CCM YARUSHA JESHI LA ANGA,MWIGULU AONGOOZA KIKOSI...WAIMARISHA USHINDI WA KISHINDO MAJIMBO YA NZEGA

CCM YARUSHA JESHI LA ANGA,MWIGULU AONGOOZA KIKOSI...WAIMARISHA USHINDI WA KISHINDO MAJIMBO YA NZEGA

September 26, 2015
Chama Cha Mapinduzi hii leo kimerusha Helcopta yake ya kwanza kwenye kila pembe ya Nchi kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu kwenye nafasi zote za Udiwani,Ubunge na Urais.Kazi ya kupasua anga hilo linaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Ushindi Ndg.Mwigulu Nchemba ambaye katika Jimbo lake la Iramba kwa asilimia 98 amejihakikishia Ushindi wa kishindo hapo Tar.25.10.2015
Vijana Imara wa Chama cha Mapinduzi Fieldmarshall Mwigulu Nchemba na Hamis Kigwangalla wakipiga Push-Up kuonesha sapoti kwa Mgombea wao J.Pombe Magufuli aliyefanya tukio hilo siku si nyingi kwenye Jukwaa la Kampeni.
Picha na Sanga Festo Jr.

Mwigulu Nchemba ambaye ni Mjumbe wa kamati ya CCM ya Ushindi na Mgombea Ubunge Jimbo la Nzega Vijijini Ndg.Kigwangalla akiwasili kwenye Ufunguzi wa kampeni za Ubunge Jimbo la Nzega Mjini hii leo.Mjumbe wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi Comrade Mwigulu NChemba ambaye hii leo ameanza safari za Anga kwa Anga kusaka kura Nchi nzima,Hapa akizungumza na Wananchi wa Nzega namna CCM ilivyosimamisha Mgombea Bora wa Urais ambaye sifa yake kuwa ni KAZI na rafiki yake Mkubwa ni TANZNAIA.Mwigulu amesema,Uchaguzi wa mwaka 2015 ni mwepesi sana kwa chama cha Mapinduzi kwakuwa wagombea wote ni zao la CCM na wanawajua vizuri.Pia wagombea wengine wa vyama vya Upinzani wanazungukwa na makundi ya Ubadhilifu wa mali za Umma wakati Magufuli yeye anazungukwa na Watu wa kazi.
Hivyo Uchaguzi huu ni DILI vs KAZI,Hivyo kazi mbayo ni J.Pombe Magufuli itashinda kwa kishindo.
 Mbunge Mtarajiwa wa Nzega Mjini Mh.Bashe akizungumza na Wananchi wake wakati wa Ufunguzi wa kampeni kwa Jimbo la Nzega Mjini hii leo.Bashe amewaomba Wananzega kumpatia Ridhaa ya kuwambunge wa Jimbo hilo ili aweze kusimamia vyema shughuli za Maendeleo kama Uimarishaji wa Huduma za Afya kwa Hospitali ya Nzega,Kusimamia haki za Bodaboda na Mamantilie wa Nzega,Kusimamia shughuli za Halmashauri ya Mji wa Nzega kwa Ufanisi.Pia amesisitiza yeye ni TEAM MAGUFULI na anaamini Maendeleo ya kweli na ya kasi yataletwa na Magufuli kwa awamu hii ya tano ya Uongozi wa Taifa letu.Wananchi wakifurahia jambo kutoka kwa Mbunge wao mtarajiwa Mh.Hussein Bashe.Mbunge Mtarajiwa wa Chama cha Mapinduzi Jimbo jipya la Nzega Vijijini Mh.Hamis Kigwangala akisalimiana na Wananchi wa Nzega mjini alipokwenda kusapoti Ufunguzi wa kampeni za Mgombea Jirani Ndg.Hussein Bashe."Ndani ya CCM ni Raha na
Furaha"Kigwangalla na Bashe wakiwasalimia Wananchi wa Nzega Mjini ikiwa ni ishara ya Wazi kuwa CCM ni Moja na Wamejipanga kwa Ushindi.Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taiga Ndg.Mwigulu Nchemba na Comrade Emmanuel Nchimbi wakiteta jambo wakati wa Ufunguzi wa kampeni Jimbo la Nzega Mjini hii leo;.Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg.Emmanuel Nchimbi akizungumza na Wananchi wa Nzega Mjini wakat wa Ufunguzi wa Kampeni za Ubunge kwa jimbo hilo,Nchimbi amewasisitiza wananchi wa Nzega kuendelea kuwa na Imani na Chama cha Mapinduzi kwakua ndio chama pekee chenye Mgombea anayeweza kupambana na kasi ya maendeleo tunayoyahitaji.Pia amesisitiza kuwa CCM haijafanya kosa kumsimamisha Mh.J.Pombe Magufuli kwenye nafasi ya Urais,Chama kilizingatia Ubora wa wagombea na hatimaye Magufuli alikuwa Bora kupeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi mkuu ngazi ya Urais.
Mbali na hilo Nchimbi amewaomba Wananchi kufanya siasa za kistaarabu na kujitokeza kwa wingi siku ya Tar.25.10.2015 kwenye vituo vya kupiga kura wakiwa na vitambulisho vyao.Wananchi wakifuatilia MkutanoMwigulu,Nchimbi na Bashe wakisuka Mkakati wa kuhamasisha Wananchi kujitokeza kuipigia Kura CCM siku ya Uchaguzi.Comrade Emmanuel Nchimbi na Mwigulu Nchemba wakimnadi Mbunge mtarajiwa wa Nzega ndg Bashe kwa Wananzega.Wananchi wa Kata ya Ndala Jimbo la Nzega Vijijini wakiwa wamembeba Mbunge wao mtarajiwa Ndg.Hamis Kigwangala hii leo mara baada ya Mkutano wa kuomba kura kwa wananchi ili aweze kushinda nafasi ya Ubunge kwenye Uchaguzi mkuu wa tar 25/10/2015.KIgwangala akiomba Kura kwa Wananchi wa kata ya Ndala.Mwigulu Nchemba na Hamis Kigwangalla wakiagana na Wananchi wa kata ya ndala mara baada ya Mkutano wa kampeni wa chama cha Mapinduzi jimbo la Nzega Vijijini.Wananchi wa kata ya shimbo wakifuatilia Mkutano wa Chama cha Mapinduzi wa kampeni za Ubunge wa Mh.Kigwangalla hii leo kwenye Kata ya Shimbo.Wananchi wa kata ya Shimbo wakionesha Ishara ya kuwa KURA zao zote ni kwa J.Pombe Magufuli,Ubunge kwa Kigwangalla na Madiwani wa CCM kwa jimbo la Nzega Vijijini.Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Kata ya shimbo juu ya Umuhimu wa Kuichagua CCM kwa maendeleo ya Nzega na Jimbo jirani jipya la Igunga Kusini.Mwigulu,KIgwangalla,Gulamali na Diwani wa kata ya Shimbo wakionesha Uimara wao wa kiafya  "Wanamuunga MKono Magufuli kwa Push Up"Sehemu ya Maelfu ya Wananchi waliofika kwenye mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Ubunge jimbo la Nzega Mjini hii leo.

No comments:

Post a Comment

BASI LA TASHRIF LAPINDUKA NA DEREVA KUFARIKI HAPO HAPO

September 26, 2015



 JESHI la Polisi Mkoani Tanga linamshikilia Mkandarasi mkazi wa Bombo Tanga, Endrew Kimunga (54) kwa tuhuma za kusababisha ajali iliyopelekea kupinduka basi la kampuni la Tashrif na dereva wake kufa papo hapo
Tukio hilo lililotokea leo asubuhi eneo la Kange nje kidogo ya jiji la Tanga baada ya dereva wa gari aina ya Nissan Wagon, Kimunge kutoka kituo cha kuweka Petrol na kuingia barabarani kizembe jambo lililosababisha basi la Tashrif kushindwa kulikwepa na kuingia katika korongo na kupinduka.
Basi hilo ambalo lilikuwa likielekea kituo kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani cha Kange na kuelekea Dodoma lilipinduka baada ya dereva wake kushindwa kulikwepa jambo ambalo alilisukuma katika korongo na kupinduka .
Akizungumza na Tangakumekuchablog, Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Zubery Mombeji, alisema tukio hilo lilitokea saa 12 ; 15 asubuhi eneo la Kange na kupeleka Dereva  wa basi, Mohammed Ayoub  kufa papo hapo  na kusababisha majeruhi wanne.
Alisema uchunguzi wa awali unaonyesha dereva wa Nissan Wagon, alishindwa kuzingatia sheria za barabarani na kusababisha uzembe baada ya kuingia barabara kuu bila kuangalia magari pande zote mbili.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha dereva wa gari ndogo ndie chanzo cha ajali----kwa sasa tunaendelea na uchunguzi na tunamshikilia kwa mahojiano zaidi ya tukio zima” alisema Mombeji na kuongeza
“Dereva wa basi hakuwa na makosa ila ni kuwa amefariki pale pale----lakini niseme kuwa bado tuko katika uchunguzi na dereva wa Nissan tunamshikilia kituo kikuu cha Chumbageni” alisema
Aliwataja majeruhi kuwa ni Twaha Juma(42) mkazi wa Msambweni  pamoja na Idd Omary  ambao wote ni wafanyakazi wa kampuni ya Tashrif
Akizungumzia tukio zima la ajali hiyo, Kamanda Mombeji, alisema Dereva wa basi hilo la Tashrif , Mohammed Ayoub, hakufunga mkanda na kuwa chanzo cha kifo chake baada ya kurushwa mbele ya kioo cha mbele na gari kumkokota na kupelekea kusagwasagwa.
Alisema kama angelifunga mkanda angelisalimika kifo kama ilivyokuwa kwa wenzake wawili ambao walikuwa siti za katikati na kupelekea kupata majeraha madogo madogo.
                                                   



Viongozi wa CHADEMA Gairo, Mikumi Wakimbilia CCM, Bi. Suluhu Awapokea...!

September 26, 2015
Msafara wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan ukiwasili Gairo mkoani Morogoro.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) akiwashukuru baadhi ya wananchi waliofika kumpokea mpakani mwa Mkoa wa Dodoma na Morogoro alipokuwa akiwasili kuanza ziara ya kampeni mkoani Morogoro leo.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais CCM, Bi. Suluhu (kushoto) akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Morogoro walipofika kupokea akitokea mkoani Dodoma. Mgombea huyo ameanza ziara ya kampeni Mkoa wa Morogoro leo.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alipowasili Mkoa wa Morogoro tayari kwa ziara ya kampeni.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alipowasili katika mkutano mdogo wa kwanza kuinadi ilani ya CCM Jimbo la Gairo leo Morogoro.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alipowasili katika mkutano mdogo wa kwanza kuinadi ilani ya CCM Jimbo la Gairo leo Morogoro.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alipowasili katika mkutano mdogo wa kwanza kuinadi ilani ya CCM Jimbo la Gairo leo Morogoro.
WanaCCM na wananchi wengine wakiwa katika mkutano wa kwanza wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Suluhu (hayupo pichani) katika Jimbo la Gairo.
WanaCCM na wananchi wengine wakiwa katika mkutano wa kwanza wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Suluhu (hayupo pichani) katika Jimbo la Gairo.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby akizungumza na wanaCCM na wananchi waliofika katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby (kulia) akizungumza jambo na mgombea mwenza wa nafasi ya urais CCM, Bi. Suluhu katika mkutano wa kampeni Gairo.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alipowasili katika mkutano mdogo wa kwanza kuinadi ilani ya CCM Jimbo la Gairo leo Morogoro.
Mbunge wa Afrika Mashariki, Angela Kiziga akizungumza katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika Jimbo la Gairo.
Baadhi ya vijana wakiwa wamepanda juu ya gari lililoegeswa ili kumuona mgombea mwenza wa CCM, alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni Gairo.
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akiwahutubia wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Gairo Mkoani Morogoro.
Baadhi ya wanachama wa CCM na wapenzi wa chama hicho wakimpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu alipowasili katika Jimbo la Mvomero leo ambapo alifanya mkutano wa kampeni.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby akiwahutubia wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Gairo Mkoani Morogoro.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano wa mgombea mwenza wa CCM, alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni Gairo.
CCM Oyeeeeeeee....! Mkutano Jimboni Gairo.
Baadhi ya viongozi wa CCM (kulia) wakimpa zawadi ya sare kada mkogwe wa CCM Jimbo la Gairo.

Wakereketwa na wanaCCM wakimpokea mgombea mwenza wa CCM Jimbo la Gairo.
Wakereketwa na wanaCCM wakimpokea mgombea mwenza wa CCM Jimbo la Gairo.

Mmoja wa viongozi na makada wa Chadema wilaya ya Gairo (kushoto) akitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza, Bi. Samia Suluhu. 
Katibu wa Chadema Wilaya ya Gairo, Yona Senyagwa (kushoto) akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katibu huyo pamoja na makada wenzake wametangaza kukihama chama cha Chadema na kujiunga na CCM leo.
Bi. Samia Suluhu akiwa amesimamishwa na wananchi njiani alipokuwa akielekea Wilayani Kilosa kufanya mikutano ya kampeni.
Kada mkongwe wa Chadema Kata ya Dumila, Tegemea Mnhambo akitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais, Bi. Suluhu.
WanaCCM na wananchi wakifuatilia mkutano wa kampeni juu ya gari lililoegeshwa.
Wananchi na wapenzi wa CCM wakiwa wamemsimamisha mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu.
WanaCCM na Wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM.
Wakitumia mbinu mbadala kumlaki mgombea mwenza wa CCM
Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Inspecta Harun akihamasisha wanaCCM na wananchi mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi.  
Mmoja wa makada wa Chadema waliojiunga na CCM, katika mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi akisalimia wananchi.
Mgombea mwenza Bi. Suluhu akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi. 
Mmoja wa makada wa Chadema waliojiunga na CCM, katika mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi akionesha kadi yake kabla ya kumkabidhi mgombea mwenza.

Mgombea mwenza Bi. Suluhu akimkabidhi kadi mmoja wa makada wa Chadema waliojiunga na CCM, katika mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com