MAGUFULI ASIMAMISHWA KILA MAHALA AKIWA NJIANI KUREJEA DAR ES SALAAM

July 24, 2015

 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kibaigwa  mkoani Dodoma akiwa njiani kuelekea Dar es salaam.

 Wananchi wa Dumila wakifurahia ujio wa Dk.John Pombe Magufuli mgombea wa Urais kupitia CCM ambaye aliwasalimia kabla ya kuelekea Dar es Salaam.
  Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimu wananchi wa Dumila  akiwa njiani kuelekea Dar es salaam
   Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimu wananchi wa Dumila  akiwa njiani kuelekea Dar es salaam
   Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimu wananchi wa Dumila  akiwa njiani kuelekea Dar es salaam
   Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga mara baada ya kuwasalimia wananchi wa Dumila  akiwa njiani kuelekea Dar es salaam
    Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga mara baada ya kuwasalimia wananchi wa Dumila  akiwa njiani kuelekea Dar es salaam
    Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimu wafanyabiashara ndogo ndogo wa Dumila  njia panda ya Mvomelo akiwa njiani kuelekea Dar es salaam

LISTEN TO ERICA LULAKWA’S BRAND NEW SONG “DUNDIKA”

July 24, 2015
maxresdefault
Debut Album "Piga Moyo Konde" is out! On Itunes http://itunes.apple.com/album/id10046...
Dundika is the 2nd Song released from this Album. Listen free on Spotify and Tidal. If you like the music, I would truly appreciate your support in writing a review or sharing links to iTunes or Google Play on social media.
Listen to her music on you tube below here.

CAG AONGOZA KIKAO CHA BODI YA UKAGUZI YA UMOJA WA MATAIFA

July 24, 2015

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa, Bw.Mussa Juma Assad akizungumza wakati wa hitimisho la mkutano wa siku mbili wa Bodi hiyo uliofanyika hapa Umoja wa Mataifa kuanzia Julai 22-23. Kushoto kwake ni Bw. Fransis Kitauli, Mkurugenzi wa Ukauzi wa Nje na Mwenyekiti wa Kamati ya Operesheni za Ukaguzi ( AOC) Akiwa Mwenyekiti wa AOC Bw. Kitauli ambaye alishika nafasi hiyo tangu mwaka 2012 amefanikisha utoaji wa ripoti za ukaguzi za Umoja wa Mataifa kwa miaka mitatu mfululizo.
Wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi kutoka kushoto, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya India, Bw. Shashi Kant Sharma, Sir Amyas Morse, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kutoka Serikali ya India na Bw. Mussa Juma Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kutoka Serikali ya Tanzania wakitia saini zao katika ripoti 28 za ukaguzi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa zilizorejewa na kupitishwa na Bodi hiyo wakati wa mkutano wake wa siku mbili. ripoti hizo ni matokeo ya kazi kubwa ya Bodi hiyo.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Bodi wakiwa pamoja na wataalamu wao na wajumbe kutoka Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa.
Ujumbe wa Bodi ya Uingereza ukiongozwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Sir Amyas Morse.
Ujumbe wa Bodi ya India ukiongozwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Bw. Shadhi Sharma.
Ujumbe wa Bodi ya Tanzania ambao ni kutoka kushoto Jerome Francis, Naibu Mkurugenzi ukaguzi wa Nje, Bw. Salhina Mkumba, Naibu Mkurugenzi, Ukaguzi wa Nje na ambaye amefanya kazi kwa karibu sana na Bw. Fransis Kitauli tangu Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ilipoteuliwa kuingia kwenye Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa wa mwisho ni Bw. Athuman S. Mbuttuka, Naibu Mkaguzi Mkuu.

MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA AJITOSA UBUNGE JIMBO LA KOROGWE MJINI.

July 24, 2015
KULIA NI MWENYEKITI WA JUMUIYA YA UMOJA WA VIJANA MKOA WA TANGA(UVCCM)ABDI MAKANGE AKIKABIDHIWA FOMU ZA KUOMBA KUTEULIWA NA CCM KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KOROGWE MJINI








MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Tanga, Abdi Makange juzi alichukua fomu za kuomba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Ubunge Jimbo la Korogwe mjini katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwaka huu hapa nchini.

Makange anakuwa ni kada wa kumi na tatu wa chama hicho kujitokeza kuomba ridhaa hiyo huku wengine Allen Nyangasa,Proffesa Catherbet Mhiliu,Kanali Iddi Kipingu,Salma Mntambo,Mussa Bareko,Yusuph Abdallah Nassir,William Mgaza.

Wengine ambao waliokwisha kujitokeza kutaka nafasi hiyo kupitia (CCM) ni Deogratius Augustino, Marry Chatanda, Thobias Mugweta,Seif Abdallah Shekalage,Fransis Shalimbago na Mjata Daffa Abdallah.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi mara baada ya kuchukua fomu hizo, Makange alisema kuwa dhamira yake ya kuwania nafasi hiyo ni kutaka kuhakikisha jimbo hilo linapata maendeleo ndani kipindi chake cha miaka mitano katika sekta mbalimbali ikiwemo huduma za Afya, Miundombinu na huduma za upatikanaji maji ya uhakika kwa wakazi.

Alisema kuwa katika kipindi ambacho ataliongoza jimbo hilo endapo atapewa ridhaa na wananchi hao atahakikisha anaweka mipango mizuri itakayopelekea kwenye Jimbo hilo kuwa na hospitali ya wilaya ili kuipunguzia mzigo ile ya Magunga ambayo wananchi kutoka maeneo mbalimbali wilayani humo na nje wanakwenda kupata matibabu.

Aidha alisema kuwa suala la wakina mama ambao wanajifungulia kwenye mifuko ya rambo kutokana na ukosefu wa vifaa atahakikisha analivalia njuga jambo hilo kwa kuboresha vifaa tiba kwenye hospitali na vituo vya afya vilivyopo kwenye Jimbo hilo ili kuondoa adha kwa wakinamama ambao wamekuwa wakipata matibabu kwenye hospitali wilayani humo.

   “Hili ni tatizo kubwa sana hivyo nisema tu suala hili nitahakikisha
ninalipa kipaumbele kikubwa sana wakati nitakapokuwa mbunge wenu kwa kuweka mipango imara itakayoleta ufanisi na hatimaye kuweza kuondoa kabisa “Alisema Makange.

Alisisitiza katika suala la Afya akiwa kama mbunge atatilia mkazo
wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambapo yeye
atachangia asilimia 10 ya mshahara wake kuwalipia ili kuweza kupata matibabu wakati wote wanapokuwa wakiugua jambo ambalo litasaidia kuendeleza huduma za afya.

Akizungumzia suala la miundombinu, Makange alisema kuwa katika Jimbo hilo zipo baadhi ya barabara hazina hadhi ya mji huo kutokana na nyingi kuwa za changarawe hivyo atahakikisha analifanyia kazi suala hilo kwa kuweka lami ili mji huo kuwa na muonekana mzuri.

Kwa upande wa huduma za upatikanaji wa maji,Makange alisema kuwa suala hilo atalivalia kibwebwe kwa kutumia vizuri mto Ruvu kupitia wahisani ili kutoa maji kwenye mto huo ili kuondoa kero hiyo kwa wananchi kwenye Jimbo hilo sambamba na kuchimba visima kwenye baadhi ya maeneo

SIMBA SC WANAVYOJIFUA ZENJI, WAKITOKA HUKO NI KUCHINJA CHINJA TU HADI UBINGWA

July 24, 2015


Wachezaji wa Simba SC wakiwa mazoezini kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar kujiandaa na mechi dhidi ya AFC Leopards mwezi ujao katika tamasha la Simba Day litakalofanyika na baadaye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Kulia ni kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili, Mserbia Dušan Momcilovic.

WASIMAMIZI, WAHARIRI NA WADADISI WA UTAFITI WA AFYA YA MAMA NA MTOTO NA MALARIA WA MWAKA 2015,WAPEWA MAFUNZO

July 24, 2015
Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Takwimu ,Ephraim Kwesigabo akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo.


Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wasimamizi,wahariri na wadadisi wa utafiti wa afya ya mama na mtoto na Maralia yanayofanyika kwa siku 36 katika ukumbi wa YMCA mjini Moshi.


Baadhi ya washiriki.


Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akizindua matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.


Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Afya ,Zanzibar Halima Maulid Saleh  matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.


Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akimkabidhi Mganga mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Andrewleon Qweker matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.


Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akimkabidhi Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Hafidh Rajab  matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.


Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akimkabidhi Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu  Ephraim Kwesigabo matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.


Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Hafidh Rajab akitoa neno la shukrani wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.


Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ambao ni wauguzi kutoka maeneo mbalimbali nchini.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.


Baadhi ya wauguzi wanaoshiriki mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa YMCA mjini Moshi.
Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Zanzibar Halima Maulidi Saleh akiwa na ,Mganga mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Andrewleon Qweker (katikati) na Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Hafidh Rajab wakifuatilia ufunguzi wa mafunzo hayo.

NHIF YATENGA ENEO MAALUMU LA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA MKOA WA TANGA BOMBO KWA WAGONJWA WALIOJIUNGA NA MFUKO HUO

July 24, 2015
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umetenga eneo maalumu kwa ajili ya kutolea huduma za matibabu na kulazwa kwa wagonjwa wake wanaohudumiwa na mfuko huo kwenye hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo.

Kauli hiyo ilitolewa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Tanga(NHIF) Ally Mwakababu wakati wa semina ya siku moja kwa madereva wa malori ya masafa marefu,mabasi ya abiia na waendesha boda boda.

Alisema ni ya kufanya hivyo ni kuhakikisha wanachama wa mfuko huo wanapata huduma bora ambazo zipo kwenye mazingira mazuri zaidi ili waone manufaa ya kuwa wanachama wa mfuko huo.

Aidha alisema kuwa hivi sasa mfuko huo unapokea wanachama hata wale ambao hawako katika mfuko usio rasmi na kuwashauri kujiunga na mfuko kwa kiwango kidogo cha fedha na kupata huduma za afya bure kwa kipindi cha mwaka mzima.

Wakizungumza baadhi ya madereva hao waliupongeza mfuko huo kwa kuanzisha huduma hiyo ya hiari kwani itasaidia wananchi wengi wa kipato cha chini kuweza kujiunga na NHIF na kupata huduma za Matibabu kwa urahisi hasa wakati wanapougua tofauti na ilivyo sasa.





 MENEJA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOA WA TANGA(NHIF) ALLLY MWAKABABU AKIZUNUMZA NA MADEREVA WA MALORI YA MASAFA MAREFU,MABASI YA ABIRIA PAMOJA NA WAENDESHA BODABODA JIJINI TANGA WAKATI WA SEMINA YA SIKU MOJA YA KUHIMIZA UMUHIMU WA WAO KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF)

AFISA MATEKELEZO WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA(NHIF) KUTOKA MAKAO MAKUU,SALVATORY OKUMU AKISISITIZA JAMBO WAKATI WA SEMINA HIYO


KATIKATI NI MENEJA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOA WA TANGA(NHIF) ALLLY MWAKABABU AKIANDIKA MAONI YA MADEREVA WA MALORI YA MASAFA MAREFU,MABASI YA ABIRIA PAMOJA NA WAENDESHA BODABODA JIJINI TANGA WAKATI WA SEMINA YA SIKU MOJA YA KUHIMIZA UMUHIMU WA WAO KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF) KUSHOTO NI AFISA UANACHAMA MKOA WA TANGA (NHIF) MIRAJI KISILE

MENEJA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOA WA TANGA(NHIF) ALLY MWAKABABU KULIA AKIMSIKILIZA AFISA UANACHAMA MKOA WA TANGA,MIRAJI KISILE.


MADEREVA WA MALORI YA MASAFA MAREFU,MABASI YA ABIRIA PAMOJA NA WANDESHA BODABODA WAKIFUTILIA SEMINA ILIYOKUWA IKIHUSU KUHAMASISHA KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA NHIF ILI WAWE KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA MATIBABU WAKATI WANAPOUGUA