RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI MKOANI DODOMA

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI MKOANI DODOMA

April 24, 2017
unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
A
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
A 1
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
A 2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
A 3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Abdallah Bulembo mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
A 4
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma. Pembeni yake ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai.
A 5
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa  na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma. PICHA NA IKULU
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ALAANI VURUGU ZILIZOTOKEA KATIKA MKUTANO WA WANAOSEMEKANA KUWA NI VIONGOZI WA CUF NA WAANDISHI WA HABARI

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ALAANI VURUGU ZILIZOTOKEA KATIKA MKUTANO WA WANAOSEMEKANA KUWA NI VIONGOZI WA CUF NA WAANDISHI WA HABARI

April 24, 2017
331 

Nimesoma na kuona katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu vurugu zilizotokea tarehe 22 Aprili, 2017 katika hoteli ya Vina, Mabibo hapa Dar es salaam, zinazosemekana kuhusisha wanachama wa CUF.

Ni ukweli usiopingika kuwa, suala la mgogoro wa uongozi katika chama cha CUF lipo mahakamani, lakini nikiwa msimamizi wa Sheria ya Vyama vya Siasa na kutambuliwa na jamii kuwa ni mlezi wa vyama vya siasa; nimelazimika kuwasihi wadau wa siasa hususani wanachama wa chama cha CUF, kutambua kwamba, kuwapo kwa shauri mahakamani siyo fursa ya kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani, kwani jambo hili ni uvunjifu wa sheria na linaleta sura mbaya kwa jamii.

Hivyo, ninalaani vurugu hizo, ambazo zilionekana kuvunja amani na utulivu na watu kuumizwa, tofauti na tunu zetu za taifa za amani na utulivu. Pia, nawaasa wanachama wa CUF pamoja na tofauti walizonazo, madhali masuala haya yapo mahakamani hebu tuheshimu utawala wa Sheria.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na hata Jeshi la Polisi lipo kushughulikia malalamiko yoyote yanayohusu uendeshaji na shughuli za chama chochote cha siasa. Hivyo, hakuna haja ya wanachama wa chama cha CUF kukiuka taratibu za kuendesha chama hicho au kujichukulia Sheria mkononi.

Aidha, ninaviasa vyama vya siasa kuelewa kuwa havipo juu ya Sheria, vinapaswa kuheshimu na kufuata Sheria za nchi, ikiwamo kutunza amani na utulivu tulionao.

Mwisho, ninaomba vyombo vya ulinzi na usalama katika nchi yetu kulifanyia kazi tukio hilo, ili wahusika wafahamike na kuchukuliwa hatua za kisheria. Kwa upande wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inayosimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa, haitasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria. 
                  Jaji Francis S.K. Mutungi                                
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA
24 Aprili, 2017
SERIKALI KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA MAGONJWA.

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA MAGONJWA.

April 24, 2017
C
Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeanza hatua za awali za uainishaji wa gharama,uandaaji wa mfumo mbadala na upembuzi wa kina wa aina ya ubia ili kushirikiana na Sekta binafsi katika utoaji wa huduma za uchunguzi wa magonjwa.
Hayo yamesemwa leo bungeni na Naibu Waziri, Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Hamis Kigwangalla wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.
“Kufuatia kukua kwa kasi kwa Sayansi na Teknolojia ya uchunguzi wa magonjwa,Wizara inakubaliana na wazo hili juu ya kuangalia namna nzuri ya kushirikiana na sekta binafsi katika utoaji wa huduma hizi,”Alisema Mhe.Kigwangalla.
Amesema kwa kuanzia sasa Wizara yake inafikiria kuanzisha ushirikiano kwa kupitia ukodishaji wa vifaa ambapo Serikali itakodisha mashine hizo ambazo zitakuwa za mbia na Serikali haitahusika na ununuzi,ufungaji na matengenezo kinga ya mashine hizo.
Aidha amebainisha kuwa katika mfumo huo,Wizara itakuwa na jukumu la kusimamia utoaji wa huduma na itapata gawio lake kutokana na makusanyo yatokanayo na uchangiaji wa huduma kulingana na mkataba.
“Ni imani ya Wizara kuwa kutumia mfumo wa ubia na sekta binafsi(PPP) huduma za uchunguzi wa magonjwa zitaimarika na kuipunguzia Serikali mzigo wa gharama”,Aliongeza Mhe.Kigwangalla.
SERIKALI YAONDOA TOZO ZISIZO ZA LAZIMA KATIKA ZAO LA KOROSHO

SERIKALI YAONDOA TOZO ZISIZO ZA LAZIMA KATIKA ZAO LA KOROSHO

April 24, 2017
g
Na Daudi Manongi-MAELEZO,DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvivu imesema imeshughulikia malalamiko  ya wakulima wa Korosho kwa kuondoa makato yasiyokuwa muhimu katika zao hilo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Wizara hiyo Mhe.William Ole Nasha wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge leo Mjini Dodoma.
“Serikali imekwisha fanyia marekebisho maeneo ambayo wakulima walikuwa wanalalamikia kwa kuondoa kabisa makato hayo katika zao hilo”, Aliongeza Mhe.Ole Nasha.
Amesema kuwa Serikali imefuta ushuru wa shilingi 20 kwa kilo kwa ajili ya chama kikuu cha Ushirika,Shilingi 50 za usafirishaji wa Korosho,Shilingi 10 kwa kilo ajili ya mtunza ghala na pia shilingi 10 kwa kilo kwa ajili ya kikosi kazi cha Masoko.Aidha Sekta ina utaratibu maalum wa kupanga bei dira kwa kutumia vigezo vinavyokubaliwa kwa pamoja na wadau wote.
Kwa upande wa manunuzi ya pembejeo za korosho amesema hufanywa kwa pamoja na vyombo rasmi ndani ya Tasnia ambapo awali ilikuwa ikisimamiwa na mfuko wa Maendeleo ya Korosho na sasa Bodi ya korosho Tanzania.
Aidha ameeleza changamoto zinazojitokeza katika kufikisha pembejeo hizo kwa wakulima wa korosho na hatua zimechukuliwa kwa kushirikisha vyama vya ushirika ili kudhibiti mianya ya pembejeo kwenda kwa wasio lengwa.
Pia Serikali imeweka mfumo wa usambazaji wa pembejeo wenye lengo la kuhakikisha kwamba pembejeo hizo zinawafikia walengwa pekee.
“Utaratibu huu unazingatia kutambua wakulima wenye uhitaji na pembejeo na hununuliwa kwa kutumia utaratibu wa ununuzi wa pamoja n akusambazwa kwa wakulima kwa kutumia wakala  walioteuliwa na kudhibitishwa na Halmashauri husika”,Alisisitiza Mhe.Ole Nasha.

JOKATE MWEGELO ATEULIWA KUWA KAIMU KATIBU HAMASA NA CHIPUKIZI UVCCM

April 24, 2017

Ndugu zangu, vijana wenzangu wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na vijana wote wenye mapenzi mema na chama chetu na Watanzania wote kwa ujumla.

Nitangulie kwa kuwashukuru kamati ya utekelezaji ya UVCCM TAIFA kwa kuonyesha mapenzi makubwa na imani kubwa kwangu kwa kukubali kuniteua ku-kaimu nafasi ya Katibu wa UHamasa na Chipukizi. 

Imani yenu kwangu inabaki kuwa deni na chachu ya kujitoa kwa nguvu zote, kwa akili zote kuitumikia vizuri nafasi hii. Mwenyezi Mungu anisaidie.

Pili, kama ilivyo alama ya kwenye nembo ya jumuia yetu, ile alama ya mwenge wa uhuru. Mwenge wa Uhuru unaashiria nuru na mwanga. Mwenge huu unamulika nchini na nje ya mipaka ili kuleta matumaini pale ambapo kuna kukata tamaa, upendo pale kwenye chuki na heshima pale penye dharau- hii nimenukuu. 

Hivyo sifa kuu ya mwenge wetu wa uhuru kwenye nembo ya jumuiya yetu ya vijana ni kutoa mwanga, na sifa kuu ya mwanga ni kuweza kutokomeza giza na kutoa tumaini. Hivyo sisi kama vijana tunategemewa kuwa tumaini. Sisi kama vijana tunategemewa kuonyesha si tu njia bali kuwa tumaini kwamba taifa lilioasisiwa na waasisi wa nchi hii "our founding fathers" lipo katika mikono salama. 

Na hatuishii hapo bali jukumu la kuleta tumaini hili liko kwenye sehemu sahihi kupitia jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama chetu Cha Mapinduzi. Sehemu pekee ambapo viongozi wa sasa na baadae hupikwa vilivyo kuweza kuitumikia nchi yetu kwa weledi na uadilifu uliotukuka. Hivyo basi ni lazima kutengeneza taswira itakayowapa hamu vijana wa Tanzania kutamani kuwa sehemu ya UVCCM. Ni lazima tuwe wabunifu na kuvutia vijana wengi zaidi ili kupanua wigo wetu pia.

Tatu, hii nafasi niliopewa ni ya uwakilishi tu sio yangu, mimi nawakilisha tu vijana milioni nne na ushee amabao ni wanachama wa jumuiya hii. Walikuwepo viongozi kwenye nafasi hii kabla yangu na watakuja wengine baada yangu. Hivyo basi natoa rai tushirikiane, tufanye kazi wote tujenge jumuiya hii kwa umoja wetu. Nahitaji sana maoni na ushirikiano wenu. Ni muda jumuiya yetu iendane na nyakati za sasa ili tusipoteze watu na vile vile watu wasiachwe nyuma katika harakati zetu hizi. Na hasa katika kipindi hiki tunavyojiandaa na uchaguzi wa ndani ya chama.

Nne, hivi karibuni tutazindua njia ya kisasa na kampeni itakayosaidia kurahisisha upatikanaji wa habari ndani ya jumuiya yetu. Naomba mkae tayari kupokea mapinduzi hayo ambayo ni ya kwanza ndani ya Chama chetu cha Mapinduzi (CCM).

Kuelekea sherehe za Muungano tarehe 26/04/2017, ambapo kwa mara ya kwanza yatafanyika katika makao makuu ya nchi, Dodoma. Nawakaribisha tumuunge mkono Rais wetu Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli kwa kushiriki katika mazoezi asubuhi na kisha matembezi yatakayo hitimishwa kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Taarifa rasmi itatoka hivi punde.

Nihitimisha kwa kuwashukuru wote walionipongeza na kunitakia kheri katika utumishi huu. Katika falsafa za ubuntu - umuntu ngumuntu ngabantu, tunasema "I am because we are".

Nawataki kazi njema,

Wenu Katika Utumishi,

Jokate Mwegelo.
K/Katibu Hamasa na Chipukizi.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hapa Kazi Tu!

Wadau wakutana kujadili uwekezaji katika kilimo

April 24, 2017
 Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kushirikiana na Mfuko wa Kukuza Sekta ya Fedha (FSDT) imewakutanisha pamoja wadau kutoka sekta mbalimbali za maendeleo nchini kujadili masuala mbalimbali yatakayosaidia uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo Tanzania.

Akizungumza katika kikao kazi hicho mwenyekiti wa Kikundi Kazi, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Peniel Lyimo alisema kuna haja ya  dhamira ya dhati na uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo nchini ili kusaidia juhudi za Serikali za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini.
Mwenyekiti wa Kikundi Kazi, Bw. Peniel Lyimo (Katikati) akizungumza na wajumbe wa Kikundi Kazi (Hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili uwekezaji katika sekta ya kilimo uliofanyika katika Hoteli ya Court Yard, Dar es Salaam. Wanaomsikiliza Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga na Mkuu wa Kilimo na Fedha Vijijini wa FSDT, Bw. Mwombeki Baregu (Kulia).

Bw. Lyimo alisema kuwa ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa hali inayorudisha nyuma mapinduzi katika sekta ya kilimo nchini.

“Kuna haja ya kutafuta suluhisho la changamoto za upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya Kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga akizungumza juu ya umuhimu wa wadau katika kuchagiza uwekezaji katika sekta ya kilimo nchini.

MATUKIO KATIKA PICHA: KIKAO CHA 11 MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO APRIL 24, 2017

April 24, 2017
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongoza kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017.
Naibu Waziri wa Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Nyonyani akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017. 
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017. 
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017. 

WANAWAKE KANISA LA PENTEKOSTE WAOMBA AMANI ILIYOPO NCHINI IDUMISHWE

April 24, 2017
 Mwenyekiti wa Muungano wa Wanawake wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (MMPT) Misheni ya Kijitonyama,  Maines Mhama (kulia), akimkabidhi maua mgeni rasmi wa maadhimisho ya siku ya wanawake wa kanisa hilo, Anitha Mshighati (katikati), mara baada ya kuwasili kwenye sherehe hiyo iliyofanyika Kanisa la Pentekoste la Kituo cha Tabata Kisiwani Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mchungaji Ibrahim Mshighati mume wa mgeni rasmi.

MASHINDANO YA MEI MOSI KITAIFA YAZINDULIWA MJINI MOSHI

April 24, 2017
Timu ya Watumishi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakiingia uwanjani kwa maandamano wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Mei Mosi kitaifa yanayofanyika mjini Moshi.
Timu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakiingia uwanjani .
Timu ya Wizara ya Uchukuzi wakingia uwanjani.
Timu za Mashirika na Taasisi mbalimbali wakiwa wamebeba mabango wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya Mei Mosi yanayofanyika kitaifa mjini Moshi.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Mashindano ya Mei Mosi kitaifa ,Awadi Safari akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano hayo uliodfanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano ya Mei Mosi Kitaifa ,Joyce Benjamini akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano hayo katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Mgeni rasmi katika ufunguzi rasmi wa mashindano hayo ,Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akitoa hotuba ya ufunguzi wa mashindano hayo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba (aliyevaa suti) akiongozana na Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Mei Mosi kitaifa ,Joyce Benjamin kwa ajili ya ukaguzi wa timu zinazoshiriki mashindano hayo.
Mwamuzi wa Kike ,Salma akimtambulisha Mkuu wa wilaya timu mbalimbali zilizopo pamoja na kumkaribisha kwa ajili ya ukaguzi.

VIJANA DAR ES SALAAM WAANZISHA KLABU ZA MABADILIKO KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA MASOKONI

April 24, 2017
Mwezeshaji wa Kisheria wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Mariam Rashid (kulia), akitoa mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa vijana wafanyabiashara katika Soko la Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam kabla ya kufungua klabu za mabadiliko za kupinga ukatili huo katika soko hilo mwishoni mwa wiki.

Droo ya pili ya biko

April 24, 2017
Msanii wa nyota wa filamu Tanzania, Kajala Masanja kulia, akichezesha droo ya pili ya kuwania Sh Milioni 10 ya mchezo wa Bahati Nasibu ya Biko 'Nguvu ya Buku' iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam ambapo mshindi wake Nicholaus Mlasu kutoka Ukonga Mombasa, Ilala alinyakua kitita hicho na kuhudhuriwa na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo mwenye kitabu mkoni. Katikati ni mshindi wa Biko wa wiki iliyopita, Christopher Mgaya. Picha na Mpiga Picha Wetu.

Nicholaus Mlasu azoa milioni 10 za Biko ‘Nguvu ya Buku’

Na Mandishi Wetu, Dar es Salaam
DROO ya pili ya wiki kutafutwa mshindi wa shindano la Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ ya kuwania Sh Milioni 10 imefanyika leo asubuhi huku mkazi wa Ukonga Mombasa, Ilala, jijini Dar es Salaam, ameibuka na ushindi huo na kuwa mtu wa pili kufaidika na mamilioni ya Biko, baada ya Christopher Mgaya kushinda wikiiliyopita na kukabidhiwa mamilioni yake.
Picha nyingine Kajala Masanja akimtangaza mshindi wa Biko wa wiki hii Nicholaus Mlasu kunyakua Sh Milioni 10 za Biko katika droo hiyo.

Mshindi huyo amepatikana katika droo iliyochezeshwa jana na Balozi wa Biko, Kajala Masanja pamoja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo pamoja na Mgaya mshindi wa wiki iliyopita.
Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania kwenye notebook mkononi pamoja na mshindi wa wiki iliyopita, Chiristopher Mgaya wakiisoma namba ya mshindi wa wiki hii ambaye bwana Nicholaus Mlasu alitangazwa mshindi.

Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba ni furaha yao kubwa kuona wamempata mshindi mwingine aliyeshinda Sh Milioni 10 kutoka kwenye shindano lao linalofanyika kila mwisho wa wiki.

Alisema bahati nasibu ya Biko imezidi kujizolea umaarufu mkubwa kwa siku chache kutokana na urahisi wake wa kucheza pamoja na kutumia muda mdogo kulipa washindi wake, hususan wa zawazi za papo kwa papo zinazopatikana baada ya kucheza kwa kufanya miamala ya kifedha kwa simu za Vodacom, Tigo na Airtel Money.

“Ni rahisi kucheza Biko kwa sababu mtu anafanya muamala kwenye simu yake kuanzia Sh 1000 ambapo kwanza katika kipengele cha lipa bili, atakwenda kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 kisha ataweka 2456 kama namba yetu ya kumbukumbu.

“Baada ya kufanya hivyo mteja atapokea ujumbe wa maandishi katika simu yake kumjulisha hatua aliyofikia baada ya kucheza na tunashauri wateja wacheze biko mara nyingi ili wajiwekee nafasi nzuri ya kushinda kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Milioni 1,000,000 kama zawadi zetu za papo kwa hapo, pamoja kupata nafasi ya kuingia kwenye droo ya wiki kuwania donge nono la Sh Milioni kumi (10,000,000) ambalo leo ndugu yetu Mlasu ameibuka na ushindi huo mnono,” Alisema Heaven na kumpongeza mshindi wao pamoja na kuwataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kuwania mamilioni ya Biko.

Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Jehud Ngolo alisema kwamba ni hatua nzuri kuona washindi wa Biko wanapatikana kila wiki sambamba na kupokea zawadi zao haraka.

“Bodi tunafarijika kwa sababu wale washindi wanapopatikana hupokea malipo yao kwa haraka hivyo wanaweza kuzitumia fedha zao katika mambo ya kimaendeleo na kujikwamua kiuchumi kwa kupitia mchezo wa Biko, hivyo nawaomba Watanzania waendelee kucheza biko ili wapate nafasi ya kuvuna fedha mbalimbali kwa kupitia bahati nasibu ya Biko,” alisema.

Naye mshindi wa Sh Milioni 10, Nicholaus Mlasu, alipokea simu ya ushindi kwa furaha na kusema amefurahishwa kwa sababu alikuwa akicheza Biko kwa malengo ya kushinda sambamba na kumuomba Mungu atimize maombi yake ili azoe mamilioni ya Biko.

Nimefurahi sana kwa kushinda Biko, namshukuru Mungu kwa kuniona maana sasa nimeweza kuibuka na mamilioni hayo ambayo nitayatumia vizuri maana ndio malengo yangu ya kucheza Biko kila siku ili niweze kushinda donge nono, alisema Mlasu.

Bahati nasibu ya Biko Ijue Nguvu ya Buku imezidi kushika kasi huku tayari ikiwa imeshamkabidhi mshindi wake wa kwanza Christopher Mgaya Sh Milioni 10 zake wiki iliyopita sambamba na kupewa elimu ya fedha kutoka benki ya NMB, Makao Makuu jijini Dar es Salaam.