SERIKALI INATAMBUA NISHATI NI MUHIMU KATIKA KUCHOCHEA MAENDELEO YA KIUCHUMI

April 10, 2024

 Na Janeth Raphael  -Dodoma


Tanzania imendelea kushirikiana na wataalum sambamba na michango ya wadau wa nje na ndani ya nchi katika kuhimiza matumizi ya nishati Mbadala katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Afrika Dream na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt James Mataragio wakati wa ufunguzi wa warsha iliyolenga kuhamasisha wananchi juu ya kutumia Nishati Jadilifu.

Dkt Mataragio amesemae Serikali inatambua kwamba nishati ni muhimu katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2025 ambayo Serikali imejipangia.

“zaidi sera yetu ya nishati ya 2015 inatambua umuhimu wa wadau na katika kufikia malengo ya kuwa na nishati jadilifu, kulingana na mahitaji ya upatikanaji nishati nchi nzima na kwa bei himilivu ambayo ni hitaji la msingi katika kukuza uchumi, na kuboresha maisha,” albainisha.

Aidha Matarajio ya Taifa ni kuweka Misingi thabiti na kuchochea matumizi ya nishati jadilifu, katika kukuza maendeleo ya nchi na ustawi wa watu.

Pia katika kutizama mabadiliko ya hali ya hewa na kuondoa umasikini, Serikali imeendelea kuweka mkazo katika upunnguzaji wa hewa ya kaboni kupitia sera zake ikiwemo ya Mwaka 2021 ambayo inaainisha malengo ya 30-35% ya kupunguza matumizi ya hewa ya ukaa.

Ameongeza kusema kuwa mashirika ya Climate Action Network Tanzania na Power Afrika na taasisi ya suistainable Futures wanaanda taarifa yenye mchanganuo wa njia ya mbalimbali zinaweza kusaidia kujikita katika matumizi ya nishati jadilifu.

“Tunahitaji michango ya mawazo katika taarifa hii kusaidia kufikia malengo ya matumizi endelevu ya nishati yakayosaidia wizara kutumia taarifa katika mipango yake iliyoainisha,” alisema.







 

BILIONI 96.5 KUONGEZA KASI YA MRADI WA UMEME WA KAKONO

April 10, 2024

 Na. Saidina Msangi, WF- Dodoma.


Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa zimesaini mkataba wa Euro milioni 34.86 sawa na takribani shilingi bilioni 96.47 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa Kakono.

Mkataba huo umesainiwa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa nchini Tanzania, Bi. Celine Robert.

Alisema kuwa mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwaka 2026 na kukabidhiwa kwa Serikali mwaka 2028, utaongeza umeme wa megawati 87.8 kwenye gridi ya Taifa hivyo kuongeza uzalishaji wa umeme nafuu wa nguvu za maji ili kukabiliana na upungufu wa umeme katika gridi ya Taifa maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

‘’Mradi huu unafadhiliwa na Washirika watatu wa Maendeleo ambao ni AFD (Euro 110 milioni sawa na takriban TZS 304.37 bilioni), Benki ya Maendeleo ya Afrika (USD 161.47 milioni sawa na takriban TZS 413.95 bilioni) na Umoja wa Ulaya (Euro 34.86 milioni sawa na TZS 96.47 kusimamiwa na AFD) ambayo tumesaini leo’’, alisema Dkt. Mwamba.

Alisema kuwa Mradi wa Umeme wa Maji wa Kakono unaenda sambamba na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP III) wenye kaulimbiu ya kujenga Uchumi wa Kiushindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu kwa kuboresha miundombinu yenye tija, upatikanaji wa nishati ya uhakika, kuimarisha biashara na uwekezaji, mazingira wezeshi pamoja na mifumo ya elimu na mafunzo.

Alifafanua kuwa mbali na kusambaza umeme kwa watumiaji, mradi huo pia unatarajiwa kutoa fursa za ajira takribani 1,000 zitatolewa wakati wa awamu ya utekelezaji pamoja na ajira 100 za kudumu wakati wa awamu ya uendeshaji na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi wa watu wanaozunguka mradi na kuboresha Maisha yao.

Dkt. Mwamba aliishukuru AFD kwa jitihada zote za kuhakikisha kwamba, ruzuku hiyo inapatikana kwa ajili ya mradi na kuwa Serikali itaendelea kufanya kazi kwa karibu na AFD na Washirika wengine wa Maendeleo ili kuhakikisha utekelezaji wa mradi huo unafanikiwa na kufikia lengo lililokusudiwa la maendeleo.

Mtambo unaotarajiwa kujengwa wa kufua umeme wa Kakono upo mto Kagera, takriban kilometa 90 magharibi mwa Manispaa ya Bukoba, ambayo ni kona ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania utakuwa mbadala wa mitambo ya kufua umeme kwa kutumia mafuta ambayo hutumika kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa umeme kwenye gridi ya Taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa nchini, Bi. Celine Robert, alisema kuwa mradi huo unaenda sambamba na malengo ya kimataifa ya tabia nchi na utasaidia Tanzania katika hatua ya kupunguza kiwango cha kaboni katika sekta ya nishati.

‘‘Mradi huu unatarajiwa kuwa na matokeo makubwa katika maendeleo ya kiuchumi ya eneo hili linalokua kwa kasi, ambalo liko katikati mwa eneo la Maziwa Makuu, kukuza uchumi wa viwanda na kuchochea ukuaji sio tu Tanzania bali hata katika nchi jirani,’’, alisema Bi. Celine Robert

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio alisema Wizara hiyo kupitia Shirika la Umeme nchini (TANESCO) watahakikisha mradi huo unatekelezwa kwa ufanisi na kuhakikisha unafikia malengo yaliyokusudiwa.

Alisema mradi huo utarahisisha upatikaji wa umeme wa uhakika katika Mkoa wa Kagera na mikoa ya jirani, utaongeza ajira, utapunguza gharama za umeme na kuongeza mapato ya TANESCO.

Dkt. Mataragio alilipongeza Shirika la Maendeleo la Ufaransa kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali huku akiitaja baadhi ya miradi ya nishati iliyofadhiliwa na shirika hilo ikiwemo Mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu, Mradi wa kuungamisha Tanzania na Zambia pamoja na Mradi wa Umeme wa Jua Mafia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El – Maamry Mwamba na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa nchini, Bi. Celine Robert, wakionesha mikataba ya Euro milioni 34.86 sawa na shilingi bilioni 96.47 kwa ajili ya mradi wa kufua umeme wa nguvu za maji wa Kakono, baada ya hafla ya kusaini mikataba hiyo iliyofanyika jijini Dodoma. 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El – Maamry Mwamba na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa nchini, Bi. Celine Robert wakipongezana baada ya kusaini mkataba wa Euro milioni 34.86 sawa na shilingi bilioni 96.47 kwa ajili ya mradi wa kufua umeme wa nguvu za maji wa Kakono, katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa nchini, Bi. Celine Robert, wakisaini mikataba ya Euro milioni 34.86 sawa na shilingi bilioni 96.47 kwa ajili ya mradi wa kufua umeme wa nguvu za maji wa Kakono, katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio, akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa Euro milioni 34.86 sawa na shilingi bilioni 96.47 kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa kwa ajili ya mradi wa kufua umeme wa nguvu za maji wa Kakono, katika hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.

Baadhi ya wawakilishi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati wakifuatilia kwa karibu hotuba mbalimbali zilizotolewa katika hafla ya utiaji saini wa Euro milioni 34.86 sawa na shilingi bilioni 96.47 kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa kwa ajili ya mradi wa kufua umeme wa nguvu za maji wa Kakono, katika hafla iliyofanyika Jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Fedha Dodoma)

WAFADHILI WATOA FEDHA KWA AJILI YA UTEKELEZAJI MRADI WA KUFUA UMEME KAKONO

April 10, 2024

 Na Janeth Raphael -MichuziTv -Dodoma


Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana Shirika la Maendeleo la Ufaransa wamesaini mkataba ambapo kiasi cha Euro Millioni 110 kitatolewa na shirika hilo na Benki ya maendeleo ya Maendeleo ya Afrika itatoa Dolla Million 161 na umoja wa Ulaya utatoa Euro millioni 134 kwa ajili ya Mradi wa kuzalisha umeme wa Kakono.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Hazina na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Natu El- maamry Mwamba ambaye ameshukuru wafadhili wote wa tatu Kwa michango yao muhimu ambayo itasaidia kupatikana fedha kwa ajli ya mradi huo muhimu.

Mradi wa kufua umeme wa Kakono unaendana na mpango wa maendeleo wa Taifa ambao unamaudhui ya kujenga uchumi shindani na viwanda kwa ajili ya maendeleo ya watu kupitia uboreshaji wa miundo mbinu na upatikanaji wa nishati ya uhakika na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji wa mifumo ya elimu na ujuzi, amesema.

“Nifuraha kuona kwamba Sekta ya nishati ni moja ya mradi wa kipaumbele kwa Shirika la Maendeleo la Ufaransa pamoja na umoja wa Ulaya,” alibainisha Dkt, Natu

Aidha mpango wa Nishati wa Umeme wa Kakono unaendana na Mkakati wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ya Mwaka 2021-2025 ambavyo kati ya vipaumbele vyake vya kiuendeshaji ni pamoja na sekta nishati .

Ameongeza kusema ujenzi wa mradi huo utasaidia Kuongeza uzalishaji wa umeme nafuu kwa nguvu za maji kukabiliana na upungufu wa umeme katika gridi ya Taifa kwa maeneo ya kusini magharibi mwa Tanzania.

“Ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa Kakono utakuwa Mbadala wa Mitambo ya kufua umeme kwa mafuta ambayo hutumika kuongeza uzalishaji wa umeme kwenye gridi ya taifa ili kupunguza mgao,” alibainisha

Imeelezwa kwamba Utekelezaji wa mradi huu unaoendelea na utakamailika mwaka 2026 na kukabidhiwa kwa serikali mwaka 2028, mradi unatarajia kuongeza megawati 87.8 kwenye gridi ya taifa pindi utakapokamilika.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt James Mataragio amesema miradi inayofadhiliwa ni pamoja na Mradi wa kuongeza usambazaji kwenye Gridi (Upgrade Transmission Grade) Mradi wa kuzalisha megawati 150 wa jua Kishapu, kuna mradi mwingine unaohusisha Tanzania na Zambia (Tanzania Zambia Interconnection) Mradi wa umeme wa jua Mafia ambao utazalisha megawati 5.

“Sisi kama Serikali tunawashukuru sana kwa kuendelea kutoa ufadhili katika hii miradi kwa sababu licha ya kusaidia ujenzi wa miradi wamekuwa wakitoa msaada wa kiufundi,” alibanisha.

Dkt, Mataragio amesema Serikali itahakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El – Maamry Mwamba na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa nchini, Bi. Celine Robert wakipongezana baada ya kusaini mkataba wa Euro milioni 34.86 sawa na shilingi bilioni 96.47 kwa ajili ya mradi wa kufua umeme wa nguvu za maji wa Kakono, katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El – Maamry Mwamba na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa nchini, Bi. Celine Robert, wakionesha mikataba ya Euro milioni 34.86 sawa na shilingi bilioni 96.47 kwa ajili ya mradi wa kufua umeme wa nguvu za maji wa Kakono, baada ya hafla ya kusaini mikataba hiyo iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa nchini, Bi. Celine Robert, wakisaini mikataba ya Euro milioni 34.86 sawa na shilingi bilioni 96.47 kwa ajili ya mradi wa kufua umeme wa nguvu za maji wa Kakono, katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio, akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa Euro milioni 34.86 sawa na shilingi bilioni 96.47 kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa kwa ajili ya mradi wa kufua umeme wa nguvu za maji wa Kakono, katika hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.


Baadhi ya wawakilishi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati wakifuatilia kwa karibu hotuba mbalimbali zilizotolewa katika hafla ya utiaji saini wa Euro milioni 34.86 sawa na shilingi bilioni 96.47 kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa kwa ajili ya mradi wa kufua umeme wa nguvu za maji wa Kakono, katika hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.


TARURA PWANI YAONGEZA MTANDAO WA BARABARA

April 10, 2024

 Na. Catherine Sungura,Pwani


Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imezidi kuimarisha mtandao wa barabara ndani ya mkoa wa Pwani na kufungua uchumi wake na wananchi kwa ujumla.

Mkoa wa Pwani una mtandao wa barabara jumla ya Km 5,140 kati ya hizo Km 95 ni za lami, Km 1,100 za changarawe na Km 3,945 ni udongo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Meneja wa TARURA Mkoa wa Pwani, Mhandisi Leopold Runji amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa katika kuimarisha miundombinu ya barabara za Wilaya nchini.

Mhandisi Runji amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti ya TARURA mkoa wa Pwani kutoka shilingi Bilioni 11 mpaka kufikia shilingi Bilioni 32 kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi na ukarabati wa barabara kwa mwaka.

“Tumeongeza mtandao wa barabara za lami kutoka Km 56 hadi kufikia zaidi ya Km 97, huu ni mkoa ambao umejielekeza zaidi kwenye shughuli za viwanda kama sehemu ya uchumi na eneo mojawapo ambalo limenufaika ni barabara ya Visiga- Zegereni ambapo zaidi ya Km 12.5 za barabara zimeshakamilika”.

Amesema pia wana miji kama Mafia, Ikwiriri, Kibiti ambapo hawakuwa na mtandao wa lami kabisa na sasa Serikali imejenga.

“Tumejenga Km 2 upande wa Mafia, Km 1.6 upande wa Kibiti na Km zaidi ya 15 katika Mji wa Kibaha", amebainisha.

Upande wa bagamoyo amesema ni mji mkongwe hivyo barabara nyingi zinahitaji matengenezo kila mwaka kuna zaidi ya Km 1 ambazo wanazifanyia matengenezo ili kuzirudisha kuwa katika hali nzuri.

“Lakini pia tunashuhudia ujenzi wa madaraja makubwa katika mkoa wetu wa Pwani, tuna daraja la Mbuchi ambalo ni zaidi ya mita 61 limekamilika, daraja la Mbwera linatumika lina zaidi ya mita 43 na pia tunatarajia kuanza kujenga daraja la Bibititi Mohamed (Mohoro) lenye urefu wa zaidi ya mita 80”.

Amesema Daraja la Mbwera limeweza kupunguza gharama za usafiri na usafirishaji ambapo wananchi wanaotoka Mbwera walikuwa wanaenda kuungana na wenzao wa Muhoro ili kuunganisha na barabara kuu iendayo Mtwara kwa zaidi ya Shilingi 30,000 lakini sasa hivi wanatumia kati ya 10,000 hadi 15,000 haya ni mafanikio makubwa ya serikali ya awamu ya sita kwani barabara nyingi zimefungua maeneo mbalimbali katika mkoa wa Pwani.







RAIS SAMIA ASHIRIKI IBADA YA EID EL FITRI MSIKITI MKUU WA BAKWATA MFALME WA (VI) WA MOROCCO DAR ES SALAAM

RAIS SAMIA ASHIRIKI IBADA YA EID EL FITRI MSIKITI MKUU WA BAKWATA MFALME WA (VI) WA MOROCCO DAR ES SALAAM

April 10, 2024




Rais Samia Suluhu Hassan ameshiriki ibada ya Eid El Fitri katika Msikiti Mkuu wa Bakwata (Mfalme Mohammed VI wa Morocco), Kinondoni Dar es Salaaam, tarehe 10 Aprili, 2024.
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na waumini wengine wa dini ya Kiislam katika ibada ya Eid El Fitri Msikiti Mkuu wa Bakwata (Mfalme Mohammed VI wa Morocco), Kinondoni Dar es Salaaam, tarehe 10 Aprili, 2024.
Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waumini wengine mara baada ya ibada ya Eid El Fitri katika Msikiti Mkuu wa Bakwata (Mfalme Mohammed VI wa Morocco), Kinondoni Dar es Salaaam, tarehe 10 Aprili, 2024.
Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Zuberi muda mfupi kabla ya kuanza kwa ibada ya Eid El Fitri katika Msikiti Mkuu wa Bakwata (Mfalme Mohammed VI wa Morocco), Kinondoni Dar es Salaaam, tarehe 10 Aprili, 2024.

STAMICO KUENDELEA KUWAPA SHUGHULI ZA KIUCHUMI WATU WA MAKUNDI MAALUMU.

April 10, 2024

 Shirika la Madini la Taifa STAMICO, limejiwekea malengo ya kuendelea kuwasaidia watu wa makundi maalumu kama vile walemavu ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa shughuli za kiuchumi kama vile Uwakala wa Kusambaza wa Nishati safi ya Rafiki Briquettes na kuwapa mafunzo ya uchimbaji madini na kuwasimamia ili waweze kunufaika na Rasilimali madini zilizoko nchini.


Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse ameeleza hayo Tarehe 8 Aprili 2024 wakati wa Futari ya pamoja na watumishi wa STAMICO pamoja na watu kutoka makundi maalumu tukio lilofanyika Dodoma. Tukio hili lilihudhuriwa na viongozi wa kidini, akiwepo Mwakilishi wa Sheikn wa Wilaya, Sheikn Abdurahman Issa pamoja na Katibu Sheikn Shafii Husein Ramadhan.

“Hii sio mara ya kwanza kwa sisi kufuturisha watu wa makundi maalumu kipindi hiki cha mwezi Mtukufu tayari tumefanya hivyi katika Mkoa wa Lindi kabla ya kufanya tukio hili leo Jijini Dodoma na hatuishii tu kuwapa chakula bali tunawapa mafunzo, na fursa za kiuchumi kama vile uwakala wa usambazaji wa nishati safi, kuwajengea uwezo wa kushiriki kwenye shughuli za Madini kwa kuwapa mafunzo na kuwasimamia ili nao waweze kunufaika na Rasilimali hizi za Madini”, alisema Dkt Mwasse.

Aidha Dkt. Mwasse ameeleza kuwa tayari STAMICO wamewawezesha wenye usikivu hafifu mkoa wa Geita kupata mafunzo ya uchimbaji Madini na kuwapa leseni ya uchimbaji Madini ya Dhahabu na kwa sasa wanachimba Dhahabu katika mgodi uliopo Masumbwe, Geita, na Shirika linaendelea kuwasimimamia ili waweze kunufaika na Rasilimali hiyo ya Madini.

Muwakilishi wa Sheikh wa Wilaya Sheikn Abdurahman Issa amewapongeza STAMICO na kuwaomba kuendelea na utaratibu huo kwani wanafanya jambo zuri kwa Jamii hiyo ya watu wa Makundi Maalumu na ni sambamba na matakwa ya Mwenyezi mungu.





Timu Ya Mawaziri Kuongeza Nguvu Rufiji, Kibiti-Majaliwa

April 10, 2024

 WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Timu ya Mawaziri itakwenda wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani kuungana na timu ya watalaam ili kufanya tathmini ya pamoja kutokana na athari zilizosababishwa na mafuriko yaliyotokea wilayani humo.


Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne Aprili 09, 2024) wakati wa hafla ya Futari aliyoiandaa kwa ajili ya watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake, Mlimwa jijini Dodoma.

“Sisi ndio tunaratibu Idara ya Maafa kitaifa, hapa tunapozungumza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama pamoja na Katibu Mkuu Dkt. Jim Yonaz wako njiani wanaelekea mkoani Pwani, mto rufiji umejaa na kata nne zipo kwenye maji, Mawaziri wengine wa Sekta ikiwemo Afya, Kilimo, Mifugo nao pia wanakwenda ili kuimarisha uratibu wa zoezi”

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameipongeza Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya namna inavyodhibiti biashara ya dawa za kulevya nchini.

“Kamishna amefanya kazi nzuri na kuboresha kwenye sekta yake, hivi sasa Taasisi yake haiishii tu Makao Makuu ya nchi, ameshusha kwenye kanda na tayari wakurugenzi wameshaenda kwenye maeneo hayo ambao watakamata wazalishaji, wasafirishaji, wafanyabiashara na watumiaji wa dawa za kulevya”

Viongozi wengine walioshiriki katika iftar hiyo ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Ummy Nderiananga, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mary Maganga na Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.