RAIS MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA IJUMAA KUU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

March 25, 2016

 Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa na waumini wengine katika Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016
 Msalaba ukipelekwa altereni kuanza ibada ambayo imehudhuriwa pia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa katika Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akijiandaa kuubusu Msalaba wakati wa Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016
 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akibusu Msalaba wakati wa Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akibusu Msalaba wakati wa Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016
Sehemu ya waumini katika Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na watu wenye ulemavu baada ya  Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016. Picha na IKULU

MUTFI WA TANZANIA AMUOMBEA DUA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA

March 25, 2016
 Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubery akiwa nyumbani kwake.
 Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubery (wa pili kushoto), akimuombea dua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum, Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Khalid na Msaidizi wa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Othman Mkambaku.
 Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum (kulia), akizungumza na wanahabari kabla ya kufanyika dua hiyo. Kushoto ni Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Khalid.
 Mufti Zubery, akifanya mazungumzo na Makonda.
 Dua ikiendelea nyumbani kwa mufti Mikocheni.
Wapiga picha kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Makonda akiagana na Sheikh Abubakar Khalid na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.

Na Dotto Mwaibale

MUFTI wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubery amemuombea dua, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Rais Dk. John Magufuli ili waweze kulitumikia vema taifa na kuliletea maendeleo.

Zubery alimfanyia dua hiyo Makonda Dar es Salaam leo asubuhi alipofika nyumbani kwake kujitambulisha na kumjulia hali pamoja na kumueleza mambo kadhaa ya maendeleo yaliyofanyika.

"Tunakuomba mola wetu kuwapa moyo wa imani na uzalendo na kuwaepusha na mabaya yote  Mkuu wetu wa Mkoa Paul Makonda, Rais wetu Magufuli pamoja na viongozi wote ili waliongoze taifa letu kwa amani" alisema Mufti Zubery"  wakati akiomba dua hiyo.

Makonda akizungumza na Mufti Zubery nyumbani kwake Mikocheni alimwambia kuwa kuna mambo kadhaa ameyafanya kwa kushirikiana na watendaji wenzake kwa kukutana na waendesha boda boda ili kuwawezesha kupata mkopo utakaowasaidia kupata vitendelea kazi zao kama kupata kofia ngumu mbili za kuvaa dereva na abiria wake ili kuwasaidia katika shughuli zao za kusafirisha abiria.

Makonda alitaja mambo mengine kuwa ni suala nzima la kupambana na uhalifu ambao bado unaonesha kupamba moto hasa ujambazi wa kutumia silaha za moto.

Alitaja mambo mengine kuwa ni mkutano alioufanya hivi karibuni wa kukutana na wenyeviti wa mitaa na maofisa watendaji ili kuzungumzia suala la utunzaji wa mazingira na mambo mengine ambapo alisema ameandaa mpango wa kumzawadia mwenyekiti atakayefanya vizuri kwenye mtaa wake.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum alisema jambo alilofanya Makonda la kumtembea Mufti ni jambo zuri na kuwa kumuona mufti ni sawa kama amewaona waislam wote nchini.

Alisema wanamuombea Makonda mungu amzidishie wepesi katika kazi zake kwani ni viongozi wachache wanaopata madaraka ambao uwakumbuka viongozi wa dini kama alivyofanya Makonda.

Katika hatua nyingine Makonda alifanya ukaguzi wa barabara kadhaa za Manispaa ya Kinondoni ambazo hivi karibuni aliagiza zifanyiwe marekebisho ikiwa ni pamoja na kuchimba mifereji baada ya kuharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.


TAARAB RASMI YA KUMPONGEZA DK.SHEIN KWA USHINDI WAKE

TAARAB RASMI YA KUMPONGEZA DK.SHEIN KWA USHINDI WAKE

March 25, 2016

1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Omar Kinana wakati alipowasili viwanja vya Ukumbi wa Salama Hotel ya Bwawani Mjini Zanzibar kuhudhuria katika Taarab rasmi ya kumpongeza kwa ushindi mkubwa wa Kishindo katika uchaguzi Mkuu wa marudio,iliyocharazwa na Vikundi vya Culture Muzicul Club,BigStar na Zanzibar One (katikati) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mama Asha Balozi katika Ukumbi wa Salama Hotel ya Bwawani Mjini Zanzibar jana katika Taarab rasmi ya kumpongeza kwa ushindi mkubwa wa Kishindo aliyoupata katika uchaguzi Mkuu wa marudio,iliyocharazwa na Vikundi vya Culture Muzicul Club,BigStar na Zanzibar One,
3 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Ukumbi wa Salama Hotel ya Bwawani Mjini Zanzibar jana alipohudhuria katika Taarab rasmi ya kumpongeza kwa ushindi mkubwa wa Kishindo aliyoupata katika uchaguzi Mkuu wa marudio,iliyocharazwa na Vikundi vya Culture Muzicul Club,BigStar na Zanzibar One
4 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Abdalla Mwinyi Khamis (kushoto) na Mama Asha Balozi (kulia) wakiangalia ratiba ya Taarab rasmi ya kumpongeza Rais kwa ushindi mkubwa wa Kishindo alioupata katika uchaguzi wa marudio,taarab rasmi iliyocharazwa na Vikundi vya Culture Muzicul Club,BigStar na Zanzibar One jana katika ukumbi wa Salama Hotel Bwawabi Mjini Unguja,
5 
Baadhi ya Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM waliohudhuria katika taarab rasmi ya kumpomgeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) kwa ushindi mkubwa wa Kishindo alioupata katika uchaguzi wa marudio,taarab rasmi iliyocharazwa na Vikundi vya Culture Muzicul Club,BigStar na Zanzibar One jana katika ukumbi wa Salama Hotel Bwawabi Mjini Unguja
6 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Abdalla Mwinyi Khamis (kushoto) na Mama Asha Balozi (wa pilikulia) na Mama Fatma Karume pamoja na Viongozi wengine wakiangalia Taarab rasmi ya kumpongeza Rais kwa ushindi mkubwa wa Kishindo alioupata katika uchaguzi wa marudio, Vikundi vya Culture Muzicul Club,BigStar na Zanzibar One ndio vilivyotoa burudani hiyo jana katika ukumbi wa Salama Hotel Bwawabi Mjini Unguja
7 
Msanii Makame faki (Sauti ya Zege) akiimba wimbo wa “Katumbukia Mwenyewe” wakati wa Taarab rasmi ya kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa ushindi mkubwa wa Kishindo alioupata katika uchaguzi wa marudio, iliyocharazwa na Vikundi vya Culture Muzicul Club,BigStar na Zanzibar One jana katika ukumbi wa Salama Hotel Bwawabi Mjini Unguja
8 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Mke wa makamo wa Pili wa Rais Mstaafu Mama Asha Suleiman Iddi wakitunza wakati wa Taarab rasmi ya kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa ushindi mkubwa wa Kishindo alioupata katika uchaguzi wa marudio, iliyocharazwa na Vikundi vya Culture Muzicul Club,BigStar na Zanzibar One jana katika ukumbi wa Salama Hotel Bwawabi Mjini Unguja
9Mwimbaji wa Rukia Ramadhan wa Zanzibar One akiimba wimbo unaosema”Kupata Majaaliwa”wakati wa Taarab rasmi ya kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa ushindi mkubwa wa Kishindo alioupata katika uchaguzi wa marudio, iliyocharazwa na Vikundi vya Culture Muzicul Club,BigStar na Zanzibar One jana katika ukumbi wa Salama Hotel Bwawabi Mjini Unguja,
[Picha naIkulu.]

WAZIRI WA UGANDA AFANYA ZIARA MKOANI TANGA KUJIONE SEHEMU LITKAPOJENGWA BOMBA LA MAFUTA

March 25, 2016




Kapteni wa Mamlaka ya Bandari Tanzania  (TPA), Andrew Matilya, akimuonyesha Waziri wa Maendeleo Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni eneo ambalo litajengwa bomba la mafuta kutoka Tanga hadi Uganda. Wa nyuma ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella.




 Waziri wa Maendeleo Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni, akiangalia ramani ya eneo ambalo litajengwa bomba la Mafuta kutoka Tanga hadi Uganda ambalo litajengwa eneo la Raskazone. Wapi kushuto mwenye suti ya blue ni Mkurugenzi wa Shirika la POetrol Tanzania (TPDC) James Mataragio (kulia) mwenye shati jeupeni Kapteni wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Andrew Matilya na kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari Tanga, Hendry Arika.

WANAFUNZI WA FEZA BOYS HIGH SCHOOL WATEMBELEA VIRGINIA INTERNATIONAL UNIVERSITY

March 25, 2016

Wanafunzi wa Feza Boys High School kutoka jijini Dar es Salaam wakipata picha ya pamoja walipokua Virginia International University iliyopo jimbo la Virginia siku ya Alhamisi March 24, 2016, wanafunzi hao wapo kwa ziara maalum ya kuangalia uwezekano wa kujiunga na chuo hicho katika masomo ya juu.
 Makamu Rais wa Chuo hicho Dr. Suleyman Bahceci (kulia) akiwaeleza wanafunzi hao taratibu za kufuata kwa ajili ya kujiunga na VIU
Kushoto ni Alex Luketa Mtanzania anayefanyakazi chuoni hapo kwa ajili ya kusajili wanafunzi kutoka Afrika Mashariki akiwa pamoja na wanafunzi wa Feza Boys High School wakimsikiliza Makamu Rais wa chuo (hayupo pichani) alipokua akielezea wanafunzi hao utaratibu wa kujiunga na masomo VIU.
Wanafunzi wa Feza Boys wakipata mulo.
Mazungumuzo yakiendelea.
 Picha ya pamoja

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ASHUHUDIA KUORODHESHWA KWA HISA STAHILI ZA MAENDELEO BANK PLC, KATIKA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM (DSE)

March 25, 2016

Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji, Mwenyekiti wa Maendeleo Benki, Amulike Ngeliama (kushoto) na Mkurugenzi wa Tafiti, Sera na Mipango wa(CMSA) Nicodemus Mukama wakifuatilia jambo katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji akipiga kengele kuashiria uorodheshwaji rasmi wa Maendeleo Benki katika soko la hisa DSE jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Maendeleo Benki, Amulike Ngeliama na Mkurugenzi wa Capital Markets na Securities Authoriy (CMSA) Nicodemus Mukama 
Emmanuel Nyalali, Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji DSE akizungumza katika hafla hiyo. 
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji akiongea wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa Maendeleo Benki katika soko la hisa DSE
Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Benki, Ibrahim Mwangalaba akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisah Mwenyekiti wa Benki hiyo kuzungumza na washiriki wa hafla hiyo. 
……………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Bank PLC ni benki iliyoanzishwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani na inamilikiwa na Wananchi mbalimbali kwa njia ya HISA bila kujali, kabila, itikadi, dini wala rangi, kwani benki hii imesajiliwa na soko la hisa la Dar es Salaam (DSE), kupitia dirisha dogo yaani Enterprise Growth Market (EGM) na inaendeshwa kwa kufuata taratibu zote za BOT na Soko la Hisa la Dar es S alaam. Maendeleo Bank ilianza kutoa huduma za kibenki tarehe 9/9/2013 baada ya kupewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania na tarehe 05/11/2013 ilisajiliwa rasmi katika soko la hisa la Dar es Salaam baada ya kukidhi vigezo vyote vilivyowekwa na mamlaka husika. Benki hii ilianza na mtaji wa shilingi bilioni 4.5 kutoka kwa wanahisa zaidi ya 3,000 wa rika na itikadi mbalimbali walionunua wakati wa mauzo ya awali (IPO) yaliyofanyika mwaka 2013.
Tarehe 9/11/2015 benki ilipata kibali cha kuuza hisa stahili ambapo matarajio yake yalikuwa kupata shilingi bilioni 3.06 ambazo zitatumika kuimarisha shughuli za uendeshaji wa benki pamoja na kuongeza matawi. Katika zoezi la uuzaji wa hisa stahili benki imeweza kupata jumla ya shilingi bilioni 2.8 na kufikisha jumla ya mtaji wa benki kuwa shilingi bilioni 7.3.
Kusudi kubwa la kuanzishwa kwa Maendeleo Bank PLC ni kufikisha huduma za kibenki kwa wananchi wa kipato cha chini na cha kati kwani hao ndio walio wengi na upatikanaji wa huduma za kibenki kwao ni changamoto kubwa. Benki hii imepata mafanikio mengi tangia kuanzishwa kwake takribani miaka miwili iliyopita ambapo mpaka tarehe 31/12/2015, benki imefikisha wateja zaidi ya 12,000, amana zaidi ya shilingi bilioni 46.0, mali za benki zimefikia zaidi ya shilingi bilioni 55, imetoa mikopo zaidi ya shilini bilioni 21.0 na mwaka 2015 imepata faida ya takribani shilingi milioni 200.0 baada ya kodi. 
Benki hii inatoa huduma mbalimbali za ubunifu ambazo zinawalenga wananchi wa kada mbalimbali, zikiwemo: huduma za kibenki kwa njia ya simu, huduma za BIMA, ATM kupitia mtandao wa UMOJA Switch, akaunti mbalimbali zenye gharama rafiki, kutuma na kupokea pesa kutoka nje na ndani ya nchi, na kutoa mikopo ya aina mbalimbali, ikiwemo kwa wajasiliamali wadogo ambayo haina dhamana, yaani mikopo ya vikundi.
 Zaidi ya watu 150 wamejitokeza kuhakiki silaha zao.  diwani_athumani

Zaidi ya watu 150 wamejitokeza kuhakiki silaha zao. diwani_athumani

March 25, 2016
diwani_athumani 
                                            Na. Immaculate Makilika –MAELEZO
……………………………………..
Mkurugenzi  wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna wa Polisi Diwani Athumani amesema hadi kufikia sasa zaidi ya watu 150  wamejitokeza  kuhakiki wa  silaha zao, katika hatua ya  kutii agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul  Makonda.
“Baada ya Mheshimiwa Rais John Pombe  Magufuli  kufanya uhakiki wa silaha zake  hivi karibuni, watu zaidi ya 150 wakiwemo viongozi mbalimbali waliopo Serikalini, Viongozi wastaafu, Mabalozi wa nchi mbalimbali, wafanyabiashara na  wabunge wamejitokeza  kuhakiki  silaha zao, na wengine wameonesha nia ya kufanya hivyo,  hata hivyo tusingependa kutaja majina yao kwa sababu za kiusalama” amesema Kamishna wa Polisi Athumani
Athumani amesema kuwa, lengo la kufanya uhakiki wa silaha ni pamoja na kuboresha hali ya usalama na kuwajua watumiaji, kuwatambua tena wamiliki wa silaha pamoja na kuwa wanawatambua isipokuwa  zinaweza kutokea sababu mbalimbali zitakazofanya wasiendelee kumiliki silaha hizo ikiwemo vifo na ulemavu na  kusema kuwa  wangependa kufahamu taarifa za namna hiyo, ameongeza kuwa  zoezi hili sasa ni la nchi nzima si kwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee kama ilivyokuwa hapo awali.
Aidha, wakazi wa  mkoa wa Dar es Salaam wanaweza  kuhakiki silaha zao katika vituo vya  Osterbay Polisi, Temeke Chang’ombe Polisi na Ilala central Polisi, ambapo wanatakiwa kwenda na  kitabu(firearm  licence book), picha ndogo nne za mhusika,  pamoja na  anwani sahihi ya mahali anapoishi mhusika.
Vilevile, amewataka viongozi mbalimbali na wananchi wanaomiliki silaha kujitokeza kwa ajili ya kufanya uhakiki wa silaha zao huku akisisitiza kwa wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam, wanaweza kuonana na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro na kwa wakazi wa Mikoani waonanae na makamanda wa polisi wa Mikoa yao kwa ajili ya kupewa msaada na maelekezo zaidi ya taratibu  za kufuata ili waweze kufanya uhakiki wa  silaha zao.

MKURUGENZI MKUU MPYA WA NSSF ATEMBELEA DARAJA LA KIGAMBONI

March 25, 2016

Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara  akisalimiana na Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF, Yacoub Kidula.
Wataalamu wa ujenzi wa daraja la Kigamboni wakisalimiana na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara.
Barabara za kuingilia darajani upande wa Kurasini.
Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo akionyesha njia za kuingia na kutoka darajani
Barabara ya kuingilia darajani upande wa kushoto na barabara ya kutokea mjini upande wa kulia. 
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara  (wa tatu kushoto) akipata maelezo kutoka kwa wahandisi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni wakati wa ziara yake ya kutembelea daraja la Kigamboni. 
Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo akifafanua jambo
kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Prof. Godius Kahyarara  (katika) alipotembelea daraja wa Kigamboni
jijini Dar es Salaam, daraja hilo linatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni baada ya kumalizika kwa ujenzi wake

WAHOLANZI WAWILI WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA KIA NA TUMBILI 61

March 25, 2016

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa akiwa ofisini kwake muda mfupi kabla ya kuzungumza na wanahabari.

 Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .


VYOMBO vya ulinzi na usalama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) vimefanikiwa kuwanasa wafanyabiashara wawili ndugu ,raia wa Uholanzi wakiwa katika harakati ya kusafirisha wanyama Hai 61,aina ya Tumbili kuelekea nchini  Armenia.


Wanyama hao wakiwa kwenye makasha sita tofauti ya kuhifadhia wanyama walikuwa wasafirishwe kwa ndege maalumu ya mizigo yenye namba EW/364G iliyosajiliwa nchini Belarus kupitia kampuni ya Arusha Freight Limited ya jijini Arusha.


Raia hao wa Uholanzi waliokamatwa juzi majira ya saa 1:30 jioni katika uwanja wa ndege wa KIA wametambulika majina yao kuwa ni Arten Vardanian (52) aliyekuwa na hati ya kusafiria yenye namba NWF8CKJR8  na Edward Vardanian (46) aliyekuwa na hati ya kusafiria namba NY969P96.


Meneja usalama uwanja wa ndege KIA,Kisusi Justine aliliambia Tanzania Daima mbali na kukamatwa kwa raia hao wa kigeni pia walifanikiwa kumshikilia Mtanzania ,Idd Misanya anayedaiwa kuwauzia wanyama hao.


“Wahusika hawa wawili walifika eneo la Cargo ambako walikuwa katika harakati za kusafirisha wanyama hao ndipo tulipowashikilia kwa sababu taratibu za kusafirisha wanyama Hai zilikiukwa”alisema Justine.


Kuhusu mazingira ya kukamtwa kwa watuhumiwa hao ,Justine alisema ndege hiyo inaonekana ilitua katika uwanja huo mahususi kwa ajili ya kubebeba wanyama hao na kwamba ili ruhusiwa kuondoka jioni ile baada ya kukamatwa kwao.


Kamnda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna msaidizi wa Polisi ,Wilbroad Mutafungwa alithibitisha kukamatwa kwa raia hao na kwamba wamehifadhiwa katika kituo cha Polisi cha KIA huku uchunguzi zaidi ya tukio hilo ukiendelea.


“Mnamo Machi 23 mwaka huu majira ya saa 1:30 jioni huko uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA ) tulifanikiwa kuwakamata raia wawili wa Uholanzi wakiwa wanataka kusafirisha wanyama aina ya tumbili na tayari uchunguzi kwa kushirikiana na Wizara ya maliasili na Utalii unaendelea”alisema Mutafungwa.


Kamanda Mutafungwa alisema taarifa za awali zinasema wanyama hao waalisafirishwa hadi uwanjani hapo wakitokea mpakani mwa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambapo kampuni ya uwakala ya Arusha Fright Limited ilipewa kazi hiyo.


Alisema uchunguzi wa awali unaonesha ndege ya mizigo iliyokuwa isafirishe wanyama hao ni ya binafsi huku akikanusha kukamatwa kwa mtu mwingine anyetajwa kuhusika katika kuuza wanyama hao kwa raia hao wa Uholanzi.


“Mpaka sasa tumewakamata hao raia wawili ,lakini kama nilivyosema uchunguzi unaendelea tukishirikiana na wizara ya maliasili na utalii ili tuone kama kuna washiriki wengine wa tukio hilo ,so far tunao hao wawili tu”alisema Mutafungwa.


Alisema mbali na hati za  raia hao wa uholanzi kuonesha kuwa walikuwa wakiishi nchi kihalali bado vyomb vya ulinzi na usalama ikiwemo idara ya Uhamiaji vimeanza kuchunguza pia uhalali wa vibali vya raia hao vya kuishi nchini.


Mwisho.