biashara, elimu, kwa familia na kwa kujiburudisha.
 
“Tumejikita kwenye utoaji huduma katika matarajio hayo na rekodi ya mwenendo wa ubunifu wetu unatupa imani kuwa tunafanikiwa,” alisema Gutierrez.
 
Katika hatua nyingine, kampuni hiyo imetoa ofa kwa wateja wake  kwa kuuza simu ya smartphone ya aina ya Tecno Y3 kwa sh. 99,000 kuelekea msimu wa Sikukuu ya Kristmass na Mwaka Mpya.
 
 
Gutierrez alisema simu hiyo itakuwa na ‘menu’ ya Kiswahili itakayomuwezesha mteja kuitumia kwa urahisi huku ikiwa na kamera mbele na nyuma, betri linalokaa kwa muda mrefu na vitu vingine.