ZIARA YA WANAMKIKITA NCHINI THAILAND

November 24, 2017
 Wajumbe kutoka Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Living Green) wakiwa na furaha baada ya kulakiwa na wenyeji wao walipowasili hivi karibuni  katika Jiji la Bangkok, Thailand tayari kwa ziara ya utalii wa kilimo cha kisasa na ufugaji pamoja na fursa la biashara.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange (kushoto) na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mtandao huo, Dk. Kissui S. Kissui wakiwawsili kwenye uwanja wa ndege jijini Bangkoko, Thailand
 Wakiwa na wenyeji wao

HAYA NDIYO MAAJABU YA KIMONDO CHA MBOZI KILICHOPO MKOANI SONGWE,NAIBU WAZIRI WA MALIASILI AELEZA MIPANGO YA SERIKALI YA KUKIENDELEZA

November 24, 2017
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kulia) akiwa ameshikilia kivutio cha utalii cha Kimondo leo wakati wa ziara yake ya kikazi katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.

Kimondo hicho kinachokadiriwa kuwa na tani 12 kiligunduliwa wilayani Mbozi mwaka 1930 na kimeundwa kwa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11.

Aidha, kimondo hiki ni cha pili kwa ukubwa kati ya 35 vilivyopo barani Afrika na cha nane kati ya 578 vilivyopo duniani kote ambavyo vimeundwa kwa chuma. Sifa kuu ya kimondo hiki ni kuwa na ubaridi wakati wote hata mchana wa jua kali.

Pamoja na mambo mengine katika ziara hiyo, amekagua ujenzi unaoendelea wa jengo la kituo cha taarifa (Information Centre) katika kivutio hicho ambalo linagharimu Shilingi milioni 400. 

Alisema Serikali kupitia wizara yake ina mpango thabiti wa kuendeleza kivutio hicho pamoja na vivutio vya ukanda wa kusini ambapo kupitia Benki ya Dunia imepata mkopo nafuu wa Dola za Kimarekani milioni 150 sawa na shilingi bilioni 340 kwa ajili ya kuendeleza vivutio vya ukanda wa kusini ikiwemo kuimarisha miundombinu.

Vivutio vingine vya utalii vinavyopatikana Mkoani Songwe ni pamoja na chemchem ya maji moto, vitalu vya uwindaji vyenye wanyamapori mbalimbali, mifupa ya shingopana songwensis, unyayo wa mtu wa kale, mapango ya popo, maporomoko ya maji, mbega weupe, kituo cha kwanza cha polisi Tanzania, mabaki ya nyumba za kufua chuma,  na ziwa Rukwa
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Muhifadhi wa Mambo ya Kale, Winnie Msacky kuhusu kivutio cha utalii cha Kimondo wakati wa ziara yake ya kikazi katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi Mkoani wa Songwe jana. 

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AFANYA MKUTANO NA WAHARIRI ILI KUONGEZA UELEWA WA MIFUMO MIPYA KUHUSU UAGIZAJI WA MBOLEA KWA PAMOJA

November 24, 2017
 Mgeni Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Leo Novemba 24, 2017.
Mgeni Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Leo Novemba 24, 2017.
  Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati akizungumza kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Leo Novemba 24, 2017.
  Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati akizungumza kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Leo Novemba 24, 2017.
 Mgeni Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akifatilia mada kuhusu Mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Leo Novemba 24, 2017.
 Mhariri wa Magazeti ya serikali (TSN) Mgaya Kingoba akitoa neno la shukrani kwa Mgeni Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa kwa kufungua Mkutano kuhusu Mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja wakati wa mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.